Njoo, Unifuate
Septemba 23–29. Wagalatia: ‘Enendeni kwa Roho’


“Septemba 23–29. Wagalatia: ‘Enendeni kwa Roho’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya 2019 (2019)

“Septemba 23–29. Wagalatia,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2019

Kristo akimtokea Paulo gerezani

Septemba 23–29

Wagalatia

“Enendeni kwa Roho”

Unaposoma Wagalatia, andika misukumo unayopokea. Kufanya hivyo kutakusaidia kuikumbuka na kuitafakari baadaye.

Andika Misukumo Yako

Injili ya Yesu Kristo hutoa uhuru kutoka kwenye utumwa wa kiroho. Lakini wakati mwingine watu ambao wamepata uzoefu wa uhuru wa injili hugeuka kutoka kwenye uhuru huo na “kutaka tena kuwa utumwani” (Wagalatia 4:9). Hiki ndicho baadhi ya Watakatifu wa Galatia walikuwa wakifanya—walikuwa wakigeuka kutoka kwenye uhuru Kristo aliowapatia (ona Wagalatia 1:6). Hivyo, waraka wa Paulo kwa Wagalatia, ulikuwa ni wito wa umuhimu wa wao kurudi “katika ungwana ambao Kristo alituandika huru” (Wagalatia 5:1). Wito huu ni ule ambao sisi pia tunahitaji kuusikia na kuufuata kwa sababu wakati hali zinapobadilika, vita kati ya uhuru na utumwa iko pale pale. Kama Paulo alivyofundisha, haitoshi “kuitwa kupata uhuru” (Wagalatia 5:13); lazima pia “tusimame imara” katika uhuru huo (Wagalatia 5:1) kwa kumtegemea Kristo.

ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo ya Kujifunza Maandiko Binafsi

Wagalatia 1–5

Sheria ya Kristo huniweka huru.

Paulo aliwaandikia Watakatifu wa Galatia alipogundua walikuwa wakipotoshwa kwa mafundisho ya uongo. Moja ya mafundisho haya ilikuwa kwamba ili kuokolewa, Wayunani walioipokea injili walihitajika kutahiriwa na kushika tamaduni zingine za sheria ya Musa. Paulo aliziita tamaduni hizi “kongwa la utumwa” (Wagalatia 5:1) kwa sababu zilikuwa zikiwazuia Watakatifu kuishi sheria ya Kristo kikamilifu, ambayo huleta uhuru wa kweli. Je, unapata nini katika ushauri wa Paulo kwa Wagalatia ambacho kinaweza kukusaidia kuelewa uhuru wa kweli ni nini? Unaweza pia kutafakari ni kongwa zipi za utumwa zinaweza kuwepo katika maisha yako. Je, kuna kitu cho chote ambacho kinaweza kukuzuia kupata uzoefu wa uhuru ambao injili hutoa? Ni kwa jinsi gani Kristo na injili Yake “vimekufanya [wewe] huru”? (Wagalatia 5:1).

Ona pia 2 Nefi 2:27; 9:10–12.

Wagalatia 3

Mimi ni mrithi kwa baraka alizoahidiwa Ibrahimu.

Baadhi ya Watakatifu wa Galatia wahuzunika kwamba kwa sababu hawakuwa ukoo halisi (“uzao”) wa Ibrahimu, hawangepokea baraka alizoahidiwa Ibrahimu, ikiwemo zile za kuinuliwa. Kulingana na Wagalatia 3:7–9, 13–14, 27–29, nini humpa mtu sifa za kuwa “uzao wa ibrahimu”? Kujifunza kuhusu baraka alizoahidiwa Ibrahimu na baraka ambazo tunaweza kurithi kama uzao wake, ona Kamusi ya Biblia, “Ibrahimu, agano la,” na “Agano la Ibrahimu,” Mada za Injili, topics.lds.org.

Wagalatia 3:6–25

Je, Ibrahimu alikuwa na injili ya Yesu Kristo?

Nabii Joseph Smith alielezea: “Sisi hatuwezi kuamini, kwamba watu wa kale katika vipindi vyote hawakuwa na ufahamu wa utaratibu wa mbinguni kama wengi wanavyodhani, kwani yote yaliyokuwa yamehifadhiwa, yalihifadhiwa kupitia nguvu ya mpango huu mkuu wa ukombozi, kama vile kabla ya kuja kwa Kristo kama hadi wakati huo. … Ibrahimu alitoa dhabihu, na licha ya hili, Injili ilihubiriwa kwake” (“Wazee wa Kanisa katika Kirtland kwa Ndugu Zao Ugenini,” The Evening and the Morning Star, Mar. 1834, 143, josephsmithpapers.org). Maandiko yafuatayo pia huonyesha kwamba injili ya Yesu Kristo ilihubiriwa kabla ya huduma ya Mwokozi duniani: Helamani 8:13–20; Musa 6:50–66.

Wagalatia 5:13–26; 6:7–10

Kama “nikienenda kwa Roho” Nitapokea “tunda la Roho.”

Kujifunza mistari hii kunaweza kukusaidia kujichunguza jinsi gani unaenenda kikamilifu kwa Roho. Je, unaliona katika maisha yako tunda la Roho lililotajwa katika mistari 22–23? Ni tunda gani lingine, au matokeo mengine, ya kuishi kiroho umeyagundua? Tafakari kile unachohitaji kufanya ili kulilimia tunda hili kikamilifu zaidi. Je, ni kwa jinsi gani kulilimia tunda hili kunaboresha uhusiano muhimu katika maisha yako?

matufaha juu ya mti

Lazima nitafute “tunda la Roho” katika maisha yangu.

Pengine unajaribu kuenenda kwa Roho, lakini haionekani kama juhudi zako zinazaa tunda lililoahidiwa. Soma Wagalatia 6:7–10 (mara nyingi ikijulikana kama sheria ya mavuno). Je, ni ujumbe gani unahisi Bwana alionao kwako katika mistari hii? Je, ni kwa jinsi gani wewe unaweza kutumia mistari hii kumtia moyo mtu anayehangaika kuishi injili?

Ona pia Alma 32:28, 41–43; Mafundisho na Maagano 64:32–34.

ikoni  ya kujifunza kifamilia.

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Familia Nyumbani.

Unaposoma maandiko na familia yako, Roho anaweza kukusaidia kujua kanuni zipi zisisitizwe na kujadiliwa ili kukidhi mahitaji ya familia yako. Hapa kuna baadhi ya mapendekezo:

Wagalatia 3:11

Je, inamaanisha nini “kuishi kwa imani”? Je, familia yako inafanya nini ili kuonyesha kwamba mnaishi kwa imani?

Wagalatia 4:1–7

Unaweza kutambulisha Wagalatia 4 kwa kujadili tofauti kati ya watumwa wa mfalme na watoto wake. Je, ni fursa zipi au uwezekano ambao mtoto wa mfalme anazo ambazo mtumwa hana? Fikirieni kuhusu hili mnaposoma pamoja mistari 1–7. Je, mistari hii hufundisha nini kuhusu uhusiano wetu na Baba wa Mbinguni?

Wagalatia 5:22–23

Ili kuongeza viburudisho katika majadiliano yenu ya Wagalatia 5:22–23, familia yako inaweza kubandika nembo kwenye matunda tofauti kwa kutumia maneno ya Paulo kuelezea “tunda la Roho.” Kisha kila mwanafamilia anaweza kuchagua moja, kulitolea ufafanuzi, na kumzungumza juu ya mtu ambaye ana sifa mfano wa lile tunda. Hii inaweza kuwapeleka kwenye mjadala kuhusu njia ambazo familia yako inaweza kumualika Roho katika nyumba yenu na kulilimia tunda hili. Baada ya mjadala, mnaweza kufurahia saladi ya matunda pamoja.

Wagalatia 6:1

Kunaweza kuwepo nyakati ambazo mmoja katika familia yako “ameghafilika katika kosa.” Ni ushauri gani unaupata katika Wagalatia 6:1 kuhusu nini cha kufanya katika hali kama hiyo?

Wagalatia 6:7–10

Kama familia yako mmewahi kupanda kitu kwa pamoja, mnaweza kutumia uzoefu huo kuelezea kwa mfano kanuni “chochote apandacho mtu, ndicho atakachovuna” (mstari wa 7). Au unaweza kuwauliza wanafamilia kuhusu matunda au mboga wanazopenda sana na zungumza kuhusu nini kinahitajika kukuza mmea unaozaa chakula kile. (Unaweza kutumia picha ambayo huambatana na muhtasari huu kama kielelezo.) Kisha mnaweza kuwa na maongezi kuhusu baraka ambazo familia yako inatumaini kupokea na jinsi ya “kuvuna” baraka hizo.

Kwa mawazo zaidi juu ya kufundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii ndani ya Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Wasaidie familia yako wayalinganishe maandiko na wao wenyewe. Nefi alisema, “Nililinganisha maandiko yote nasi, ili yatufaidishe na kutuelimisha” (1  Nefi 19:23). Ili kuisaidia familia yako kufanya hili, unaweza kuwaalika kutafakari nyakati walipopata uzoefu wa tunda la Roho lililoelezewa katika Wagalatia 5:22–23. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 21.)

mapea juu ya mti

Paulo alifundisha kwamba tunapoenenda kwa Roho, tutapata uzoefu wa tunda la Roho katika maisha yetu.