Ujumbe wa Urais
Joto la Injili
Ni mwezi Juni na nchini Kenya tunaweza kuhisi kushuka kwa kiwango cha joto. Mlima Kenya una ndimi chache za theluji juu yake kutukumbusha kwamba majira ya baridi yamefika. Wakati nikiwa mvulana katika nyumba yangu ya Te Ahora huko New Zealand, ikiwa imepachikwa kwa uzuri chini ya mlima ambao ni kijani mwaka mzima, moto wa jikoni ungewashwa kila asubuhi ya majira ya baridi ili kupasha joto jiko na kupika uji mtamu kwa ajili ya kifungua kinywa.
Nimetafakari kuhusu kitu kingine kinachoweza kutupatia joto mwaka mzima na nimegundua ni ‘Joto linalotokana na Injili.’
Mafundisho ya Injili hutusaidia kuelewa sisi ni nani, ambayo hutupatia hisia ya joto ya sisi kuwa sehemu yake. Mimi ni, kama vile wewe ulivyo, mwana mpendwa wa Mungu. Ananitaka nirejee kuishi Naye tena. Katika nyakati zote, na hasa katika nyakati hizo za kukata tamaa, tunaweza kuhisi joto la Baba mpendwa wa Mbinguni.
Joto la ziada huja tunapofanya na kutunza maagano matakatifu kupitia Ukuhani uliorejeshwa wa Mungu. Bila kujali magumu yametuzingira kwa kiasi gani—na ni mengi—tunalo hakikisho kwamba kama maagano yanafanywa na kutunzwa, tunaweza kuishi tena katikakumbatio la joto la Bwana.
Bila kujali baridi ya asubuhi jumapili itakuwaje, tunahisi joto tuingiapo jengo la kanisa, liwe la matofali au makopo na kwa ukunjufu tunakaribishwa na waumini wenzetu.Hakuna kati yetu aliye mkamilifu, lakini sote tunataka kuwa wazuri zaidi na tunaona kwamba hamu hutoka kwa kila mmoja.waumini huudhuria mikutano ya kanisa ili kushiriki uelewa wao, kutoa tabasamu ya kutia moyo na kushuhudia, kwamba tu pamoja nao katika Injili ya Yesu Kristo.Na tuhakikishe kwamba katika matawi na kata zetu hakutakuwa na ‘wageni wala wapitaji, bali [tuwe] wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu’ (Waefeso 2:19).
Mioyo yetu hutiwa joto zaidi pale tunapokutana kila wiki kwenye huduma ya sakramenti na kushiriki ishara za sakramenti kama ukumbusho wa sadaka ya Bwana ya mwili na damu Yake ambavyo alivitoa kwa kila mmoja wetu. Kupendwa zaidi na Yesu Kristo mpaka dhabihu ya upatanisho ingefanywa naye kwa ajili yetu, hakika hututia joto mioyo yetu.
Maandiko pia huangaza njia na kutia joto nafsi za wote ambao wataweka wakfu muda wao mchache kila siku ili ‘kujifunza kuhusu Yeye.’ Kujifunza mafundisho ya Kristo huondoa kiza na kuruhusu the nuru safi ya Kristo katika nafsi zetu.
Tunafurahia ongezeko la amani ambalo Mwokozi ametuahidi na kutiwa nuru kwa maneno ya manabii pale ‘tunaposikiliza’ saut ongozi ya Bwana.
Nina shukrani sana kwa yumba ndogo ya mbao chini ya mlima ambayo hunikumbusha kwamba hata nyakati za asubuhi za majira ya baridi, wewe na mimi tunaweza kupata ‘Joto la Injili’ katika maisha yetu.