“Maongezi Muhimu,” Kwa ajili ya Nguvu Kwa Vijana, Mei 2021.
Kikao cha Jumapili Asubuhi
Mazungumzo Muhimu
Dondoo
Hatuwezi kusubiri kuongoka kutokea tu kwa watoto wetu. Kuongoka kama kwa ajali sio kanuni ya injili ya Yesu Kristo. Kuja kuwa kama Mwokozi wetu hakutatokea tu bila mpangilio. Kuwa mwenye kusudi katika kupenda, kufundisha, na kushuhudia kunaweza kuwasaidia watoto kuanza katika umri mdogo kuhisi ushawishi wa Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu ni muhimu kwa ushuhuda na uongofu wa watoto wetu kwa Yesu Kristo. …
Fikiria thamani ya mazungumzo ya familia juu ya injili ya Yesu Kristo, mazungumzo muhimu ambayo yanaweza kumwalika Roho. Tunapokuwa na mazungumzo kama hayo pamoja na watoto wetu, tunawasaidia wao kujenga msingi, “ambao ni msingi imara, msingi ambako kama [wao] wakijenga hawataanguka.”Helamani 5:12
Majadiliano haya muhimu yanaweza kuwaongoza watoto kwenye:
-
Kuelewa mafundisho ya toba.
-
Kuwa na imani katika Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.
-
Kuchagua ubatizo na kipawa cha Roho Mtakatifu wafikapo umri wa miaka minane.
-
Na kusali na “kutembea wima mbele za Bwana”[Mafundisho na Maagano 68:28]. …
Kadiri watoto wanavyojifunza na kuendelea, imani yao itajaribiwa. Lakini kama watalindwa vizuri, wanaweza kukua kiimani, kiujasiri, na kujiamini, hata katikati ya upinzani mkubwa.
Alma alitufundisha sisi “kutayarisha akili [za] watoto.”Alma 39:16 Tunakiandaa kizazi kinachoinukia kuwa walinzi wa baadaye wa imani, kuelewa “kwamba [wao] wako huru kujitendea [wao wenyewe]—kuchagua njia ya kifo kisicho na mwisho au njia ya uzima wa milele.” [2 Nefi 10:23 Watoto wanastahili kuelewa ukweli huu mkuu: ni jambo baya kutojua kuhusu umilele.
Basi mazungumzo yetu ya kawaida lakini ya muhimu na watoto wetu yawasaidie “kufurahia maneno ya uzima wa milele” sasa, ili waweze kufurahia “uzima wa milele katika ulimwengu ujao, hata utukufu katika mwili usiokufa.” [Musa 6:5919; mkazo umeongezwa].