“Kwa Nini Njia ya Agano,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Mei 2021.
Kikao
Kwa Nini Njia ya Agano
Dondoo
Njia ya agano ni nini? Ni njia moja iongozayo kwenye ufalme wa selestia wa Mungu. Tunapanda juu ya njia hiyo kwenye lango la ubatizo. …
Wengine wanaweza kusema, “ninaweza kufanya chaguzi nzuri nikiwa na, au bila ubatizo; sihitaji maagano kuwa mtu mwenye heshima na aliyefanikiwa.” Ni nini basi, tofauti ya njia ya agano?
Kwa kweli, tofauti hiyo ni ya kipekee na yenye umuhimu wa milele. …
Kwanza ni asili ya utii wetu kwa Mungu. Zaidi ya kuwa tu na nia njema, tunajitolea kwa dhati kabisa kuishi kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu. Katika hili, sisi tunafuata mfano wa Yesu Kristo. …
Kipengele cha pili cha kipekee cha njia ya agano ni uhusiano wetu na Mungu. Maagano ambayo Mungu hutoa kwa watoto Wake hufanya zaidi ya kutuongoza. Yanatuunganisha sisi Kwake. …
Hii inatuongoza kuzingatia baraka maalum ya tatu ya njia ya agano. Mungu hutoa zawadi isiyoweza kuelezeka ili kuwasaidia wafanya maagano kuwa watunza maagano: kipawa cha Roho Mtakatifu. …
Ya nne wale wanaofuata njia ya agano pia hupata baraka za kipekee katika mikusanyiko anuwai iliyochaguliwa kiungu [kama vile mikutano ya sakramenti na kuabudu hekaluni]. …
Mwisho, ni katika tu kufuata njia ya agano kwamba tunarithi baraka za Ibrahimu, Isaka, na Yakobo, baraka za juu kabisa za wokovu na kuinuliwa ambazo ni Mungu pekee anayeweza kuzitoa. …
Acha tufuate wito wa nabii wa kubaki kwenye njia ya agano.