2023
Safari ya Hekaluni Kupitia Mto Mkuu Kongo Inaziunganisha Familia kwa Maisha Haya na Milele
Juni 2023


Habari za Ndani

Safari ya Hekaluni Kupitia Mto Mkuu Kongo Inaziunganisha Familia kwa Maisha Haya na Milele

Waumini wamejitayarisha kwa miaka mingi kwa ajili ya uzoefu huu usiosahaulika.

Waumini arobaini na mmoja wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho kutoka Brazzaville, Jamhuri ya Kongo, walivuka Mto Kongo kwa boti ili wafanye maagano matakatifu ya milele ndani ya Hekalu la Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, mnamo tarehe 25 na 26 Novemba 2022. Kundi lilijumuisha wazazi ambao walioana kwa maisha haya na milele na baadaye kuunganishwa na watoto wao. Vijana wakubwa waseja pia walipokea endaumenti zao.

Waumini kutoka Brazzaville walitakiwa kusubiri kwa takribani miaka miwili kuondolewa kwa vizuizi vya Uviko-19 ili waje Hekaluni. Walifanya pia dhabihu ya kifedha ili kulipia malazi yao na safari fupi lakini ya gharama kubwa ya kuvuka mto.

“Huu ulikuwa uzoefu wa kiroho usiosahaulika kwa waumini kutoka Brazzaville,” kulingana na Rais wa Hekalu Mingotyi François Mukubu.

Aliongeza kwamba, “tulivutiwa na unyenyekevu ambao watu wazima na watoto walikuwa nao kwa ajili ya Hekalu. Hii inaonesha kwamba viongozi wa ukuhani katika mikusanyiko yao walikuwa wamewatayarisha waumini vyema na kuwafunza umuhimu wa Hekalu kwenye maisha yao. Wafanyakazi wote wa Hekaluni walikuwa na furaha kushiriki uzoefu huu wa kupendeza kwa akina kaka na akina dada hawa.”

Muumini kutoka Brazzaville alisema haya kuhusu uzoefu wake wa hekaluni, “nilianza kujitayarisha kwa ajili ya hekalu mnamo Desemba 2019, na ndoto yangu [hatimaye] imetimia. Nilihisi kana kwamba kulikuwa na kitu kinapungua ndani yangu, lakini baada ya kuomba hekaluni ninahisi wepesi na amani ya moyo. Ulikuwa uzoefu wa kipekee wa kiroho kwangu mimi. Ninamshukuru Mungu kwa kufanya yote yawezekane.”

Hekalu la Kinshasa liliwekwa wakfu mnamo 2019 na ni hekalu la kwanza katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Urais wa Kwanza umetangaza mahekalu mawili zaidi katika nchi hii kubwa ya Afrika ya kati: Lubumbashi (kwenye ujenzi) na Kananga (kwenye mpango).

Mnamo Aprili 2022 Rais Nelson alitangaza mipango ya kujenga hekalu Brazzaville, Jamhuri ya Kongo. Pale hekalu hili litakapokamilika, waumini kutoka Jamhuri ya Kongo hawatahitaji kufunga safari kwenda Kinshasa.

Brazzaville na Kinshasa ni miji mikuu iliyokaribiana ulimwenguni, lakini imetengwa na Mto Kongo, mto mmojawapo mkubwa ulimwenguni. Wasafiri lazima wavuke kwa boti kwa sababu hakuna madaraja yanayounganisha miji hii miwili.

Chapisha