2021
Kanuni Takatifu: “Mapenzi yako yatimizwe”
Aprili 2021


UJUMBE WA KIONGOZI WA ENEO

Kanuni Takatifu: “Mapenzi yako yatimizwe”

“Nimejifunza kwamba, pamoja na upendo usiojali hali kutoka kwa Baba wa Mbinguni aliye mwema na mwenye upendo na Mwanawe Yesu Kristo, hakuna hata mmoja wetu, atakayevuka maisha haya bila taabu.”

Ni msimu wa Pasaka, tunaposherehekea pamoja na wengine wa ulimwengu wa Kikristo na kwa shukrani tunasherehekea tukio hilo la kiutukufu sana katika historia ya mwanadamu, Ufufuko wa Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo. Ni muda wa kushangilia ushindi mkuu, ushindi juu ya kifo. Kuhusu Yeye, Mtume Paulo alitangaza, “Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo” (1 Wakorintho 15:57).

Daima nitakuwa mwenye shukrani kwa tangazo la ushuhuda la Mtume Paulo “Lakini sasa Kristo amefufuka katika wafu, limbuko lao waliolala.

“Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa” (1 Wakorintho 15:20, 22).

Ni ya kunyenyekeza tunapojua kwamba upendo wa Baba yetu wa Mbinguni kwetu ni zaidi ya kipimo chochote. “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

“Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye” (Yohana 3:16–17).

Katika maisha yetu ya kabla ya kuja hapa duniani, Kristo wa wakati huo alionyesha mfano wa kanuni hii ya kiungu, “Mapenzi yako yatimizwe.” Alichagua kuweka mapenzi ya Baba yake mbele ya mapenzi Yake mwenyewe. “Baba, mapenzi yako na yatimizwe, na utukufu uwe wako milele na milele (Musa 4:2).

Pia, katika huduma Yake hapa duniani, kamwe hakutafuta kujiinua Mwenyewe mbele ya Baba, mara kwa mara Alionyesha mfano wa kanuni hii ya kiungu ya kujiweka chini ya mapenzi ya Baba. “Kwa kuwa mimi sikushuka kutoka mbinguni ili niyafanye mapenzi yangu, bali mapenzi yake aliyenipeleka” (Yohana 6:38).

Nimejifunza kwamba, pamoja na upendo usiojali hali kutoka kwa Baba wa Mbinguni aliye mwema na mwenye upendo na Mwanawe Yesu Kristo, hakuna hata mmoja wetu, atakayevuka maisha haya bila taabu. Wakati taabu hizo si matokeo ya matendo yetu ya kiburi au machaguzi yasiyo ya utiifu. Ni dhahiri, Bwana anahisi kwamba tuko tayari sana kukua, kisha baraka nyingi zinatusubiria. “Kwani baada ya taabu kubwa huja baraka. Kwa hiyo siku yaja ambayo ninyi mtavikwa utukufu mkubwa; saa ingali, lakini i karibu” (Mafundisho na Maagano 58:4).

Wakati taabu za duniani zikijaa kwenye njia yetu ya agano, ni juu yetu kuamua mwelekeo wetu. Tutapita kwenye njia hiyo hiyo—njia ambayo watoto waaminifu wa Mungu waliifuata kwa kutafuta kujiweka chini ya mapenzi ya Mungu—au je tutamkufuru Mungu kama Mke wa Ayubu alivyofanya? “Ndipo mkewe [mke wa Ayubu] akamwambia, Je! Wewe hata sasa washikamana na utimilifu wako? Umkufuru Mungu, ukafe” (Ayubu 2:9).

Tunapokumbana na nyakati hizi zisizo za kawaida, basi na tusidanganywe na adui. Siku zote tukumbuke upendo wa kiungu wa Baba yetu wa Mbinguni kwetu, kwa uthabiti usiotikisika kwamba hatuko peke yetu. “Usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; Nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu” (Isaya 41:10).

Tunapotafuta kujiweka chini ya mapenzi ya Baba yetu wa Mbinguni katika mapambano na majaribu yetu, hakika, tutasikia sauti hiyo ya kutuhakikishia “Iweni hodari na moyo wa ushujaa, msiogope wala msiwahofu; kwa maana Bwana, Mungu wako, yeye ndiye anayekwenda pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha” (Kumbukumbu la Torati 31:6).

Ili kutoka mahali tulipo mpaka mahali ambapo Bwana anataka tuwe kunahitaji utakaso mkubwa wa kiroho ambao kiujumla hujumuisha usumbufu na mateso—hata hivyo wenye mwisho wa furaha. “Wapenzi, msione kuwa ni ajabu ule msiba ulio kati yenu, unaowapata kama moto ili kuwajaribu, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho.

“Lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini; ili na katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe” (1 Petro 4:12–13).

Acha kwa bidii tumwamini Yeye kwa moyo wote, tukiutambua mkono Wake wa uweza wote katika maisha yetu binafsi, huku tukitambua mipaka ya hukumu zetu za kibinadamu. “Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe.

“Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako” (Mithali 3:5–6).

Laurian P. Balilemwa aliitwa kama Sabini wa Eneo mnamo Oktoba 2020 Amemuoa Happiness Kagemulo; wao ni wazazi wa watoto wawili. Anakaa Dar es Salaam, Tanzania.

Chapisha