Agano la Kale 2022
Machi 7–13. Mwanzo 37–41: “Bwana Alikuwa Pamoja na Yusufu”


“Machi 7–13. Mwanzo 37–41; ‘Bwana Alikuwa pamoja na Yusufu’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano la Kale 2022 (2021)

“Machi 7–13. Mwanzo 37–41,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2022

Picha
Yusufu wa Misri akiwa gerezani

Mchoro wa Yusufu ndani ya gereza, na Jeff Ward

Machi 7–13

Mwanzo 37–41

Bwana Alikuwa pamoja na Yusufu”

Ni kweli gani kutoka Mwanzo 37–41 watoto katika darasa lako wanahitaji kuelewa vizuri? Zingatia misukumo inaokuja kwako unapojiandaa kufundisha.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Wape watoto dakika chache kuchora kitu fulani walichojifunza kuhusu injili nyumbani au Kanisani. Waombe watoto washiriki na kuzungumza kuhusu picha zao.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Mwanzo 37

Naweza kuwa mkarimu kwa familia yangu.

Ndugu zake Yusufu walimwonea wivu na walimtendea vibaya. Unawezaje kusaidia watoto kuelewa umuhimu wa kuwa wema kwa wengine, haswa washiriki wa familia?

Shughuli Yamkini

  • Ili kusimulia hadithi ya Yusufu na ndugu zake kutoka Mwanzo 37, unaweza kutumia picha kutoka Njoo unifuate–kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia au “Yusufu huko Misri” (katika Hadithi za Agano la Kale). Acha watoto wasaidie kwa kushiriki maelezo wanayoyajua kuhusu hadithi. Waulize maswali kama vile, ”Ni jinsi gani ndugu wa Yusufu hawakuwa na wema kwake?” Wasaidie watoto kufikiria kuhusu vitu ambavyo kaka za Yusufu wangeweza kufanya ili kumuonyesha upendo. Je, tunapaswa kufanya nini tunapohisi hasira kwa washiriki wa familia yetu?

  • Onyesha picha ya familia (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na.112), na waalike watoto wachore picha za familia zao. Waombe washiriki njia wanazoweza kuwa wenye fadhili kwa wanafamilia.

  • Imbeni pamoja wimbo kuhusu kupenda familia zetu, kama vile “A Happy Family” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 198). Tunaweza kufanya nini kuzisaidia familia zetu ziwe na furaha?

  • Acha watoto wapake rangi ukurasa wa shughuli wa wiki hii na, katika nafasi iliyotolewa, chora picha ya wanafamilia wakiwa wenye fadhili.

Mwanzo 37:18–28; 39:20–23

Mungu anaweza kunisaidia wakati mambo mabaya yanapotokea.

Mambo mengi mabaya yalitokea kwa Yusufu, lakini alichagua kutii amri na Bwana alikuwa pamoja naye. Watoto wadogo wanaweza kujifunza kutoka kwenye hili kwamba Mungu anataka kuwasaidia wakati wa hali ngumu katika maisha yao.

Shughuli Yamkini

  • Elezea baadhi ya mambo magumu yaliyotokea kwa Yusufu (ona Mwanzo 37:23–28; 39:20; au “Yusufu na Ndoto Yake” na “Yusufu huko Misri,” katika Hadithi za Agano la Kale). Baada ya kuwaambia watoto kuhusu kila shida ambayo Yusufu alikabiliana nayo, waalike warudie, “Bwana alikuwa pamoja na Yusufu” (Mwanzo 39:2).

  • Shiriki picha za Mwokozi akiwasaidia watu ambao walikuwa wanakabiliwa na changamoto (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 40–43). Waalike watoto kushiriki jinsi Mwokozi alivyokuwa akiwasaidia watu. Shiriki ushuhuda wako kwamba Bwana anaweza kutusaidia wakati mambo mabaya yanapotokea kwetu.

  • Imbeni pamoja wimbo kuhusu upendo wa Mwokozi, kama vile “Jesu is Our Loving Friend” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 58). Shiriki uzoefu wakati ulihisi upendo wa Mungu wakati wa changamoto. Onyesha picha ya Yesu, na uwaalike watoto kushiriki jinsi wanavyohisi juu Yake.

Mwanzo 41:15–36, 47–57

Mungu anaweza kunionya kuhusu hatari.

Mungu alimsaidia Yusufu kuelewa kwamba ndoto za Farao zilikuwa onyo la kuandaa nyakati ngumu za wakati ujao. Wasaidie watoto kuelewa kwamba Mungu anaweza kuwaonya kuhusu hatari, pamoja na hatari ya kiroho.

Picha
Yusufu gerezani akitafsiri ndoto

Joseph Akitafsiri ndoto za Mkuu wa Wanyweshaji na Mkuu wa Waokaji, na François Gérard

Shughuli Yamkini

  • Gawanya picha za chakula kuzunguka chumba, na waalike watoto wakusanye na “wahifadhi” kwenye chombo. Tumia shughuli hii kuwaambia watoto kuhusu jinsi Mungu alivyomwonya Farao ili ajiandae na wakati ambapo hakutakuwa na chakula (ona Mwanzo 41:15–36, 47–57). Acha watoto wachore picha za mambo ambayo Farao aliota na watumie picha zao kufundisha familia zao nyumbani.

  • Onyesha picha ya nabii wa sasa. Waambie watoto kuhusu mafundisho au maonyo ambayo Mungu ametupatia kupitia yeye. Fafanua kuwa tutabarikiwa na kulindwa tunapomfuata nabii. Waalike watoto watekeleze vitu ambavyo wanaweza kufanya kufuata ushauri wa nabii.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Mwanzo 39:1–3, 20–23; 41:38

Ikiwa mimi ni mwaminifu, Mungu atanisaidia wakati wa hali ngumu.

Pamoja na kwamba Yusufu alikuwa na majaribu mengi magumu, alibaki kuwa mwaminifu na “Bwana alikuwa pamoja naye” (Mwanzo 39:3). Uzoefu wake unaweza kuwasaidia watoto kuhisi kuwa na hakika kwamba Mungu atawasaidia wakati wa majaribu.

Shughuli Yamkini

  • Waombe watoto kupata maneno au vifungu vya maneno katika Mwanzo 39:1–3, 20–23; 41:38 ambavyo huonyesha kuwa Mungu alikuwa na Yusufu wakati wa magumu yake. Ikiwezekana, waalike watoto wafanye ishara ndogo inayoonyesha moja ya vifungu vya maneno waliyopata. Wahimize waende na ishara zao nyumbani ili kuwakumbusha kuwa Bwana atakuwa pamoja nao wakati wa majaribu yao.

  • Waalike watoto kushiriki kile wanachofikiri kifungu “Bwana alikuwa na Yusupu” kinamaanisha nini (Mwanzo 39:2). Waalike washiriki uzoefu wa wakati walipoona kuwa Bwana alikuwa pamoja nao au familia zao katika wakati mgumu. Shiriki uzoefu kama huo kutoka kwenye maisha yako.

Mwanzo 37:3–28

Naweza kuwa na furaha wakati mambo mazuri yanatokea kwa wengine.

Wivu ulisababisha ndugu wa Yusufu kufanya uchaguzi mbaya. Chaguzi zao mbaya zilimuumiza Yusufu na kuvunja moyo wa baba yao. Hadithi hii inaweza kusaidia watoto kuchagua kuwa na furaha wakati wengine wanapobarikiwa na Bwana.

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto kurudia Mwanzo 37:3–11 na wachore picha ya koti la Yusufu na ndoto zake mbili. Kaka zake Yusufu walijisikiaje kuhusu Yusufu? Wangewezaje kujibu tofauti na walivyofanya? Jadili kwa nini ni muhimu kuwa na furaha wakati vitu vizuri vinapotokea kwa watu wengine.

  • Waombe watoto kushiriki hali kadhaa ambazo mtu anaweza kuhisi wivu kuhusu mtu mwingine. Imbeni pamoja wimbo kuhusu kuonyesha upendo kwa wengine, kama vile “Love One Another” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 136–37). Sisitiza kwamba Baba wa Mbinguni anaweza kutusaidia kubadilisha hisia za wivu kwa hisia za upendo.

Mwanzo39:7–12

Kwa msaada wa Bwana, ninaweza kukimbia majaribu.

Kama watoto unaowafundisha wanakumbana na majaribu maisha yao yote, wanaweza kupata nguvu kutoka kwa mfano wa Yusufu wa kukimbia majaribu.

Shughuli Yamkini

  • Onesha picha ya Yusufu na mke wa Potifa (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na.11), na shiriki hadithi kutoka Mwanzo 39:7–12. Ni kwa vipi Yusufu alishinda kishawishi? Wasaidie watoto kutafuta maneno katika Mwanzo 39:7–12 yanayojibu swali hili—kwa mfano, Yusufu alijua kwamba kuwa na mke wa Potifa inaweza kuwa “dhambi dhidi ya Mungu” (mstari wa 9).

  • Waalike watoto wafikirie hali ambazo watoto wa rika zao wanaweza kujaribiwa kufanya chaguzi zisizo sawa. Waombe wachukue jukumu la kuigiza jinsi wanavyoweza kufuata mfano wa Yusufu katika hali hizi—kwa mfano, ni njia gani ambazo tunaweza kumkumbuka Mungu tunapojaribiwa?

  • Onyesha sumaku mbili, zinazomwakilisha Mungu na Shetani, na kitu kidogo cha chuma kama kipande cha karatasi, kikituwakilisha. Tumia sumaku kuelezea kuwa tunapokaribia zaidi kwa Mungu, nguvu Yake ya ushawishi itakuwa juu yetu, na vivo hivyo ni kweli tunapomkaribia Shetani. Ni nini tunaweza kufanya ili tubaki karibu na Mungu? Ni kwa namna gani Roho Mtakatifu anaweza kutusaidia?

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kushiriki njia za kukamilisha sentensi ifuatayo: “Naweza kuwa kama Yusufu kwa .” Waombe washiriki na familia zao jinsi walivyomalizia sentensi.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Alika kushiriki. Unapojadili kanuni za injili, waulize watoto kushiriki mawazo yao, hisia, na uzoefu. Utagundua kuwa wana ufahamu mwingi wenye maana.

Chapisha