“Kanuni za Injili Yangu,” Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana, Mei 2021.
Kikao cha Jumapili Alasiri
Kanuni za Injili Yangu (Mafundisho na Maagano 42:12)
Dondoo
Kanuni ya injili ni mwongozo uliojikita kwenye mafundisho kwa ajili ya kufanyia kazi kwa uadilifu haki ya kujiamulia kimaadili. Kanuni zinatokana na kweli pana za injili na kutoa mwelekeo na viwango wakati tunaposonga mbele kwenye njia ya agano. …
Kujifunza, kuelewa, na kuishi kanuni za injili huimarisha imani yetu kwa Mwokozi, huzidisha msimamo wetu Kwake, na kualika baraka nyingi na karama za kiroho katika maisha yetu. Kanuni za haki pia zinatusaidia kuangalia zaidi ya mapendeleo yetu binafsi na matamanio ya kujifikiria wenyewe kwa kutoa taswira ya thamani ya ukweli wa milele pale tunaposafiri katika hali tofauti, changamoto, maamuzi na uzoefu tofauti wa maisha ya duniani. …
Wakati Joseph Smith alipofungwa katika Jela ya Liberty, aliandika barua za maelekezo kwa waumini na viongozi wa Kanisa na kuwakumbusha kwamba “merikebu kubwa hufaidika kwa kiwango kikubwa sana na usukani mdogo wakati wa dhoruba, kwa kuwekwa katika kutenda kazi dhidi ya upepo na mawimbi” [Mafundisho na Maagano 123:16].
“Usukani” ni gurudumu au mkombo na kifaa kilichounganishwa kinachotumika kuongoza merikebu au boti. Na “kuwekwa katika kutenda kazi dhidi ya upepo na mawimbi” huwakilisha kugeuza merikebu ili kwamba iweze kubakia kwenye usawa wake na isipinduke wakati wa dhoruba.
Kanuni za Injili zipo kwa ajili yangu na wewe kama usukani ulivyo kwa meli. Kanuni sahihi zinatuwesha kupata njia yetu na kusimama imara, thabiti, na tusiohamishika ili tusipoteze usawa wetu na kuanguka katika ghadhabu za dhoruba za giza nene na kukanganyikiwa kwa siku za mwisho.