Njoo, Unifuate
Agosti 26–Septemba 1. 1 Wakorintho 8–13: ‘Ninyi Mmekuwa Mwili wa Kristo’


“Agosti 26–Septemba 1. 1 Wakorintho 8–13: “Ninyi Mmekuwa Mwili wa Kristo’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya (2019)

Agosti 26–Septemba 1. 1 Wakorintho 8–13,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2019

mkutano wa sakramenti

Agosti 26–Septemba 1

1 Wakorintho 8–13.

“Ninyi Mmekuwa Mwili wa Kristo”

Kwa maombi unaposoma 1 Wakorintho 8–13, Roho Mtakatifu anaweza kuongea nawe katika njia za utulivu (ona 1 Wafalme 19:11–12). Kuandika misukumo hii kutakusaidia kukumbuka hisia na mawazo uliyopata wakati wa kujifunza kwako.

Andika Misukumo Yako

Wakati wa Paulo, Korintho ilikuwa kitovu tajiri cha biashara ikiwa na wakazi kutoka maeneo yote ya Ufalme wa Rumi. Kwa tamaduni nyingi na madhehebu tofauti katika mji, waumini wa Kanisa katika Korintho walipata taabu kudumisha umoja, hivyo Paulo alitafuta kuwasaidia kupata umoja katika imani yao katika Kristo. Umoja huu ulipaswa kuwa zaidi ya kuishi pamoja kwa amani; Paulo hakuwa akiwaomba tu kuvumilia tofauti za kila mmoja. Bali, alifundisha kwamba unapojiunga na Kanisa la Yesu Kristo “unabatizwa kuwa mwili mmoja,” na kila kiungo cha mwili kinahitajika (1 Wakorintho 12:13). Muumini mmoja anapopotea, ni kama kupoteza kiungo, na mwili huwa dhaifu kama matokeo yake. Muumini mmoja anapoteseka, wote tunapaswa kuhisi mateso na kufanya sehemu yetu ili kuyapunguza. Katika aina hii ya umoja, tofauti siyo tu zinatambuliwa bali huifadhiwa kwa upendo mkubwa, kwa sababu bila waumini wenye karama na uwezo tofauti, mwili ungekuwa na uwezo mdogo. Hivyo kama unahisi kwamba daima umekuwa nyumbani ndani ya Kanisa au umejikuta unajiuliza kama kweli unastahili kuwa hapo, ujumbe wa Paulo kwako ni kwamba umoja siyo usawa. Unawahitaji Watakatifu wenzako, na Watakatifu wenzako wanakuhitaji.

ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo ya Kujifunza Maandiko Binafsi

1 Wakorintho 10:1–13

Mungu hutoa njia ya kuponyoka majaribu.

Uzoefu wa Kiroho, hata ule wa kimiujiza, hautupi msamaha wa majaribu ambayo ni “kawaida ya mwanadamu” (1 Wakorintho 10:13). Hiyo yaweza kuwa sababu moja ambayo Paulo aliandika kuhusu jinsi Waisraeli katika siku ya Musa walivyohangaika na majaribu, japokuwa walishuhudia miujiza mikuu (ona Kutoka 13:21; 14:13–31). Unaposoma 1 Wakorintho 10:1–13, ni maonyo gani katika uzoefu wa Waisraeli yanaonekana kutumika kwako? Je, ni aina gani ya “mlango” wa kuyatoroka majaribu ambao Baba wa Mbinguni ameuweka kwa ajili yako? (Ona pia Alma 13:27–30; 3 Nefi 18:18–19).

1 Wakorintho 10:16–17; 11:16–30

Sakramenti hutuunganisha kama wafuasi wa Kristo.

Japokuwa ibada ya sakramenti hujumuisha ahadi binafsi kati ya mtu na Bwana, lakini pia ni tukio ambalo tunashiriki na wengine—karibu wakati wote tunapokea sakramenti pamoja, kama mwili wa Watakatifu. Soma kile ambacho Paulo alifundisha kuhusu sakramenti, na fikiria kuhusu jinsi gani ibada hii takatifu inaweza kuwasaidia “wengi” kuwa “wamoja” katika Kristo (1 Wakorintho 10:17). Ni kwa jinsi gani unaweza kuvuta nguvu kutokana na kupokea sakramenti pamoja na waaminio wengine? Ni kwa jinsi gani hii hushawishi jinsi wewe unavyojiandaa kwa sakramenti na jinsi unavyojitahidi kushika maagano yako ya ubatizo?

1 Wakorintho 11:3–15

Kwa nini Paulo aliandika kuhusu kufunika vichwa na mitindo ya nywele?

Paulo alirejea kwenye mila za kitamaduni za mavazi na unadhifu ili kufundisha kuhusu mahusiano kati ya wanaume, wanawake, na Bwana. Ingawa hatufuati mila hizi leo, bado tunaweza kujifunza kutoka kwenye tamko la Paulo katika 1 Wakorintho 11:11 kwamba wanaume na wanawake wote wanahitajika katika mpango wa Bwana, wote katika ndoa na katika kanisa. Kama Mzee David A.Bednar alivyofundisha, “Mwanaume na mwanamke wanakusudiwa kujifunza kutoka kwa, kuimarisha, kubariki, na kukamilishana kila mmoja” wanapokua pamoja kuelekea kuinuliwa (“Tunaamini katika Kuwa Wasafi,” Ensign au Liahona, Mei, 2013, 42; ona pia Marko 10:6–9).

1 Wakorintho 12–13

Karama za kiroho hutolewa ili kuwanufaisha watoto wote wa Baba wa Mbinguni.

Orodha ya karama za kiroho katika 1 Wakorintho 12–13 siyo kamilifu. Lakini ni mahala pazuri pa kuanzia unapogundua na kutafakari karama za kiroho Baba wa Mbinguni alizokupatia. Makala “Karama za Kiroho” katika Mada za Injili (topics.lds.org) inaweza kukusaidia kuelewa karama hizi vizuri zaidi. Unaweza kuongeza kwenye orodha ya Paulo karama ulizogundua kwa wengine, au kwa watu katika maandiko. Kama una baraka za baba mkuu, inaweza pia kutaja baadhi ya karama zako za kiroho. Ni kwa jinsi gani karama hizi hutusaidia kujenga ufalme wa Mungu? Fikiria nini utafanya kutaka “sana karama zilizo kuu” (1 Wakorintho 12:31).

Ona pia Moroni 10:8–21, 30; Mafundisho na Maagano 46:8–26; Makala ya Imani 1:7.

ikoni  ya kujifunza kifamilia.

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Familia Nyumbani.

Unaposoma maandiko na familia yako, tafuta mwongozo wa kiungu ili kukidhi mahitaji ya familia yako. Mapendekezo yafuatayo yanaweza kusaidia:

1 Wakorintho 9:24–27

Kwa kuwa Paulo alilinganisha kuishi injili na mashindano ya mbio, unaweza kuwa na mbio za familia kuelezea kwa mfano hoja yake. Toa taji kwa kila mtu anayemaliza mbio, na jadili ni kwa jinsi gani wote wenye bidii katika kumfuata Yesu Kristo katika maisha haya hupokea zawadi “isiyoharibika” (1 Wakorintho 9:25; ona pia 2 Timotheo 4:7–8). Je, bingwa wa mbio anaweza kufanya nini ili kujiandaa kwa mbio? Kadhalika, sisi tunaweza kufanya nini ili kujiandaa kurudi kwa Baba wa Mbinguni?

wakimbiaji uwanjani

Paulo alifananisha kuishi injili na mashindano ya mbio.

1 Wakorintho 12:1–11

Fikiria kumpa kila mtu kipande cha karatasi kikiwa na jina la mwanafamilia mwingine juu yake. Waombe kila mmoja kuorodhesha karama za kiroho wanazogundua mtu yule anazo. Kisha mnaweza kupitisha karatasi katika duara mpaka kila mmoja amepata nafasi ya kuandika kuhusu karama za kila mwanafamilia.

1 Wakorintho 12:3.

Kwa nini Roho Mtakatifu ni muhimu katika kupata ushuhuda wa Yesu Kristo? Je, tunaweza kufanya nini katika kumualika Roho Mtakatifu ili kuimarisha shuhuda zetu kwake Yeye?

1 Wakorintho 12–27

Analojia ya Paulo ya mwili inaweza kuwa ni njia ya kukumbukwa kujadili umoja wa familia. Kwa mfano, wanafamilia wanaweza kujaribu kuchora mwili uliotengenezwa na macho tu au masikio (ona mstari wa 17). Ni nini mistari hii hupendekeza kuhusu jinsi tunavyopaswa kutendeana kila mmoja kama wanafamilia?

1 Wakorintho 13:4–8

Ufafanuzi wa Paulo juu ya hisani unaweza kutengeneza wito wenye mwongozo wa kiungu kwa familia yako. Unaweza kumpangia kila mwanafamilia kujifunza kirai katika mstari 4–8 na kufundisha wanafamilia wengine umuhimu wa kutumia maana, mifano, na uzoefu binafsi. Je, ni kwa jinsi gani Mwokozi ni mfano wa sifa hizi? Mnaweza pia kutengeneza mabango pamoja kwa kila mojawapo ya virai na kuyaweka kuzunguka nyumba yenu. Kuwa mbunifu!

Kwa mawazo zaidi juu ya kufundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii ndani ya Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Onyesha andiko. Chagua mstari unaouona una maana, na ubandike mahali ambapo wanafamilia watauona mara kwa mara. Waalike wanafamilia wengine kuchukua zamu ya kuchagua andiko la kubandika.

mkutano wa sakramenti

“Mkate tunaomega, si ushirika wa mwili wa Kristo? Kwa kuwa sisi tulio wengi tu mkate mmoja, na mwili mmoja” (1 Wakorintho 10:16–17).