Njoo, Unifuate
Henoko Alikuwa Nani?
Mti huu wa familia huonesha watu wawili walioitwa Henoko katika familia ya Adamu na Hawa. Kijana wa Kaini, Henoko, mjukuu wa Adamu (ona Musa 5), ni tofauti na kijana wa Yaredi, Henoko, ambaye alikuwa kizazi cha sita kutoka kwa Adamu na aliyejenga mji wa Sayuni (ona Musa 6–7).
Ni kwa jinsi gani nabii Henoko aliitikia wito wake?
Wakati Henoko alipoitwa kuhubiri toba, alijihisi asiyefaa, akimwelezea Bwana kwamba alikuwa “si mwepesi wa kusema” (Musa 6:31). Lakini Mungu alimpa Henoko nguvu na ahadi, “Fumbua kinywa chako, nacho kitajazwa, nami nitakupa maneno” (Musa 6:32). Wengi walikuja kuamini maneno yake na Henoko alianzisha mji wa Sayuni.
Akirejelea mfano wa Henoko, Mzee David A. Bednar alituhakikishia wale wote kati yetu ambao wanahisi kuzidiwa, kutokuwa sawa na wengine au kutostahili kwa ajili ya wito mpya au jukumu jipya kwamba “ahadi ya Bwana kwa Henoko ina matumizi sawa … leo” (“Katika nguvu ya Bwana,” mkutano mkuu, Okt. 2004).