Agano Jipya 2023
Septemba 25–Oktoba 1. Wagalatia: “Enendeni kwa Roho”


Septemba 25–Oktoba 1. Wagalatia: ‘Enendeni kwa Roho’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya 2023 (2022)

Septemba 25–Oktoba 1. Wagalatia,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2023

Picha
Kristo akimtokea Paulo gerezani

Mwokozi aliyefufuka alimtembelea Paulo gerezani (ona Matendo 23:11). Yesu Kristo anaweza kutufanya huru kutokana na “kongwa la utumwa” (Wagalatia 5:1).

Septemba 25–Oktoba 1

Wagalatia

“Enendeni kwa Roho”

Unaposoma Wagalatia, andika misukumo unayopokea. Kufanya hivyo kutakusaidia kuikumbuka na kuitafakari baadaye.

Andika Misukumo Yako

Injili ya Yesu Kristo hutoa uhuru kutoka kwenye utumwa wa kiroho. Lakini wakati mwingine watu ambao wamepata uzoefu wa uhuru wa injili hugeuka kutoka kwenye uhuru huo na “kutaka tena kuwa utumwani” (Wagalatia 4:9). Hiki ndicho baadhi ya Watakatifu wa Galatia walikuwa wakifanya—walikuwa wakigeuka kutoka kwenye uhuru Kristo aliowapatia (ona Wagalatia 1:6). Hivyo, waraka wa Paulo kwa Wagalatia, ulikuwa ni wito wa umuhimu wa wao kurudi “katika ungwana ambao Kristo alituandika huru” (Wagalatia 5:1). Wito huu ni ule ambao sisi pia tunahitaji kuusikia na kuufuata kwa sababu wakati hali zinapobadilika, vita kati ya uhuru na utumwa iko pale pale. Kama Paulo alivyofundisha, haitoshi “kuitwa kupata uhuru” (Wagalatia 5:13); lazima pia “tusimame imara” katika uhuru huo (Wagalatia 5:1) kwa kumtegemea Kristo.

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa Ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

Wagalatia 1–5

Sheria ya Kristo huniweka huru.

Paulo aliwaandikia Watakatifu wa Galatia alipogundua walikuwa wakipotoshwa kwa mafundisho ya uongo (ona Wagalatia 1:6–9). Mojawapo ya mafundisho haya ilikuwa kwamba ili kuokolewa, Wayunani walioipokea injili walihitajika kutahiriwa na kushika tamaduni zingine za sheria ya Musa (ona Wagalatia 2). Paulo aliita tamaduni hizi kama “kongwa la utumwa” (Wagalatia 5:1). Unaposoma ushauri wa Paulo kwa Wagalatia, tafuta kanuni ambazo zinaweza kukusaidia kuelewa uhuru wa kweli ni nini. Unaweza pia kutafakari ni tamaduni zipi za uongo au makongwa mengine ya utumwa yanaweza kuwepo katika maisha yako. Je, kuna kitu chochote ambacho kinaweza kukuzuia kupata uzoefu wa uhuru ambao injili hutoa? Ni kwa jinsi gani Kristo na injili Yake “vimekufanya [wewe] uwe huru”? (Wagalatia 5:1).

Ona pia 2 Nefi 2:27; 9:10–12.

Wagalatia 3

Mimi ni mrithi kwa baraka alizoahidiwa Ibrahimu.

Baadhi ya Watakatifu wa Galatia walikuwa na wasiwasi kwamba kwa sababu hawakuwa wa ukoo halisi (“uzao”) wa Ibrahimu, hawangepokea baraka alizoahidiwa Ibrahimu, ikijumuisha za kuinuliwa. Kulingana na Wagalatia 3:7–9, 13–14, 27–29, ni kitu gani humstahilisha mtu kuwa wa “uzao wa ibrahimu”?

Kujifunza kuhusu baraka alizoahidiwa Ibrahimu na baraka ambazo tunaweza kurithi kama uzao wake, ona Mada za Injili, “Agano la Ibrahimu,” topics.ChurchofJesusChrist.org. Kwa nini baraka zilizoahidiwa kwa Ibrahimu ni muhimu kwako?

Wagalatia 3:6–25

Ibrahimu alikuwa na injili ya Yesu Kristo.

Nabii Joseph Smith alielezea: “Sisi hatuwezi kuamini kwamba watu wa kale katika vipindi vyote hawakuwa na ufahamu wa utaratibu wa mbinguni kama wengi wanavyodhani, kwani yote yaliyokuwa yamehifadhiwa, yalihifadhiwa kupitia nguvu ya mpango huu mkuu wa ukombozi, kama vile ilivyo kabla ya kuja kwa Kristo tangu wakati huo. … Ibrahimu alitoa dhabihu, na licha ya hili, Injili ilihubiriwa kwake” (“The Elders of the Church in Kirtland to Their Brethren Abroadi,” The Evening and the Morning Star, Mar. 1834, 143, JosephSmithPapers.org). Kwa nini unadhani ilikuwa ni muhimu kwa Watakatifu katika siku za Paulo kujua kwamba Ibrahimu na manabii wengine wa kale walikuwa na injili ya Yesu Kristo? Kwa nini ni muhimu kwako kujua hili? (Ona Helamani 8:13–20; Musa 5:58–59; 6:50–66.)

Ona pia Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith (2007), 45–56.

Wagalatia 5:13–26; 6:7–10

Kama “nikienenda kwa Roho” Nitapokea “tunda la Roho.”

Kujifunza mistari hii kunaweza kukusaidia kutathmini jinsi gani unaenenda kikamilifu kwa Roho. Je, unaliona katika maisha yako tunda la Roho lililotajwa katika mstari wa 22–23? Ni tunda gani lingine, au matokeo mengine, ya kuishi kiroho umeyagundua? Tafakari kile unachohitaji kufanya ili kulilimia tunda hili kikamilifu zaidi. Je, ni kwa jinsi gani kulilimia tunda hili kunaboresha uhusiano muhimu katika maisha yako?

Picha
matufaha juu ya mti

Lazima nitafute “tunda la Roho” katika maisha yangu.

Kama unajaribu kuenenda kwa Roho lakini haionekani kama juhudi zako zinazaa tunda lililoahidiwa, soma Wagalatia 6:7–10. Je, ni ujumbe gani unahisi Bwana anao kwako katika mistari hii?

Ona pia Alma 32:28, 41–43; Mafundisho na Maagano 64:32–34.

Picha
ikoni ya kujifunza kama familia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko kama Familia na Jioni ya Nyumbani

Wagalatia 3:11.Maana ya “kuishi kwa imani” ni nini? Je, ni kwa jinsi gani tunaishi kwa imani kama familia?

Wagalatia 4:1–7.Unaweza kutambulisha Wagalatia 4 kwa kujadili tofauti kati ya watumwa wa mfalme na watoto wake. Je, ni fursa zipi au uwezekano upi ambao mtoto wa mfalme anao ambao mtumwa hana? Fikirieni kuhusu hili mnaposoma pamoja mstari wa 1–7. Je, mistari hii hufundisha nini kuhusu uhusiano wetu na Baba wa Mbinguni?

Wagalatia 5:16–26.Fikiria kujadili tofauti kati ya “matendo ya mwili” na “tunda la Roho.” Ili kuongeza viburudisho katika mjadala wenu, familia yako inaweza kubandika nembo kwenye matunda tofauti kwa kutumia maneno ya Paulo kuelezea tunda la Roho. Kisha kila mwanafamilia anaweza kuchagua moja, kulitolea ufafanuzi, na kuzungumza juu ya mtu ambaye ana sifa zenye mfanano wa lile tunda. Hii inaweza kuongoza kwenye mjadala kuhusu njia ambazo familia yako inaweza kumualika Roho katika nyumba yenu na kulilimia tunda hili. Baada ya mjadala, mnaweza kufurahia saladi ya matunda pamoja.

Wagalatia 6:1–2.Kunaweza kuwepo na nyakati ambapo mtu mmoja katika familia yako “ameghafilika katika kosa.” Ni ushauri gani unaoupata katika Wagalatia 6:1–2 kuhusu nini cha kufanya katika hali kama hiyo?

Wagalatia 6:7–10.Kama familia yako imewahi kupanda kitu kwa pamoja, mnaweza kutumia uzoefu huo kuelezea kwa mfano kanuni “chochote apandacho mtu, ndicho atakachovuna” (mstari wa 7). Au unaweza kuwauliza wanafamilia kuhusu matunda au mboga wanazopenda sana na zungumza kuhusu nini kinahitajika kukuza mmea unaozaa chakula kile. (Ona picha mwisho wa muhtasari huu.) Kisha mnaweza kuzungumza kuhusu baraka ambazo familia yako inatumaini kupokea na jinsi ya “kuvuna” baraka hizo.

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “Teach Me to Walk in the Light,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 177.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Isaidie familia yako kuyalinganishe maandiko na wao wenyewe. Nefi alisema, “Nililinganisha maandiko yote nasi, ili yatufaidishe na kutuelimisha” (1 Nefi 19:23). Ili kuisaidia familia yako kufanya hili, unaweza kuwaalika watafakari nyakati walipopata uzoefu wa tunda la Roho lililoelezewa katika Wagalatia 5:22–23. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi,21.)

Picha
mapea juu ya mti

Paulo alifundisha kwamba tunapoenenda kwa Roho, tutapata uzoefu wa “tunda la Roho” katika maisha yetu.

Chapisha