Mkutano Mkuu
Kuwakubali Viongozi Wakuu wenye Mamlaka, Sabini wa Eneo, na Maafisa Wakuu
mkutano mkuu wa Oktoba 2022


4:35

Kuwakubali Viongozi Wakuu wenye Mamlaka, Sabini wa Eneo, na Maafisa Wakuu

Akina kaka na akina dada, ni heshima kwangu kuwasilisha kwenu Viongozi Wakuu Wenye Mamlaka, Sabini wa Eneo, na Maafisa Wakuu wa Kanisa kwa ajili ya kura yenu ya kuwakubali.

Tafadhali onesha kukubali kwako katika njia iliyozoeleka po pote ulipo. Kama kuna wale wanaopinga mapendekezo yo yote, tunaomba kwamba muwasiliane na rais wenu wa kigingi.

Inapendekezwa kwamba tumkubali Russell Marion Nelson kama nabii, mwonaji, na mfunuzi na Rais wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho; Dallin Harris Oaks kama Mshauri wa Kwanza katika Urais wa Kwanza; na Henry Bennion Eyring kama Mshauri wa Pili katika Urais wa Kwanza.

Wale wanaounga mkono, waoneshe.

Wale wanaopinga, kama wapo, wanaweza kuonesha.

Inapendekezwa kwamba tumkubali Dallin H. Oaks kama Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili na M. Russell Ballard kama Kaimu Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili.

Wale wanaounga mkono, tafadhali onesheni.

Yeyote anayepinga anaweza kuonesha.

Inapendekezwa kwamba tuwakubali wafuatao kama washiriki wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili: M. Russell Ballard, Jeffrey R. Holland, Dieter F. Uchtdorf, David A. Bednar, Quentin L. Cook, D. Todd Christofferson, Neil L. Andersen, Ronald A. Rasband, Gary E. Stevenson, Dale G. Renlund, Gerrit W. Gong, na Ulisses Soares.

Wale wanaounga mkono, tafadhali onesheni.

Yeyote anayepinga anaweza kuonyesha.

Inapendekezwa kwamba tuwakubali washauri katika Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili kama manabii, waonaji, na wafunuzi.

Wote wanaounga mkono, tafadhali onesheni.

Kinyume, kama kuna yeyote, kwa ishara hiyo hiyo.

Tumewapumzisha Wazee Weatherford T. Clayton, LeGrand R. Curtis Jr., Randy D. Funk, Christoffel Golden, Walter F. González, Larry S. Kacher, Lynn G. Robbins, na Joseph W. Sitati kama Sabini wenye Mamlaka na kuwapa hadhi ya kuendelea na heshima hiyo.

Wale ambao wangependa kuonyesha shukrani kwa viongozi hawa na kwa wake zao na familia zao kwa miaka mingi ya kujitolea katika utumishi wanaweza kufanya hivyo kwa kuinua mkono juu.

Pia tunatambua kwa shukrani, Sabini wa Eneo ambao wamemaliza huduma yao mwaka huu uliopita na ambao majina yao yanaweza kupatikana katika newsroom.Churchof JesusChrist.org.

Wale wanaotaka kuungana pamoja nasi katika kuonyesha shukrani zetu kwa ndugu hawa kwa huduma yao bora wanaweza kuonyesha.

Inapendekezwa kwamba tuwakubali Viongozi Wakuu Wenye Mamlaka wengine, Sabini wa Eneo—ikijumuisha Sabini wa Eneo sita wapya waliotangazwa mapema wiki hii kwenye newsroom.ChurchofJesusChrist.org—na Maafisa Wakuu kama ilivyo sasa.

Wote wanaounga mkono, tafadhali onesheni kwa kuinua mkono.

Wale wanaopinga, ikiwa kuna yeyote.

Tunawashukuru, akina kaka na akina dada kwa imani na sala zenu endelevu kwa niaba ya viongozi wa Kanisa.

Mabadiliko kwa Sabini wa Eneo

Sabini wa Eneo wafuatao waliidhinishwa wakati wa kikao cha uongozi kilichofanyika kama sehemu ya mkutano mkuu:

Ricardo J. Battista, Willy Binene, Bernhard Cziesla, Nathan R. Emery, Sione Tuione, Yves S. Weidmann.

Sabini wa Eneo wafuatao walipumzishwa mnamo Agosti 1, 2022:

Luis R. Arbizú, Michael V. Beheshti, David A. Benalcázar, Berne S. Broadbent, Kevin E. Calderwood, Luciano Cascardi, Ting Tsung Chang, Ariel E. Chaparro, Pablo H. Chavez, Raymond A. Cutler, José L. Del Guerso, Alessandro Dini Ciacci, Carlos R. Fusco Jr., Jorge A. García, Gary F. Gessel, Karl D. Hirst, Ren S. Johnson, Jay B. Jones, Paul N. Lekias, Artur J. Miranda, Elie K. Monga, A. Fabio Moscoso, Yutaka Nagatomo, Juan C. Pozo, Anthony Quaisie, Martin C. Rios, Sandino Roman, Johnny F. Ruiz, Rosendo Santos, Gordon H. Smith, K. Roy Tunnicliffe.

Mzee Levi W. Heath na Mzee Inoke F. Kupu, ambao walikuwa wakitumikia kama Sabini wa Eneo, waliaga dunia katika mwaka 2022.