“Kwa Ushirikiano na Bwana——Dondoo,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Nov. 2022.
Kwa Ushirikiano na Bwana
Dondoo
Injili ya urejesho ya Yesu Kristo inatangaza kanuni ya ushirikiano kamili kati ya mwanamke na mwanamume, kote katika maisha ya duniani na ya milele yote. Ingawa kila mmoja ana sifa na majukumu maalumu, mwanamume na mwanamke hujaza nafasi zilizo sawa na muhimu katika mpango wa Mungu wa furaha kwa watoto Wake. …
… Kulingana na mafundisho ya injili, tofauti kati ya mwanamke na mwanamume haibatilishi ahadi za milele ambazo Mungu anazo kwa ajili ya wana na mabinti Zake. Mmoja hana uwezekano mkubwa zaidi wa utukufu wa selestia kuliko mwingine huko mbinguni. Mwokozi Mwenyewe anatualika sisi sote, watoto wa Mungu, “kuja Kwake, ili kupokea wema Wake, na hamkatazi yeyote ajaye Kwake” [2 Nefi 26:33]. Kwa hiyo, katika muktadha huu, sisi sote tunahesabiwa kuwa sawa mbele Zake.
Wanandoa wanapoelewa na kushirikisha kanuni hii, hawajiweki wenyewe kama rais au makamu wa rais katika familia zao. Hakuna mkuu wala mdogo katika uhusiano wao wa ndoa, na wala hakuna kutembea mbele au nyuma ya mwingine. Wanatembea bega kwa bega, kama walio sawa, wazao watakatifu wa Mungu. Wanakuwa wamoja katika wazo, matamanio, na makusudi pamoja na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo, kuiongoza na kulinda mshikamano wa familia kwa pamoja.