Ujumbe wa Makaribisho
Karibuni kwenye mkutano mkuu na kwenye fursa ya kusikia sauti ya Bwana.
Wapendwa akina kaka na dada zangu na marafiki ulimwenguni kote, ninatoa makaribisho yangu binafsi kwenye mkutano huu mkuu. Tunakusanyika kama familia kubwa ya ulimwengu tukitamani kumwabudu Bwana na Mwokozi wetu, Yesu Kristo. Asanteni kwa kujumuika nasi.
Mwaka huu uliopita umekuwa ni moja ya kumbukumbu vitabuni. Bila shaka kila mmoja wetu amejifunza mambo ambayo hatukuyajua hapo awali. Baadhi ya masomo ambayo niliyajua kabla yameandikwa katika moyo wangu katika njia mpya na ya kuelekeza.
Kwa mfano, Mimi ninajua kwa hakika kwamba Bwana anaelekeza kazi za Kanisa Lake. Yeye alisema, “Nitawaonyesha [ninyi] kwamba ninaweza kufanya kazi yangu mwenyewe.”1
Mara nyingi, mimi pamoja na washauri wangu tumetizama kwa macho yaliyojaa machozi pale Yeye alipoingilia kati katika hali zenye changamoto baada ya kuwa tumefanya kadiri ya uwezo wetu na hatuwezi kuendelea zaidi. Hakika tunasimama kwa mshangao.
Vile vile ninaelewa vizuri sasa kile Alichomaanisha wakati Aliposema, “Tazama, Nitaiharakisha kazi yangu katika wakati wake.”2 Tena na tena nimefurahi pale alipoelekeza na kutekeleza kuharakishwa kwa kazi yake—hata wakati wa janga la ulimwengu.
Kaka na dada zangu wapendwa, nguvu ya Kanisa imesimama katika juhudi na shuhuda zinazoongezeka za waumini wake. Shuhuda hujengwa vizuri zaidi nyumbani. Kipindi cha mwaka huu uliopita, wengi wenu kwa kasi mmeongeza kujifunza injili majumbani mwenu. Nawashukuru, na watoto wenu watawashukuru.
Mradi mkubwa wa kukarabati Hekalu la Salt Lake unaendelea. Kutokea ofisini kwangu nina kiti cha mbele kuangalia kazi ikifanyika katika Kituo cha Hekalu.
Kadiri nilivyowaangalia wafanyakazi wakichimbua mizizi ya miti ya zamani, kuweka mabomba, nyaya, na chemchemi inayovuja, nimefikiria juu ya uhitaji wa kila mmoja wetu kuondoa, kwa usaidizi wa Mwokozi, uchafu wa zamani katika maisha yetu.
Injili ya Yesu Kristo ni injili ya toba.3 Kwa sababu ya Upatanisho wa Mwokozi, injili Yake inatoa mwaliko wa kuendelea kubadilika, kukua, na kuwa wasafi zaidi. Ni injili ya matumaini, ya uponyaji, na ya kuleta ukuaji. Kwa hiyo, injili ni ujumbe wa furaha! Roho zetu hufurahi kwa kila hatua ndogo tunayopiga mbele.
Sehemu ya kusanyiko la Israeli, na sehemu muhimu zaidi, ni hitaji la sisi kama watu kuwa wenye kustahili na radhi kusaidia kutayarisha ulimwengu kwa ajili ya Ujio wa Pili wa Mwokozi.
Kadiri tunavyosilikiliza jumbe ambazo zimetayarishwa kwa umakini na viongozi wetu chini ya mwongozo wa Roho Mtakatifu, ninaawaalika kusali ili kutambua uchafu unaopaswa kuuondoa katika maisha yako ili uweze kuwa zaidi mwenye kustahili.
Nianawapenda, kaka na dada zangu wapendwa, na ninashuhudia kwamba Baba yetu wa Mbinguni na Mwanae Mpendwa wanawajua na kuwapenda kila mmoja wenu binafsi. Wanasimama tayari kuwasaidia katika kila hatua mnayopiga mbele. Karibuni kwenye mkutano mkuu na kwenye fursa ya kusikia sauti ya Bwana. Katika Jina la Yesu Kristo, amina.