Agano la Kale 2022
Aprili 11–17. Pasaka: “Atashinda Kifo kwa Ushindi”


“Aprili 11-17. Pasaka: ‘Atashinda Kifo kwa Ushindi,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano la Kale 2022 (2021)

“Aprili 11-17. Pasaka,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2022

Picha
jiwe la kaburi limeviringishwa mbali kutoka mlangoni

Kielelezo cha kaburi wazi na Maryna Kriuchenko

Aprili 11–17

Pasaka

“Atashinda Kifo kwa Ushindi”

Unaaposoma kuhusu na kutafakari juu ya Upatanisho wa Mwokozi wiki hii, zingatia kuandika mawazo na hisia zako kuhusu dhabihu Yake katika shajara yako au katika nafasi iliyotolewa katika muhtasari huu.

Andika Misukumo Yako

Maisha ya Yesu Kristo “ni kitovu kwa historia yote ya mwanadamu” (“Kristo Aliye Hai: Ushuhuda wa Mitume,” ChurchofJesusChrist.org). Hilo linamaanisha nini? Kwa sehemu, hakika hii inamaanisha kwamba nguvu ya maisha ya Mwokozi inagusa hatima ya milele ya kila mwanadamu ambaye amewahi kuishi au atakuja kuishi duniani. Ungeweza pia kusema kwamba maisha na misheni ya Yesu Kristo, inayomalizikia katika Ufufuko Wake siku ya Jumapili ile ya kwanza ya Pasaka, inawaunganisha watu wote wa Mungu katika historia yote: Wale waliozaliwa kabla ya Kristo walitazamia kuja Kwake kwa imani (ona Yakobo 4:4), na wale waliozaliwa baada Yake wanamuangalia kwa imani. Tunaposoma hadithi na unabii katika Agano la Kale, kamwe hatuoni jina Yesu Kristo, lakini tunaona ushahidi wa imani ya waaminifu wa kale na hamu yao ya Masiya na Mkombozi wao. Hivyo sisi ambao tunaalikwa kumkumbuka Yeye tunaweza kuhisi muunganiko na wale ambao walimtazamia Yeye. Kwani hakika Yesu Kristo ameweka juu yake “maovu yetu sisi sote” (Isaya 53:6; italiki imeongezwa), na “katika Kristo wote watahuishwa” (1 Wakorintho 15:22; italiki imeongezwa).

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

Agano la Kale linashuhudia juu ya dhabihu ya Yesu Kristo ya kulipia dhambi.

Vifungu vingi vye maneno katika Agano la Kale vinaelekeza juu ya huduma na dhabihu ya Mwokozi ya kulipia dhambi. Jedwali la hapo chini limeorodhesha baadhi ya vifungu hivyo. Unaposoma mistari hii, je, ni mawazo gani yanakuja kwako kuhusu Mwokozi?

Agano la Kale

Agano Jipya

Agano la Kale

Zekaria 9:9

Agano Jipya

Mathayo 21:1–11

Agano la Kale

Zekaria 11:12–13

Agano Jipya

Mathayo 26:14–16

Agano la Kale

Isaya 53:4

Agano Jipya

Mathayo 8:16–17; 26:36–39

Agano la Kale

Isaya 53:7

Agano Jipya

Marko 14:60–61

Agano la Kale

Zaburi 22:16;

Agano Jipya

Yohana 19:17–18; 20:25–27

Agano la Kale

Zaburi 22:18

Agano Jipya

Mathayo 27:35

Agano la Kale

Zaburi 69:21.

Agano Jipya

Mathayo 27:34, 48.

Agano la Kale

Zaburi 118:22

Agano Jipya

Mathayo 21:42

Agano la Kale

Isaya 53:9, 12

Agano Jipya

Mathayo 27:57–60; Marko 15:27–28

Agano la Kale

Isaya 25:8

Agano Jipya

Marko 16:1–6; Luka 24:6

Agano la Kale

Danieli 12:4 2

Agano Jipya

Mathayo 27:52–53

Unabii na mafundisho kuhusu Mwokozi yako mengi na ya wazi zaidi katika Kitabu cha Mormoni. Zingatia jinsi imani yako inavyoimarishwa kwa vifungu kama hivi: 1 Nefi 11:31–33; 2 Nefi 25:13; Mosia 3:2–11.

Ninaweza kupata amani na shangwe kupitia Upatanisho wa Mwokozi.

Wakati wote, Yesu Kristo, kupitia dhabihu yake ya kulipia dhambi, ametoa amani na shangwe kwa wote wanaomwendea (ona Musa 5:9–12). Fikiria kujifunza maandiko yafuatayo ambayo yanashuhudia juu ya amani na shangwe Anayotoa, na unapofanya hivyo, fikiria kuhusu jinsi unavyoweza kupokea amani na shangwe ambayo Yeye analeta: Zaburi 16:8–11; 30:2–5; Isaya 12; 25:8–9; 40:28–31; Yohana 14:27; 16:33; Alma 26:11–22.

Ona pia Dallin H. Oaks, “Kuimarishwa na Upatanisho wa Yesu Kristo,” Liahona, Nov. 2015, 61–64; Sharon Eubank, “Kristo: Nuru ing’arayo Gizani,” Liahona, Mei 2019, 73–76; “I Stand All Amazed,” Wimbo wa Kanisa, na. 193.

Picha
Kristo msalabani

Siku ya Kijivu Golgotha, na J. Kirk Richards

Kupitia Upatanisho Wake,Yesu Kristo anao uwezo wa kunisaidia mimi kushinda dhambi, kifo, majaribu, na madhaifu.

Kote katika maandiko, manabii wameshuhudia juu ya uwezo wa Yesu Kristo wa kutukomboa sisi kutokana na dhambi na mauti na kutusaidia kushinda majaribu na madhaifu yetu. Je, ni jinsi gani Kristo amefanya tofauti katika maisha yako? Je, kwa nini yeye ni muhimu kwako? Tafakari maswali haya unaposoma mistari hii, na uandike mawazo na hisia zako kuhusu Mwokozi:

Ona pia Walter F. González, “Mguso wa Mwokozi,” Liahona, Nov. 2019, 90–92.

Picha
ikoni ya kujifunza kiama familia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko kama Familia na Jioni ya Nyumbani

Kutoka 12:1-28.Unaposherehekea Pasaka, familia yako inaweza kurejelea kile mlichojifunza kuhusu Pasaka mwanzoni mwa mwezi huu. Kwa nini ni ya umuhimu wa kipekee kwamba dhabihu ya Mwokozi ilitokea wakati huo huo wa Pasaka.

Kwa muhtasari wa kile kilichotokea wakati wa wiki ya mwisho ya maisha ya Mwokozi, ona “Holy Week” katika ComeuntoChrist.org/2016/easter/easter-week. Kwa maandiko kuhusu matukio ya wiki ya mwisho ya Mwokozi, ona “Wiki ya Mwisho: Upatanisho na Ufufuko” katika Harmony of the Gospels (katika kiambatisho cha Biblia).

Isaya 53.Kusoma unabii kuhusu Yesu Kristo katika Isaya 53 kunaweza kusaidia washiriki wa familia yako kuelewa dhabihu ya Mwokozi ya kulipia dhambi. Je, ni mistari au vifungu gani vya maneno familia yako inaviona kuwa vyenye nguvu maalumu? Fikiria kuwa na mkutano wa familia wa ushuhuda ambapo mtashiriki shuhuda zenu binafsi juu ya Upatanisho wa Mwokozi.

“Mashahidi Maalumu wa Kristo.”The Gospel Library app na ChurchofJesusChrist.org zina mkusanyiko wa video zinazoitwa “Special Witnesses of Christ,” ambamo kila mshiriki wa Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili wanatoa ushahidi juu ya Yesu Kristo. Labda familia yako ingeweza kuangalia baadhi ya video hizi na kuongelea kuhusu kile mnachojifunza kuhusu Yesu Kristo kutoka kwa watumishi Wake wateule. Kama familia, zungumzeni kuhusu njia ambazo mnaweza kutoa ushahidi wenu juu ya Kristo. Kwa mfano, mnaweza kumwalika mtu kuja kuabudu pamoja nanyi kanisani Jumapili hii ya Pasaka.

Nyimbo za Kanisa na nyimbo nyinginezo.Muziki ni njia yenye nguvu ya kumkumbuka Mwokozi na kumwalika Roho katika nyumba zetu. Washiriki wa familia wangeweza kushiriki na kuimba pamoja nyimbo za kanisa na nyinginezo kuhusu Pasaka au kuhusu Yesu Kristo, kama vile “Christ the Lord Is Risen Today” (Nyimbo za Kanisa, na. 200) au “Did Jesus Really Live Again?” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 64). Ili kupata nyimbo nyingine za Kanisa au nyimbo za watoto, angalia katika kiambatisho cha mada za Nyimbo za Kanisa na Kitabu cha Nyimbo za Watoto.

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Wimbo unaopendekezwa: “Did Jesus Really Live Again?Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 64.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Ishi Injili ya Yesu Kristo. “Ili kuwa mwalimu kama Kristo [katika nyumba yako], pengine kitu muhimu zaidi unachoweza kufanya ni … kuishi injili kwa moyo wako wote … Hii ndiyo njia kuu ya kustahili kuwa na wenza wa Roho Mtakatifu. Huhitaji kuwa mkamilifu, ni kujaribu tu kwa bidii—na kutafuta msamaha kupitia Upatanisho wa Mwokozi wakati wowote unapojikwaa” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 13).

Picha
Kristo amesimama juu ya mlango uliovunjika wa jiwe la kaburi

Kwa Sababu hii Nimekuja, na Yongsung Kim

Chapisha