2022
Nira Yake ni Laini na Mzigo Wake ni Mwepesi—Dondoo
Novemba 2022


“Nira Yake ni Laini na Mzigo Wake ni Mwepesi—Dondoo,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Nov. 2022.

Nira Yake ni Laini na Mzigo Wake ni Mwepesi

Dondoo

Picha
J. Anette Dennis
Picha
Nukuu ya Dennis kwenye bango

Pakua PDF

Mahubiri mengi yametolewa na viongozi wetu wa Kanisa kuhusu hisani, umoja, upendo, wema, huruma, msamaha na rehema. Ninaamini Mwokozi anatualika tuishi kwa njia ya juu zaidi, takatifu zaidi—njia Yake ya upendo ambapo wote wanaweza kuhisi kweli ni wa thamani na wanahitajika.

Tumeamriwa kuwapenda wengine, si kuwahukumu. Hebu tuutue mzigo huo mzito; hatupaswi kuubeba. Badala yake, tunaweza kuichukua nira ya Mwokozi ya upendo na huruma. …

…Wale Aliowagusa walihisi upendo,Wake na upendo huo uliwaponya na kuwabadili. Upendo Wake uliwatia msukumo kutaka kubadili maisha yao. Kuishi njia Yake huleta shangwe na amani, na Aliwaalika wengine kwenye njia ya kuishi kwa ustarabu, uungwana, na upendo. …

…Tunapozidi kujifunza kufanya kile Anachotuamuru—si kwa ajili ya wajibu au hata kwa ajili ya baraka ambazo tunaweza kupokea bali kwa upendo halisi Kwake na kwa Baba yetu wa Mbinguni—upendo Wake utatiririka kupitia kwetu na kufanya yote anayotutaka tufanye si tu yawezekane bali hatimaye yawe rahisi na mepesi zaidi na ya shangwe zaidi kuliko tunavyoweza kufikiri. …

Kila mmoja anahitaji kuhisi kwa dhati kuwa wao wamejumuishwa na wanahitajika kwenye mwili wa Kristo. Shauku kuu ya Shetani ni kuwagawa watoto wa Mungu, na amefanikiwa sana, lakini kuna nguvu kubwa katika umoja. Yahitajika kiasi gani kutembea tukiwa tumeshikana mikono katika safari hii ya maisha yenye changamoto nyingi!

Chapisha