Agano Jipya 2023
Oktoba 23–29. 1 na 2 Timotheo; Tito; Filemoni: “Uwe Kielelezo Kwao Waaminio”


“Oktoba 23–29. 1 na 2 Timotheo; Tito; Filemoni: ‘Uwe Kielelezo Kwao Waaminio’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya 2023 (2022)

“Oktoba 23–29. 1 na 2 Timotheo; Tito; Filemoni,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2023

Picha
wanawake watatu wakitembea nje ya hekalu

Oktoba 23–29

1na 2 Timotheo; Tito; Filemoni

“Uwe Kielelezo Kwao Waaminio”

Wakati mwingine inasaidia kuanza kujifunza kwako maandiko ukiwa na swali moja au zaidi akilini. Mualike Roho akuongoze kwenye majibu unapojifunza, na andika mwongozo wa kiungu wowote unaoupokea.

Andika Misukumo Yako

Katika nyaraka ambazo Paulo aliziandika kwa Timotheo, Tito, na Filemoni, tunapata kuona kidogo ndani ya moyo wa mtumishi wa Bwana. Tofauti na nyaraka zingine za Paulo kwa mkusanyiko wote, hizi ziliandikwa kwa watu binafsi—marafiki wa karibu wa Paulo na washirika katika kazi ya Mungu—na kuzisoma ni kama kusikiliza mazungumzo. Tunaona Paulo akiwatia moyo Timotheo na Tito, viongozi wawili wa mikusanyiko, katika huduma yao ya Kanisa. Tunamuona akimsihi rafiki yake Filemoni apatanishwe na Mtakatifu mwenzake na kumchukulia kama kaka katika injili. Maneno ya Paulo hayakutulenga moja kwa moja, na hakutegemea kwamba watu wengi siku moja wangeyasoma. Bado tunapata katika nyaraka hizi ushauri na kutiwa moyo, bila kujali huduma yetu binafsi kwa Kristo.

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa Ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

Timotheo na Tito walikuwa akina nani?

Timotheo na Tito walitumikia pamoja na Paulo katika baadhi ya safari zake za kimisionari. Wakati wa huduma yao, walipata heshima na uaminifu kutoka kwa Paulo. Timotheo baadaye aliitwa kama kiongozi wa Kanisa huko Efeso, na Tito aliitwa kama kiongozi huko Krete. Katika nyaraka hizi, Paulo aliwapa Timotheo na Tito maelekezo na kuwatia moyo kuhusiana na majukumu yao, ambayo yalijumuisha kuhubiri injili na kuwaita watu kutumikia kama maaskofu.

Ona pia Kamusi ya Biblia, “Nyaraka za Paulo,” “Timotheo,” “Tito.”

Picha
wamisionari wawili wakizungumza na mwanamume mmoja

“Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio” (1 Timotheo 4:12).

1 Timotheo 4:10–16

“Uwe Kielelezo kwao waaminio”

Timotheo alikuwa bado kijana, lakini Paulo alijua kwamba angekuwa kiongozi mzuri wa Kanisa bila kujali ujana wake. Je, ni ushauri gani Paulo alimpa Timotheo katika 1 Timotheo 4:10–16? Je, ni kwa jinsi gani ushauri huu unaweza kukusaidia wewe kuwaongoza wengine kuja kwa Mwokozi na injili Yake?

Ona pia Alma 5:11.

2 Timotheo

“Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.”

2 Timotheo inaaminika kuwa ni waraka wa mwisho ulioandikwa na Paulo, na inaonekana kwamba alijua muda wake duniani ulikuwa mfupi (ona 2 Timotheo 4:6–8). Ni kwa jinsi gani Timotheo angehisi kwa kujua kwamba punde asingekuwa na mshauri na kiongozi huyu aliyemwamini? Je, Paulo alisema nini ili kumtia moyo? Ungeweza pia kusoma ukiwa na changamoto zako na hofu yako mwenyewe akilini. Je, ni jumbe gani za matumaini na kutia moyo Bwana anazo kwa ajili yako katika 2 Timotheo?

Ona pia Kelly R. Johnson, “Nguvu za Kudumu,” Liahona, Nov. 2020, 112–14.

2 Timotheo 3

Kuishi injili kunaleta usalama dhidi ya hatari za kiroho za siku za mwisho.

Tunaishi katika “siku za mwisho” ambazo Paulo aliziongelea, na “nyakati za hatari” zimekuja (2 Timotheo 3:1). Unaposoma 2 Timotheo 3, andika hatari za siku za mwisho ambazo zimetajwa (ona pia 1 Timotheo 4:1–3).

Unaweza kufikiria mifano ya hatari hizi katika ulimwengu unaokuzunguka—au katika maisha yako mwenyewe? Je, ni kwa jinsi gani hatari hizi, kama watu walioelezewa katika mstari wa 6, “huinyemelea [nyumba yako], na kukuongoza [wewe] kuwa mateka”? Je, ni ushauri gani unaupata katika 2 Timotheo 3, na pengine popote katika nyaraka hizi, ambao utakuweka wewe na familia yako salama dhidi ya hatari hizi za kiroho? (ona, kwa mfano, 1 Timotheo 1:3–11; 2 Timotheo 2:15–16; Tito 2:1–8).

Filemoni alikuwa nani?

Filemoni alikuwa Mkristo ambaye alikuwa ameongolewa kwenye injili na Paulo. Filemoni alikuwa na mtumwa aliyeitwa Onesimo, ambaye alikuwa ametoroka Rumi. Huko Onesimo alikutana na Paulo na kuongolewa katika injili. Paulo alimtuma Onesimo kurudi kwa Filemoni na barua ya kumhimiza Filemoni ampokee Onesimo “si kama mtumwa, bali zaidi ya mtumwa, ndugu mpendwa” (Filemoni 1:16).

Filemoni

Wafuasi wa Yesu Kristo hutendeana kama kaka na dada.

Unaposoma waraka wa Paulo kwa Filemoni, tafakari jinsi ambavyo wewe ungetumia ushauri wake katika uhusiano wako wewe na wengine. Haya ni baadhi ya maswali ambayo ungeweza kuyafikiria:

  • Mstari wa 1–7: Ni nini maneno kama vile “mtenda kazi pamoja nasi” na “askari mwenzetu” yanapendekeza kwako kuhusu uhusiano miongoni mwa Watakatifu? Ni wakati gani umehisi “umeburudishwa” na kaka au dada katika Kristo?

  • Mstari wa 8–16: Ni nini maana ya “kuagiza” na “kusihi”? Kwa nini Paulo alichagua kumsihi Filemoni badala ya kumwagiza yeye? Ni nini Paulo alitumaini angetimiza kwa kumtuma Onesimo kurudi kwa Filemoni?

  • Mstari wa 16:Je, inamaanisha nini kuwa “kaka au dada mpendwa … katika Bwana? Je, unamjua mtu yeyote ambaye unahitaji kumpokea kwa njia hii?

Picha
ikoni ya kujifunza kama familia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko kama Familia na Jioni ya Nyumbani

1 Timotheo 2:9–10.Inamaanisha nini “wajipambe [wenyewe] … kwa matendo mema”? Je, ni yapi baadhi ya matendo mema familia yako inaweza kufanya wiki hii? Imbeni wimbo pamoja kuhusu kutenda wema, kama vile “Have I Done Any Good?” (Nyimbo za Kanisa, na. 223).

1 Timotheo 4:12.Kuwasaidia wanafamilia yako kutamani kuwa “kielelezo kwao waaminio,” fikiria kuwaalika wachore picha za watu ambao wamekuwa vielelezo bora kwao. Ni kwa jinsi gani watu hawa wametushawishi kumfuata Yesu Kristo? Ujumbe wa Rais Thomas S. Monson, “Kuwa Mfano na Nuru” (Liahona, Nov. 2015, 86–88) unaweza kutoa baadhi ya mawazo ya kuwa kielelezo kwa wengine.

1 Timotheo 6:7–12.Je, kwa nini unafikiri “shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha”? Hatari za kufokasi maisha yetu kwenye fedha na mali ni zipi? Je, ni kwa jinsi gani tunaweza kuridhika na baraka tulizo nazo?

2 Timotheo 3:14–17.Kulingana na mistari hii, ni baraka zipi huja kwa wale wote wanaojua na kujifunza maandiko? Pengine wanafamilia wanaweza kuelezea maandiko waliyoona kuwa “yenye faida” maalumu kwao.”

Filemoni 1:17–21.Je, Paulo alikuwa tayari kufanya nini kwa ajili ya Onesimo? Je, ni kwa jinsi gani hii ni sawa na kile Mwokozi alichotufanyia sisi kwa hiyari? (ona 1 Timotheo 2:5–6; Mafundisho na Maagano 45:3–5). Je, ni kwa jinsi gani tunaweza kufuata mfano wa Paulo na Mwokozi?

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “Shine On,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 144.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Fundisha kwa uwazi na mafundisho rahisi. Injili ya Bwana ni nzuri katika urahisi wake (ona Mafundisho na Maagano 133:57). Kuliko kujaribu kuwafurahisha familia yako kwa masomo yanayohitaji maandalizi mengi, jitahidi kufundisha mafundisho yaliyo wazi na rahisi (ona 1 Timotheo 1:3–7).

Picha
watoto wawili wakijifunza maandiko

“Na ya kuwa tangu utoto umeyajua maandiko matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu”(2 Timotheo 3:15).

Chapisha