Mlango wa 55
Moroni anakataa kubadilisha wafungwa—Walinzi wa Walamani wanashawishiwa kulewa, na Wanefi wafungwa wanakuwa huru—Mji wa Gidi unakamatwa bila kumwaga damu. Karibia mwaka 63–62 K.K.
1 Sasa ikawa kwamba Moroni alipopokea hii barua alikasirika zaidi, kwa sababu alijua kwamba Amoroni alikuwa na fahamu kamili ya hila yake; ndiyo, alijua kwamba Amoroni alijua kwamba haikuwa sababu ya haki ambayo ilimsababisha kuanzisha vita dhidi ya watu wa Nefi.
2 Na akasema: Tazama, sitabadilisha wafungwa na Amoroni isipokuwa aondoe kusudi lake, vile nimeeleza kwenye barua yangu; kwani sitamkubalia kwamba awe na uwezo kuliko uliyonayo.
3 Tazama, najua mahali ambapo Walamani wanasimamia watu wangu ambao wamewachukua wafungwa; na kwa vile Amoroni hataki kukubaliana na barua yangu, tazama, nitampatia kulingana na maneno yangu; ndiyo, nitatafuta kifo miongoni mwao mpaka watakapoomba amani.
4 Na sasa ikawa kwamba wakati Moroni alikuwa amesema maneno haya, alisababisha kwamba msako ufanywe miongoni mwa watu wake, kwamba labda angepata mtu ambaye alikuwa wa uzao wa Lamani miongoni mwao.
5 Na ikawa kwamba walimpata mmoja, ambaye jina lake lilikuwa Lamani; na alikuwa mmojawapo wa watumishi wa mfalme ambaye aliuawa na Amalikia.
6 Sasa Moroni alisababisha kwamba Lamani na idadi ndogo ya watu wake waende mbele hadi kwenye walinzi ambao walikuwa wanalinda Wanefi.
7 Sasa Wanefi walisimamiwa kwenye mji wa Gidi; kwa hivyo Moroni alimchagua Lamani na kusababisha kwamba idadi ndogo ya watu iende na yeye.
8 Na kulipokuwa usiku Lamani aliwaendea walinzi waliokuwa juu ya Wanefi, na tazama, walimwona akija na wakamuita; lakini aliwaambia: Msiogope; tazama, mimi ni Mlamani. Tazama, tumetoroka kutoka kwa Wanefi, na wanalala; na tazama tumechukua baadhi ya divai yao na kuja nayo.
9 Sasa wakati Walamani waliposikia maneno haya walimpokea kwa shangwe; na wakamwambia: Tupatie divai yako, ili tunywe; tuna furaha kwamba ulichukua divai ukaja nayo kwani sisi tumechoka.
10 Lakini Lamani aliwaambia: Acha sisi tuweke divai yetu mpaka tutakapoenda dhidi ya Wanefi kupigana. Lakini kusema hivi kuliwafanya kuwa na tamaa zaidi ya kutaka kunywa divai;
11 Kwani, walisema: Tumechoka, kwa hivyo acha tunywe divai, na baadaye tutapata divai kwa posha yetu, ambayo itatuimarisha kwenda dhidi ya Wanefi.
12 Na Lamani akawaambia: Mnaweza kufanya kulingana na vile mnavyotaka.
13 Na ikawa kwamba walikunywa divai bila kuzuiliwa; na ilikuwa nzuri walipoionja, kwa hivyo waliinywa kwa wingi; na ilikuwa kali, ikiwa imetayarishwa na nguvu yake.
14 Na ikawa walikunywa na wakafurahi, na baadaye wote walilewa.
15 Na sasa Lamani na watu wake walipoona kwamba wote wamelewa, na wamelala sana, walimrudia Moroni na kumwelezea vitu vyote vilivyotendeka.
16 Na sasa hii ilikuwa kulingana na mpango wa Moroni. Na Moroni alikuwa ametayarisha watu wake na silaha za vita; na akaenda kwenye mji wa Gidi, wakati Walamani walipokuwa katika usingizi mkubwa na wamelewa, na akawatupia wafungwa silaha za vita, mpaka walikuwa wote wamejihami kwa silaha;
17 Ndiyo, hata kwa wanawake wao, na kwa wale watoto wao wote, wote ambao wangeweza kutumia silaha ya vita, wakati Moroni alikuwa amewaami kwa silaha wale wafungwa wote; na hivyo vitu vyote vilifanyika kwa unyamavu mkuu.
18 Lakini kama wangewaamsha Walamani, tazama walikuwa wamelewa na Wanefi wangewachinja.
19 Lakini tazama, hii haikuwa tamaa ya Moroni; hakufurahia mauaji au umwagaji wa damu, lakini alifurahia kuokoa watu wake kutoka maangamizo; na kwa hii sababu hakutaka kujiletea yasiyo ya haki, hakuwashambulia Walamani na kuwaangamiza katika ulevi wao.
20 Lakini alikuwa amepata mahitaji yake; kwani alikuwa amewahami kwa silaha wafungwa wa Wanefi ambao walikuwa ndani ya ukuta wa mji, na alikuwa amewapatia uwezo kupata umiliki wa zile sehemu ambazo zilikuwa ndani ya kuta.
21 Na kisha akasababisha wale watu ambao walikuwa na yeye warudi nyuma kiwango fulani kutoka kwao, na kuzunguka majeshi ya Walamani.
22 Sasa tazama hii ilifanyika wakati wa usiku, ili wakati Walamani walipoamka asubuhi waliona kwamba wamezungukwa na Wanefi nje ya ukuta, na kwamba wafungwa wao walikuwa wamejihami kwa silaha ndani.
23 Na hivyo waliona kwamba Wanefi walikuwa na nguvu juu yao; na kwa hali hii waliona kwamba haikuwa ya manufaa kupigana na Wanefi; kwa hivyo makapteni wao wakuu waliitisha silaha zao za vita, na wakazileta mbele na kuzitupa miguuni mwa Wanefi, wakiomba kuonewa huruma.
24 Sasa tazama, hili lilikuwa pendeleo la Moroni. Aliwachukua kuwa wafungwa wa vita na kuumiliki mji, na kusababisha kwamba wafungwa wote waachiliwe, ambao walikuwa Wanefi; na wakajiunga na jeshi la Moroni, na waliongeza nguvu nyingi katika jeshi lake.
25 Na ikawa kwamba alisababisha Walamani, ambao alikuwa amechukua wafungwa, kwamba waanze kazi ya kuimarisha ulinzi kuzunguka mji wa Gidi.
26 Na ikawa kwamba alipoimarisha mji wa Gidi, kulingana na mahitaji yake, alisababisha kwamba wafungwa wake wapelekwe kwenye mji wa Neema; na pia akalinda huo mji kwa nguvu nyingi.
27 Na ikawa kwamba, licha ya hila za Walamani, waliwaweka na kuwalinda wafungwa wote ambao walikuwa wamewachukua, na pia kudumisha ardhi yote na faida ambayo walikuwa wamechukua tena.
28 Na ikawa kwamba Wanefi walianza tena kuwa washindi, na kudai haki zao na mapendeleo yao.
29 Mara nyingi Walamani walijaribu kuwazunguka usiku, lakini kwa haya majaribio walipoteza wafungwa wengi.
30 Na safari nyingi walijaribu kutoa divai kwa Wanefi, ili wawaangamize na sumu au ulevi.
31 Lakini tazama, Wanefi hawakuwa wapole kumkumbuka Bwana Mungu wao kwa huu wakati wa mateso. Hawakuanguka katika mitego yao; ndiyo, hawakunywa divai yao, isipokuwa wawe wamewapatia kwanza wafungwa wa Walamani.
32 Na wakawa hivyo waangalifu kwamba sumu yoyote isitolewe miongoni mwao; kwani divai ikimuua Mlamani kadhalika itamuua Mnefi; na hivyo ndivyo walijaribu pombe yao yote.
33 Na ikawa kwamba ilikuwa ya maana kuwa Moroni afanye mipango kushambulia mji wa Moriantoni; kwani tazama, Walamani walikuwa, kwa kazi yao, wameimarisha mji wa Moriantoni mpaka ukawa wenye nguvu sana.
34 Na walikuwa kila wakati wakileta askari wapya katika mji, na pia ruzuku mpya za vyakula.
35 Na hivyo ukaisha mwaka wa ishirini na tisa wa utawala wa waamuzi juu ya watu wa Nefi.