2023
Kutunza Maagano
Juni 2023


Member Voices

Kutunza Maagano

Ninapojiandaa kwa ujio wa pili wa Bwana Yesu Kristo, nimeongozwa na vitu vidogo na rahisi ambavyo vimebariki maisha yangu kwa kupita kushika maagano.

Ni takribani miaka ishirini na sita tangu nipate fursa ya kukutana na wamisionari kupitia binamu yangu ambaye ni muumini. Nilikuwa na fursa ya kupata mafunzo yaliyopelekea kwenye ubatizo wangu. Hiyo ilikuwa ni hatua yangu ya kwanza ya kufanya agano katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Tangu kipindi hicho, sijawahi kuangalia nyuma tena. Licha ya changamoto nilizopitia, siku zote nimetiwa moyo kwa kujua kwamba Baba yetu wa Mbinguni ataandaa njia kwa ajili ya watoto Wake ambao wanajitahidi kushika maagano waliyoyaweka.

Tunaposonga zaidi na zaidi katika njia ya agano, mimi pamoja na wewe tunakua katika ukweli wa injili. Alma na Amuleki katika kitabu cha Mormoni hutukumbusha kwamba maisha ya hapa duniani ni, “wakati wa kujitayarisha kukutana na Mungu” (Alma 12:24). Tunaweza kufanya hivyo tu kupitia kufanya maagano okozi na Baba yetu wa Mbinguni.

Ninapojiandaa kwa ujio wa pili wa Bwana Yesu Kristo, nimeongozwa na vitu vidogo na rahisi ambavyo vimebariki maisha yangu kwa kupitIa kushika maagano.

Kwanza, Kuikumbuka siku ya Sabato kwa kuhudhuria mkutano wa sakramenti na kushiriki katika kuhudumu.

Pili, Kujitahidi kuheshimu na kuishi maagano yangu ya ukuhani kama yalivyoorodheshwa kwenye M&M 84:33–44.

Injili hii rahisi ambayo tunaamriwa kuikumbatia, na ushauri ninaopokea kupitia maneno ya manabii wanaoishi, hunipa ujasiri wa kuendelea kutafuta kujifunza kupitia mwongozo wa Roho Mtakatifu.

Enzi nikiwa kama kijana mseja, nilijiunga na kushiriki chuo. Hiyo ilinipa fursa ya kukutana na mke wangu kipenzi ambaye amekuwa ni nguvu kuu kwangu na kwa watoto wangu katika kutusaidia kutembea kwenye njia ya agano. Kama kiongozi wa kanisa na nikiwa na hamu ya kuongoza kwa mfano, niliamua kurejea shuleni kama mtu mzima—nikianza na kazi ya shule ya msingi na kusonga mpaka sekondari ya juu.

Hivi karibuni nikiwa natafakari maneno ya Rais Russell M. Nelson, katika hubiri lake “Tenga Muda kwa ajili ya Bwana”1, ilinitia moyo kutumikia wengine na kujifunza maandiko yangu katika njia ambayo huongoza Roho Mtakatifu kunipa uelewa wa kina wa jinsi ya kubakia kwenye njia ya agano. Nina shukrani kwamba tunaye nabii anayeishi anayetuongoza turejee kwa Baba yetu wa Mbinguni katika hatua zote za maisha, ya kiroho na kimwili.

Ningependa kuwaalikeni “mje kwa Kristo na mkamilishwe ndani yake” (Moroni 10:32), kwa kufanya maagano ambayo yatakuunganisha wewe na familia yako kwake. Ninajua kwamba kupitia injili ya Yesu Kristo tunaweza kuishi kwa furaha katika maisha haya na yajayo kupitia utii kwenye maagano yetu na kufuata mafundisho ya Mwokozi wetu Yesu Kristo.

Muhtasari

  1. Ona Russell M. Nelson, “Tenga Muda kwa ajili ya Bwana”, Liahona, Nov. 2021, 120–121.

Chapisha