“Ujumbe wa Makaribisho,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Mei 2021.
Kikao cha Jumamosi Asubuhi
Ujumbe wa Makaribisho
Dondoo
Wapendwa kaka na dada zangu na marafiki ulimwenguni kote, ninatoa makaribisho yangu binafsi kwenye mkutano huu mkuu.
Mwaka huu uliopita umekuwa ni moja ya kumbukumbu vitabuni. Bila shaka kila mmoja wetu amejifunza mambo ambayo hatukuyajua hapo awali. Baadhi ya masomo ambayo niliyajua kabla yameandikwa katika moyo wangu katika njia mpya na za kuelekeza.
Kwa mfano, Mimi ninajua kwa hakika kwamba Bwana anaelekeza kazi za Kanisa Lake. …
Vile vile ninaelewa vizuri sasa kile Alichomaanisha wakati Aliposema, “Tazama, Nitaiharakisha kazi yangu katika wakati wake.” [Mafundisho na Maagano 88]. …
… Kipindi cha mwaka huu uliopita, wengi wenu kwa kasi mmeongeza kujifunza injili majumbani mwenu. Nakushukuruni, na watoto wenu watakushukuruni.
Sehemu ya kusanyiko la Israeli, na iliyo sehemu muhimu zaidi, ni hitaji la sisi kama watu kuwa wenye kustahili na tulioradhi kusaidia kutayarisha ulimwengu kwa ajili ya Ujio wa Pili wa Bwana.
Kadiri tunavyosikiliza jumbe ambazo zimetayarishwa kwa umakini na viongozi wetu chini ya mwongozo wa Roho Mtakatifu, ninaawaalika kusali ili kutambua mabaki ya mvunjiko unayopaswa kuondoa katika maisha yako ili uweze kuwa mwenye kustahili zaidi.
Karibuni kwenye mkutano mkuu na kwenye fursa ya kusikia sauti ya Bwana.