2022
Kulisha na Kutoa Ushuhuda Wako—Dondoo
Novemba 2022


“Kulisha na Kutoa ushuhuda Wako—Dondoo,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Nov. 2022.

Kulisha na Kutoa Ushuhuda Wako

Dondoo

Nukuu ya Stevenson kwenye bango

Pakua PDF

Je, Ninajua na Kuelewa Ushuhuda ni Nini?

Ushuhuda wako ni jambo la thamani zaidi, mara nyingi ukihusiana na hisia nzuri za kiroho. Hisia hizi kwa kawaida huwasilishwa kwa utulivu na kuelezewa kama “sauti ndogo ya utulivu” [1 Wafalme 19:12]. Ni imani yako au ufahamu wako wa ukweli, unaotolewa kama ushahidi wa kiroho kupitia ushawishi wa Roho Mtakatifu. …

Je, Ninajua Jinsi ya Kutoa Ushuhuda Wangu?

Unatoa ushuhda wako pale unaposhiriki hisia zako za kiroho pamoja na wengine. Kama muumini wa Kanisa, unazo fursa za kutoa ushuhuda wako wa maneno katika mikutano rasmi ya Kanisa au isiyo rasmi, maongezi ya mmoja kwa mwingine pamoja na familia na watu wengine.

Njia nyingine unayoshiriki ushuhuda wako ni kupitia tabia njema. …

Waumini wa Kanisa wanasimama kama mashahidi wa Mungu nyakati zote, katika vitu vyote, na mahali popote. Fursa za kufanya hivi katika ulimwengu wa kidijitali kwa kutumia maudhui yetu wenyewe ya kuinua au kushiriki maudhui yenye kuinua yaliyoandaliwa na wengine hazina mwisho. …

Je, Vikwazo vya Kushiriki Ushuhuda Wangu ni Vipi?

Vikwazo vya kushiriki ushuhuda wako vyaweza kujumuisha kutokuwa na uhakika kuhusu kitu cha kusema. …

Kikwazo kingine … ni woga. …

… Kuwa na imani … kutakusaidia kuzishinda hisia hizi. …

Je, Ninawezaje Kuutunza Ushuhuda Wangu?

Ninaamini ushuhuda ni wa asili ndani yetu, lakini, ili kuutunza na kuukuza kikamilifu, Alma alifundisha kwamba ni lazima tuulishe ushuhuda wetu kwa uangalifu mwingi [ona Alma 32:37]. …

Wapendwa akina kaka na dada zangu, ninawaahidi kwamba kadiri unavyoelewa kikamilifu ushuhuda ni kitu gani, na unapoushiriki, utashinda vizuizi vya mashaka na woga, kukupelekea wewe kuilea na kuitunza hazina hii ya thamani zaidi, ushuhuda wako.