Njoo, Unifuate
Septemba 1–7: “Kwa Ajili ya Wokovu wa Sayuni”: Mafundisho na Maagano 94–97


“Septemba 1–7, ‘Kwa Ajili ya Wokovu wa Sayuni’: Mafundisho na Maagano 94–97,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: Mafundisho na Maagano 2025 (2025)

“Mafundisho na Maagano 94–97,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Nyumbani na Kanisani: 2025

Hekalu la Kirtland

Hekalu la Kirtland, na Al Rounds

Septemba 1–7: “Kwa Ajili ya Wokovu wa Sayuni”

Mafundisho na Maagano 94–97

Hapo kale, Bwana alimwamuru Musa kujenga tabenakulo, “kwa mfano ule ulioonyeshwa [kwake] katika mlima.” (Waebrania 8:5; ona pia Kutoka 25:8–9). Tabenakulo lilipaswa kuwa kiini cha kambi ya Israeli nyikani (ona Hesabu 2:1–2).

Mnamo 1833, Bwana alimwamuru Joseph Smith kujenga mahekalu “siyo kwa jinsi ya ulimwengu” bali “kwa jinsi ambayo nitaionyesha” (Mafundisho na Maagano 95:13–14.; ona pia 97:10). Kama vile tabenakulo katika nyika, hekalu lilikusudiwa kuwa sehemu kuu katika Kirtland (ona Mafundisho na Maagano 94:1).

Leo, mahekalu yanapatikana ulimwenguni kote. Hata kama hayapo katikati ya majiji yetu, yanatuelekeza sisi kwa Kristo, ambaye anapaswa kuwa kiini cha maisha yetu. Ingawa kila hekalu linatofautiana katika mwonekano, ndani yake tunajifunza mpangilio mtakatifu ulio sawa—mpango wa mbinguni wa kuturudisha kwenye uwepo wa Mungu. Ibada na maagano matakatifu yanatuunganisha sisi na Kristo na kuziimarisha familia zetu “siyo kwa jinsi ya ulimwengu” bali kwa mpangilio ambao Mungu anatuonesha.

Ona Saints, 1:169–70.; “A House for Our God,” katika Revelations in Context, 165–73.

ikoni ya kujifunza

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Nyumbani na Kanisani

Mafundisho na Maagano 94; 97:10–17

Ninaweza “kujitoa kikamilifu kwa Bwana.”

Katika Mafundisho na Maagano 94, Bwana anatoa maelekezo kuhusu kujenga majengo ya utawala katika Kirtland—ofisi na nyumba ya uchapishaji. Ni kipi kinakuvutia wewe juu ya kile Bwana anachokisema kuhusu majengo haya katika Mafundisho na Maagano 94:2–12? Ni kwa jinsi gani hii inalingana na kile Yeye anachokisema kuhusu hekalu katika 97:10–17?

Inamaanisha nini kwako “kujitoa kikamilifu kwa Bwana”?

Mafundisho na Maagano 95

Bwana huwarudi wale anaowapenda.

Wakati ufunuo katika sehemu ya 95 ulipopokelewa, karibia miezi mitano ilikuwa imepita tangu Bwana awaamuru Watakatifu waijenge nyumba ya Bwana (ona Mafundisho na Maagano 88:117–19)—na walikuwa bado hawajaanza. Tazama jinsi Bwana alivyowasahihisha katika ufunuo huu. Unaweza hata kutengeneza orodha ya kanuni unazozipata za usahihishaji wenye mwongozo. Unajifunza nini kumhusu Bwana kutokana na jinsi alivyowasahihisha Watakatifu Wake?

Ona pia Mafundisho na Maagano 121:43–44; D. Todd Christofferson, “Kadiri ya Wengi Niwapendao, Ninawakemea na Kuwarudi,” Liahona,, Mei 2011, 97–100.

8:40

God Loves His Children

Elder Wakolo testifies of God’s love and describes how He shows that love to His children.

Mafundisho na Maagano 95:8, 11–17; 97:10–17

ikoni ya seminari
Hekalu ni nyumba ya Bwana.

Baada ya kuwarudi kwa kutokuijenga nyumba ya Bwana huko Kirtland, viongozi wa Kanisa walitafuta eneo kwenye shamba la ngano ambapo wangejenga. Hyrum Smith, Kaka wa Nabii, haraka alikimbia kuchukua fyekeo kuanza kulishafisha shamba. “Tunatayarisha kuijenga nyumba kwa ajili ya Bwana,” alisema, “na nimekusudia kuwa wa kwanza kazini” (katika Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith [2007], 271, 273). Ni kwa nini unadhani Hyrum ilikuwa na ari sana ya kujenga hekalu? Tafakari hili unaposoma, Mafundisho na Maagano 95:8, 11–17; 97:10–17.

Katika siku yetu, Bwana “anaharakisha kasi ambayo kwayo tunajenga mahekalu” (Russell M. Nelson, “Fokasi kwenye Hekalu,” Liahona, Nov. 2022, 121). Kama mtu angekuuliza kwa nini Kanisa ya Yesu Kristo linajenga mahekalu mengi hivi, ungesema nini? Tafuta majibu yamkini katika:

5:40

What Is a Temple?

The difference between chapels, where Latter-day Saints meet for regular Sunday worship, and temples is also explained.

Ungeweza kulinganisha juhudi za Watakatifu za kujenga Hekalu la Kirtland na juhudi zako za kujiandaa kwa ajili ya uzoefu wenye maana ukiwa na Bwana katika hekalu. Ni kwa jinsi unaweza kuonesha hali hiyo hiyo ya haraka ambayo Hyrum Smith aliihisi juu ya nyumba takatifu ya Bwana? Kwa mfano, ni kipi ungeweza kufanya ambacho kingekuwa kama kusafisha shamba, kama Hyrum alivyofanya? Ni dhabihu zipi unahisi Bwana anakutaka wewe ufanye? (ona Mafundisho na Maagano 97:12).

Ona pia “Mahekalu Matakatifu juu ya Mlima Sayuni,” Nyimbo za Dini, na. 162; Topics and Questions, “Temples,” Maktaba ya Injili.

mkulima akivuna

Hyrum Smith akisafisha ardhi kwa ajili ya Hekalu la Kirtland.

Mafundisho na Maagano 97:8–9

“Wanakubaliwa kwangu.”

Fikiria juu ya wakati ulipokubalika—au kutokubalika—kwenye kundi au timu. Ni kwa jinsi gani hilo ni sawa au ni tofauti na kile Mafundisho na Maagano 97:8–9 inachokifundisha kuhusu kile inachomaanisha kukubaliwa na Bwana? Ni kipi unadhani Bwana anajaribu kukufundisha kwenye sitiari hii katika mstari wa 9?

Ona pia Erich W. Kopischke, “Kukubaliwa na Bwana,” Liahona, Mei 2013, 104–6.

Tengeneza mazingira ya kiroho kwa ajili ya kujifunza na kufundisha. “Roho Mtakatifu,” Yesu aliahidi, “atawafundisha yote” (Yohana 14:26). Kwa hiyo iwe unajifunza mwenyewe au pamoja na wengine, fanya kumwaalika Roho kuwe kipaumbele. Muziki mtakatifu, sala, na michangamano yenye upendo inaweza kusaidia kutengeneza mazingira ya amani ya kiroho ambapo Roho Mtakatifu anaweza kukufundisha ukweli.

Mafundisho na Maagano 97:18–28

Sayuni ni “walio safi moyoni.”

Kwa Watakatifu mnamo miaka ya 1830, Sayuni ilikuwa ni mahali. Katika ufunuo kwenye sehemu ya 97, Bwana alipanua wigo wa ufafanuzi huu kuelezea watu—“walio safi moyoni” (mstari wa 21). Unaposoma mstari wa 18–28, ungeweza kubadili ufafanuzi huu wakati unaposoma neno Sayuni. Inamaanisha nini kwako kuwa safi moyoni?

Ona pia Musa 7:18.

Kwa mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la majarida ya Liahona na Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana

ikoni ya 02 ya sehemu ya watoto

Mawazo kwa ajili ya Kuwafundisha Watoto

Mafundisho na Maagano 95:8; 97:10–17

Hekalu ni nyumba ya Bwana.

  • Kwa ajili ya historia juu ya sehemu ya 95 na 97, ungeweza kushiriki na watoto wako “Hekalu la Kirtland” katika Hadithi za Mafundisho na Maagano kwa ajili ya Wasomaji Wadogo (Maktaba ya Injili; ona pia Saints, 1:210). Watoto wako wangeweza kufurahia kujifanya wanasaidia kujenga Hekalu la Kirtland (kukata miti, kupigilia misumari, kupaka rangi kuta, na kadhalika). Ungeweza pia kuwaonesha picha ya Hekalu la Kirtland, kama zile zilizopo katika muhtasari huu, wakati mkisoma Mafundisho na Maagano 95:8 ili kuwafundisha watoto wako kwa nini Bwana anatutaka tujenge mahekalu.

1:17

The Kirtland Temple

  • Baada ya kusoma pamoja Mafundisho na Maagano 97:15–16, wewe na watoto wako mngeweza kushiriki mmoja na mwingine kwa nini hekalu ni maalumu kwenu. Mngeweza pia kuimba pamoja wimbo ili kuwasaidia watoto wako wahisi staha kwa ajili ya nyumba ya Bwana, kama vile “I Love to See the Temple” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 95). Ni kwa nini hekalu ni takatifu?

Mafundisho na Maagano 97:1–2, 8–9, 21

Sayuni ni “walio safi moyoni.”

  • Ili kuwasaidia watoto wako waelewe kile neno safi linachoweza kumaanisha katika Mafundisho na Maagano 97:21, mngeweza kuangalia glasi ya maji safi pamoja na mkaongeza kitu ndani ya maji ambacho kinayafanya yawe machafu (kama vile mchanga au pilipili). Kwa nini ni muhimu kwa maji kuwa masafi? Kisha watoto wako wangeweza kusoma mstari wa 21 na kuweka vidole vyao kwenye neno safi. Inamaanisha nini kwa mioyo yetu kuwa safi? Mstari wa 1–2 na 8–9 ingeweza kukupa baadhi ya mawazo. Ni jinsi gani Mwokozi anasaidia kuifanya mioyo yetu iwe safi?

maji machafu na maji safi

Baba wa Mbinguni ananitaka niwe safi moyoni.

Mafundisho na Maagano 97:8–9

Bwana huwabariki watu ambao wanashika maagano na Yeye.

  • Je, watoto wako wanajua ni maagano yapi tunafanya na Bwana wakati tunapobatizwa au ndani ya hekalu? Zingatia kupitia tena maagano hayo pamoja nao kwa kusoma Mosia 18:9–10 au Kitabu cha Maelezo Jumla, 27:2. Shirikini mmoja na mwingine jinsi mnavyojitahidi “kuyatunza maagano [yenu] kwa dhabihu” (Mafundisho na Maagano 97: 8).

  • Ungeweza kuwaalika watoto wako wachore picha za kile Mafundisho na Maagano 97:9–16 inachokieleza. Wanaposhiriki picha zao, zungumza kuhusu jinsi ambavyo Bwana amekubariki kwa kuyatunza maagano yako. Ni kwa jinsi baraka hizo ni kama kuwa “mti wenye matunda ambao umepandwa … karibu na kijito safi”?

Kwa mawazo zaidi, ona toleo la mwezi huu la jarida la Rafiki.

ujenzi wa Hekalu la Kirtland

Kujenga Hekalu la Kirtland, na Walter Rane

ukurasa wa shughuli kwa ajili ya watoto