Agano la Kale 2022
Septemba 12–18. Isaya 13–14; 24–30; 35: “Kazi ya Ajabu na Mwujiza”


“Septemba 12–18. Isaya 13–14; 24–30; 35: ‘Kazi ya Ajabu na Mwujiza’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano la Kale 2022 (2021)

“Septemba 12–18. Isaya 13–14; 24–30; 35,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2022

Picha
Joseph Smith anamwona Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo katika Kijisitu Kitakatifu

Kijisitu Kitakatifu, na Brent Borup

Septemba 12–18

Isaya 13–14; 24–30;35

“Kazi ya Ajabu na Mwujiza”

Baada ya kujifunza kwa sala Isaya 13–14; 24–30;35, panga shughuli za kuwasaidia watoto kujifunza. Mawazo ya shughuli hapa chini yanaweza kutumiwa kwa ajili ya kikundi cha umri wowote.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waalike watoto wasimame ikiwa wanataka kushiriki kitu fulani walichojifunza kuhusu injili nyumbani au Kanisani. Mpe kila mtoto fursa ya kushiriki.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Isaya 14:12–14

Palikuwa na vita mbinguni.

Kabla ya ulimwengu kuumbwa, Baba wa Mbinguni alimchagua Yesu Kristo kuwa Mwokozi wetu. Isaya 14:12–14 inaelezea kiburi ambacho Shetani alionesha katika Mkutano wa Mbinguni kabla ya kuja duniani.

Shughuli Yamkini

  • Tumia “Utangulizi: Mpango wa Baba Yetu wa Mbinguni” (katika Hadithi za Agano Jipya, 1–3) au wimbo “I Lived in Heaven” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,4) kuwaelezea watoto kuhusu Vita Mbinguni kabla hatujazaliwa. (Unapofanya hivyo, jumuisha vifungu vya maneno kutoka Isaya 14:12–14 ambavyo humwelezea Shetani.) Kisha waalike watoto wafanye zamu kukusimulia wewe hadithi hiyo. Sisitiza kwamba Yesu Kristo alifuata mpango wa Baba wa Mbinguni na kuwa Mwokozi wetu.

  • Ubaoni, chora moyo na neno Shetani na uso wa huzuni ndani yake. Eleza kwamba Shetani alisema moyoni mwake, “Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu” (Isaya 14:13), ambayo ina maana kwamba alitaka kuwa bora kuliko Baba wa Mbinguni. Mwalike mtoto achore moyo mwingine, huu ukiwa na neno Yesu na uso wa furaha ndani yake. Wasaidie watoto waelewe kwamba Yesu alitaka kufanya kile Baba wa Mbinguni alichomtaka Yeye afanye (ona Musa 4:1–2). Je, ni kwa jinsi gani sisi tunaweza kufuata mfano wa Yesu?

Picha
Yesu aliyefufuka akimtokea mwanamke kwenye kaburi

“Ataimeza mauti katika ushindi” (Isaya 25:8).

Isaya 25:8

Yesu Kristo alifufuka.

Yesu Kristo anaweza kutupa faraja kwa huzuni tunayoisikia kuhusu kifo. Kwa sababu alishinda mauti, sote tutafufuliwa pia.

Shughuli Yamkini

  • Onesha picha ya Ufufuko wa Yesu Kristo na waombe watoto kushiriki kile wanachojua kuhusu picha hiyo. Kama itahitajika, shiriki pamoja nao hadithi ya Yesu akifufuka (ona “Yesu Amefufuka,” katika Hadithi za Agano Jipya, 139–44). Piga au imbeni wimbo kuhusu Ufufuko, kama vile “Jesus Has Risen,” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,70), na waalike watoto kushiriki jinsi inavyowafanya wahisi kwa kujua kwamba Yesu alifufuka kutoka kwa wafu.

  • Waeleze watoto kuhusu mtu fulani unayemjua ambaye amefariki. Je, tunajisikiaje wakati mtu tunayempenda anapofariki? Waalike watoto wachore uso wa mtu akilia. Kisha wasomee Isaya 25:8. Je, Yesu atafanya nini na machozi yetu wakati tunapomkumbuka mtu aliyefariki? Waalike watoto wachore uso wenye furaha. Toa ushuhuda wako kwamba kwa sababu Yesu Kristo alifufuka, tunaweza kuhisi kufarijika wakati mtu anapofariki na kujua kwamba siku moja sote tutafufuliwa.

Isaya 29:12,14

Bwana alirejesha Kanisa Lake kupitia Joseph Smith.

Urejesho wa injili ni “kazi ya ajabu na mwujiza” (Isaya 29:14). Shiriki na watoto baadhi ya mambo ya ajabu ambayo Bwana alifanya—na anaendelea kufanya—ili kurejesha injili Yake katika siku yetu.

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto wakusimulie kile wanachojua kuhusu Joseph Smith. Kama itahitajika, shiriki nao “Ono la Kwanza la Joseph Smith” (katika Hadithi za Mafundisho na Maagano, 9–12). Soma Isaya 29:12, na eleza kwamba ijapokuwa Joseph Smith hakufikiriwa kuwa “msomi” na watu wengi, Yesu Kristo alirejesha injili kupitia yeye.

  • Wasomee watoto Isaya 29:14 na shiriki nao maneno mengine ambayo yana maana sawa na “ajabu” na “mwujiza.” Onesha vitu vinavyowakilisha baadhi ya kazi za ajabu za Bwana katika kipindi hiki cha siku za mwisho, kama vile picha ya Ono la Kwanza au Joseph Smith akipokea ukuhani (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 90, 93,94) au nakala ya Kitabu cha Mormoni. Waalike watoto wachague moja ya vitu hivi na kuwaelezea wengine kwa nini ni ya ajabu kwao.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Isaya 24:3–5; 29:7–10; 30:8–14

Ukengeufu humaanisha kugeuka kutoka kwa Bwana na manabii Wake.

Kusoma maonyo ya Isaya kuhusu hatari za ukengeufu kunaweza kuwasaidia watoto kuweka msimamo wa kubaki wakweli kwa Bwana na kuwafuata manabii Wake.

Shughuli Yamkini

  • Andika neno ukengeufu ubaoni. Waalike watoto kutafuta maana ya “Ukengeufu” katika Mwongozo wa Maandiko (scriptures.ChurchofJesusChrist.org). Waalike wasome Isaya 24:5; 30:9–11 na watengeneze orodha ya mambo ambayo watu walikuwa wakifanya katika kipindi cha Isaya ambayo yaliwaongoza kwenye ukengeufu. Kisha waalike watoto wabadili vitu katika orodha kuwa mambo tunayoweza kufanya ili kubaki wakweli kwa Bwana.

  • Gawanya darasa katika jozi, na wapangie kila jozi kusoma moja ya vifungu vifuatavyo: Isaya 24:3–5; Isaya 29:7–10; au Isaya 30:8–14. Waalike wachore picha ambazo zinawakilisha kile wanachosoma. Wanaposhiriki michoro yao, wasaidie kujadili kile maneno ya Isaya yanachofundisha kuhusu kwa nini tunapaswa kubaki wakweli kwa Bwana.

Isaya 29:13–15, 18,24

Urejesho wa injili ni “kazi ya ajabu.”

Unawezaje kuwasaidia watoto waelewe kuwa wao ni sehemu ya “kazi ya ajabu” ya Bwana (Isaya 29:14) ya siku za mwisho?

Shughuli Yamkini

  • Onesha picha ya baadhi ya matukio ya ajabu ambayo yalitukia wakati injili ilipokuwa inarejeshwa (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 90–95, au ukurasa wa shughuli ya wiki hii). Someni pamoja Isaya 29:14, 18,24, na waalike watoto watafute maneno na virai ambavyo vinahusiana na matukio katika picha. Waulize watoto ni jinsi gani wanaweza kusaidia kwenye “kazi ya ajabu” ya Bwana (mstari wa14).

  • Elezea tukio fupi lenye kuwasaidia watoto kuelewa urejesho maana yake ni nini. Kwa mfano, zungumza kuhusu kitu ambacho kilikuwa kimepotea na jinsi ulivyokipata. Wasaidie watoto walinganishe hili na Urejesho wa injili. Kulingana na Isaya 29:13–15, kwa nini tunahitaji Urejesho? Ni kazi zipi za ajabu Bwana alizifanya ili kurejesha injili Yake?

Isaya 14:3; 25:8; 28:16

Mafundisho ya Isaya yananielekeza mimi kwa Yesu Kristo.

Mafundisho ya Isaya yanaweza kuwaelekeza watoto unaowafundisha kwa Mwokozi na kuwasaidia kukumbuka mambo ambayo Yeye amefanya kwa ajili yao.

Shughuli Yamkini

  • Andika marejeleo yafuatayo ya maandiko kwenye vipande tofauti vya karatasi: Isaya 14:3; Isaya 25:8; Isaya 28:16; Mathayo 11:28–30; 1Wakorintho 15:53–57; Helamani 5:12. Toa karatasi kwa watoto na waalike waandike kwenye karatasi ukweli wanaojifunza kutoka kwenye mistari na kushirikiana kuoanisha mistari ambayo inawafundisha ukweli sawa na huo. Kulingana na mistari hii, ni mambo gani makubwa Bwana amefanya kwa ajili yetu?

  • Waombe watoto wachague kifungu cha maneno kutoka Isaya 14:3; 25:8; au 28:16 ambacho kinawafundisha kuhusu Yesu Kristo. Waalike waandike kifungu cha maneno kwenye kipande cha karatasi na wachore picha ya Mwokozi ambayo wanaweza kuiweka katika nyumba zao.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto waandike ujumbe au wachore picha kuhusu kitu walichojifunza darasani leo. Wahimize kukishiriki na familia zao au mshiriki wa darasa ambaye hakuhudhuria darasa la Msingi leo.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tumia shughuli zilizopo humu ili kukidhi mahitaji ya watoto wenye ulemavu. Mabadiliko madogo kwenye shughuli yanaweza kuhakikisha kwamba watoto wote wanajifunza. Kwa mfano, kama shughuli inapendekeza kuonesha picha, mnaweza kuimba wimbo badala yake ili kuwajumuisha watoto wenye mapungufu ya kuona.

Chapisha