“Oktoba 2–8. Waefeso: ‘Kwa Kusudi la Kuwakamilisha Watakatifu’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2023 (2021)
“Oktoba 2–8. Waefeso,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2023
Oktoba 2–8
Waefeso
“Kwa Kusudi la Kuwakamilisha Watakatifu”
Fikira na mawazo kuhusu jinsi na namna ya kufundisha vitakuja wakati kwa sala ukijifunza Waefeso, hotuba za mkutano mkuu wa hivi karibuni, muhtasari huu na Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia..
Alika Kushiriki
Fikiria kuwaalika washiriki wa darasa kuandika ubaoni sentensi moja kwa ufupi juu ya kitu walichojifunza katika kusoma kwao wiki hii. Pasipo mpangilio maalumu chagua sentensi chache, na waalike washiriki wa darasa walioziandika kuelezea mawazo yao.
Fundisha Mafundisho
Manabii na mitume—na sisi sote—tunaliimarisha na kuliunganisha Kanisa.
-
Je, wewe na washiriki wa darasa lako mngeweza kujenga kitu kwa pamoja ili kuonyesha jinsi gani Kanisa “linajengwa juu ya msingi wa mitume na manabii” na jinsi gani Mwokozi ni “jiwe kuu la pembeni”? (Waefeso 2:20). Labda washiriki wa darasa wangeweka alama kwenye matofali au vikombe vya karatasi na kuvipanga kama mnara au piramidi, na Yesu Kristo na mitume na manabii wakiwa ndio msingi. Kisha ungeweza kuonyesha nini kingetokea kama Kristo na mitume na manabii wangeondolewa. Kwa nini jiwe kuu la pembeni ni mfano mzuri wa Yesu Kristo na kazi Yake katika Kanisa? (Kwa maelezo juu ya jiwe kuu la pembeni, ona “Nyenzo za Ziada.”) Washiriki wa darasa wangeweza kupekua Waefeso 2:19–22; 4:11–16 kwa ajili ya baraka ambazo tunapokea kwa sababu ya mitume, manabii na viongozi wengine wa Kanisa. Tunaweza kufanya nini ili kujenga maisha yetu juu ya mafundisho yao?
-
Kama washiriki wa darasa lako walisikiliza mkutano mkuu tangu mlipokutana kwa mara ya mwisho, waalike kuelezea ni kwa jinsi gani mambo yaliyofundishwa wakati wa mkutano yaliwasaidia kutimiza kusudi lililosemwa katika Waefeso 4:11–16.
-
Labda ungeweza kuwapa muda washiriki wa darasa kuorodhesha baadhi ya kazi au majukumu ambayo wameombwa kuyatimiza kanisani (ona Waefeso 4:1)—kwa mfano, kaka au dada watumishi, mzazi, mfuasi wa Kristo na kadhalika. Kisha wangeweza kubadilishana orodha na mshiriki mwingine wa darasa, kusoma Waefeso 4:4–8, 11–16, na kuelezea ni kwa namna gani kutimiza majukumu katika orodha zao kunasaidia kujenga mwili wa Kristo. Tunawezaje kufanya kazi pamoja ili kuwa na umoja chini ya “Bwana mmoja, imani moja, na ubatizo mmoja”?
Kufuata mfano wa Mwokozi kunaweza kuimarisha uhusiano wa kifamilia.
-
Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kutumia ushauri wa Paulo kuhusu uhusiano wa kifamilia, unaweza kuandika maswali kama yafuatayo ubaoni: Tunawezaje kufuata mfano wa Mwokozi kwa jinsi tunavyowatendea wanafamilia wetu? (ona Waefeso 5:25). Inamaanisha nini kwako wewe “kuwaheshimu baba na mama yako”? (Waefeso 6:1–3). Tunawaleaje watoto katika “adabu na maonyo ya Bwana”? Waefeso 6:4 Washiriki wa darasa wangeweza kujadili maswali haya, katika makundi au kama darasa, wanaposoma maandiko yanayohusiana nayo. Unaweza kuwaalika washiriki wa darasa kutoa mifano waliyoiona ya watu wakiishi katika njia ambazo Paulo ameelezea.
Silaha za Mungu zitasaidia kutulinda dhidi ya uovu.
-
Ni kitu gani kingeweza kuwasaidia washiriki wa darasa kujitahidi kuvaa silaha za Mungu kila siku? Ungeweza kuandaa shughuli ambayo washiriki wa darasa wangeoanisha vipande vya silaha na kanuni au maadili, kama ilivyoelezewa katika Waefeso 6:14–17. Ni kwa namna gani kila kipande cha silaha kinasaidia kutulinda kutokana na uovu? (Kwa msaada, ona “Nyenzo za Ziada.”) Tunavaaje silaha hii? Tunaweza kufanya nini ili kutambua na kuimarisha udhaifu wowote katika silaha yetu?
Nyenzo za Ziada
Je, jiwe kuu la pembeni ni nini?
Jiwe kuu la pembeni ni jiwe la kwanza linalowekwa kwenye kona ya msingi. Linatumika kama rejeleo katika upimaji na upangaji wa mawe mengine, ambapo ni lazima yalingane na jiwe kuu la pembeni. Kwa sababu linabeba uzito wa jengo zima, jiwe kuu la pembeni lazima liwe imara, bila kutikisika na ni la kutegemewa (ona “Jiwe la pembeni,” Ensign, Jan. 2016, 74–75).
Silaha za Mungu
-
Kiuno kimefungwa na mshipi wa ukweli:Kipande hiki cha silaha ni kama mkanda unaofungwa kuzunguka kiuno. Neno funga linaweza pia kumaanisha kujikinga na, kuimarisha au kuweka mkazo.
-
Dirii ya hakiDirii huulinda moyo na viungo vingine muhimu vya mwili.
-
Kufungiwa miguu utayari tupatao kwa injili ya amaniHii humaanisha kifuniko cha ulinzi kwa miguu ya mwanajeshi.
-
Ngao ya ImaniNgao inaweza kulinda karibia kila sehemu ya mwili kutokana na mashambulizi mbalimbali.
-
Chepeo ya wokovuChepeo ya chuma hulinda kichwa
-
Upanga wa RohoUpanga unaturuhusu kuchukua hatua dhidi ya adui.