“Julai 11–17. 2 Wafalme 17–25: Alimtumaini Bwana, Mungu wa Israeli” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano la Kale 2022 (2021)
“Julai 11–17 . 2 Wafalme 17–25,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2022
Julai 11–17
2 Wafalme 17–25
“Alimtumaini Bwana Mungu wa Israeli”
Rejelea misukumo uliyoiandika wakati wa kujifunza kwako binafsi 2 Wafalme 17–25 wiki hii. Ni vifungu gani vya maneno kutoka kwenye sura hizi unahisi vitakuwa na maana kwa washiriki wa darasa lako?
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Wakati washiriki wa darasa wanaposhiriki kile wanachojifunza nyumbani katika masomo yao ya maandiko, washiriki wengine wa darasa wanaweza kuhisi msukumo wa kusoma maandiko kwa wiki nzima. Unaweza kuanza darasa kwa kualika washiriki wa darasa kujibu swali kama “Roho Mtakatifu amekufundisha nini wakati uliposoma sura ulizopangiwa kusoma wiki hii?”
Fundisha Mafundisho
2 Wafalme 18:28–36; 19:1–7, 14–19
Tunaweza kubaki wakweli kwa Bwana wakati imani yetu inapingwa.
-
Ukweli katika 2 Wafalme 18–19 unaweza kutusaidia kujua jinsi ya kujibu wakati imani yetu inapopingwa. Ni kwa jinsi gani utaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kugundua ukweli huu? Ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa kushiriki sababu kadhaa kwa nini wanamwamini Mungu na mpango Wake. Kisha wanaweza kupekua 2 Wafalme 18:28–35, wakitafuta sababu ambazo Waashuru waliwapa watu huko Yerusalemu wasimtumaini Bwana. Ni jinsi gani Shetani hujaribu kutushawishi sisi tuwe na shaka na imani yetu leo? Washiriki wa darasa kisha wangeweza kupekua 2 Wafalme 19:1–7, 14–19 kwa ajili ya kile tunachoweza kujifunza kutoka kwa Hezekia juu ya jinsi ya kujibu wakati imani yetu inapopingwa. Ni kwa jinsi gani Bwana anatusaidia kushinda changamoto za imani yetu? Je, ni mapendekezo gani mengine ambayo washiriki wa darasa wanayo ya kufanya upya imani yao na kumwamini Bwana?
-
Unaweza kumwalika mshiriki wa darasa aje darasani akiwa amejiandaa kufupisha mazungumzo ambayo Waashuru walikuwa nayo na maafisa wa Hezekia karibu na kuta za Yerusalemu (ona 2 Wafalme 18:17–36). Kabla hajasimulia hadithi, waalike washiriki wa darasa kufikiria kwamba wao ni wakazi wa Yerusalemu wakisikiliza mazungumzo haya. Wangeweza kuwa na mawazo au hisia gani? Wangeweza kufanya nini? Unaweza kuwapa washiriki wa darasa sehemu za ujumbe wa Mzee David A. Bednar “Kwa hiyo Walinyamazisha Hofu Zao” (Liahona, Mei 2015, 46–49) na waalike kutafuta ushauri ambao ungeweza kuwasaidia wakati wa hofu au shaka. Je, imani yetu kwa Yesu Kristo imetusaidiaje wakati wa changamoto?
Maandiko yanaweza kugeuza mioyo yetu ielekee kwa Bwana.
-
Kujadili juu ya nguvu ambayo neno la Mungu ilivyokuwa katika maisha ya Mfalme Yosia na watu wake inaweza kuwahamasisha washiriki wa darasa kutafuta nguvu hiyo katika maisha yao wenyewe. Unaweza kuanza majadiliano kwa kuwaalika washiriki wa darasa kufikiria jinsi maisha yao yanavyoweza kuwa tofauti kama hawangekuwa na maandiko. Kisha wanaweza kupekua 2 Wafalme 22:8–11; 23:1–6, 24 ili kujua jinsi Yosia na watu wake walivyobadilika waliposikia neno la Mungu kutoka kwenye maandiko ambayo yaligunduliwa tena hivi karibuni katika hekalu. Je, maandiko yametusaidiaje kuja karibu zaidi na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo?
-
Mabadiliko makubwa ambayo neno la Mungu lilikuwa nayo juu ya Yosia na watu wengi katika ufalme wake linaweza kuwahamasisha washiriki wako wa darasa kutafuta mabadiliko kama hayo katika maisha yao. Baada ya kujadili mabadiliko haya (ona 2 Wafalme 23:1–6, 21, 24), washiriki wa darasa wangeweza kushiriki uzoefu ambao kifungu cha maandiko au hadithi hii ilivyoleta mabadiliko katika maisha yao. Labda wangeweza kuzungumza juu ya kwa nini walikuwa wakipokea ujumbe wa andiko hilo wakati huo katika maisha yao. Maelezo katika “Nyenzo za Ziada” yanaweza kuongezea kwenye mjadala wako.
Nyenzo za Ziada
Gundua tena maandiko.
Rais Spencer W. Kimball alisema:
“Nina hakika kwamba kila mmoja wetu, wakati fulani katika maisha yetu, lazima tuyagundue maandiko sisi mwenyewe—na sio kuyagundua mara moja tu, lakini tuyagundue tena na tena. …
Kwa nguvu kabisa napata hisia kwamba ni lazima sisi sote turudi kwenye maandiko kama vile Mfalme Yosia alivyofanya na kuyaacha yafanye kazi kwa nguvu ndani yetu, yakituhamasisha kufanya uamuzi usiotetereka wa kumtumikia Bwana. …
“Mimi ninajikuta hivyo wakati ninapochukulia mahusiano yangu na uungu kuwa kitu cha kawaida na wakati inapoonekana kwamba hakuna sikio la kiungu linasikiliza na hakuna sauti ya kiungu inayozungumza, kwamba niko mbali, mbali sana. Kama nikijizamisha mwenyewe katika maandiko umbali hupungua na hali ya kuwa wa kiroho hurudi. Hujikuta nikiwapenda zaidi wale ambao lazima niwapende kwa moyo wangu wote na akili na nguvu, na nikiwapenda zaidi, Huona kuwa ni rahisi kuishi kulingana na ushauri wao” (Teachings of Presidents of the Church: Spencer W. Kimball [2006], 62–63, 67).