“Desember 30–Januari 5: ‘Urejesho Ulioahidiwa Unasonga Mbele’: Urejesho wa Utimilifu wa Injili ya Yesu Kristo,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: Mafundisho na Maagano 2025 (2025)
“Urejesho wa Utimilifu wa Injili ya Yesu Kristo,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2025
Desemba 30–Januari 5: “Urejesho Ulioahidiwa Unasonga Mbele”
Urejesho wa Utimilifu wa Injili ya Yesu Kristo
Je, unaadhimishaje kumbukizi ya miaka 200 ya tukio lililoubadilisha ulimwengu? Hilo ndilo swali ambalo Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili walitafakari Aprili 2020 ilipokaribia, inapotimia miaka 200 tangu Ono la Kwanza la Joseph Smith. “Tulijiuliza ikiwa mnara unapaswa kujengwa,” Rais Russell M. Nelson anasema. “Lakini tulipofikiria matokeo ya kipekee ya kihistoria na ya kimataifa ya Ono hilo la Kwanza, tulihisi msukumo wa kutengeneza mnara usio wa granaiti au jiwe bali wa maneno … ,sio kuchongwa katika mbao za mawe bali zaidi kuchongwa katika ‘mbao za nyama’ za mioyo yetu [2 Wakorintho 3:3]” (“Msikilize Yeye,” Liahona, Mei 2020, 90).
Mnara wa maneno wa waliotengeneza unaitwa “Urejesho wa Uti milifu wa Injili ya Yesu Kristo: Tangazo kwa Ulimwengu la Maadhimisho ya Miaka Mia Mbili.” Ni ukumbusho sio tu kwa Ono la Kwanza bali pia kwa kila kitu Yesu Kristo alichofanya—na bado anafanya—tangu wakati huo. Urejesho wa Injili Yake ulianza pale mtu mmoja alipomgeukia Mungu na akamsilikiza Yeye. Unaendelea kwa njia hiyo hiyo; moyo mmoja, tukio moja takatifu kwa wakati mmoja—ikijumuisha la kwako wewe.
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani
“Mungu anawapenda watoto Wake katika kila taifa la ulimwengu.”
Katika maoni yako, kwa nini tangazo kuhusu Urejesho lianze na maelezo kuhusu upendo wa Mungu? Unapojifunza tangazo hili, tafuta onyesho la upendo wa Mungu kwa “watoto Wake katika kila taifa la ulimwengu.” Ni kwa jinsi gani Urejesho wa injili umekusaidia wewe kuhisi upendo Wake?
Ona pia Gerrit W. Gong, “Mataifa Yote, Kabila na Lugha,” Liahona, Nov. 2020, 38–41.
Urejesho ulianza na jibu kwa swali.
Ingeweza kusemwa kwamba Mwokozi ndiye aliyeanzisha Urejesho wa injili Yake kwa kujibu swali. Ni ujumbe gani unaohisi tangazo la Urejesho linao kwa mtu mwenye maswali kuhusu Mungu, injili au “wokovu wa nafsi yake”? Ungeweza pia kujifunza Joseph Smith—Historia ya 1:5–20 ili kuona ni kitu gani unaweza kujifunza kutoka kwa Joseph Smith kuhusu kutafuta majibu ya maswali ya injili.
Ona pia Mada na Maswali, “Kutafuta Majibu,” Maktaba ya Injili.
Yesu Kristo amerejesha Kanisa Lake.
Je, Unajua nini kuhusu “Kanisa la Kristo la Agano Jipya,” ambalo Mwokozi amelirejesha kupitia Joseph Smith? Fikiria kujifunza maandiko haya na kuorodhesha baadhi ya sifa za Kanisa Lake:
Halafu, ungeweza kulinganisha maandiko ya hapo juu na ya chini, ambayo yanaelezea jinsi gani Yesu Kristo amerejesha sifa hizo za Kanisa Lake kupitia Joseph Smith:
Kwa nini wewe unashukuru kwa Urejesho wa injili ya Yesu Kristo?
Mzee Jeffrey R. Holland na mke wake wakati fulani walijaribu kufikiria jinsi gani wangehisi kuishi kabla ya kurejeshwa kwa Kanisa. “Tungetamani tungekuwa na nini?” walijiuliza wao wenyewe. Soma kuhusu uzoefu wao “Mwangaza Kamili wa Tumaini” (Liahona, Mei 2020, 81–82). Ni kwa jinsi gani Urejesho umesaidia kutimiza matumaini yako ya kiroho?
Ona pia Mada na Maswali, “Ukengeufu na Urejesho wa Injili,” Maktaba ya Injili.
“Urejesho ulioahidiwa unasonga mbele.”
Je, Umewahi kujifikiria wewe mwenyewe kama ni sehemu ya Urejesho wa injili? Fikiria maneno haya kutoka kwa Rais Dieter F. Uchtdorf: “Wakati mwingine tunafikiria juu ya Urejesho wa injili kama kitu ambacho kimekamilika, tayari kiko nyuma yetu. … Katika uhalisia, Urejesho ni mchakato endelevu; tunaishi ndani yake hivi sasa” (“Je, Unalala hadi mwisho wa Urejesho?,” Liahona, Mei 2014, 59).
Unapojiandaa kujifunza jinsi gani injili ilirejeshwa miaka ya 1800, ungeweza kuanza kwa kutafakari jinsi gani imeanza kurejeshwa katika maisha yako. Soma tangazo la Urejesho ukiwa na maswali kama haya akilini: Nimekujaje kujua kwamba hii ni kweli? Je, Ni kwa namna gani ninashiriki katika Urejesho leo?
“Mbingu zi wazi.”
Kirai “mbingu zi wazi” kina maanisha nini kwako? Ni ushahidi gani unauona—katika tangazo la Urejesho, katika Kanisa leo, katika maandiko na katika maisha yako—kwamba mbingu hakika zi wazi?
Ungeweza pia kujumuisha “Asubuhi Kunakucha” (Nyimbo za Dini, na. 1) kama sehemu ya kujifunza kwako. Unaona nini katika wimbo huu ambacho kinaongeza uelewa wako juu ya kirai “mbingu zi wazi”?
Ona pia Quentin L. Cook, “Baraka ya Ufunuo Endelevu kwa Manabii na Ufunuo Binafsi ili Kuongoza Maisha Yetu,” Liahona, Mei 2020, 96–100.
Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto
“Kwa moyo wa dhati tunatangaza.”
-
Unaposoma sehemu za tangazo la Urejesho pamoja na watoto wako (au kutazama video ya Rais Nelson akilisoma), wasaidie kutafuta virai vinavyoanza kama “tunatangaza,” “tunatamka,” au “tunashuhudia.” Je, ni kweli gani manabii na mitume wetu wanazitamka? Labda wewe na watoto wako mngeweza kushiriki shuhuda zenu juu ya baadhi ya kweli hizo hizo.
“Joseph Smith … alikuwa na maswali.”
-
Yawezekana kuwa ya kupendeza kwa watoto wako kuchunguza baadhi ya maswali ambayo Joseph Smith alikuwanayo ambayo yaliongoza kwenye Urejesho wa injili ya Mwokozi. Wasaidie kutafuta baadhi ya mifano katika Joseph Smith—Historia ya 1:10, 29, 68. Je, Ni kwa jinsi gani tumebarikiwa leo kwa sababu Mungu alijibu maswali ya Joseph Simth?
-
Ungeweza pia kuwapatia watoto wako nafasi ya kuzungumza kuhusu maswali waliyo nayo. Tunajifunza nini kutoka kwa Joseph Smith kuhusu jinsi ya kutafuta majibu? (ona Joseph Smith—Historia ya 1:8–17; ona pia mstari wa 3 na wa 4 wa “This Is My Beloved Son,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 76).
“Wajumbe wa Mbinguni walikuja kumwelekeza Joseph.”
-
Ni nani walikuwa “wajumbe wa Mbinguni [ambao] walikuja kumwelekeza Joseph”? Watoto wako wanaweza kufurahia kutafuta picha za watu hao katika Kitabu cha Sanaa za Injili (ona na 91, 93, 94, 95). Je, ni kwa jinsi gani kila mmoja wa wajumbe hawa alisaidia “kuanzishwa upya kwa Kanisa la Yesu Kristo”? Maandiko yaliyopendekezwa katika wiki hii kwenye ukurasa wa shughuli yanaweza kuwasaidia watoto wako kujibu swali hili.
Yesu Kristo amerejesha Kanisa Lake.
-
Unawezaje kuwasaidia watoto wako kuelewa inamaanisha nini kwa Kanisa la Mwokozi kurejeshwa? Pengine wangeweza kujenga mnara rahisi kwa matofali au vikombe na “kurejesha,” au kujenga upya. Au, kama watoto wako wamewahi kurudishia kitu kwa sababu kilipotea au kuharibiwa, ungeweza kulinganisha tukio hilo na lille la Mwokozi kurejesha Kanisa Lake. Wasaidie kutafuta vitu maalumu vilivyotajwa katika tangazo la Urejesho ambavyo Mwokozi amevirejesha.
“Mbingu zi wazi.”
-
Ili kuonyesha kile kirai “mbingu zi wazi” kina maana gani, pengine ungeweza kushiriki ujumbe pamoja na watoto wako, kwanza nyuma ya mlango uliofungwa na kisha kupitia mlango ulio wazi. Waruhusu wafanye zamu kushiriki ujumbe pia. Je, ni jumbe gani Yesu Kristo alizonazo kwa ajili yako? Ni mambo gani yametusaidia kujua kwamba mbingu ziko wazi kwetu sisi?