“Juni 17–23: ‘Yesu Kristo Atakuja Kuwakomboa Watu Wake.’ Alma 8–12,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: Kitabu cha Mormoni 2024 (2024)
“Juni 17–23. Alma 8–12,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2024 (2024)
Alma 17–23: Yesu Kristo Atakuja Kuwakomboa Watu Wake
Alma 8–12
Kazi ya Mungu haitakosa kufaulu. Lakini juhudi zetu za kusaidia kazi Yake wakati mwingine huonekana kutofaulu—ingawa, yawezekana tusione kwa haraka matokeo tunayotumainia. Mara zingine tunaweza kuhisi kidogo kama Alma wakati alipohubiri injili kule Amoniha—kukataliwa, kutemewa mate na kufukuzwa. Lakini wakati malaika alipomuamuru arudi na ajaribu tena, Alma kwa ujasiri “alirudi haraka” (Alma 8:18), na Mungu aliandaa njia mbele yake. Hakumpa tu Alma chakula na mahali pa kukaa, bali Yeye pia alimuandaa Amuleki, ambaye alikuja kuwa mtumishi mwenzake, mtetezi shujaa wa injili na rafiki mwaminifu. Tunapokabiliana na vikwazo na kuvunjika moyo pale tunapohudumu katika ufalme wa Bwana, tunaweza kukumbuka jinsi gani Mungu alimsaidia na kumuongoza Alma na tunaweza kutumaini kwamba Mungu atatusaidia na kutuongoza sisi pia, hata katika hali ngumu.
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani
Juhudi zangu za kushiriki injili ya Yesu Kristo zinahitaji subira.
Je, umewahi kushiriki injili ya Yesu Kristo na mtu fulani, lakini mwaliko wako ukakataliwa? Alma alipitia hili pia. Unajifunza nini kutoka kwake katika Alma 8:13–16 kuhusu kushiriki injili licha ya changamoto na upinzani? Endelea kusoma katika mistari 17–32, na tafuta vifungu vya maneno ambavyo vinakushawishi wewe uendelee kushiriki injili, hata kama unaona kama hufanikiwi.
Manabii na mitume ni mashahidi maalumu wa Kristo, hivyo wanao ushauri mwingi wa kushiriki wenye mwongozo wa kiungu kuhusu kushuhudia juu Yake. Angalia kile Mzee Dieter F. Uchtdorf alichokisema katika “Lakini Inakuwaje Kama ni Vigumu?” (kipengele katika “Kazi ya Umisionari: Kushiriki Kilichopo katika Moyo Wako,” Liahona, Mei 2019, 18) au kile ambacho Mzee Gary E. Stevenson alikishiriki katika “Penda, Shiriki, Alika,” (Liahona, Mei 2022, 84–87). Je, unapata nini ambacho kingeweza kumsaidia mtu ambaye anaanza kuhisi kukata tamaa kuhusu kushiriki injili?
Je, ungewezaje kufupisha yote ambayo umejifunza hapa na kuyaweka katika kauli moja au mbili za kutia moyo kuhusu kushiriki injili? Fikiria kutengeneza bango au utani ambao utakutia hamasa wewe (na wengine) kuendelea kujaribu.
Ona pia “Niwezeshe Kufundisha,” Nyimbo za Dini, na. 155; “Alma Is Commanded by an Angel to Return to Ammonihah” (video), Gospel Library; Mada za Injili, “Kuwaalika Wote Kupokea Injili ya Yesu Kristo,” Gospel Library.
Baraka za Mungu huja na majukumu makubwa.
Unaposoma kuhusu jinsi Wanefi huko Amoniha walivyowafanyia watumishi wa Mungu, ni rahisi kusahau kwamba wakati fulani watu hao waliishi injili na walikuwa “watu waliopendwa sana na Bwana” (Alma 9:20). Unaposoma kuhusu baraka kuu ambazo Mungu aliwapa watu wa Nefi (ona hasa Alma 9:14–23), tafakari kuhusu baraka kuu ambazo Amekupa wewe. Je, ni majukumu yapi huja pamoja na baraka hizo? Je, wewe unafanya nini ili kubakia mkweli katika majukumu haya?
Ona pia Mafundisho na Maagano 50:24; 82:3; 93:39.
Mpango wa Mungu ni mpango wa ukombozi.
Katika Alma 11–12, Alma na Amuleki waliuelezea mpango wa Mungu kama mpango wa ukombozi. Unaposoma milango hii, tafakari kwa nini neno ukombozi linatumika kuelezea mpango wa Mungu Fikiria kuandika muhtasari mfupi kuhusu kile ambacho Alma na Amuleki walifundisha kuhusu vipengele vifuatavyo vya mpango huu:
-
Anguko
-
Mkombozi
-
Toba
-
Kifo
-
Ufufuko
-
Hukumu
Tazama matokeo ambayo maneno ya Amuleki yalikuwa nayo kwa watu (ona Alma 11:46). Je, ni kwa namna gani kujua kuhusu mpango wa Mungu kunakusaidia wewe?
Ona pia Dallin H. Oaks, “Mpango Mkuu,” Liahona, Mei 2020, 93–96; “Amulek Testifies of Jesus Christ” (video), Gospel Library.
Ikiwa sitashupaza moyo wangu, naweza kupokea ziada ya neno la Mungu.
Watu wengine wanaweza kujiuliza kwa nini Baba wa Mbinguni hafanyi kila kitu kijulikane kwetu. Katika Alma 12:9–14, Alma alieleza sababu mojawapo yamkini. Maswali haya yangeweza kukusaidia utafakari kile ambacho alikifundisha:
-
Je, kushupaza mioyo yetu humaanisha nini? Je, ni yapi matokeo ya kuwa na mioyo uliyoshupazwa? (Ona pia Alma 8:9–11; 9:5, 30–31; na 10:6, 25).
-
Unaweza kufanya nini ili kugeuza moyo wako umwelekee Mungu? (ona Yeremia 24:7; Alma 16:16; Helamani 3:35).
-
Je, unaweza kufanya kipi ili kuhakikisha kwamba neno la Mungu “lipo ndani [yako]”? (Alma 12:13). Je, unapokuwa na neno la Mungu ndani yako ni matokeo yapi unaweza kuwa nayo kwenye “maneno,” “matendo,” na “mawazo” yako? (Alma 12:14).
Je, uzoefu wa Amuleki unakufundisha nini kuhusu baraka za kuwa na moyo laini? (ona Alma 10:1–11).
Ona pia “Alma Warns Zeezrom” (video), Gospel Library.
Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto
Ninaweza kushiriki injili ya Yesu Kristo.
-
ukurasa wa shughuli ya wiki hii ungeweza kukusaidia ufupishe matukio katika Alma 8–10 kwa ajili ya watoto wako. Yawezekana ukataka kuwasaidia watafute kanuni ambazo ziliwafanya Alma na Amuleki kuwa wamisionari wazuri. Kwa mfano, hawakukata tamaa (ona Alma 8:8–13), walishuhudia juu ya Kristo (ona Alma 9:26–27), na walifanya kazi pamoja (ona Alma 10:12).
-
Wimbo kuhusu kazi ya umisonari kama vile “I Want to Be a Missionary Now” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,168), ungeweza kuwapa watoto wako mawazo kuhusu njia za kushiriki injili na rafiki zao. Waalike waandae orodha ya mawazo wanayopata na watu ambao wangeweza kushiriki nao injili. Ungeweza hata kuwaruhusu waigize kile ambacho wangekisema au kukifanya.
Mpango wa Mungu ni mpango wa ukombozi.
-
Pengine watoto wako wangeweza kuchora picha inayowakilisha kanuni za mpango wa ukombozi, kama Anguko la Adamu na Hawa, Upatanisho wa Yesu Kristo, toba, kifo, ufufuko na hukumu. Kisha ungewasaidia waoanishe picha zao na mistari katika Alma11–12 ambayo inafundisha kuhusu kanuni hizi.
Ninaweza kuwa rafiki mzuri.
-
Ungeweza kumwalika mtoto mmoja ajifanye kuwa Amuleki na mtoto mwingine ajifanye kuwa Alma pale unaposimulia hadithi katika Alma 8:18–22. Ni kwa jinsi gani Amuleki alikuwa rafiki mzuri wa Alma? Kisha watoto wako wangeshiriki jinsi gani mtu fulani amekuwa rafiki kwao na jinsi gani uzoefu huo ulivyowafanya wahisi.
-
Pengine ungetengeneza fumbo la urafiki: tafuta au chora picha ikiwakilisha urafiki na kata vipande kwa ajli ya fumbo hilo la urafiki. Nyuma ya kila kipande cha fumbo, andika kitu ambacho tunaweza kufanya ili kuwa rafiki mzuri, ikijumuisha vitu vilivyofanywa na Alma na Amuleki. Watoto wako wangefanya zamu ya kuchagua kipande na kuongeza kwenye fumbo wakati ukisoma kilichoandikwa nyuma ya kipande hicho. Ni yupi anahitaji urafiki wetu?
Kwa sababu ya Yesu Kristo, mimi nitafufuka.
-
Fikiria somo la vitendo kama hili kuhusu Ufufuko: mkono wako ungeweza kuwakilisha roho yako, na glavu ingeweza kuwakilisha mwili wako. Toa mkono wako nje ya glavu ili kuonesha kwamba roho na miili yetu vitatenganishwa kwenye kifo. Kisha weka mkono wako tena ndani ya glavu ili kuonesha kwamba roho na miili yetu vitaunganishwa tena kwenye Ufufuo. Waruhusu watoto wako wafanye zamu za kuvaa na kuvua glavu wakati ukiwasomea Alma 11:43. Onesha picha ya Mwokozi aliyefufuka (ona Kitabu cha Sanaa za Injili, na.59), na shuhudia kwamba Yesu Kristo alifanya iwezekane kwa kila mtu kufufuka.