2021
Safari Binafsi ya Mtoto wa Mungu
Mei 2021


“Safari Binafsi ya Mtoto wa Mungu,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Mei 2021.

Kikao cha Jumamosi Alasiri

Safari Binafsi ya Mtoto wa Mungu

Dondoo

Picha
mtoto

Kila mtu anayekuja duniani ni mwana au binti wa kipekee wa Mungu. Safari yetu binafsi haikuanzia wakati wa kuzaliwa. Kabla ya sisi kuzaliwa, tulikuwa pamoja katika ulimwengu wa matayarisho ambapo “tulipokea masomo [yetu] ya kwanza katika ulimwengu wa roho” [Mafundisho na Maagano 138:56]. …

Kama watoto wa agano wa Mungu, tunapenda, tunaheshimu, tunalisha, tunalinda, na kukaribisha wale roho wanaokuja kutoka kwenye ulimwengu wa kabla ya kuzaliwa duniani . …

… Rais Gordon B. Hinckley … alisema: “… Utoaji mimba ni uovu … ambao unaifagia dunia yote.”

… Acha tushiriki hisia zetu za kina juu ya utakatifu wa maisha na wale wanaofanya maamuzi katika jamii. Wanaweza kutothamini kabisa kile tunachoamini, lakini tunaomba kwamba wataelewa zaidi kwa nini, kwetu sisi, maamuzi haya yanaenda mbali zaidi ya kile mtu anachotaka kwa ajili ya maisha yake mwenyewe. …

Nashuhudia kwamba safari yako binafsi wewe mwenyewe kama mtoto wa Mungu haikuanzia kwako kwa mtiririko wa kwanza wa hewa ya dunia ilipokuja ikikimbilia ndani ya mapafu yako, na haitakoma wakati unashusha pumzi yako ya mwisho katika mwili wenye kufa.

Na tukumbuke daima kwamba kila mtoto wa kiroho wa Mungu anakuja duniani kwa safari binafsi ya kwake mwenyewe. Naomba tuwakaribishe, tuwalinde, na tuwapende daima. Unapowapokea watoto hawa wa thamani katika jina la Mwokozi na kuwasaidia katika safari yao ya milele, nakuahidi kwamba Bwana atakubariki na kumwaga upendo na idhini Yake juu yako.

Chapisha