“Shughuli za Njoo, Unifuate,” Rafiki, Machi 2024, 28–29.
Shughuli za Njoo, Unifuate
Kwa ajili ya jioni ya nyumbani au kujifunza maandiko—au kwa ajili ya burudani tu!
Februari 26–Machi 3
Mahekalu ya karatasi
Kwa ajili ya 2 Nefi 11–19
Isaya alifundisha kwamba mahekalu ni sehemu maalumu ambapo tunajifunza kuhusu Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo (ona 2 Nefi 12:3). Tengeneza hekalu lako mwenyewe! Kunja kipande cha karatasi katika theluthi. Kata mwisho mmoja katika pembe tatu. Kunjua karatasi ile na ujichore mwenyewe hapo katikati.
Machi 4–10
Shuhuda za Kuimba
Kwa ajili ya 2 Nefi 20–25
Isaya alishiriki ushuhuda wake juu ya Yesu Kristo. Alisema Yesu alikuwa nguvu yake na wimbo wake (ona 2 Nefi 22:2). Ni nyimbo zipi kuhusu Yesu unazozipenda? Zungumza kuhusu kwa nini unazipenda. Kisha ziimbeni pamoja!
Machi 11–17
Mstari juu ya Mstari
Kwa ajili ya 2 Nefi 26–30
Baba wa Mbinguni hutusaidia sisi tujifunze “mstari juu ya mstari,” au kidogo kidogo kwa wakati (2 Nefi 28:30). Kwa pamoja, simulieni hadithi pendwa ya maandiko mstari mmoja kwa wakati! Kila mtu anachukua zamu kusema sentensi moja ya hadithi mpaka hadithi imalizike.
Machi 18–24
Hatua za Kumfuata Yesu
Kwa ajili ya 2 Nefi 31–33
Nefi alifundisha kwamba tunamfuata Yesu Kristo wakati tunapokuwa na imani katika Yeye, kutubu, kubatizwa, kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu na kuvumilia hadi mwisho (ona 2 Nefi 31). Andika kila hatua kwenye kipande tofauti cha karatasi, kisha vitandaze sakafuni. Mtu mmoja anafumba macho yake na kuhesabu mpaka 10 huko kila mtu mwingine anasimama juu ya karatasi. Mtu aliyehesabu kisha anasema mojawapo ya hatua za kumfuata Yesu. Mtu aliyesimama juu ya karatasi hiyo kisha atahesabu.
Machi 25–31
Yungiyungi za Pasaka
Kwa ajili ya Pasaka
Kwa sababu ya Yesu Kristo, sisi pia tutaishi tena baada ya kufa (ona Alma 40:22–25). Tengeneza kazi ya mikono ya yungiyungi ya Pasaka iliyo kwenye ukurasa wa 17. Weka yungiyungi zako mahali ambapo familia yako inaweza kuziona ili kuwasaidia wamkumbuke Mwokozi wiki hii.