Rafiki
Matone ya Imani
Machi 2024


“Matone ya Imani,” Rafiki, Machi 2024, kurasa za 30–31.

Matone ya Imani

Jacob alikuwa na shida—yeye daima alikuwa na usingizi sana!

Hadithi hii ilitokea huko Brazil.

alt text

“Jacob, je, unajua jibu?” Bi. Lelis aliuliza.

Jacob alifumbua macho yake na kuinua kichwa chake kutoka kwenye dawati. Wanadarasa wenzake wote walikuwa wakimtazama. Mwalimu wake pia alikuwa amemkazia macho. Alihisi mashavu yake yakipata joto. Alikuwa amelala tena darasani!

“Samahani, Bi. “Lelis,” alisema. “Unaweza kuuliza swali hilo tena?”

“Hakika. Lakini tafadhali acha kusinzia darasani.”

Alikaa tena kwenye kiti chake. “Ndiyo, mwalimu,”

Jacob alijiunga na shule yake mpya wiki chache tu zilizopita. Alipenda kujifunza, na wanadarasa wenzake walikuwa wakarimu. Lakini kulikuwa na shida moja—alikuwa na uzingizi sana!. Shule yake mpya ilikuwa mbali sana, kwa hiyo ilimbidi aamke mapema sana ili kuwahi.

Mwanzoni, ilikuwa rahisi kufokasi darasani. Lakini ikawa vigumu na vigumu sana baadaye. Wakati mwingine Jacob alichoka sana mpaka akawa analala.

Siku iliyofuata, mkuu wa shule aliomba kukutana na Jacob na wazazi wake. Mkuu alitabasamu na kuwakaribisha katika ofisi yake.

“Ninashuruku mmefika hapa,” mkuu alisema. “Jacob ni mwanafunzi mzuri. Lakini mwalimu wake anasema hajishugulishi katika madarasa yake. Wakati mwingine yeye hafokasi na huonekana kuchoka sana. “Je, yuko SAWA?”

Mama yake aliitikia kwa kichwa. “Jacob amefanya bidii sana kuweza kufika shuleni hapa, lakini ni mbali na tunapokaa. Anahitaji kuamuka mapema sana kila siku. Kwa hiyo anasinzia katika madarasa yake ya asubuhi.”

“Aha, kumbe ni hivyo?” mkuu wa shule aliuliza. “Jaribu matone ya kahawa! Weka matone machache ya kahawa chungu katika kinywaji cha Jacob kila asubuhi. Hii itamfanya awe macho.”

Jacob alikunja uso. “Lakini mwalimu, familia yetu hainywi kahawa.”

Mwalimu mkuu alionekana kukanganyikiwa. “Itakuwa vigumu kwako kujifunza kama utaendela kulala. Unapaswa angalau kulifikiria suala hili.”

Walipotoka kwenye ofisi ya mwalimu mkuu, mawazo ya Jacob yalikuwa yamechanganyikana. Alitaka kufanya vyema shuleni, lakini alitaka pia kufuata amri.

Usiku huo, familia yake ilisoma kuhusu Neno la Hekima katika maandiko.

Ilipofika zamu ya Jacob, yeye alisoma, “Na watakatifu wote ambao wanakumbuka kushika na kutenda maneno haya . . . watapata hekima na hazina kubwa ya maarifa. Na watakimbia na wasichoke, na watatembea wala hawatazimia.”*

Kisha alipata wazo!

Akasimama kutoka kwenye kiti chake. “Badala ya matone ya kahawa, nitatumia matone ya imani!

“Unamaanisha nini?” baba yake aliuliza.

Jacob alitabasamu. “Kila asubuhi kabla ya mlo wa asubuhi, tunaweza kusali na kumuomba Baba wa Mbinguni anibariki ili nisihisi kulala sana. Sala zetu zitakuwa kama matone ya imani!”

Mama na Baba walitabasamu pia. “Hilo linaonekana kama wazo bora!” Baba alisema.

Asubuhi iliyofuata, familia yake ilipiga magoti na kusali kwamba Jacob angetiwa nguvu za kutosinzia. Walifanya vivyo hivyo siku iliyofuatia. Na hata siku baada ya hiyo. Kila usiku, Jacob alijaribu pia kwenda kulala mapema. Na kila asubuhi familia ya Jacob ilikuwa na imani ya kwamba Baba wa Mbinguni angemsaidia.

Baada ya muda, matone yao ya imani yalifanya kazi. Jacob angeweza kufokasi siku nzima! Mungu alikuwa amejibu sala zao. Na Jacob alijua kwamba Mungu alikuwa anapendezwa naye kwa kufuata Neno la Hekima.

alt text

“Je, upo tayari kwa ajili ya darasa, Jacob?” Bi. Lelis aliuliza asubuhi moja alipokuwa akiingia darasani.

Jacob aliitikia kwa kichwa kwa tabasamu pana usoni mwake. Alikunywa matone yake ya imani kabla ya kuja shule. Alikuwa tayari kwa chochote!

PDF ya hadithi

Vielelezo na Raquel Martin