Njoo, Unifuate 2024
Novemba 25–Desemba 1: “Kwa Imani Vitu Vyote Hutimizwa.” Etheri 12–15


“Novemba 25– Desemba 1:‘Kwa Imani Vitu Vyote Hutimizwa.’ Etheri 12–15,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: Kitabu cha Mormoni 2024 (2023)

“Novemba 25–Desemba1. Etheri 12–15,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2024 (2023)

Picha
Etheri akiingia pangoni

Etheri Akijificha kwenye Pango la Mwamba, na Gary Ernest Smith

Novemba 25–Desemba 1: “Kwa Imani Vitu Vyote Hutimizwa”

Etheri 12–15

Unabii wa Etheri kwa Wayaredi ulikuwa “mkubwa na wa ajabu” (Etheri 12:5). Yeye “aliwaambia juu ya vitu vyote, kutokea mwanzo wa binadamu” (Etheri 13:2). Aliziona “siku za Kristo” zijazo na Yerusalemu Mpya ya siku za mwisho (Etheri 13:4). Na alizungumzia juu ya “tumaini kwa ajili ya ulimwengu bora, ndio, hata mahali katika mkono wa kuume wa Mungu” (Etheri 12:4). Lakini Wayaredi waliyakataa maneno yake, sawa na vile ambavyo watu mara nyingi hukataa unabii wa watumishi wa Mungu—“kwa sababu [hawauoni]” (Etheri 12:5). Inahitaji imani kuamini ahadi au maonyo kuhusu vitu ambavyo hatuwezi kuviona, kama vile ilivyochukua imani kwa Etheri kutabiri juu ya “vitu vikubwa na vya ajabu” kwa watu wasioamini. Ilihitaji imani kwa Moroni kuamini kwamba Bwana angeweza kuchukua “unyonge wake katika maandishi” na kuugeuza kuwa nguvu (ona Etheri 12:23–27). Ni aina hii ya imani ambayo inatufanya “tuwe na uhakika na thabiti, siku zote tukizidi sana katika kutenda kazi njema, tukiongozwa kumtukuza Mungu” (Etheri 12:4). Na ni aina hii ya imani ambayo kupitia kwayo “vitu vyote hutimizwa” (Etheri 12:3).

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani

Etheri 12

Imani katika Yesu Kristo inaweza kuongoza kwenye miujiza.

Ni kawaida leo, kama vile ilivyokuwa katika siku za Etheri, kutaka kuona ushahidi kabla ya kuamini katika Mungu na uwezo Wake. Unajifunza nini kutoka Etheri 12:5–6 kuhusu wazo hili?

Mnaposoma Etheri 12, ungeweza kuandika muhtasari wa kila wakati unapopata neno “imani.” Fikiria kile ambacho kila hali inakufundisha kuhusu imani. Maswali kama haya yanaweza kusaidia: Imani ni nini? Inamaanisha nini kutumia imani? Ni yapi matunda ya imani katika Yesu Kristo? Ungeweza pia kuandika mawazo yako kuhusu ushahidi ulioupata “baada ya jaribu la imani yako” (Etheri 12:6).

Ona pia Russell M. Nelson, “Kristo Amefufuka; Imani Kwake Itahamisha Milima,” Liahona, Mei 2021, 101–4.

Waalike wengine washiriki, na wakati mwingine wafundishe. Watu wanajifunza vyema wakati wanapokuwa na fursa za kushiriki kile wanachojifunza au hata kufundisha katika mazingira rasmi. Iwe ni nyumbani au kanisani, fikiria kuwaruhusu wengine, ikijumuisha vijana, wafundishe sehemu ya somo.

Etheri 12:1–9, 28, 32

Yesu Kristo hutupatia “tumaini lililo bora zaidi.”

Kwa kuongezea kwenye umaizi mkubwa kuhusu imani, Etheri 12 pia ina mengi ya kusema kuhusu tumaini. Ruhusu maswali haya yaongoze kujifunza kwako:

  • Ni sababu zipi Etheri alikuwa nazo za “kutumaini ulimwengu bora”? (ona Etheri 12:2–5).

  • Je, ni nini dhumuni la nanga? Ni kipi tumaini hufanya kwa nafsi yako ambacho kinafanana na kile ambacho nanga hufanya kwa mashua? (ona Etheri 12:4).

  • Je, ni kipi tunatakiwa kukitumainia? (ona Etheri 12:4; Moroni 7:41).

  • Ni kwa jinsi gani injili ya Yesu Kristo imekupa “tumaini lililo bora zaidi.” (Etheri 12:32).

Ona pia Moroni 7:40–-41; Jeffrey R. Holland, “Mng’aro Mkamilifu wa Tumaini,” Liahona, Mei. 2020, 81–84.

Etheri 12:23–29

Picha
ikoni ya seminari
Yesu Kristo anaweza kugeuza udhaifu uwe nguvu.

Wakati tunaposoma maandishi yenye nguvu ya Moroni, ni rahisi kusahau kwamba alikuwa na wasiwasi kuhusu “unyonge wake katika kuandika” na aliogopa kwamba watu wangedhihaki maneno yake (ona Etheri 12:23–25). Kama umewahi kuhisi wasiwasi kuhusu udhaifu wako mwenyewe, soma kuhusu mahangaiko ya Moroni—na majibu ya Mwokozi—katika Etheri 12:23–29. Ungeweza pia kutafakari nyakati ambapo Yesu Kristo amekusaidia utambue udhaifu wako na kukufanya uwe na nguvu—hata kama Yeye hakuuondoa udhaifu huo. Pia fikiria kuhusu udhaifu ambao kwa sasa unapambana nao. Tunahitaji kufanya nini ili tupokee ahadi ya Mwokozi ya “kufanya vitu dhaifu kuwa vyenye nguvu? (Etheri 12:27).

Fikiria kuchunguza vifungu vifuatavyo ili kuona jinsi wengine katika maandiko walivyopata nguvu kupitia neema ya Yesu Kristo.

Ona pia Mada za Injili, “Neema,” Maktaba ya Injili; “Bwana Ni Nuru,” Nyimbo za Dini, na. 41.

Etheri 13:13–22; 14–15

Kuwakataa manabii wa Bwana huniweka katika hatari za kiroho.

Kuwa mfalme wa Wayaredi ilikuwa, kihistoria, wadhifa hatari. Hii ilikuwa kweli hasa kwa Koriantumuri, kwa maana, “watu wenye nguvu … walitafuta kumwangamiza” (Etheri 13:15–16). Katika Etheri 13:15–22, tambua kile ambacho Koriantumuri alifanya ili kujilinda na kile ambacho nabii Etheri alimshauri afanye kama mbadala. Unaposoma sehemu iliyosalia ya kitabu cha Etheri, tafakari matokeo ya kuwakataa manabii. Nini hutokea kwa watu wakati “Roho wa Bwana [anapokoma] kuwaongoza”? (Etheri 15:19). Ni kipi Bwana angeweza kukutaka wewe ujifunze kutokana na matukio haya? Zingatia kile unachoweza kufanya ili kuwafuata manabii Wake.

Kwa mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la Liahona na magazeti ya Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana.

Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto

Etheri 12:6–22

Imani ni kusadiki katika mambo ambayo siwezi kuyaona.

  • Fikiria kuwasaidia watoto wako warudie pamoja nawe “Imani ni vitu ambavyo vinatumainiwa na havionekani” kutoka Etheri 12:6. Wangeweza kufurahia kutafuta picha ambazo zinaonesha mifano ya imani katika Etheri 12:13–15, 19–21 (ona Kitabu cha Sanaa za Injili, na. 78, 85, na ukurasa wa shughuli ya wiki hii). Waruhusu watoto wako waeleze kile wanachokijua kuhusu kila hadithi. Hapa kuna baadhi ya maswali ya kukusaidia ujadili mifano ya imani:

    • Watu hawa walitumainia nini?

    • Ni kwa jinsi gani imani yao ilijaribiwa?

    • Ni nini kilitendeka kwa sababu ya imani yao?

    Ungeweza pia kushiriki uzoefu wako mwenyewe wa kuitumia imani.

Etheri 12:4, 32

Tumaini ni kama nanga ya nafsi yangu.

  • Ili kuelewa kile ambacho Etheri 12:4 hufundisha kuhusu tumaini, wewe na watoto wako mngeweza kutafuta picha ya mashua na nanga. Kwa nini mashua zinahitaji nanga? Nini kingeweza kutokea kwa mashua ambayo haina nanga? Mnaposoma Etheri 12:12 pamoja, zungumzeni kuhusu jinsi ambavyo tumaini hutusaidia kama vile nanga inavyosaidia mashua. Waalike watoto wako wachore picha za mashua na nanga ili waweze kuwafundisha wengine kuhusu tumaini.

  • Kama watoto wako wanahitaji maelezo ya tumaini, wasaidie wapate moja ya maelezo hayo katika Mwongozo wa Maandiko, “Tumaini” (Maktaba ya Injili). Kulingana na maana hii na Etheri 12:4, 32, ni kipi tunapaswa kukitumainia? (ona pia Moroni 7:40–42). Wasaidie watoto wako wafikirie maneno mengine ya tumaini, pamoja na maneno ambayo yanamaanisha kinyume cha tumaini. Mngeweza pia kushiriki kila mmoja na mwenzake baadhi ya kweli za injili ambazo zinawapa tumaini.

Etheri 12:23–29

Yesu Kristo anaweza kunisaidia niwe imara kiroho.

  • Watoto wakati mwingine wanakumbana na hali ambazo huwafanya wahisi kuwa dhaifu, kama vile Moroni alivyohisi. Wasaidie watoto wako wajue kwa nini Moroni alihisi hivyo katika Etheri 12:23–25, na waulize kama wamewahi kuwa na hisia sawa na hizo. Kisha waalike wasome mistari 26–27 ili kuona ni jinsi gani Bwana alimsaidia Moroni.

  • Pengine watoto wako wangeweza kuchora picha ya kitu dhaifu na kitu chenye nguvu. Kisha waalike waongeze kwenye michoro yao baadhi ya maneno na virai kutoka Etheri 12:23–29 ambavyo vinawafundisha kuhusu jinsi Mwokozi anavyoweza kutusaidia tugeuze udhaifu wetu uwe nguvu. Wahimize watoto wafikirie kuhusu udhaifu walionao na kisha watafute msaada wa Mwokozi ili wawe wenye nguvu. Ungeweza pia kushiriki uzoefu ambapo Mwokozi alikusaidia uwe imara vya kutosha kufanya jambo gumu.

Kwa ajili ya mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la gazeti la Rafiki.

Picha
Etheri akiwa amepiga magoti katika mlango wa pango

Unabii wa Etheri Ulikuwa wa Ajabu, na Walter Rane

Chapisha