Mkutano Mkuu
Safari Binafsi ya Mtoto wa Mungu
Mkutano mkuu wa Aprili 2021


Safari Binafsi ya Mtoto wa Mungu

Kama watoto wa agano wa Mungu, tunapenda, kuheshimu, kutunza, kulinda, na kukaribisha roho zile zinazokuja kutoka ulimwengu wa maisha ya kabla ya kuzaliwa hapa duniani.

Kila mmoja wetu ameathiriwa na janga la ulimwengu, kwani familia na marafiki wamefariki bila kutarajia. Acha niwatambue watatu tunaoowapenda sana, wakiwakilisha wale wote tuwapendao sana.

Picha
Kaka na Dada Nsondi

Huyu ni Kaka Philippe na Dada Germaine Nsondi. Kaka Nsondi alikuwa akifanya kazi kama patriaki wa Kigingi cha Brazzaville Jamuhuri ya Kongo mpaka alipofariki. Alikuwa daktari ambaye alishiriki talanta zake kwa ukarimu na wengine.1

Picha
Clara Ruano de Villareal

Huyu ni Dada Clara Elisa Ruano de Villareal kutoka Tulcán, Ecuador. Alikubali injili akiwa na umri wa miaka 34 na alikuwa kiongozi anayependwa. Familia yake ilisema kwaheri ikiimba wimbo alioupenda, “I Know That My Redeemer Lives.”2

Picha
Ray Tuineau na familia yake

Huyu ni Kaka Ray Tuineau kutoka Utah, na familia yake nzuri. Mke wake, Juliet, alisema, “Nataka [wavulana wangu] [kumbuka kwamba baba yao] siku zote alijaribu kumtanguliza Mungu kwanza.”

Bwana amesema, “Nawe utaishi pamoja katika upendo, kwa kiasi kwamba utalia kwa upotevu wa wale wanaokufa.”4

Wakati tunalia, tunashangilia pia katika Ufufuo mtukufu wa Mwokozi wetu. Kwa sababu Yake, wapendwa wetu na marafiki wataendelea na safari yao ya milele. Kama vile Rais Joseph F. Smith alivyoeleza: “Hatuwezi kuwasahau; hatuachi kuwapenda. … Wao wametangulia; nasi tunafuatia; tunakua kama vile walivyokua.”5 Rais Russell M. Nelson alisema, “Machozi yetu ya huzuni … hugeuka kuwa machozi ya matarajio.”6

Tunajua kuhusu Maisha Kabla ya Kuzaliwa

Mtazamo wetu wa milele sio tu unaongeza uelewa wetu wa wale wanaoendelea na safari yao baada ya maisha haya lakini pia hufungua uelewa wetu juu ya wale ambao ndio wameianza safari yao na wale ambao ndio wanaingia katika maisha haya ya duniani.

Kila mtu anayekuja duniani ni mwana au binti wa kipekee wa Mungu.7 Safari yetu ya kibinafsi haikuanzia wakati wa kuzaliwa. Kabla ya kuzaliwa, tulikuwa pamoja katika ulimwengu wa matayarisho ambapo “tulipokea masomo [yetu] ya kwanza katika ulimwengu wa roho.”8 Yehova alimwambia Yeremia, “Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa.”9

Wengine wanaweza kuuliza ikiwa maisha huanza kwa kufanyika kwa kiinitete, au wakati moyo unapoanza kupiga, au wakati mtoto anapozaliwa, lakini kwetu sisi, hakuna ubishi kwamba binti za kiroho na wana wa Mungu wako kwenye safari zao za kibinafsi za kuja ulimwenguni kupokea mwili na kupata uzoefu wa maisha ya duniani.

Kama watoto wa agano wa Mungu, tunapenda, tunaheshimu, tunalisha, tunalinda, na kukaribisha roho zile zinaokuja kutoka ulimwengu wa kabla ya maisha haya.

Mchango wa Kuvutia wa Wanawake

Kwa mwanamke, kupata mtoto inaweza kuwa dhabihu kubwa kimwili, kihisia na kiuchumi. Tunawapenda na kuwaheshimu wanawake wa Kanisa hili. Kwa akili na hekima, mnabeba mizigo ya familia zenu. Mnapenda. Mnahudumu. Mnatoa dhabihu. Mnaimarisha imani, kuhudumia wenye mahitaji na mnachangia sana katika jamii.

Jukumu Tukufu la Kulinda Maisha

Miaka iliyopita, akikwazwa sana juu ya idadi ya utoaji mimba ulimwenguni, Rais Gordon B. Hinckley alihutubia wanawake wa Kanisa kwa maneno ambayo yanatufaa leo. Alisema: “Ninyi ambao ni wake na ni akina mama ninyi ni nanga za familia. Mnazaa watoto. Hilo ni jukumu kubwa na takatifu kiasi gani. … Je, ni nini kinachotokea kwenye kuthamini kwetu utakatifu wa maisha ya mwanadamu? Utoaji mimba ni uovu, mkali na wa kweli na wenye kuchukiza, ambao unaenea juu ya dunia. Ninawasihi wanawake wa Kanisa hili waachane nao, wasimame juu yake, wakae mbali na hali kama hizo ambazo hufanya ionekane kama swala la kutamanika. Kunaweza kuwa na hali chache ambazo zinaweza kupelekea hilo, lakini ni chache sana.”10 … Ninyi ni akina mama wa wana na mabinti wa Mungu, ambao maisha yao ni matakatifu. Kuwalinda ni jukumu la kiungu ambalo haliwezi kupuuzwa hata kidogo.”1112

Mzee Marcus B. Nash alishiriki nami hadithi ya mwanamke mwenye umri wa miaka 84 ambaye, wakati wa mahojiano yake ya ubatizo, “alikiri kutoa mimba [miaka mingi kabla].” Kwa hisia za moyoni, alisema: “Nimebeba mzigo wa kutoa mimba kila siku ya maisha yangu kwa miaka arobaini na sita. … Hakuna kitu nilichofanya ambacho kingeondoa maumivu na hatia. Sikuwa na tumaini mpaka nilipofundishwa injili ya kweli ya Yesu Kristo. Nilijifunza jinsi ya kutubu … na ghafla nilijazwa na tumaini. Hatimaye nilipata kujua kwamba ningeweza kusamehewa ikiwa nitatubu dhambi zangu kwa dhati.”12

Tuna furaha kiasi gani kwa vipawa vitakatifu vya toba na msamaha.

Tunaweza Kufanya Nini?

Je, jukumu letu kama wanafunzi wa amani wa Yesu Kristo ni lipi? Acha tuishi amri za Mungu, tuzifundishe kwa watoto wetu, na tuzishiriki na wengine ambao wako tayari kusikiliza.13 Acha tushiriki hisia zetu za kina juu ya utakatifu wa maisha na wale wanaofanya maamuzi katika jamii. Wanaweza kutothamini kabisa kile tunachoamini, lakini tunaomba kwamba wataelewa zaidi kwa nini, kwa ajili yetu, maamuzi haya huenda zaidi ya kile mtu anachotaka kwa ajli ya maisha yake mwenyewe.

Ikiwa mtoto ambaye hakutarajiwa anatarajiwa, basi tuonyeshe upendo, kutia moyo, na, panapohitajika, msaada wa kifedha, kumuimarisha mama ili kuruhusu mtoto wake azaliwe na kuendelea na safari yake hapa duniani.14

Uzuri wa Kuasili

Katika familia yetu, tumebarikiwa sana kwa miongo miwili iliyopita, kijana wa miaka 16 aligundua kuwa alikuwa anatarajia mtoto. Yeye na baba wa mtoto hawakuoana na hawakuweza kuona njia ya kusonga mbele pamoja. Mwanadada huyo aliamini kwamba maisha ya kichanga alichobeba yalikuwa ya thamani. Alizaa mtoto wa kike na aliruhusu familia ya haki kumuasili kama mtoto wao. Kwa Bryce na Jolinne, kichanga hicho kilikuwa ni jibu la sala zao. Walikiita Emily na kukifundisha kumtegemea Baba yake wa Mbinguni na Mwanawe, Yesu Kristo.

Picha
Emily na Christian

Emily alikua. Ni furaha iliyoje kwetu kwamba Emily na mjukuu wetu, Christian, walipendana na walioana katika nyumba ya Bwana. Emily na Christian sasa wana msichana wao mdogo.

Picha
Emily na binti yake

Emily aliandika hivi karibuni: “Katika miezi hii yote tisa iliyopita ya ujauzito, nilikuwa na wakati wa kutafakari juu ya matukio [ya] kuzaliwa kwangu mwenyewe. Nilimuwaza mama yangu mzazi, ambaye alikuwa na umri wa miaka 16 tu. Nilipokuwa nikipitia maumivu na mabadiliko ambayo mimba huleta, sikuweza kujizuia kufikiria jinsi ingekuwa vigumu kwa umri mdogo wa miaka 16. … Machozi hunitiririka hata sasa ninapomfikiria mama yangu mzazi, ambaye alijua kuwa hangeweza kunipa maisha [aliyotamani kunipa na bila kuwa mbinafsi aliniweka] ili niasiliwe. Siwezi kufahamu kile alichopitia miezi hiyo tisa—akiangaliwa na macho ya kuhukumu wakati mwili wake ukibadilika, uzoefu wa ujana aliukosa, akijua kwamba mwisho wa kazi hii ya upendo wa mama, angemweka mtoto wake mikononi mwa mwingine. Ninashukuru sana kwa uchaguzi wake wa kujitolea, kwamba hakuchagua kutumia uhuru wake katika njia ambayo ingeondoa uhuru wangu mwenyewe.” Emily anamalizia, “Ninashukuru sana kwa mpango wa kimungu wa Baba wa Mbinguni, kwa wazazi wangu wazuri ambao [walinipenda na kunijali] mimi, na kwa mahekalu ambapo tunaweza kuunganishwa na familia zetu milele yote.”15

Picha
Kolagi ya picha

Mwokozi “alitwaa mtoto, akamweka katikati yao; na alipomchukua mikononi mwake, aliwaambia, Yeyote atakayempokea mmoja wa watoto hawa kwa jina langu, ananipokea mimi”16

Wakati Matamanio ya Haki Hayajafikiwa

Ninatoa upendo wangu na huruma kwa wanandoa waadilifu ambao wanaoana na hawawezi kupata watoto ambao wanatarajia kwa hamu kubwa na kwa wale wanawake na wanaume ambao hawajapata nafasi ya kuoa/kuolewa kulingana na sheria ya Mungu. Ndoto ambazo hazijafikiwa za maisha ni ngumu kuzielewa ikiwa zinatazamwa kwa mtazamo wa maisha haya. Kama mtumishi wa Bwana, nakuahidi kwamba kama wewe ni mwaminifu kwa Yesu Kristo na maagano yako, utapokea fidia ya baraka katika maisha haya na matamanio yako ya haki katika majira ya milele ya Bwana.17 Kunaweza kuwa na furaha katika safari katika maisha haya hata wakati matumaini yetu yote ya haki hayatimizwi.18

Baada ya kuzaliwa, watoto wanaendelea kuhitaji msaada wetu. Wengine wanauhitaji sana. Kila mwaka kupitia maaskofu wanaojali na michango yenu ya ukarimu ya matoleo ya mfungo na fedha za misaada ya kibinadamu, maisha ya mamilioni na mamilioni ya watoto yamebarikiwa. Hivi karibuni Urais wa Kwanza ulitangaza nyongeza ya dola milioni 20 kuisaidia UNICEF katika juhudi zao za ulimwengu za kutoa chanjo bilioni mbili.19 Watoto wanapendwa na Mungu.

Uamuzi Mtakatifu wa Kupata Mtoto

Inahuzunisha kwamba hata katika nchi zilizo na mafanikio zaidi ulimwenguni, ni watoto wachache wanazaliwa.20 “Amri ya Mungu kwa watoto Wake ya kuzaana na kujaza dunia imebaki ikizingatiwa.”21 Wakati wa kupata mtoto na ni watoto wangapi ni maamuzi ya kibinafsi yanayofaa kufanywa kati ya mume na mke na Bwana. Kwa imani na sala, maamuzi haya matakatifu yanaweza kuwa uzoefu mzuri, wa ufunuo.22

Ninashiriki hadithi ya familia ya Laing ya Kusini mwa California. Dada Rebecca Laing anaandika:

Picha
Familia ya Laing

“Katika msimu wa joto wa 2011, maisha kwenye familia yetu yalionekana kuwa sawa. Tulikuwa na ndoa yenye furaha pamoja na watoto wanne—umri wa miaka 9, 7, 5, na 3. …

“Mimba zangu na kujifungua [vilikuwa] na hatari kubwa … [na] tulihisi [kubarikiwa] kupata watoto wanne, [tukifikiria] kwamba familia yetu ilikuwa kamili. Mnamo Oktoba wakati nikisikiliza mkutano mkuu, nilihisi hisia isiyo na shaka kwamba tunapaswa kupata mtoto mwingine. Wakati mimi na LeGrand tukitafakari na kuomba, … tulijua kwamba Mungu alikuwa na mpango tofauti kwetu kuliko ule tuliokuwa nao sisi wenyewe.

“Baada ya ujauzito mwingine mgumu na kujifungua, tulibarikiwa kupata mtoto mzuri wa kike. Tulimwita Brielle. Alikuwa ni muujiza. Muda mfupi baada ya kuzaliwa kwake, nikiwa bado katika [chumba cha kujifungulia], nilisikia sauti isiyo na shaka ya Roho: ‘Kuna mmoja zaidi.’

“Miaka mitatu baadaye, muujiza mwingine, Mia. Brielle na Mia ni furaha kubwa kwa familia yetu.” Anahitimisha, “Kuwa muwazi kwa mwongozo wa Bwana na kufuata mpango Wake kwetu daima kutaleta furaha kubwa kuliko … kutegemea uelewa wetu wenyewe.”23

Picha
Brielle na Mia Laing

Mwokozi humpenda kila mtoto

“Na akawachukua watoto wao wadogo, mmoja mmoja, na kuwabariki. …

“Na … walielekeza macho yao mbinguni, … na wakaona malaika wakiteremka kutoka mbinguni … katikati ya moto; na [malaika] … waliwazunguka wale wachanga, … na malaika waliwahudumia.”24

Nashuhudia kwamba safari yako mwenyewe ya kibinafsi kama mtoto wa Mungu haikuanzia kwako kwani mtiririko wa kwanza wa hewa ya dunia ulikuja ukikimbilia kwenye mapafu yako, na hautakoma wakati unashusha pumzi yako ya mwisho ya kifo.

Na tukumbuke kila wakati kwamba kila mtoto wa kiroho wa Mungu anakuja duniani kwa safari yake ya kibinafsi.25 Na tuwakaribishe, tuwalinde, na tuwapende daima. Unapopokea watoto hawa wa thamani katika jina la Mwokozi na kuwasaidia katika safari yao ya milele, nakuahidi kwamba Bwana atakubariki na kukumwagia upendo na idhini Yake juu yako. Katika Jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Personal correspondence.

  2. Personal correspondence. Ona “I Know That My Redeemer Lives,” Nyimbo za Kanisa, na. 136.

  3. Personal correspondence.

  4. Mafundisho na Maagano 42:45.

  5. Joseph F. Smith, katika Ripoti ya Mkutano Mkuu, Apr. 1916, 3.

  6. In Trent Toone, “‘A Fulness of Joy’: President Nelson Shares Message of Eternal Life at His Daughter’s Funeral,” Church News, Jan. 19, 2019, thechurchnews.com.

  7. Ona “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu,” ChurchofJesusChrist.org.

  8. Mafundisho na Maagano 138:56.

  9. Yeremia 1:5 Agano Jipya linasimulia juu ya Yohana Mbatizaji ambaye hajazaliwa akiruka ndani ya tumbo wakati Elisabeti alikutana na Mariamu, ambaye alikuwa akimtarajia mtoto Yesu (ona Luka 1:41).

  10. Azma ya Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.

    Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho huamini katika utakatifu wa maisha ya binadamu. Kwa hivyo, Kanisa linapinga utoaji wa mimba kwa hiari kwa sababu za kibinafsi au kijamii, na inawashauri washiriki wake kutokukubali, kutotekeleza, kutohimiza, kutolipia, au kupanga utoaji wa mimba wa aina hiyo.

    “Kanisa linaruhusu matukio kama haya kwa washiriki wake wakati:

    “Mimba itokanayo na ubakaji au uhusiano wa kiukoo, au

    “Daktari bingwa amegundua kwamba maisha au afya ya mama iko katika hatari kubwa, au

    “Daktari bingwa amegundua kuwa kijusi kina kasoro kubwa ambazo hazitaruhusu mtoto kuishi baada ya kuzaliwa.

    “Kanisa linawafundisha waumini wake kwamba hata kwenye matukio haya ya nadra usihalalishe utoaji mimba moja kwa moja. Utoaji mimba ni jambo zito sana na linapaswa kuzingatiwa tu baada ya watu wanaohusika kushauriana na viongozi wa kanisa lao na kuhisi kupitia maombi ya kibinafsi kwamba uamuzi wao ni sahihi.

    “Kanisa halijakubaliana na au kupinga maandamano ya mapendekezo ya bunge au umma kuhusiana na utoaji mimba” (“Abortion,” Newsroom, newsroom.ChurchofJesusChrist.org; see also General Handbook: Serving in The Church of Jesus Christ of Latter-day Saints, 38.6.1, ChurchofJesusChrist.org).

  11. Gordon B. Hinckley, “Kutembea katika Nuru ya Bwana,” Ensign, Nov. 1998, 99; Liahona, Jan. 1999, 117.

    Rais Gordon B. Hinckley alisema:

    “Utoaji mimba ni jambo baya, jambo linalodhalilisha, jambo ambalo bila shaka linaleta kujilaumu na huzuni na majuto.

    “Wakati tunakemea, tunatoa ruhusa katika hali kama vile wakati ujauzito huhusiana na undugu au ubakaji, wakati mamlaka bingwa ya afya imeonyesha kwamba maisha au afya ya mama iko kwenye hatari kubwa, au wakati mamlaka bingwa ya afya imeamua kwamba kijusi kina kasoro kubwa ambazo hazitaruhusu mtoto kuishi baada ya kuzaliwa.

    “Lakini visa kama hivyo ni nadra, na kuna uwezekano mdogo wa kutokea kwao. Katika hali hizi wale ambao wanakabiliwa na swali hilo wanaombwa kushauriana na viongozi wao wa kanisa na kusali kwa bidii kubwa, wakipata uthibitisho kupitia maombi kabla ya kuendelea” (Gordon B. Hinckley, “What Are People Asking about Us?”, Ensign, Nov. 1998, 71); Liahona, Jan. 1999, 83–84).

  12. Neil L. Andersen, Zawadi Takatifu ya Msamaha (2019), 25.

    Wakati mmoja huko Ufaransa, wakati wa mahojiano ya ubatizo, mwanamke mmoja alizungumza nami juu ya utoaji wake wa mimba miaka mingi kabla. Nilishukuru kwa wema wake. Alikuwa amebatizwa. Karibu mwaka mmoja baadaye, nilipokea simu. Mwanamke huyu mzuri katika mwaka tangu ubatizo wake alikuwa amefundishwa na Roho Mtakatifu. Alilia wakati alipopiga simu: “Unakumbuka nilikuambia juu ya utoaji mimba kwa miaka iliyopita? Nilijisikia vibaya kwa kile nilichokifanya. Lakini mwaka uliopita umenibadilisha. … Moyo wangu umemgeukia Mwokozi. … Nimeumizwa sana na uzito wa dhambi yangu kwamba sina njia ya kutatua.”

    Nilihisi upendo mkubwa wa Bwana kwa mwanamke huyu. Rais Boyd K. Packer alisema, “Kurejesha kile ambacho huwezi kurejesha, uponyaji wa jeraha ambalo huwezi kuponya, kutengeneza kile ambacho ulikivunja na hakiwezi kutengenezeka ndio lengo hasa la upatanisho wa Kristo. Wakati hamu yako i thabiti na uko tayari kulipa ‘senti ya mwisho kabisa,’ [ona Mathayo 5:25-26] sheria ya marekebsho itawekwa. Ombi lako litafikishwa kwa Bwana. Yeye Atalipa madeni yako, (“The Brilliant Morning of Forgiveness,” Ensign, Nov. 1995, 19–20). Nilimhakikishia upendo wa Mwokozi. Bwana alikuwa ameondoa dhambi kutoka kwake; aliimarisha na kuisafisha roho yake. (Ona Neil L. Andersen, Zawadi Takatifu ya Msamaha, 154–156.)

  13. Ona Dallin H. Oaks, “Kuwalinda Watoto,” Liahona,, Nov. 2012, 43–46.

  14. Kulinda maisha ya binti au mwana wa Mungu pia ni jukumu la baba. Kila baba ana jukumu la kihisia, kiroho na kifedha kumkaribisha, kumpenda na kumtunza mtoto anayekuja duniani.

  15. Personal correspondence.

  16. Marko 9:36–37.

  17. Ona Neil L. Andersen, “A Compensatory Spiritual Power for the Righteous” (Brigham Young University devotional, Aug. 18, 2015), speeches.byu.edu.

  18. Ona Dallin H. Oaks, “Mpango Mkubwa wa Furaha,” Ensign, Nov. 1993, 75; ona pia Russell M. Nelson, “Chaguzi,” Ensign, Nov. 1990, 75.

  19. Ona “Bishop Caussé Thanks UNICEF and Church Members for COVID-19 Relief,” Newsroom, Mar. 5, 2021, newsroom.ChurchofJesusChrist.org.

  20. Kwa mfano, ikiwa Marekani ingeweza kudumisha kiwango chake cha kuzaa cha 2008, miaka 13 tu iliyopita, kungekuwa na watoto milioni 5.8 zaidi walio hai leo (ona Lyman Stone, “5.8 Million Fewer Babies: America’s Lost Decade in Fertility,” Institute for Family Studies, Feb. 3, 2021, ifstudies.org/blog).

  21. Familia: Tangazo kwa Ulimwengu,” ChurchofJesusChrist.org. Maandiko yanaandika kwamba “watoto ni urithi wa Bwana” (Zaburi 127:3). Ona Russell M. Nelson, “Msingi Wetu ni Imara Jinsi Gani,” Liahona, July 2002, 83–84; ona pia Dallin H. Oaks, “Ukweli na Mpango,” Liahona, Nov. 2018, 27.

  22. Ona Neil L. Andersen, “Watoto,” Liahona,, Nov. 2011, 28.

  23. Personal correspondence, Mar. 10, 2021.

  24. 3 Nefi 17:21, 24.

  25. “Kwa kweli, sisi sote ni wasafiri—hata wachunguzi katika maisha haya. Hatuna faida ya uzoefu wa kibinafsi uliopita. Lazima tuvuke milima mikali na maji yenye msukosuko katika safari yetu hapa duniani” Thomas S. Monson,Mjenga Daraja,” Liahona, Nov. 2003, 67).

Chapisha