“Kuilinda Katiba Yetu Yenye Mwongozo wa Kiungu,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Mei 2021.
Kikao cha Jumapili Alasiri
Kuilinda Katiba Yetu Yenye Mwongozo wa Kiungu
Dondoo
Katika wakati huu wa msukosuko, nimejisikia kuzungumza kuhusu Katiba hii yenye mwongozo wa kiungu ya Marekani. Katiba hii ni yenye umuhimu maalum kwa waumini wetu katika Marekani, lakini pia ni urithi wa kawaida wa katiba ulimwenguni kote. …
Imani yetu katika mwongozo mtakatifu wa kiungu inawapa Watakatifu wa Siku za Mwisho jukumu la kipekee kutetea na kuilinda Katiba ya Marekani na kanuni za masharti ya katiba popote tunapoishi. Tunapaswa kutumaini katika Bwana na kuwa na hakika kuhusu siku za baadaye za taifa hili.
Ni nini kingine Watakatifu wa Siku za Mwisho wanaweza kufanya? Lazima tuombe kwa ajili ya Bwana kuongoza na kubariki mataifa yote na viongozi wake. Hii ni sehemu ya makala yetu ya imani. Kuwa chini ya marais au watawala kwa vyovyote hakuweki kizuizi kwa sisi kupinga sheria au sera moja moja. Inahitajika kwamba tutumie ushawishi wetu kiraia na kwa amani, ndani ya mfumo wa katiba zetu na sheria zinazotumika. Kwenye masuala ya migogoro, tunapaswa kutafuta kurekebisha na kuunganisha.
Kuna kazi zingine ambazo ni sehemu ya kulinda Katiba yenye mwongozo wa kiungu. Tunapaswa kujifunza na kutetea kanuni za Katiba zenye mwongozo wa kiungu. Tunapaswa kuwatafuta na kuwasaidia watu wenye hekima na wema ambao wataunga mkono kanuni hizo katika matendo yao kwa umma (ona Mafundisho na Maagano 98:10). Tunapaswa tuwe raia wenye uelewa ambao ni watendaji katika kufanya ushawishi wetu uonekane katika masuala ya umma.