Agano Jipya 2023
Oktoba 16–22. 1 na 2 Wathesalonike: “Kikamilishe Kinachopungua katika Imani Yako”


“Oktoba 16–22. 1 na 2 Wathesalonike: Kikamilishe Kinachopungua katika Imani Yako,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2023 (2021)

“Oktoba 16–22. 1 na 2 Wathesalonike,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2023

Picha
Dada mmisionari akiongea na mvulana

Oktoba 16–22

1 na 2 Wathesalonike

“Kikamilishe Kinachopungua katika Imani Yako”

Alma alifundisha, “Na msimwamini yeyote kuwa mwalimu wenu wala mhubiri wenu, ila tu awe mtu wa Mungu, anayetembea katika njia zake na kutii amri zake” (Mosia 23:14). Andiko hili takatifu linapendekeza nini kuhusu jinsi unavyotakiwa kujiandaa kufundisha?

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Wape washiriki wa darasa dakika chache ili kwa haraka wapitie 1na 2 Wathesalonike ili kupata mstari ambao unawavutia. Waalike washiriki mistari hiyo na mtu mwingine katika darasa, na kisha uliza baadhi yao kushiriki walichojifunza kutoka kwa kila mmoja wao.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

1 Wathesalonike 1:5–8; 2:1–13

Wahudumu wa Bwna wanapaswa kuhubiri kwa uaminifu na upendo.

  • Paulo alianza Waraka kwa Wathesalonike kwa kuwakumbusha Watakatifu namna ambayo yeye pamoja na wengine walivyoshiriki injili na wao. Hii inaweza kuwa fursa nzuri kwa washiriki wa darasa kutathmini ni kwa kiasi gani wanafanya katika kufundisha na kujifunza kutoka kwa kila mmoja wao. Ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa kusoma 1 Wathesalonike 1:5–8; 2:1–13 na kutambua kanuni zinazohusiana na kushiriki injili kwa tija. Kisha wangeweza kuandika maswali kulingana na mistari hii ambayo itawasaidia wao kutathmini juhudi zao za kufundisha injili kwa wengine. Kwa mfano, swali moja lingeweza kuwa “Je, mimi ni mfano wa yale niyajuayo?” (ona 1 Wathesalonike 1:7). Ni kwa namna gani kufuata kanuni katika kipengele hiki hutusaidia kuhudumu vizuri zaidi kwa wale tunaowafundisha?

1 Wathesalonike 3:9–13; 4:1–12

Tunapomfuata Yesu Kristo, Yeye anaweza kutufanya kuwa watakatifu.

  • Paulo aliwafundisha watakatifu wa Wathesalonike kwamba “Mungu hakututia uchafu, bali tuwe katika utakaso” (1 Wathesalonike 4:7). Ili kuanza mjadala kuhusu utakatifu, darasa lako au mtu mmoja angeweza kuimba “More Holiness Give Me, (Wimbo wa Kanisa, na.131). Waombe washiriki wa darasa kujadili sifa za utakatifu zilizoorodheshwa katika wimbo ambao umewapendeza. Andika ubaoni Utakatifu zaidi nipeni, zaidi … , na alika washiriki wa darasa kuangalia maneno au virai kutoka 1 Wathesalonike 3:9–13; 4:1–12 ili kumalizia sentensi. Ni kwa namna gani tunaweza kukuza sifa hizi?

  • Mwaliko wa kuwa watakatifu unaweza kuonekana mgumu. Ingeweza kusaidia kama washiriki wa darasa wangeelewa kwamba kukuza utakatifu ni mchakato wa taratibu ambao unatuhitaji sisi “kuongezeka zaidi na zaidi” kadiri ya muda unavyokwenda (1 Wathesalonike 4:10). Ili kuonyesha mchakato huu, ungeweza kumwalika mshiriki wa darasa kuzungumza kuhusu kipaji au mafanikio ambayo yalichukua juhudi endelevu kwa muda, kama vile kutengeneza farishi au kupiga chombo cha muziki. Je, hii ni sawa kiasi gani na mchakato wa kuwa mtakatifu? Alika washiriki wa darasa kurejelea 1 Wathesalonike 3:9–13; 4:1–12 na kushiriki umaizi wao kuhusu juhudi ambazo huhitajika ili kuwa mtakatifu katika njia iliyoelezwa na Paulo. Ni nini kilitusaidia sisi kuendelea kuelekea kwenhe utakatifu?

1 Wathesalonike 4:11–12; 2 Wathesalonike 3:7–13

Tunapaswa kufanya kazi ili tuweze kutimiza mahitaji yetu na ya wale wenye shida.

  • Swali kama lifuatalo lingeweza kuhamasisha mjadala kuhusu ushauri wa Paulo kuhusu kazi: Ni nini madhara ya kutokuwa na shughuli yoyote? Ni zipi baraka za kazi? Unafikiri Paulo alimaanisha nini kwa maneno “kutulia” na “utulivu”? (1 Wathesalonike 4:11; 2 Wathesalonike 3:12). Ungetaka kuandika maswali kama haya kwenye ubao kwa ajili ya washiriki wa darasa kutafakari wakati wakisoma 1 Wathesalonike 4:11–12 na 2 Wathesalonike 3:7–13. Ni maandiko gani mengine ambayo hutusaidia sisi kuelewa umuhimu wa kazi na majanga ya kutokufanya shughuli yoyote? (Ona mapendekezo katika “Nyenzo za Ziada”).

2 Wathesalonike 2

Ukengeufu ulipaswa kutangulia Ujio wa Pili wa Yesu Kristo.

  • Ingeweza kusaidia kujadili baadhi ya mifano manabii waliyoitumia ili kuelezea Ukengeufu, kama vile kuanguka (ona 2 Wathesalonike 2:3), njaa (ona Amosi 8:11–12), mbwa mwitu wakali wakiingia kwenye kundi (ona Matendo ya Mitume 20:28–30), na masikio ya utafiti (ona 2 Timotheo 4:3–4). Fikiria kuligawanya darasa katika jozi na waombe kusoma moja au zaidi ya maandiko ( au mengine ambayo umechagua) na waelezee mistari hiyo inafundisha nini kuhusu Ukengeufu Mkuu. Manabii walifundisha nini kuhusu Ukengeufu na nini yangekuwa matokeo yake?

  • Ingawa Kanisa halitapitia “anguko” jingine (2 Wathesalonike 2:3) kama lilivyofanya hapo zamani, lakini bado tunaweza kuanguka kama mtu binafsi. Je, 2 Wathesalonike 2 inapendekeza nini kuhusu jinsi kuanguka huku kunavyoweza kutokea (ona mistari ya 9–10) na jinsi tunavyoweza kuepuka? (ona mistari ya 15–17).

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Maandiko kuhusu kazi na uzembe.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tumia njia mbalimbali. Inaweza kuwa rahisi kuridhika na aina fulani ya ufundishaji, lakini njia mbalimbali za ufundishaji huwafikia washiriki tofauti wa darasa. Tafuta njia za kubadilisha namna ya ufundishaji wako, kama vile kutumia video, michoro, muziki, au kutoa nafasi za kufundisha kwa washiriki wa darasa (ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi22).

Chapisha