“Ufuasi wa Kudumu—Dondoo,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Nov. 2022.
Ufuasi wa Kudumu
Dondoo
Uzoefu kama mikutano ya KNV, kambi, mikutano ya sakramenti na misheni inaweza kusaidia kuwasha shuhuda zetu, ikitupeleka kupitia tao la ukuaji na ugunduzi wa kiroho hadi sehemu za amani. Lakini ni nini lazima tufanye ili tuendelee kubaki hapo na kuendelea “kusonga mbele tukiwa na imani imara katika Kristo” (2 Nefi 31:20), badala ya kuteleza kurudi nyuma? Lazima tuendelee kufanya mambo yale ambayo yalituleta hapo tangu mwanzo, kama vile kuomba kila mara, tukizama katika maandiko na kuhudumu kwa dhati. …
Katika KNV, vijana wetu laki moja na zaidi walikuja kumjua vyema Mwokozi kwa kutumia mbinu rahisi ya kuja pamoja ambapo wawili wao au zaidi walikusanyika katika jina Lake (ona Mathayo 18:20), wakijishughulisha na injili na maandiko, wakiimba pamoja, wakiomba pamoja na kupata amani katika Kristo. Hili ni agizo lenye nguvu kwa ajili ya mwamko wa kiroho. …
Vijana hodari wa Sayuni wanasafiri kupitia nyakati nzuri mno. Kupata furaha katika dunia hii ya vurugu iliyotabiriwa, bila kuwa sehemu ya dunia hiyo, ikiwa na giza kuelekea utukufu, ni agizo lao hasa. …
Ninajua kwamba kupitia kumtumaini Bwana Yesu Kristo na njia Yake ya agano, tunaweza kupata kujiamini na amani ya kiroho tunapokuza tabia za utakatifu na desturi za haki ambazo zinaweza kuendeleza na kuchochoea moto wa imani yetu. Na kila mmoja wetu asogee karibu na ule moto wenye kuleta joto na, lolote liwalo, tubakie.