2022
Kusogea Karibu Zaidi na Mwokozi—Dondoo
Novemba 2022


“Kusogea Karibu na Mwokozi—Dondoo,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Nov. 2022.

Kusogea Karibu Zaidi na Mwokozi

Dondoo

Nukuu ya Andersen kwenye bango

Pakua PDF

Tunatambua kwamba kadiri uovu unavyoongezeka katika ulimwengu, kunusurika kwetu kiroho na kunusurika kiroho kwa wale tunaowapenda, kutahitaji kwamba tulee, tuwekee ulinzi na tuimarishe mizizi ya imani yetu katika Yesu Kristo. …

Kama tunavyojua vyema, kuwa na imani katika Yesu Kristo na kuwa mfuasi wa kweli ni uamuzi wa zaidi ya mara moja—zaidi ya tukio la mara moja. Ni mchakato mtakatifu, endelevu ambao unakua na kutanuka kupitia majira ya maisha yetu, ukiendelea hadi tutakapopiga magoti miguuni Pake.

Kukiwa na ngano ikikua miongoni mwa magugu duniani, ni kwa jinsi gani tunaweza kuongeza na kuimarisha msimamo wetu kwa Mwokozi katika siku zilizo mbele?

Hapa kuna mawazo matatu:

Kwanza, tunaweza kujikita kikamilifu kwenye maisha ya Yesu, mafundisho Yake, ukuu Wake, nguvu Zake na dhabihu Yake ya kulipia dhambi. …

Pili, tunapomjua na kumpenda vyema zaidi Mwokozi, tutatamani hata zaidi kumwahidi Yeye utii na uaminifu wetu. Tunafanya maagano na Yeye. …

Kufanya na kushika maagano kunaruhusu upendo wa Mwokozi kuzama ndani kwa kina katika mioyo yetu. …

Mwisho, wazo langu la tatu: katika jtihada hii takatifu, tunathamini, kulinda na kutetea kipawa cha Roho Mtakatifu. …

…Unaporuhusu upendo wako kwa Mwokozi na upendo Wake kwako uzame kwa kina ndani ya moyo wako, ninakuahidi ongezeko la kujiamini, amani na shangwe katika kukabiliana na changamoto za maisha yako.