Mlango wa 2
Helamani, mwana wa Helamani, anakuwa mwamuzi mkuu—Gadiantoni anaongoza kikundi cha Kishkumeni—Mtumishi wa Helamani anamuua Kishkumeni, na kundi la Gadiantoni linatorokea nyikani. Karibia mwaka 50–49 K.K.
1 Na ikawa katika mwaka wa arubaini na mbili wa utawala wa waamuzi, baada ya Moroniha kuanzisha tena amani miongoni mwa Wanefi na Walamani, tazama hakukuwa na yeyote wa kuchukua kiti cha hukumu; kwa hivyo kulianza kuwa na ubishi tena miongoni mwa watu kuhusu ni nani atakayechukua kiti cha hukumu.
2 Na ikawa kwamba Helamani, ambaye alikuwa mwana wa Helamani, alichaguliwa kuchukua kiti cha hukumu, kwa sauti ya watu.
3 Lakini tazama, Kishkumeni, ambaye alimuua Pahorani, alivizia kumwangamiza Helamani pia; na alisaidiwa na kundi lake, ambao walikuwa wameingia katika agano kwamba uovu wake usijulikane na yeyote.
4 Kwani kulikuwa na mtu mmoja aliyejulikana kama Gadiantoni, ambaye alikuwa stadi sana kwa maneno mengi, na pia kwa hila yake, kutenda kazi yake ya siri ya mauaji na unyangʼanyi; kwa hivyo, alikuwa kiongozi wa kundi la Kishkumeni.
5 Kwa hivyo aliwadanganya, na pia Kishkumeni, kwamba ikiwa watampatia kiti cha hukumu angewakubalia wale ambao walikuwa wa kundi lake kwamba wangewekwa kwenye uwezo na mamlaka miongoni mwa watu; kwa hivyo Kishkumeni alitafuta kumwangamiza Helamani.
6 Na ikawa kwamba aliposonga mbele kuelekea kwenye kiti cha hukumu ili kumwangamiza Helamani, tazama mmoja wa watumishi wa Helamani, ambaye alikuwa nje usiku, na akiwa amepata, taarifa ya mipango hiyo kwa njia ya kujibadilisha ambayo ilikuwa imewekwa na hili kundi kumwangamiza Helamani—
7 Na ikawa kwamba alikutana na Kishkumeni, na kumwonyesha ishara; kwa hivyo Kishkumeni alitambua nia ya mahitaji yake, akitaka kwamba amsaidie kufika kwenye kiti cha hukumu ili amuue Helamani.
8 Na wakati mtumishi wa Helamani alipojua lengo lote la Kishkumeni, na vile kusudi lake lilikuwa kuua, na pia kwamba kusudi la wote ambao walikuwa wa kundi lake lilikuwa ni kuua, na kunyangʼanya, na kupata mamlaka, (na huu ulikuwa mpango wao wa siri, na shirika lao) mtumishi wa Helamani akamwambia Kishkumeni: Acha twende kwenye kiti cha hukumu.
9 Sasa hii ilimpendeza Kishkumeni sana, kwani aliona kwamba atatimiza kusudi lake; lakini tazama, vile walipokuwa wanaenda mbele kwenye kiti cha hukumu, mtumishi wa Helamani alimchoma kisu Kishkumeni, hata mpaka kwenye moyo, kwamba alianguka na kufa bila kugumia. Na alikimbia na kumwambia Helamani vitu vyote ambavyo alikuwa ameviona, na kusikia, na kufanywa.
10 Na ikawa kwamba Helamani alituma walinzi kushika hili kundi la wezi na wauaji wa siri, ili wauawe kulingana na sheria.
11 Lakini tazama, wakati Gadiantoni alipogundua kwamba Kishkumeni hakurudi aliogopa kwamba asije akaangamizwa; kwa hivyo aliamuru kundi lake limfuate. Na walikimbia kutoka nchini, kwa njia ya siri, hadi kwenye nyika; na hivyo wakati Helamani alipotuma wachukuliwe hawakupatikana.
12 Na mengine ya huyu Gadiantoni yatazungumzwa baadaye. Na hivyo ukaisha mwaka wa arubaini na mbili wa utawala wa waamuzi juu ya watu wa Nefi.
13 Na tazama, mwishoni mwa kitabu hiki mtaona kwamba Gadiantoni alithibitisha upinduzi, ndiyo, karibu kuangamizwa kwote wa watu wa Nefi.
14 Tazama simaanishi mwisho wa kitabu hiki cha Helamani, lakini mwisho wa kitabu cha Nefi, ambamo nimepata historia yote ambayo nimeandika.