Agano Jipya 2023
Mei 1–7. Luka 12–17; Yohana 11: “Furahini pamoja Nami; kwa kuwa Nimekwisha Kumpata Kondoo Wangu Aliyepotea”


“Mei 1–7. Luka 12–17; Yohana 11: ‘Furahini pamoja Nami; kwa kuwa Nimekwisha Kumpata Kondoo Wangu Aliyepotea’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya 2023 (2022)

“Mei 1–7. Luka 12–17; Yohana 11,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia:2023

Picha
mtu akimkumbatia mwanawe

Mwana Mpotevu, na Liz Lemon Swindle

Mei 1–7

Luka 12–17; Yohana 11

“Furahini pamoja Nami; kwa kuwa Nimekwisha Kumpata Kondoo Wangu Aliyepotea”

Unaposoma Luka 12–17 na Yohana 11, kwa maombi tafuta kile ambacho Baba wa Mbinguni anakutaka ujue na ufanye. Kujifunza kwako sura hizi kunaweza kufungua moyo wako kwenye jumbe zilizokusudiwa kwa ajili yako tu.

Andika Misukumo Yako

Katika hali nyingi, 99 kati ya 100 wangeweza kufikiriwa kuwa bora sana—lakini siyo wakati idadi kama hizo husimamia watoto wapendwa wa Mungu (ona Mafundisho na Maagano 18:10). Kama ni hivyo, hata nafsi moja hustahili kwa ukamilifu, kutafutwa “mpaka [sisi] tuipate” (Luka 15:4), kama Mwokozi alivyofundisha katika fumbo la kondoo aliyepotea. Ndipo kushangilia kunaweza kuanza, kwani “kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa ajili ya wenye haki tisini na kenda, ambao hawana haja ya kutubu” (Luka 15:7). Kama hilo linaonekana si sawa, itasaidia kukumbuka kwamba, katika ukweli, hakuna yeyote ambaye “hahitaji toba.” Sote tunahitaji kuokolewa. Na wote tunaweza kushiriki katika kuokoa, kufurahi pamoja juu ya kila nafsi inayookolewa (ona Mafundisho na Maagano 18:15–16).

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa Ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

Luka 12; 14–16

Ninabarikiwa pale ninapouweka moyo wangu juu ya mambo ya milele.

Kwa nini Mungu aseme “Mpumbavu wewe” kwa mchapakazi, mwenye mafanikio ambaye alijenga maghala makubwa na kuyajaza matunda ya kazi zake? (ona Luka 12:16–21). Katika sura hizi katika Luka, Mwokozi anafundisha mifano kadhaa inayoweza kutusaidia sisi kuinua mtazamo wetu kupita mambo ya ulimwengu kwenda umilele. Baadhi ya mafumbo haya yameorodheshwa hapa. Ni kwa jinsi gani unaweza kufanyia muhtasari ujumbe wa kila fumbo? Unafikiri Bwana anakuambia nini?

Ona pia Mathayo 6:19–34; 2 Nefi 9:30; Mafundisho na Maagano 25:10.

Luka 15

Baba wa Mbinguni hufurahia wakati wale waliopotea wanapopatikana.

Unaposoma mafumbo Yesu aliyofundisha katika Luka 15, unajifunza nini kuhusu jinsi Baba wa Mbinguni anavyohisi kuhusu wale waliotenda dhambi au kwa upande mwingine “waliopotea”? Je, ni kwa jinsi gani kiongozi wa kiroho—au yeyote kati yetu anapaswa kuhisi juu yao? Fikiria, ni kwa namna gani Mafarisayo na waandishi wangejibu maswali haya (ona Luka 15:1–2). Majibu ya Yesu yanaweza kupatikana katika haya mafumbo katika Luka 15. Unaposoma, fikiria kuhusu kile Yesu alichokuwa anawafundisha waandishi na Mafarisayo katika mafumbo haya.

Ungeweza pia kufikiria kutengeneza orodha ya mifanano na tofauti kati ya mafumbo haya. Kwa mfano, unaweza kutambua kile kilichopotea na kwa nini kilipotea, jinsi kilivyopatikana, na jinsi watu walivyofanya wakati kilipopatikana. Ni jumbe gani Yesu alikuwa nazo kwa wale “waliopotea”—ikijumuisha wale ambao hawadhani kuwa wamepotea? Ni jumbe gani alikuwa nazo kwa watu wanaowatafuta wale waliopotea?

Ona pia Mafundisho na Maagano 18:10–16; Jeffrey R. Holland, “Mwana Mpotevu Mwingine,” Ensign, Mei 2002, 62–64.

Picha
mwanamke akitafuta sarafu

Fedha Moja Iliyopotea, na James Tissot

Luka 16:1–12

Ni nini Kristo alikuwa akifundisha katika fumbo la wakili dhalimu?

Mzee James E. Talmage alielezea somo moja tunaloweza kujifunza kutoka kwenye fumbo hili: “Kuwa mwenye bidii; kwani siku ambayo unaweza kutumia utajiri wako wa duniani i karibu kupita. Chukua funzo hata kutoka kwa wasio waaminifu na waovu; kama wana busara ya kujiandaa kwa ajili ya wakati ujao wanaoweza tu kuufikiria, jinsi gani zaidi unapaswa wewe, wewe unayeamini katika milele ijayo, kujiandaa kwa ajili ya hiyo! Kama hujajifunza hekima na busara katika matumizi ya ‘utajiri usio wa haki,’ ni kwa jinsi gani unaweza kuaminiwa na utajiri wenye kudumu zaidi?” (Yesu Kristo [1916], 464). Ni masomo gani mengine unayoyapata katika fumbo hili?

Luka 17:11–19

Shukrani kwa ajili ya baraka zangu zitanisogeza karibu na Mungu.

Kama ungekuwa mmoja wa wenye ukoma kumi, unafikiri ungerudi kumshukuru Mwokozi? Ni baraka gani za ziada mkoma mwenye shukrani alipokea kwa sababu alitoa shukrani?

Pia ungeweza kutafakari maneno ya Mwokozi, “Imani Yako Imekuponya” (mstari wa 19). Kwa maoni yako, ni kwa jinsi gani shukrani na imani vinahusiana? Je, vyote vinatusaidiaje sisi kuponywa? Video “President Russell M. Nelson on the Healing Power of Gratitude” (ChurchofJesusChrist.org) inaweza kukusaidia kutafakari maswali haya.

Ona pia Dale G. Renlund, “Tafakari Wema na Ukuu wa Mungu,” Liahona, Mei 2020, 41–44

Yohana 11:1–46

Yesu Kristo ndiye Ufufuo na Uzima.

Muujiza wa kumfufua Lazaro kutoka wafu ulikuwa ni ushuhuda wa nguvu na dhahiri kwamba Yesu alikuwa kweli Mwana wa Mungu na Masiya aliyeahidiwa. Ni maneno gani, virai, au maelezo ya kina katika Yohana 11:1–46 huimarisha imani yako kwamba Yesu Kristo ndiye “ufufuo, na uzima”? Inamaanisha nini kwako kwamba Yesu ndiye “ufufuo, na uzima”?

Picha
ikoni ya kujifunza kama familia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko kama Familia na Jioni ya Nyumbani

Luka 15:1–10.Je, wanafamilia wako wanaelewa jinsi ilivyo kupoteza kitu—au kupotea? Kuzungumza kuhusu uzoefu wao kunaweza kuanzisha majadiliano kuhusu mafumbo ya kondoo aliyepotea na sarafu iliyopotea. Au mnaweza kucheza mchezo ambapo mmoja anajificha na wanafamilia wengine wanajaribu kumtafuta. Ni kwa jinsi gani shughuli hii inatusaidia kuelewa mafumbo haya?

Luka 15:11–32.Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwa kama baba katika hadithi hii wakati tunapokuwa na mpendwa aliyepotea? Tunaweza kujifunza nini kutokana na uzoefu wa kijana mkubwa kinachoweza kutusaidia kuwa zaidi kama Kristo? Ni kwa njia zipi baba katika fumbo hili ni kama Baba yetu wa Mbinguni?

Luka 17:11–19.Ili kuwasaidia wanafamilia kutumia hadithi hii ya wakoma kumi, unaweza kuwaalika waachiane ujumbe wa siri wa shukrani. Mnaweza pia kuimba pamoja “Hesabu Baraka Zako,” (Nyimbo za Kanisa, na. 241) na kujadili baraka ambazo familia yako imezipokea.

Yohana 11:1–46.Wanafamilia wanaweza kuangalia video “Lazarus Is Raised from the Dead” (ChurchofJesusChrist.org) na kushiriki shuhuda zao juu ya Yesu Kristo.

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “Dear to the Heart of the Shepherd,” Nyimbo za Kanisa, na. 221.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tumia hadithi na mifano kufundisha kanuni za injili. Mwokozi mara nyingi alifundisha kuhusu kanuni za injili kwa kutumia hadithi na mafumbo. Fikiria juu ya mifano na hadithi kutoka kwenye maisha yako mwenyewe ambazo zinaweza kufanya kanuni za injili kuwa hai kwa familia yako (ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi,22).

Picha
mtu akiwa amepiga magoti kwa shukrani mbele ya Yesu

Wako Wapi wale Kenda, na Liz Lemon Swindle

Chapisha