Mafundisho na Maagano 2021
Kutumia Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi


“Kutumia Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi,Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Kutumia Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi,Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2021

Picha
Darasa la Msingi wakifanya shughuli

Kutumia Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi

Kujiandaa Kufundisha katika Msingi

Kujifunza kibinafsi na kifamilia nyumbani kunapaswa kuwa kitovu cha kujifunza injili. Hii ni kweli kwako na kwa watoto unaowafundisha. Unapojiandaa kufundisha, anza kwa kuwa na uzoefu wako mwenyewe katika maandiko. Maandalizi yako muhimu zaidi yatatokea wakati unapopekua maandiko na kutafuta mwongozo wa Roho Mtakatifu.

Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia pia ni sehemu muhimu kwa vyote kujifunza kwako binafsi na maandalizi yako ya kufundisha. Itakusaidia kupata ufahamu wa kina zaidi wa kanuni za mafundisho zinazopatikana katika maandiko.

Wakati wa maandalizi yako, mawazo na misukumo itakujia kuhusu watoto unaowafundisha. Utapokea utambuzi juu ya jinsi kanuni katika maandiko zitakavyobariki maisha yao. Utaongozwa ili uwahamasishe kugundua kanuni hizo wakati wanapojifunza kutoka katika maandiko wao wenyewe na pamoja na familia zao. Kumbuka kuwa mwangalifu kwa watoto ambao hali zao za familia haziwezi kumudu kujifunza maandiko kama familia kila mara na jioni ya familia nyumbani.

Mawazo ya Kufundisha

Unapojiandaa kufundisha, ungeweza kupata mwongozo wa ziada kwa kuchunguza mihtasari katika nyenzo hii. Usifikirie mawazo haya kama maelekezo ya hatua kwa hatua lakini badala yake ni kama mapendekezo ya kuchochea mwongozo wako mwenyewe. Unawajua watoto hawa—na utapata kuwajua hata vizuri zaidi pale unapochangamana nao darasani. Bwana anawajua pia, na Atakuongoza kwa njia bora za kuwafundisha na kuwabariki watoto.

Nyenzo nyingine nyingi zinapatikana kwa ajili yako ili kuweza kutumia wakati unapojiandaa, ikiwa ni pamoja na mawazo katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia na magazeti ya Kanisa. Kwa maelezo zaidi kuhusu nyenzo hizi na nyingine, ona “Nyenzo za Ziada za Kufundishia Watoto” katika nyenzo hii.

Baadhi ya Vitu vya Kukumbuka

  • Wazazi wana jukumu la msingi la kuwafundisha watoto wao. Kama mwalimu, una jukumu muhimu la kusaidia, kuhimiza, na kujenga juu ya kujifunza injili nyumbani. Kuwa mwangalifu kwa watoto ambao wazazi wao hawafundishi injili nyumbani mwao. Jumuisha watoto wote katika majadiliano ya injili, bila kujali mazingira yao ya nyumbani.

  • Watoto wanaweza kujifunza kwa kuelezana kile wanachojua. Nyakati zingine muda bora wa kufundisha unatokea wakati watoto wanapofundishana kitu fulani walichojifunza kutoka kwenye maandiko. Toa fursa nyingi za watoto kushirikiana na wengine.

  • Kuelewa mafundisho katika Mafundisho na Maagano ni rahisi zaidi kwa watoto wanapokuwa wanajua mazingira ya kihistoria ya mafundisho hayo. Unaweza kupata mazingira ya kihistoria katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia na Hadithi za Mafundisho na Maagano.

  • Kurudia rudia ni vyema. Watoto hujifunza kweli za injili kwa ufanisi zaidi wakati kweli hizi zinapofundishwa kwa kurudiwa rudiwa kupitia shughuli mbalimbali. Ikiwa unaona kuwa shughuli ya kujifunza inafaa kwa watoto, fikiria kuirudia, hasa ikiwa unafundisha watoto wadogo zaidi. Unaweza pia kurejea tena shughuli kutoka kwenye somo lililopita.

  • Baba wa Mbinguni anataka wewe ufanikiwe kama mwalimu. Ametoa nyenzo nyingi ili kukusaidia, ikiwa ni pamoja na mikutano ya baraza la walimu. Katika mikutano hii unaweza kushauriana na walimu wengine kuhusu changamoto zinazokukabili. Unaweza pia kujadili na kufanyia mazoezi kanuni za kufundisha kama Kristo.

  • Kama unafundisha watoto wadogo na unahitaji msaada wa ziada, tazama “Kukidhi Mahitaji ya Watoto Wadogo” katika nyenzo hii.

  • Nyenzo hii inajumuisha mihutasari ya kila wiki ya mwaka. Katika Jumapili ambazo darasa la Msingi halipo kwa sababu ya mkutano mkuu, mkutano wa kigingi au sababu nyingine yoyote, familia zinapaswa kuendelea kusoma Mafundisho na Maagano nyumbani kulingana na ratiba iliyooneshwa. Usiogope kuhusu masomo uliyokosa; fundisha muhtasari uliopangwa kila wiki.

Picha
mwanamke akisoma kitabu cha kiada

Chapisha