Kitabu cha Moroni
Mlango wa 1
Moroni anaandika kwa manufaa ya Walamani—Wanefi ambao hawatamkana Kristo wanauawa. Karibia mwaka 401–421 B.K.
1 Sasa mimi, Moroni, baada ya kumaliza kufupisha historia ya watu wa Yaredi, sikudhania kama ningeandika zaidi, lakini bado sijafa; na sitaki kujionyesha kwa Walamani wasije wakaniangamiza.
2 Kwani tazama, vita vyao ni vikali sana miongoni mwao wenyewe; na kwa sababu ya chuki yao wanaua kila Mnefi ambaye hatamkana Kristo.
3 Na mimi, Moroni, sitamkana Kristo; kwa hivyo, ninarandaranda popote niwezapo kwa usalama wa maisha yangu.
4 Kwa hivyo, ninaandika vitu vingine vichache, kinyume cha kile nilichotarajia; kwani nilidhani kuwa sitaandika zaidi ya hayo; lakini ninaandika vitu vichache zaidi, kwamba vingekuwa vya manufaa kwa ndugu zangu, Walamani, katika siku zijazo, kulingana na mapenzi ya Bwana.