Rafiki
Muda Zaidi pamoja na Max
Machi 2024


“Muda Zaidi pamoja na Max,” Rafiki, Machi 2024, 42.

Imeandikwa na Wewe

Muda Zaidi pamoja na Max

Siku moja nilienda kukita kambi ufukweni pamoja na familia yangu, marafiki wachache na mbwa wangu Max. Tuliogelea na kucheza siku nzima. Kisha tukatazama baruti wakati giza lilipoinga. Sote tulikuwa na wakati mzuri sana.

Baruti zilipoisha, nilimtafuta Max. Lakini alikuwa hayupo! Niliingiwa wasiwasi na kupiga yowe kwamba Max amepotea. Machozi yalipokuwa yakinitiririka usoni , sote tulimtafuta msituni. Nilihisi sauti ndogo ikiniambia nisali, kwa hiyo nilifanya hivyo. Lakini mwili wangu wote ulihisi kunyong’onyea kama tambi na nilimhofia Max.

Hatukumpata, kwa hiyo tulirejea hadi kwenye hema letu. Niliendelea kusali kichwani mwangu, lakini nilianza kupoteza tumaini. Nililia mpaka nikalala.

Masaa machache baadaye, wazazi wangu waliniamsha. Max alikuwa ameketi kando yangu! Wazazi walisikia sauti ya mlio wa njuga wa mkanda wa Max nje ya hema letu. Nilimkumbatia sana na kimya kimya nikamshukuru Mungu kwa kujibu sala zangu.

Picha
alt text

Miaka mitatu baadaye, Max aliumiza mgongo wake na alikuwa na maumivu makali sana. Hakuweza kupona, kwa hiyo ilibidi tuachane naye. Baba wa Mbinguni alinifariji na kunipa amani. Roho Mtakatifu alinikumbusha kwamba tungempoteza Max miaka mitatu iliyopita, lakini Mungu alitusaidia tumpate. Nina shukrani kwamba Yeye alitupatia muda zaidi wa kumpenda Max.

Ninajua Mungu hujibu sala na kutoa faraja katika majaribu. Upatanisho wa Yesu Kristo ni kwa ajili ya kila mtu. Ninashukuru sana kwa ajili ya kile ambacho Yesu Kristo na Baba wa Mbinguni wamenifanyia mimi na familia yangu.

Picha
PDF ya hadithi

Kielelezo na Camarie Brunson

Chapisha