Fokasi kwenye Hekalu
Ninaahidi kwamba kutumia muda mwingi katika hekalu kutabariki maisha yako katika njia ambazo hakuna chochote kinaweza.
Akina kaka na dada wapendwa, wakati wa vikao hivi vitano vya kuvutia vya mkutano mkuu, tumepata uzoefu tena kwamba mbingu zi wazi! Natumaini kwamba mmerekodi misukumo yenu na mtaendelea kuifuata misukumo hiyo. Baba yetu wa Mbinguni na Mwanawe Mpendwa, Yesu Krito, wako tayari kukusaidia. Ninawasihi kuongeza jitihada zenu za kutafuta msaada Wao.
Hivi karibuni, Mimi pamoja na Dada Nelson tulikuwa na fursa ya kupitia toleo jipya la 4 la mwendelezo wa Video za Kitabu cha Mormoni.1 Tulipendezwa nazo! Ngoja niwaonyeshe dondoo fupi kutoka kwenye tukio ikionyesha kutokeza kwa Mwokozi kwa Wanefi.
Ni muhimu kwamba Mwokozi alichagua kuwatokea watu kwenye hekalu. Ni nyumba Yake. Imejazwa na nguvu Zake. Hebu tusipoteze mwelekeo wa kile Bwana anachotutendea. Anafanya mahekalu yake yafikike zaidi. Yeye anaongeza kasi ya sisi kujenga mahekalu. Anaongeza uwezo wetu wa kusaidia kukusanya Israeli. Pia anafanya iwe rahisi kwa kila mmoja wetu kutakaswa kiroho. Ninaahidi kwamba kutumia muda mwingi katika hekalu kutabariki maisha yako katika njia ambazo hakuna chochote kinaweza.
Kwa sasa tuna mahekalu 168 yanayofanya kazi na mapya 53 yanayojengwa, na mengine 54 katika hatua za usanifu kwa ajili ya kujengwa! 2 Nina furaha kutangaza mipango yetu ya kujenga hekalu jipya katika moja ya maeneo yafuatayo: Busan, Korea; Naga, Ufilipino; Santiago, Ufilipino; Eket, Nigeria; Chiclayo, Peru; Buenos Aires City Center, Argentina; Londrina, Brazil; Ribeirão Prêto, Brazil; Huehuetenango, Guatemala; Jacksonville, Florida; Grand Rapids, Michigan; Prosper, Texas; Lone Mountain, Nevada and Tacoma, Washington.
Pia tunapanga kujenga mahekalu mengi katika sehemu za majiji makubwa zilizochaguliwa ambapo muda wa kusafiri kufika kwenye hekalu lililopo ni changamoto kubwa. Kwa hiyo, ninayo furaha kutangaza maeneo manne ya ziada karibu na Jiji la México ambapo mahekalu mapya yatajengwa huko Cuernavaca, Pachuca, Toluca and Tula.
Wapendwa akina kaka na dada zangu, muendelee kufokasi kwenye hekalu katika njia ambazo hujawahi hapo kabla. Ninawabariki ili msonge karibu na Mugu na Yesu Kristo kila siku. Ninawapenda. Mungu awe nanyi mpaka tutakapokutana tena, ninaomba katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.