Mafundisho na Maagano 2021
Nyenzo za Ziada za Kufundishia Watoto


“Nyenzo za Ziada za Kufundishia Watoto,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Nyenzo za Ziada za Kufundishia Watoto,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi: 2021

Nyenzo za Ziada za Kufundishia Watoto

Nyenzo hizi zinaweza kupatikana katika Gospel Library app na kwenye ChurchofJesusChrist.org.

Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia

Unaweza kubadilisha shughuli kutoka Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia kwa ajili ya matumizi katika darasa lako la Msingi. Usihofu kama watoto tayari wamekwisha fanya shughuli hizi pamoja na familia zao nyumbani; marudio husaidia watoto kujifunza. Wakati wa darasa la Msingi, watoto wanaweza kutaka kushiriki na wengine kitu wanachojifunza nyumbani kuhusu Mwokozi na injili Yake.

Nyimbo za Kanisa na Kitabu cha Nyimbo za Watoto

Muziki mtakatifu humwalika Roho na hufundisha mafundisho katika njia ya kukumbukwa. Katika kuongezea kwenye toleo lililochapishwa la Nyimbo za Kanisa na Kitabu cha Nyimbo za Watoto, unaweza kupata rekodi za sauti na video za nyimbo nyingi za kanisa na nyimbo za watoto kwenye music.ChurchofJesusChrist.org na katika app za Music na Gospel Media.

Behold Your Little Ones

Mada nyingi kati ya zilizotajwa katika kitabu cha kiada cha Behold Your Little Ones: Nursery ni sawa na zile utakazofundisha katika Msingi. Hususani kama unafundisha watoto wadogo, fikiria kuangalia katika kitabu cha kiada cha chekechea kwa ajili ya nyimbo za ziada, hadithi, shughuli, na ufundi.

Magazeti ya Friend na Liahona

Magazeti ya Friend na Liahona hutoa hadithi na shughuli ambazo zinaweza kuwa nyongeza ya kanuni unazofundisha kutoka katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi.

Hadithi za Mafundisho na Maagano

Hadithi za Mafundisho na Maagano hutumia picha na lugha iliyo rahisishwa ili kuwasaidia watoto kujifunza kutoka kwenye Mafundisho na Maagano. Unaweza pia kupata video za hadithi hizi katika Gospel Library app na Gospel Media Library kwenye ChurchofJesusChrist.org.

Kitabu cha Kupaka Rangi cha Maandiko: Mafundisho na Maagano

Nyenzo hii ina kurasa za shughuli zilizokusudiwa kuongeza kujifunza kwa watoto kutoka kwenye Mafundisho na Maagano.

Video na Sanaa

Sanaa za mchoro, video, na vyombo vingine vya habari vinaweza kuwasaidia wale unaowafundisha kupata taswira ya mafundisho na hadithi zinazohusiana na maandiko. Tembelea Gospel Media Library kwenye ChurchofJesusChrist.org ili kupitiapitia mkusanyiko wa nyenzo za Kanisa za vyombo vya habari. Nyenzo hizi pia zinapatikana katika Gospel Media app, na pia picha nyingi zinapatikana katika Kitabu cha Sanaa Ya Injili.

Picha
woman and child reading Church material

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi

Kufundisha katika Njia ya Mwokozi inaweza kukusaida kujifunza kuhusu, na kutumia kanuni za kufundisha kama Kristo. Kanuni hizi zinajadiliwa na kutumiwa katika mikutano ya baraza la walimu.

Watakatifu

Watakatifu ni juzuu nyingi za hadithi za kusimuliwa za historia ya Kanisa. Juzuu ya 1, The Standard of Truth, na juzuu ya 2, No Unhallowed Hand, zinaelezea habari za kipindi kinachofanana cha historia ya Kanisa kama ilivyo katika Mafundisho na Maagano. Historia hizi zinaweza kukupa utambuzi katika muktadha unaozunguka mafunuo unayojifunza katika Mafundisho na Maagano.

Chapisha