Mkutano Mkuu
Kuilinda Katiba Yetu Takatifu Yenye Uvuvio
Mkutano mkuu wa Aprili 2021


Kuilinda Katiba Yetu Takatifu Yenye Uvuvio

Imani yetu katika uvuvio mtakatifu inawapa Watakatifu wa Siku za Mwisho jukumu la kipekee kutetea na kuilinda Katiba ya Marekani na kanuni za masharti ya katiba.

Katika wakati huu wa msukosuko, nimejisikia kuzungumza kuhusu Katiba yenye uvuvio ya Marekani. Katiba hii ni yenye umuhimu maalumu kwa waumini wetu katika Marekani, lakini pia ni urithi wa kawaida wa katiba ulimwenguni kote.

I.

Katiba ni msingi wa serikali. Inatoa muundo na ukomo kwa ajili ya matumizi ya nguvu za serikali. Katiba ya Marekani ni Katiba iliyoandikwa zamani sana na bado inatumika leo. Ingawa kwa asili ilikubaliwa na idadi ndogo tu ya makoloni, punde ilikuwa mfano wa kuigwa ulimwenguni. Leo, kila taifa isipokuwa matatu yamechukuwa mfumo wa katiba zilizoandikwa.1

Katika maoni haya sizungumzi kwa ajili ya chama chochote cha siasa au kundi lolote. Ninazungumza kwa ajili ya katiba ya Marekani, ambayo nimeisoma kwa zaidi ya miaka 60. Ninazungumza kutokana na uzoefu wangu mwenyewe kama karani wa sheria wa jaji mkuu wa Mahakama Kuu ya Marekani. Ninazungumza kutoka miaka yangu 15 kama profesa wa sheria, miaka yangu 3½ kama jaji kwenye Mahakama Kuu ya Utah. Muhimu zaidi, Ninazungumza kutoka miaka 37 kama Mtume wa Yesu Kristo, mwenye wajibu wa kujifunza maana ya Katiba takatifu ya yenye uvuvio ya Marekani kama kwenye kazi ya Kanisa Lake lililorejeshwa.

Katiba ya Marekani ni ya kipekee kwa sababu Mungu alifunua kwamba Yeye “aliiweka” “kwa ajili ya haki na ulinzi wa wote wenye mwili” (Mafundisho na Maagano 101:77; ona pia mstari wa 80). Hiyo ndiyo sababu katiba hii ni ya umuhimu maalum kwa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho ulimwenguni kote. Kama au jinsi gani kanuni zake zinapaswa kutumika katika mataifa mengine ya ulimwengu ni juu yao kuamua.

Nini lilikuwa lengo la Mungu katika kuianzisha Katiba ya Marekani? Tunaona katika mafundisho ya haki ya kujiamulia ya maadili. Katika muongo wa kwanza wa kanisa lililorejeshwa, waumini kwenye mpaka wa magharibi walikuwa wakiteseka mateso binafsi na ya umma. Kwa sehemu, hii ilikuwa kwa sababu ya upinzani wao juu utumwa ambao ulikuwepo Marekani wakati ule. Katika hali hizi mbaya, Mungu alifunua kupitia Nabii Joseph Smith kweli za milele kuhusu mafundisho Yake.

Mungu amewapa watoto Wake haki ya kujiamulia ya maadili—uwezo wa kuamua na kutenda. Hali ya kufaa sana kwa ajili ya matumizi ya haki hiyo ni upeo wa juu wa uhuru kwa ajili ya wanaume na wanawake kuamua na kutenda kulingana na uchaguzi wao binafsi. Kisha, ufunuo unaeleza, ili kwamba “kila mtu aweze kuwa mwenye kuwajibika kutokana na dhambi zake mwenyewe katika siku ya hukumu” (Mafundisho na Maagano 101:78). “Kwa hiyo,” Bwana alifunua, “siyo sahihi kwamba mtu yoyote awe mtumwa kwa mtu wingine” (Mafundisho na Maagano 101:79). Hii kwa uwazi humaanisha kwamba utumwa wa binadamu ni kosa. Na kulingana na kanuni hiyo hiyo, si sahihi kwa wananchi kutokuwa na sauti katika uchaguzi wa viongozi wao au utungaji wa sheria zao.

II.

Imani yetu kwamba katiba ya Marekani ilikuwa na uvuvio mtakatifu haimaanishi kwamba ufunuo mtakatifu ulitoa imla ya kila neno na kirai, kama vile utoaji na ugawaji wa idadi ya wawakilishi kutoka kila jimbo au umri wa chini wa kila mmoja wao.2 Katiba haikuwa “hati iliyotimia,” alisema Rais J. Reuben Clark. “Kinyume chake,” alielezea, “Tunaamini lazima inahitaji kukua na kukomaa ili kukidhi mahitaji yanayobadilika ya ulimwengu unaoendelea.”3 Kwa mfano, marekebisho yenye uvuvio yalipiga marufuku utumwa na kuwapa wanawake haki ya kupiga kura. Hata hivyo hatuoni uvuvio katika kila uamuzi wa Mahakama Kuu unaoifafanua Katiba.

Ninaamini Katiba ya Marekani ina angalao kanuni tano zenye uvuvio.4

Kwanza ni kanuni ambayo chanzo cha nguvu ya serikali ni watu. Katika wakati ambapo mamlaka ya kuongoza kwa ujumla yalidhaniwa kutoka kwenye haki takatifu ya wafalme au kutoka nguvu ya kijeshi, wakipata mamlaka ya kuongoza kutoka kwa watu ilikuwa mageuzi makubwa sana. Wanafilosofia walipigania hili, lakini Katiba ya Marekani ilikuwa ya kwanza kuitumia. Mamlaka ya kuongoza kwa watu haimaanishi kwamba magenge au makundi mengine ya watu yanaweza kuingilia kutishia au kulazimisha serikali kuchukua hatua. Katiba iliyoanzisha jamhuri ya demokrasia chini ya katiba, ambapo watu hutumia nguvu zao kupitia wawakilishi wao waliochaguliwa.

Kanuni ya pili yenye uvuvio ni mgawanyo wa nguvu iliyonaibishwa kati ya taifa na majimbo yake saidizi. Katika mfumo wetu wa shirikisho, kanuni hii isiyo na mfano wakati mwingine imebadilishwa na marekebisho yenye uvuvio, kama vile yale ya kukomesha utumwa na kutoa haki ya wanawake kupiga kura, yaliyotajwa hapo awali. Kwa kiasi kikubwa, Katiba ya Marekani inawekea ukomo serikali ya kitaifa kwenye kutumia nguvu iliyopewa waziwazi au kwa mapendekezo, na inahifadhi nguvu zingine za serikali kwenye Majimbo husika au kwa watu.”5

Kanuni nyingine yenye uvuvio ni mgawanyo wa madaraka. Vyema zaidi ya karne kabla ya mapatano yetu ya Kikatiba ya mwaka 1787, Bunge la Uingereza liliasisi utenganisho wa baraza la kutunga sheria na mamlaka ya utendaji wakati walipopokonya uwezo fulani kutoka kwa mfalme. Uvuvio katika mapatano ya Marekani ulikuwa kunaibisha utendaji huru baraza la kutunga sheria, na nguvu za kisheria ili matawi haya matatu yaweze kusimamiana wao kwa wao.

Kanuni ya nne yenye uvuvio ipo kwenye mkusanyiko wa dhamana muhimu ya haki za mtu binafsi na ukomo mahususi kwenye mamlaka ya serikali katika Sheria ya Haki za binadamu, iliyokubalika miaka mitatu tu baada ya Katiba kuanza kutumika. Sheria ya haki za binadamu haikuwa mpya. Hapa, uvuvio ulikuwa katika utekelezaji wa utendaji wa kanuni zilizoasisiwa Uingereza, kuanzia na Hati ya Haki za Binadamu. Waandishi wa Katiba walikuwa na uzoefu wa hili kwa sababu baadhi ya hati za kikoloni zilikuwa na dhamana kama hizo.

Bila Hati ya Haki za Binadamu, Marekani isingeweza kuhudumia kama taifa mwenyeji kwa ajili ya Urejesho wa injili, ambao ulianza miongo mitatu tu baadaye. Kulikuwa na uvuvio mtakatifu katika toleo la kwanza kwamba pasiwepo kigezo cha dini kwa ajili ya ofisi ya umma,6 lakini nyongeza ya uhuru wa kidini na dhamana ya kutokuwa na serikali ya dini katika Rekebisho la Kwanza ilikuwa muhimu. Tunaona pia uvuvio mtakatifu katika Rekebisho la Kwanza la uhuru wa kujieleza na magazeti na katika ulinzi binafsi katika marekebisho mengine, kama vile kwa ajili ya kuendesha mashtaka ya jinai.

Picha
Sisi watu.

Tano na ya mwisho, ninaona uvuvio mtakatifu katika lengo muhimu la Katiba yote. Watu utawaliwa na sheria na si na watu binafsi, na uaminifu wetu kwa Katiba na kanuni zake na michakato, na si mshikilia ofisi yeyote. Katika njia hii, watu wote ni sawa mbele za sheria. Kanuni hizi zinapinga tamaa za udikteta, ambazo zimeharibu demokrasia katika baadhi za nchi. Pia zinamaanisha kwamba hakuna kati ya matawi matatu ya serikali linapaswa kuwa na nguvu juu ya lingine au kuzuia lingine kutenda vyema kazi zake za kikatiba za kusimamiana kila moja.

III.

Licha ya kanuni takatifu zenye uvuvio za Katiba ya Marekani, kama zilivyotumiwa na binadamu wasio wakamilifu matokeo yanayodhamiriwa siku zote hawajawahi kutimizwa. Mada muhimu za utungaji wa sheria, kama vile baadhi ya sheria zinazotawala mahusiano ya familia, zimeondolewa kutoka majimboni na serikali ya shirikisho. Rekebisho la Kwanza la dhamana ya uhuru wa kujieleza wakati mwingine limedhaifishwa na ukandamizaji wa kauli zisizo na umaarufu. Kanuni ya mgawanyo wa madaraka siku zote imekuwa chini ya msukumo na utofauti wa tawi moja la serikali kutumia au kuzuia nguvu zilizotolewa kwa lingine.

Kuna vitisho vingine ambavyo vinadhoofisha kanuni zenye uvuvio za katiba ya Marekani. Uzito wa Katiba umedhoofishwa na juhudi za kupunguza mwelekeo wa kijamii wa sasa kama sababu kwa kuanzishwa kwake, badala ya uhuru na serikali binafsi. Mamlaka ya Katiba yamepuuzwa wakati wagombea au viongozi wanapuuza kanuni zake. Heshima na nguvu ya Katiba imepunguzwa na wale wanaoitaja kama jaribio la heshima au msemo wa kisiasa, badala ya hadhi yake ya juu sana kama chanzo cha uidhinishaji wa na ukomo kwa mamlaka ya serikali.

IV.

Imani yetu katika uvuvio mtakatifu inawapa Watakatifu wa Siku za Mwisho jukumu la kipekee kutetea na kuilinda Katiba ya Marekani na kanuni za masharti ya katiba popote tunapoishi. Tunapaswa kutumaini katika Bwana na kuwa na hakika kuhusu siku za baadaye za taifa hili.

Ni nini kingine Watakatifu wa Siku za Mwisho wanaweza kufanya? Lazima tuombe kwa ajili ya Bwana kuongoza na kubariki mataifa yote na viongozi wao. Hii ni sehemu ya makala yetu ya imani. Kuwa chini ya marais au watawala7 kwa vyovyote hakuweki kizuizi kwa sisi kupinga sheria au sera binafsi. Inahitajika kwamba tutumie ushawishi wetu kiraia na kwa amani, ndani ya mfumo wa katiba zetu na sheria zinazotumika. Kwenye masuala ya migogoro, tunapaswa kutafuta kukadiria na kuungana.

Kuna kazi mbili zingine ambazo ni sehemu ya kulinda Katiba yenye uvuvio. Tunapaswa kujifunza na kutetea kanuni zenye uvuvio za Katiba. Tunapaswa kutafuta na kusaidia watu wenye hekima na wema ambao wataunga mkono kanuni hizo katika matendo yao kwa umma.8 Tunapaswa tuwe raia wenye uelewa ambao ni watendaji katika kufanya ushawishi wetu uonekane katika masuala ya umma.

Katika Marekani na katika demokrasia zingine, ushawishi wa kisiasa unapatikana kwa kugombea ofisi (jambo ambalo tunahimiza), kwa kupiga kura, kwa msaada wa kifedha, kwa uanachama na huduma katika vyama vya siasa, na kwa mawasiliano endelevu kwa maofisa, vyama, na wagombea. Ili ifanye kazi vizuri, demokrasia inahitaji vyote hivi, lakini raia yeyote makini haitaji kutoa hivyo vyote.

Kuna masuala mengi ya kisiasa, na hakuna chama, jukwaa, au mgombea binafsi anayeweza kutosheleza mapendeleo yote ya mtu binafsi. Kila raia lazima afanye uamuzi ni masuala yapi ni muhimu zaidi kwake katika wakati fulani wowote. Kisha waumini wanapaswa kutafuta uvuvio juu ya jinsi kutumia ushawishi wao kulingana na vipaumbele vyao. Mchakato huu si rahisi. Inaweza kuhitaji kubadili msaada wa chama au chaguzi za mgombea, hata kutoka uchaguzi hadi uchaguzi.

Vitendo huru kama hivi wakati mwingine vitahitaji wapiga kura kuwasaidia wagombea au vyama vya siasa au majukwaa ambayo nafasi zao zingine hawawezi kuziidhinisha.9 Hii ni sababu moja ya kuwahimiza waumini wetu kuepuka kuhukumiana katika mada za kisiasa. Hatupaswi kamwe kudai kwamba Mtakatifu wa Siku za Mwisho mwaminifu hawezi kuwa katika chama fulani au kumpigia kura mgombea fulani. Tunafundisha kanuni sahihi na kuwaacha waumini wetu wachague jinsi ya kuweka kipaumbele na kutumia kanuni hizo kwenye masuala yanayotolewa mara kwa mara. Pia tunasisitiza, na kuwaomba viongozi wetu wa maeneo husika kusisitiza, kwamba chaguzi na muunganiko wa kisiasa visiwe mada ya mafundisho au utetezi katika mikutano yetu yoyote ya Kanisa.

Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho litatumia, bila shaka, haki yake ya kuidhinisha au kupinga mapendekezo maalum ya sheria ambayo tunaamini yataathiri matumizi huru ya dini au masilahi muhimu ya mipangilio ya Kanisa.

Ninashuhudia juu ya Katiba takatifu yenye uvuvio ya Marekani na kuomba kwamba sisi ambao tunamtambua Kiumbe Mtakatifu aliyeivuvia siku zote tutatetea na kulinda kanuni zake kuu. Katika Jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Ona Mark Tushnet, “Constitution,” in Michel Rosenfeld and András Sajó, eds., The Oxford Handbook of Comparative Constitutional Law (2012), 222. Nchi tatu zisizo na hati ya katiba iliyoandikwa ni Uingereza, New Zealand na Israeli. Kila moja ya hizi ina tamaduni imara za utekelezaji wa katiba, japokuwa masuala ya utawala hayako kwenye hati moja.

  2. Katiba ya Marekani, makala ya 1, sehemu ya 2.

  3. J. Reuben Clark Jr., “Constitutional Government: Our Birthright Threatened,” Vital Speeches of the Day, Jan. 1, 1939, 177, quoted in Martin B. Hickman, “J. Reuben Clark, Jr.: The Constitution and the Great Fundamentals,” katika Ray C. Hillam, ed., By the Hands of Wise Men: Essays on the U.S. Constitution (1979), 53. Bigham Young alikuwa na mtazamo ule ule wa kuendeleza Katiba, akifundisha kwamba walioianzisha “waliweka msingi, na ulikuwa kwa ajili ya vizazi vijavyo kulea muundo bora juu yake” (Discourses of Brigham Young, sel. John A. Widtsoe (1954), 359.

  4. Hizi tano ni sawa lakini hazifanani na zile zilizopendekezwa katika J. Reuben Clark, Stand Fast by Our Constitution (1973), 7, na Ezra Taft Benson, “Our Divine Constitution,” Ensign, Nov. 1987, 4–7; “The Constitution—A Glorious Standard,” Ensign, Sept. 1987, 6–11. Ona, kwa ujumla, Noel B. Reynolds, “The Doctrine of an Inspired Constitution,” katika By the Hands of Wise Men.

  5. Katiba ya Marekani, rekebisho la 10.

  6. Katiba ya Marekani, makala ya 6.

  7. Ona Makala ya Imani 1:12.

  8. Ona Mafundisho na Maagano 98:10.

  9. Ona Davd B, Magleby, “The Necessity of Political Parties and the Importance of Compromise,” BYU Studies, no. 4 (2015), 7–23.

Chapisha