Agano la Kale 2022
Septemba 5–11. Isaya 1–12: “Mungu Ni Wokovu Wangu”


“Septemba 5–11. Isaya 1–12: ‘Mungu Ni Wokovu Wangu’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano la Kale 2022 (2021)

“Septemba 5–11. Isaya 1–12,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2022

Picha
nabii wa kale akiandika

Nabii Isaya Anatabiri Kuzaliwa kwa Kristo, na Harry Anderson

Septemba 5–11

Isaya 1–12

“Mungu Ni Wokovu Wangu”

Maneno ya Isaya yanaweza kuwa magumu kuelewa. Unapofikiria jinsi ya kuwafundisha watoto kuhusu Isaya, fokasi kwenye ukweli rahisi ambao unaweza kuimarisha imani yao katika Yesu Kristo.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waalike watoto kushiriki jambo ambalo wamefanya hivi karibuni ili kuishi injili, kama vile kusali, kuonesha ukarimu kwa mtu au kutii amri zingine.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Isaya 2:2–3

Ndani ya hekalu tunajifunza kuhusu Yesu Kristo.

Isaya aliona mapema wakati ambapo hekalu, “mlima wa nyumba ya Bwana,” litawavutia watu kutoka “mataifa yote.” Unaweza kutumia unabii huu kuwasaidia watoto watazamie wakati ambapo wanaweza kwenda hekaluni.

Shughuli Yamkini

  • Waombe watoto kuchora picha za nyumba zao. Kisha someni pamoja Isaya 2:2, na waalike kuchora picha ya “nyumba ya Bwana,” ambayo ni hekalu. Someni mstari wa 3 pamoja, na waalike waongeze kwenye picha zao watu wengi wakija hekaluni, ikiwa ni pamoja na familia zao. Je, kwa nini tunataka kwenda kwenye nyumba ya Bwana? Shiriki ushuhuda wako juu ya baraka ambazo huja tunapojifunza kuhusu Bwana katika nyumba Yake.

  • Mruhusu mtoto ashikilie picha ya hekalu na waombe watoto wazungumze kuhusu kile wanachokiona katika picha. Waulize kitu gani wanachopenda kuhusu hekalu. Someni pamoja Isaya 2:2–3 na watake wasikilize sababu zaidi za kwa nini tunaweza kupenda hekalu. Waambie watoto kwa nini wewe unalipenda hekalu.

  • Imba pamoja na watoto wimbo kuhusu hekalu, kama vile “I Love to See the Temple” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,95). Wasaidie watafute maneno na virai katika wimbo ambavyo hufundisha hekalu ni nini na kile tunachofanya humo hekaluni.

  • Chora njia ubaoni, na weka picha ya hekalu au Mwokozi mwisho wa njia (ona Personal Development: Children’s Guidebook, 2–3). Waruhusu watoto wafanye zamu kujichora wenyewe wakitembea kwenye njia. Wanapofanya hivyo, waalike warudie kirai hiki kutoka Isaya 2:3: “Tutakwenda katika mapito yake.” Je, tunaweza kufanya kitu gani ili kutembea katika mapito ya Bwana?

Picha
mwanamke amemshikilia mtoto

“Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto mwanamume” (Isaya 9:6).

Isaya 9:6

Isaya alitoa unabii juu ya Yesu Kristo.

Manabii wote wanashuhudia juu ya Yesu Kristo, ikiwa ni pamoja na wale walioishi zamani kabla ya Yeye kuzaliwa, kama vile Isaya. Fikiria kile watoto wanachoweza kujifunza kuhusu Yesu kutokana na unabii wa Isaya katika Isaya 9:6.

Shughuli Yamkini

  • Shiriki pamoja na watoto “Isaya Nabii” (katika Hadithi za Agano la Kale). Pumzika mara kwa mara ili watoto waweze kuzungumza juu ya kile Isaya alichojua kuhusu Yesu Kristo miaka mingi kabla hajazaliwa. Wasomee watoto Isaya 9:6, na waalike warudie pamoja nawe kila “jina” ambalo Isaya alisema Yesu Kristo “angeitwa.”

  • Andika kwenye vipande vya karatasi majina machache ya Yesu Kristo yanayopatikana katika Isaya 9:6 (ona ukurasa wa shughuli ya wiki hii). Mualike kila mtoto achague moja, na msaidie mtoto kusoma jina kwa darasa. Zungumza na watoto kuhusu kile kila jina linachomaanisha kwako. Mpe picha ya Kristo mmoja wa watoto, na muombe ashiriki jambo kuhusu Yesu na kisha pitisha picha kwa mtoto mwingine. Rudia shughuli hii mpaka watoto wote wawe wamepata nafasi ya kushiriki.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Isaya 1:2–4, 16–19

Kwa sababu ya Yesu Kristo, ninaweza kutubu na kuwa safi.

Isaya aliishi katika kipindi ambacho wengi wa watu wake walikuwa wamegeuka mbali na Bwana. Lakini Bwana aliwaahidi kwamba dhambi zao zingesamehewa ikiwa wangetubu. Yeye anatoa ahadi hii kwetu sisi pia.

Shughuli Yamkini

  • Waombe watoto wasome Isaya 1:2–4 na wazungumze kuhusu baadhi ya sababu za kwa nini Bwana hakuwa na furaha na watu wa Yuda. Kisha someni Isaya 1:16–19 pamoja ili kujifunza kile Bwana alichowaalika watu kufanya. Kadiri inavyohitajika, wasaidie watoto waelewe maneno na vifungu vya maneno vilivyo vigumu kueleweka. Ili kuwasaidia kupata taswira ya mstari wa 18, onesha kitu chenye rangi nyekundu inayong’ara na kitu chenye weupe safi. Je, tunajifunza nini kuhusu huruma ya Yesu Kristo kutoka kwenye mistari hii? Waalike watoto kushiriki jinsi wanavyohisi kuhusu zawadi ya Yesu Kristo ya msamaha, na shiriki hisia zako vilevile.

  • Wasaidie watoto wakariri Isaya 1:18. Andika mstari huo ubaoni na waalike watoto waukariri mara kadhaa, wakifuta neno moja kila mara mpaka waweze kuukariri kutoka kwenye kumbukumbu. Unaweza pia kutumia vipande vya karatasi vyenye maneno kutoka kwenye mstari yakiwa yameandikwa juu yake. Kwa nini ni muhimu daima kukumbuka kile ambacho mstari huu unatufundisha? Jadili jinsi kubatizwa na kupokea sakramenti kunavyofanya ahadi hii ipatikane kwetu.

Isaya 2:2–5

Ndani ya hekalu tunajifunza kuhusu Yesu Kristo.

Unabii wa Isaya kuhusu “mlima wa nyumba ya Bwana” unafunua baadhi ya baraka ambazo huja kutokana na kuabudu hekaluni, sambamba na baraka zingine zitakazokuja katika siku za mwisho. Tafakari jinsi utakavyowashawishi watoto watafute baraka hizi.

Shughuli Yamkini

  • Waombe watoto wasome kuhusu kile Isaya alichoona katika Isaya 2:2–3 na wachore picha ya vile wanavyodhani kingeonekana. Eleza kwamba Isaya aliita hekalu “mlima wa nyumba ya Bwana.” Kwa nini mlima ni ishara nzuri kwa ajili ya hekalu?

  • Waalike watoto wasome Isaya 2:2–3,5 na watambue katika kila moja ya mistari hii jambo ambalo linawavutia wao kwenda hekaluni siku moja. Kisha someni mstari wa 4 pamoja, na mjadili jinsi hekalu linavyosaidia kuleta amani iliyoelezewa katika mstari huu. Wasaidie kufikiria jinsi wanavyoweza kujiandaa sasa kwenda hekaluni siku moja.

Isaya 7:14; 9:6–7

Isaya alitoa unabii juu ya Yesu Kristo.

Isaya alitoa unabii juu ya kuzaliwa mtoto ambaye angeketi kwenye kiti cha enzi cha Daudi na kuanzisha ufalme ambao hauna mwisho. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto unaowafundisha waelewe unabii huu kuhusu Yesu Kristo?

Shughuli Yamkini

  • Waombe watoto watoe mifano ya majina ambayo mtu anaweza kuwa nayo, kama vile majina yanayohusiana na kazi, wito, timu au familia. Majina haya yanasema nini kuhusu mtu mwenye majina hayo? Wasaidie watoto kupata majina ya Yesu Kristo katika Isaya 7:14 na 9:6–7. Je, kila moja ya majina haya linatufundisha nini kuhusu Yeye? Je, tunajifunza nini kingine kuhusu Yesu Kristo kutoka kwenye mistari hii?

  • Someni pamoja Mathayo 1:21–23 na Luka 1:31–33, na mjadili jinsi unabii wa Isaya katika Isaya 7:14; 9:6–7 ulivyotimizwa wakati Yesu alipozaliwa.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waombe watoto wafikirie juu ya jambo walilojifunza kuhusu Mwokozi ambalo wanaweza kushiriki nyumbani pamoja na familia zao, kama vile moja ya majina Yake.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Wasaidie watoto kujenga kujiamini. Baadhi ya watoto wanaweza wasihisi kuwa na uwezo wa kujifunza injili wao wenyewe. Njia moja ya kuwasaidia kujenga kujiamini ni kuwasifia wakati wanaposhiriki katika darasa. Waahidi watoto kwamba Roho Mtakatifu atawasaidia pale wanapojifunza.

Chapisha