“Kristo Amefufuka; Imani Kwake Itahamisha Milima,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Mei 2021.
Kikao cha Jumapili Asubuhi
Kristo Amefufuka; Imani Kwake Itahamisha Milima
Dondoo
Imani katika Yesu Kristo ni msingi wa kusadiki na ni bomba lipitishalo nguvu za kimungu.
Kila kitu chema maishani—kila baraka inayowezekana ya umuhimu wa milele—huanza na imani. Kumruhusu Mungu ashinde katika maisha yetu huanza na imani kwamba Yeye yuko tayari kutuongoza.
Wapendwa kaka zangu na dada zangu, wito wangu kwenu asubuhi hii ya Pasaka ni anzeni leo kuongeza imani yenu. Kupitia imani yako, Yesu Kristo ataongeza uwezo wako wa kuihamisha milima katika maisha yako. …
Milima yako inaweza kuwa upweke, shaka, magonjwa, au shida zingine za kibinafsi. Milima yenu itatofautiana, na bado jibu kwa kila changamoto yenu ni kuongeza imani yenu. …
… Naomba nitoe mapendekezo matano ili kukusaidia wewe kukuza imani na matumaini hayo.
Kwanza, soma. …
Pili, chagua kuamini katika Yesu Kristo. …
Tatu, tenda kwa imani. …
Nne, shiriki ibada takatifu kwa ustahiki. ….
Na tano, muombeni Baba yenu wa Mbinguni, katika jina la Yesu Kristo kwa ajili ya msaada. …
Imani katika Yesu Kristo ndiyo nguvu kubwa zaidi inayopatikana kwa ajili yetu sisi katika maisha haya. Yote yawezekana kwao waaminio [ona Marko 9:23].
Imani yako inayoongezeka Kwake itahamisha milima—sio milima ya mwamba ambayo huipamba dunia bali milima ya taabu katika maisha yako. Imani yako inayostawi itakusaidia kuzigeuza changamoto kuwa ukuaji unaoendana na fursa.
Katika Jumapili hii ya Pasaka, pamoja na hisia zangu za kina za upendo na shukrani, ninatoa ushuhuda wangu kwamba Yesu Kristo hakika amefufuka. Amefufuka ili aliongoze Kanisa Lake. Amefufuka ili kubariki maisha ya watoto wote wa Mungu, popote wanapoishi. Kwa imani Kwake, tunaweza kusogeza milima katika maisha yetu.