Miito ya Misheni
Sura ya 1: Timiza Dhumuni Lako la Umisionari


“Sura ya 1: Timiza Dhumuni Lako la Umisionari,” Hubiri Injili Yangu: Mwongozo wa Kushiriki Injili ya Yesu Kristo (2023)

“Sura ya 1,” Hubiri Injili Yangu

Picha
Dan Jones akihubiri

Dan Jones, mmojawapo wa wamisionari mashuhuri katika kipindi hiki cha maongozi ya Mungu, anahubiri injili huko Wales.

© 1993 Clark Kelley Price. Usinakili.

Sura ya 1

Timiza Dhumuni Lako la Umisionari

Dhumuni Lako: Waalike wengine waje kwa Kristo kwa kuwasaidia wapokee injili ya urejesho kupitia imani katika Yesu Kristo na Upatanisho Wake, toba, ubatizo, kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu na kuvumilia hadi mwisho.

Zingatia Hili

  • Dhumuni langu ni nini kama mmisionari?

  • Ni mamlaka yapi na nguvu zipi huja pamoja na wito wangu?

  • Ni kwa jinsi gani ninategemea, ninatambua, na kufundisha kwa Roho?

  • Injili ya Yesu Kristo ni nini?

  • Ujumbe wa Urejesho ni nini? Kwa nini ujumbe huo ni muhimu sana?

  • Jukumu langu ni lipi katika kustawisha na kujenga Kanisa la Yesu Kristo?

  • Ni kwa jinsi gani nitajua kama mimi ni mmisionari mwenye mafanikio?

Wajibu Wako wa Kufundisha Injili ya Urejesho ya Yesu Kristo.

Umezungukwa na watu. Unapishana nao mtaani na unasafiri miongoni mwao. Unawatembelea majumbani mwao, na unaungana nao mtandaoni. Wote ni watoto wa Mungu— kaka na dada zako. Mungu anawapenda kama vile Yeye anavyokupenda wewe.

Wengi wa watu hawa wanatafuta kujua dhumuni la maisha yao. Wanahangahika kwa ajili ya siku zao za usoni na za familia zao. Wanahitaji hisia ya kujumuishwa ambayo huja kutokana na kujua wao ni watoto wa Mungu na ni washiriki wa familia Yake ya milele. Wanataka kuhisi usalama katika ulimwengu huu wenye maadili yanayobadilika. Wanatamani “amani katika ulimwengu huu na uzima wa milele katika ulimwengu ujao” (Mafundisho na Maagano 59:23).

Wengi “wamezuiliwa kuupata ukweli kwa sababu tu hawajui mahali pa kuupata”Mafundisho na Maagano 123:12). Injili ya Yesu Kristo, kama ilivyorejeshwa kupitia Nabii Joseph Smith, inatoa ukweli wa milele. Ukweli huu unajibu mahitaji ya kiroho ya watu na huwasaidia watimize matamanio yao ya kina.

Kama mwakilishi aliyeidhinishwa wa Yesu Kristo, unafundisha kwamba “ukombozi unakuja kupitia Masiya Mtakatifu” (2 Nefi 2:6). Unawaalika watu waje kwa Kristo na wawe waongofu Kwake na kwenye injili Yake ya Urejesho. Wanapokubali mwaliko wako, watapata furaha kuu, tumaini, amani, na dhumuni.

Ili kuja kwa Mwokozi, watu wanahitaji kuwa na imani katika Yeye. Unaweza kuwasaidia wakuze imani hii wakati:

  • Unapowafundisha injili ya urejesho ya Yesu Kristo na kushuhudia ukweli wake.

  • Unapowaalika waweke ahadi ya kuishi kulingana na mafundisho yake.

  • Unapofuatilia na kuwasaidia wao watende juu ya ahadi walizoziweka.

  • Unapowasaidia wapate uzoefu ambao kupitia huo wanahisi ushawishi wa Roho Mtakatifu (ona 1 Nefi 10:17–19).

Imani katika Yesu Kristo itawaongoza watu kutubu. Kwa kulipa adhabu kwa ajili ya dhambi zetu, Yesu hufanya toba iwezekane. Watu wanapotubu, watatakaswa kutokana na dhambi na kukua karibu zaidi na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Watapata shangwe na amani ya kupokea msamaha.

Toba huwaandaa watu kwa ajili ya agano la ubatizo na kipawa cha Roho Mtakatifu. “Mje kwangu,” Mwokozi alisema, “na mbatizwe katika jina langu kwamba muweze kutakaswa kwa kupokea Roho Mtakatifu, ili msimame mbele yangu bila mawaa katika siku ya mwisho.(3 Nefi 27:20).

Uelewa na ushuhuda wako wa Mwokozi na Upatanisho Wake unapokua, hamu yako ya kushiriki Injili itaongezeka. Utahisi, kama Lehi, alivyohisi “umuhimu … mkubwa kuwajulisha wakazi wa dunia kuhusu vitu hivi” (2 Nefi 2:8).

Picha
ono la Mti wa Uzima

Mti wa Uzima, na Damir Krivenko.

Kujifunza Binafsi au Kujifunza na Mwenza

Chunguza picha iliyoambatishwa pale unapojifunza ono la mti wa uzima katika 1 Nefi 8 na 11.

  • Mti wa uzima unaashiria nini katika ono hili? (Ona 1 Nefi 11:21–23.)

  • Ni nini Lehi alitamani baada ya kula lile tunda? (Ona 1 Nefi 8:10–18.)

  • Katika ono hili, watu walihitaji kufanya nini ili waweze kupokea tunda hili? Tunahitaji kufanya nini ili tupokee baraka zote za Upatanisho wa Mwokozi? Ni kwa njia gani ahadi na maagano hutusaidia tupokee baraka hizi?

  • Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia wengine wapokee matunda ya injili?

Mamlaka na Nguvu ya Wito Wako

Unaitwa na kusimikwa “[kutangaza] habari njema za shangwe kuu, hata injili isiyo na mwisho” (Mafundisho na Maagano 79:1). Kama wana wa Mosia, unaweza kufundisha kwa mamlaka na uwezo wa Mungu (ona Alma 17:2–3).

Chini ya maelekezo ya Kristo, mamlaka ya kuhubiri injili yalirejeshwa tena kupitia kwa Nabii Joseph Smith. Wakati uliposimikwa kama mmisionari, ulipokea mamlaka haya. Pamoja na mamlaka hayo huja haki, heshima, na jukumu la kumwakilisha Bwana na kufundisha injili Yake.

Mamlaka haya hujumuisha jukumu la kuishi kwa kustahili wito wako. Chukulia kusimikwa kwako kama kitu halisi. Kaa mbali na dhambi na mbali na chochote ambacho si adilifu au kichafu. Kaa mbali na njia na fikra za ulimwengu. Fuata viwango katika Viwango vya Umisionari kwa Wafuasi wa Yesu Kristo. Kama mwakilishi wa Bwana, “uwe … kielelezo kwao waaminio” (1 Timotheo 4:12). Heshimu jina la Yesu Kristo kwa matendo yako na maneno yako.

Kama nyongeza ya mamlaka, unahitaji nguvu za kiroho ili kutekeleza wito wako. Mungu hutoa nguvu za kiroho pale unapofanya kazi kwa uthabiti kuimarisha ushuhuda wako juu Yake, juu ya Yesu Kristo, na juu ya kweli za injili unazozifundisha. Yeye anakupa nguvu ya kiroho unaposali, kujifunza maandiko, na kutafuta kutekeleza dhumuni lako la umisionari. Yeye anatoa nguvu za kiroho kadiri unavyojitahidi kushika amri Zake na maagano uliyoyafanya wakati ulipopokea ibada za wokovu (ona Mafundisho na Maagano 35:24)).

Nguvu za kiroho zinaweza kujidhihirisha wakati:

Kujifunza Maandiko

Ni kwa jinsi gani unapokea na kuimarisha ushuhuda wako?

Ni kwa jinsi gani unapokea nguvu ya kiroho?

Kujifunza Binafsi

Rejelea na tafakari maagano yafuatayo uliyoyafanya kwa Mungu. Jifunze baraka ambazo Mungu ameahidi kwa wale wanaoshika maagano haya. Tafakari juu ya baraka ulizopokea kwa kuyashika maagano hayo. Andika misukumo yako katika shajara yako ya kujifunzia.

Ubatizo na Uthibitisho

Kutawazwa kwenye Ukuhani (kwa ajili ya wazee)

Endaumenti ya Hekaluni

  • Ishi sheria ya utiifu.

  • Tii sheria ya dhabihu.

  • Tii sheria ya injili ya Yesu Kristo.

  • Shika sheria ya usafi wa kimwili.

  • Shika sheria ya wakfu.

  • (Ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla, 27.2.)

Kujifunza Binafsi au Pamoja na Mwenza

Soma Yohana 15:1–16. Ni kwa njia gani Kristo ni mzabibu? Je, ni kwa jinsi gani wewe ni tawi la mzabibu huo? Je, ni kwa jinsi gani kusimikwa kwako kunahusiana na uhusiano huu?

Soma cheti chako cha utumishi. Andika hisia zako na mawazo yako kuhusu kile ulichosoma. Kila wakati unapojifunza sura hii, fikiria kurudia mchakato huu. Tazama jinsi hisia zako zinavyobadilika baada ya muda.

Kujifunza Binafsi

Soma Mafundisho na Maagano 109:13–15, 21–30, 38–39, 55–57. Mistari hii ni dondoo kutoka kwenye sala yenye mwongozo wa kiungu ya Nabii Joseph Smith kwa ajili ya Hekalu la Kirtland.

Andika orodha ya baraka ambazo Joseph Smith aliziomba kwa ajili ya waaminifu waliokuwa wamepata endaumenti katika nyumba takatifu ya Bwana. Ni zipi hisia zako kuhusu baraka hizi?

Omba ili Roho Mtakatifu apate kuwa Nawe

Ulipokea kipawa cha Roho Mtakatifu wakati ulipothibitishwa kuwa muumini wa Kanisa. Kama mmisionari—na katika maisha yako yote—mojawapo ya mahitaji yako makubwa yatakuwa ni kuwa na Roho Mtakatifu pamoja nawe (ona 1 Nefi 10:17; 3 Nefi 19:9). Roho Mtakatifu ni mshiriki wa tatu wa Uungu.

Roho Mtakatifu hukuongoza, hukufundisha, na hukufariji. Yeye hukusafisha na hukutakasa. Yeye hushuhudia juu ya ukweli na hutoa ushahidi juu ya Baba na Mwana. Yeye huleta uongofu wako na uongofu wa wale unaowafundisha. (Ona 3 Nefi 27:20; 28:11; Etheri 12:41; Moroni 8:26; 10:5; Yohana 15:26.)

Roho Mtakatifu “atakuonesha vitu vyote unavyopaswa kufanya” (2 Nefi 32:5). Yeye atakuza uwezo wako na huduma yako zaidi ya vile ambavyo ungeweza kufanya wewe mwenyewe.

Kutafuta Roho Mtakatifu kuwa pamoja nawe inapaswa kuwa moja ya matamanio yako ya dhati kabisa. Utahisi wenza Wake wakati:

Picha
Rais Russell M. Nelson

“Ninawasihi muongeze uwezo wenu wa kiroho wa kupokea ufunuo. … Chagua kufanya kazi ya kiroho inayotakiwa ili kufurahia kipawa cha Roho Mtakatifu na kuisikia sauti ya Roho mara nyingi zaidi na kwa uwazi zaidi” (Rais Russell M. Nelson, “Ufunuo kwa Ajili ya Kanisa, Ufunuo kwa Ajili ya Maisha Yetu,” Liahona, Mei 2018, 96).

Jifunze Kumtambua Roho

Ni vyema zaidi kukamilisha dhumuni lako la umisionari pale unapojifunza kutambua na kufuata mwongozo kutoka kwa Roho Mtakatifu. Roho kwa kawaida huwasiliana kimya kimya, kupitia hisia zako na mawazo yako. Jitolee mwenyewe kutafuta, kutambua, na kufuata hii misukumo ya upole. Inakuja katika njia nyingi (ona sura ya 4; ona pia Mafundisho na Maagano 8:2–3; 11:12–14; Wagalatia 5:22–23).

Fundisha kupitia Roho

Injili ya Yesu Kristo ni “uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye” (Warumi 1:16). Kwa sababu hiyo, ujumbe wa Urejesho wa injili unahitaji kufundishwa kwa uwezo mtakatifu—uwezo wa Roho Mtakatifu.

Bwana alisema, “Roho atatolewa kwenu kwa sala ya imani; na msipompokea roho msifundishe” (Mafundisho na Maagano 42:14; ona pia 50:13–14, 17–22.) Unapofundisha kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, Yeye:

Bwana atakubariki sana kadiri unavyotafuta, kutegemea, na kufundisha kwa Roho Mtakatifu (ona Sura ya 4 na10).

Picha
Mmoja Mmoja, na Walter Rane

Injili ya Kristo na Mafundisho ya Kristo

Injili ya Yesu Kristo huelezea vyote, ujumbe wako na dhumuni lako. Hutoa vyote “nini” na “kwa nini” ya huduma yako ya umisionari. Injili Yake inajumuisha mafundisho, kanuni, sheria, amri, ibada, na maagano yote muhimu kwa ajili ya wokovu na kuinuliwa.

Ujumbe wa injili ni kwamba tunaweza kupata nguvu ya kuokoa, ya kukomboa ya Yesu Kristo kwa kutumia imani katika Yeye, kutubu, kubatizwa, kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu, na kuvumilia hadi mwisho (ona 3 Nefi 27:13–22).

Hili pia linajulikana kama mafundisho ya Kristo. Kuishi mafundisho haya ndiyo jinsi tunavyoweza kuja kwa Kristo na kuokolewa (ona 1 Nefi 15:14). Hii inafundishwa kwa nguvu zaidi katika Kitabu cha Mormoni (ona 2 Nefi 31; 32:1–6; 3 Nefi 11:31–40). Dhumuni lako ni kuwasaidia watu waje kwa Kristo kwa kuwasaidia wayaishi mafundisho Yake.

Picha
Hyrum Smith

“Hubiri kanuni za kwanza za Injili—zihubiri tena na tena; utaona kwamba siku baada ya siku, mawazo mapya na nuru ya ziada juu yake vitafunuliwa kwako. Unaweza kuzipambanua zaidi kiasi cha kuzielewa kwa uwazi zaidi. Kisha utaweza kuzifanya zieleweke kwa uwazi zaidi kwa wale unaowafundisha” (Hyrum Smith, in History, 1838–1856 [Manuscript History of the Church– 30 1844], 1994, josephsmithpapers.org).

Kujifunza Maandiko

Je, maandiko na tangazo lifuatalo vinafundisha nini kuhusu injili ya Yesu Kristo na mafundisho ya Kristo? Tengeneza mihutasari katika shajara yako ya kujifunzia ili ikusaidie uelewe na ukumbuke.

Picha
Nguvu ya Kuongoa ya Kitabu cha Mormoni, na Ben Sowards

Imani katika Yesu Kristo

Imani ndiyo msingi wa kanuni zingine zote za injili. Ni kanuni ya tendo na nguvu.

Imani yetu inahitaji kuwa na kiini katika Yesu Kristo ili ituongoze kwenye wokovu. Mwokozi alifunza, “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanaye wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16).

Imani katika Yesu Kristo inajumuisha kuamini kwamba Yeye ndiye Mwana Pekee wa Mungu. Ni kumtumainia Yeye kama Mwokozi wetu na Mkombozi wetu (ona Mosia 3:17: 4:6–10: Alma 5:7–15). Ni kuwa na ujasiri mkamilifu katika Yeye na neno Lake, mafundisho, na ahadi Zake. Imani yetu katika Kristo hukua kadiri tunavyofuata mafundisho Yake na mfano Wake kwa kusudi halisi la moyo (ona 2 Nefi 31:6–13; 3 Nefi 27:21–22).

Kama mmisionari, wasaidie watu waweke na watimize ahadi zao ambazo zinajenga imani katika Yesu Kristo. Ahadi hizi zinawaandaa wao kupokea ibada na kufanya na kushika maagano matakatifu waliyoyafanya kwa Mungu.

Toba

Imani katika Yesu Kristo hutuongoza kutubu (ona Helamani 14:13). Toba ni mchakato wa kumgeukia Mungu na kugeuka kutoka kwenye dhambi. Tunapotubu, matendo yetu, matamanio, na fikra zetu hubadilika na kuwiana zaidi na mapenzi ya Mungu.

Kupitia dhabihu Yake ya kulipia dhambi, Mwokozi alilipia adhabu ya dhambi zetu (ona Mosia 15:9; Alma 10:34–15). Tunapotubu, tunaweza kusamehewa kwa sababu ya Yesu Kristo na dhabihu Yake, kwani Yeye hudai haki Zake za rehema kwa ajili ya wanaotubu (ona Moroni 7:27–28. Katika maneno ya nabii Lehi, “ukombozi wetu unakuja—kupitia fadhila, na rehema, na neema za Masiya Mtakatifu” (2 Nefi 2:6, 8).

Toba ni zaidi ya kufanyia mazoezi utashi wa kubadili tabia au kushinda udhaifu. Toba ni kumgeukia Kristo kwa dhati, Yeye ambaye anatupatia nguvu ya kupata “badiliko kuu” katika mioyo yetu (ona Alma 5:12–14). Inajumuisha kumkubali Roho kwa unyenyekevu na kujiweka chini ya mapenzi ya Mungu. Tunapotubu, tunaongeza ahadi yetu ya kumtumikia Mungu na kutii amri Zake. Tunazaliwa tena kiroho katika Kristo.

Toba ni kanuni chanya ambayo huleta shangwe na imani. Hutuleta “kwenye nguvu za Mkombozi, kwenye wokovu wa roho [zetu]”(Helamani 5:11).

Kuwa mkakamavu na mwenye upendo katika kuwasaidia wengine waelewe kwa nini wanapaswa kutubu. Kwa kuwaalika watu unaowafundisha kuweka ahadi, unawaalika watubu na unawapa tumaini.

Kujifunza Maandiko

Je, unaweza kujifunza nini kutoka kwenye maandiko yafuatayo kuhusu kutangaza toba?

Ubatizo

Imani katika Yesu Kristo na toba hutuandaa kwa ajili ya ibada ya ubatizo. “Na tunda la kwanza la toba ni ubatizo” (Moroni 8:25). Tunaingia lango la uzima wa milele wakati tunapobatizwa kwa kuzamishwa na mtu ambaye ana mamlaka kutoka kwa Mungu.

Wakati tunapobatizwa, tunafanya agano na Mungu. Tunaposhika agano hili, Mungu anaahidi kutupatia wenza wa Roho Mtakatifu, anatusamehe dhambi zetu, na kutupatia uumini katika Kanisa la Yesu Kristo (ona Mafundisho na Maagano 20:77, 79; Moroni 6:4). Tunakusanywa kwa Bwana na kuzaliwa tena kiroho kupitia ibada hii yenye shangwe na tumaini.

Kuwabatiza na kuwathibitisha watu unaowafundisha ni kiini cha dhumuni lako. Wasaidie waelewe kwamba ili kustahili kwa ajili ya ubatizo, wanahitaji kufikia masharti yaliyomo katika Mafundisho na Maagano 20:37.

Kujifunza na Mmisionari Mwenza

Pekua maandiko yafuatayo:

Kulingana na kujifunza kwako maandiko hapo juu, tengeneza orodha mbili zilizoandikwa:

  1. Sifa za ubatizo

  2. Maagano yanayofanywa wakati wa ubatizo.

Jadiliana na mwenza wako jinsi ya kufundisha hili kwa wengine.

Uthibitisho na Kipawa cha Roho Mtakatifu

Ubatizo huja katika sehemu mbili: ubatizo kwa maji na ubatizo kwa Roho. Baada ya kuwa tumebatizwa kwa maji, ubatizo unakamilika wakati tunapokuwa tumethibitishwa kwa kuwekewa mikono juu yetu na mtu aliye na mamlaka kutoka kwa Mungu. Kupitia uthibitisho tunaweza kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu na ondoleo la dhambi zetu.

Nabii Joseph Smith alifundisha, “Ubatizo kwa maji ni nusu tu ya ubatizo, na hauna faida yoyote bila ya nusu ile nyingine—ambayo ni, ubatizo kwa Roho Mtakatifu.”(Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith [2007],95).

Alma alifundisha, “Wanadamu wote … lazima wazaliwe mara ya pili; ndio, wazaliwe na Mungu, wabadilishwe kutoka hali yao ya kimwili na ya kuanguka, kuwa hali ya utakatifu, na kukombolewa na Mungu, na kuwa wana na mabinti zake; na hivyo wanakuwa viumbe vipya (Mosia 27:25–26).

Kwa wanaotubu, ubatizo kwa maji na kwa Roho ni kuzaliwa tena kiroho.

Kujifunza Maandiko

Ni zipi baadhi ya baraka za kuwa na kipawa cha Roho Mtakatifu?

Kwa nini tunapaswa kutamani kipawa cha Roho Mtakatifu?

Kuvumilia hadi Mwisho

Kumfuata Yesu Kristo ni ahadi ya maisha yote. Tunavumilia hadi mwisho pale tunapoendelea kote katika maisha yetu kwa kutumia imani katika Kristo, kutubu kila siku, kupokea ibada na maagano yote ya injili, kuyashika maagano hayo, na kuwa na wenza wa Roho Mtakatifu. Hii inajumuisha kufanya upya maangano tuliyoyafanya kwa kula sakramenti.

Picha
Bwana Ndiye Mchungaji Wangu, na Yongsung Kim

Bwana Ndiye Mchungaji Wangu, na Yongsung Kim. Picha kwa hisani ya Havenlight.

Injili—Njia ya Baba Yetu wa Mbinguni ya Kurudi Kwake

Injili ya Yesu Kristo inaweza kubadili jinsi tunavyoishi na nani tunakuwa. Kanuni zake siyo tu hatua ambazo kwazo tunapata uzoefu wa mara moja katika maisha yetu. Wakati tunapozirudia maishani mwetu, zinatuleta karibu sana na Mungu na kuwa mpangilio wa kuishi wenye ongezeko la thawabu. Zinaleta amani, uponyaji, na msamaha. Pia zinafafanua njia ambayo Baba yetu wa Mbinguni ameitoa kwa ajili yetu sisi ili tuwe na uzima wa milele pamoja Naye.

Injili ya Yesu Kristo huongoza jinsi gani wewe ufanye kazi kama mmisionari. Pia inazipa fokasi juhudi zako. Saidia watu wapate imani katika Yesu Kristo hadi kwenye toba (ona Alma 34:34–15). Fundisha na ushuhudie kwamba utimilifu wa injili ya Yesu Kristo na mamlaka ya ukuhani vimerejeshwa. Waalike watu wabatizwe na waishi kwa mafundisho ya Mwokozi.

Injili ya Yesu Kristo Huwabariki Watoto Wote wa Mungu

Injili ya Yesu Kristo ni kwa ajili ya watoto wote wa Mungu. Maandiko hufundisha kwamba “wote ni sawa” kwa Mungu. Yeye huwaalika “wote kuja Kwake, ili kupokea wema Wake, na hamkatazi yeyote anayemjia” (2 Nefi 26:33).

Injili hutubariki sisi katika maisha yetu yote ya duniani na milele yote. Tuna uwezekano mkubwa wa kuwa na furaha—sote kama watu binafsi na kama familia—tunapoishi kwa mafundisho ya Yesu Kristo (ona Mosia 2:41; “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu,” ChurchofJesusChrist.org). Kuishi injili huongeza shangwe yetu, hushawishi matendo yetu, na hurutubisha uhusiano wetu.

Mojawapo ya jumbe kuu za injili ya urejesho ni kwamba sisi sote ni sehemu ya familia ya Mungu. Sisi ni wana na mabinti Zake wapendwa. Bila ya kujali hali ya familia yetu hapa duniani, kila mmoja wetu ni mshiriki wa familia ya Mungu.

Sehemu nyingine kubwa ya ujumbe wetu ni kwamba familia zinaweza kuunganishwa milele. Familia imeamriwa na Mungu. Manabii wa siku za mwisho wamefundisha:

“Mpango mtakatifu wa furaha wa [Baba wa Mbinguni] unawezesha uhusiano wa familia kuendelezwa zaidi ya kaburi. Ibada takatifu na maagano yanayopatikana katika mahekalu matakatifu yanafanya iwezekane kwa watu binafsi kurudi katika uwepo wa Mungu na kwa familia kuwa zimeunganishwa milele” (“Familia: Tangazo kwa Ulimwengu”).

Watu wengi wana fursa chache za uhusiano wa ndoa au fursa za uhusiano wa familia yenye upendo. Wengi wametalikiana na wengine wana hali ngumu za kifamilia. Hata hivyo, injili hutubariki kila mtu binafsi bila kujali hali ya familia yetu. Tunapokuwa waaminifu, Mungu atatoa njia kwa ajili yetu kuwa na baraka za familia zenye upendo, iwe ni katika maisha haya au katika maisha yajayo (ona Mosia 2:41).

Ujumbe wa Urejesho: Msingi wa Imani

Bila kujali mahali unapohudumu au ni nani unayemfundisha, weka kiini cha mafundisho yako juu ya Yesu Kristo na Urejesho wa Injili Yake. Unapojifunza mafundisho katika masomo ya umisionari, utaona kwamba tuna ujumbe mmoja: Yesu ndiye Kristo, Mwokozi, na Mkombozi wetu. Kupitia nabii wa sasa, Baba wa Mbinguni amerejesha ufahamu kuhusu mpango Wake kwa ajili ya wokovu wetu. Mpango huu kiini chake ni Yesu Kristo. Kupitia dhabihu Yake ya kulipia dhambi, Mwokozi hufanya iwezekane kwetu sisi wote kuokolewa kutoka kwenye dhambi na mauti na kurudi kwa Baba wa Mbinguni.

Wasaidie watu unaowafundisha waelewe yafuatayo:

  • Mungu ni Baba yetu halisi wa mbinguni. Yeye anatupenda kikamilifu. Kila mtu hapa duniani ni mtoto wa Mungu na mshiriki wa familia Yake.

  • Baba wa Mbinguni alitoa mpango kwa ajili yetu wa kupokea kutokufa na uzima wa milele, ambazo ni baraka zake kuu (ona Musa 1:39). Tumekuja duniani kujifunza, kukua, na kujiandaa kwa ajili ya utimilifu wa baraka Zake.

  • Kama sehemu ya mpango Wake, Baba wa Mbinguni ametoa amri za kutuongoza wakati wa maisha haya na kutusaidia kurudi Kwake (ona, kwa mfano, Kutoka 20:3–17).

  • Katika maisha haya, sote tunatenda dhambi, na sisi sote tutakufa. Kwa sababu ya upendo wa Baba wa Mbinguni kwetu sisi, Yeye alimtuma Mwanaye, Yesu Kristo, kutukomboa kutokana na dhambi na mauti.

  • Kwa sababu ya dhabihu ya Yesu ya kulipia dhambi, tunaweza kutakaswa dhambi zetu pale tunapotubu na kubatizwa na kuthibitishwa. Hii inatuletea amani na kufanya iwezekane kwa sisi kurudi kwenye uwepo wa Mungu na kupokea utimilifu wa shangwe.

  • Kwa sababu ya Ufufuko wa Yesu, sisi sote tutafufuka baada ya kufa. Hii inamaanisha kwamba roho na mwili wa kila mtu vitaunganika na kuishi milele.

  • Kote katika historia ya biblia, Bwana alifunua injili Yake na kuanzisha Kanisa Lake kupitia manabii. Kila mara, watu wengi waliikataa. Mpangilio wa kuanguka kutoka kwenye injili na haja ya kulirejesha ilianza katika nyakati za Agano la Kale.

  • Baada ya kifo na Ufufuko wa Mwokozi, Mitume Wake waliongoza Kanisa kwa muda. Hatimaye, walikufa, mamlaka ya ukuhani yalipotea, na pakawa na anguko jingine kutoka kwenye mafundisho ya Mwokozi. Watu walibadili mafundisho na ibada.

  • Injili ya Yesu Kristo ilirejeshwa na Baba wa Mbinguni kupitia Nabii Joseph Smith. Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo walimtokea Joseph majira ya kuchipua ya mwaka 1820. Joseph Smith baadaye alipokea mamlaka ya ukuhani na aliagizwa kuanzisha Kanisa la Yesu Kristo tena duniani.

Fundisha kwamba Kanisa la Yesu Kristo si tu dini nyingine. Wala si kanisa la Kiamerika. Badala yake, ni urejesho wa “utimilifu wa injili ya Yesu Kristo (Mafundisho na Maagano 1:23). Kamwe halitaondolewa tena duniani.

Kitabu cha Mormoni: Ushuhuda Mwingine wa Yesu Kristo hutoa ushuhuda juu ya Yesu Kristo na kazi Yake takatifu kama Mwokozi wa dunia. Pia ni ushahidi wenye nguvu ya kwamba Yesu Kristo alirejesha injili na Kanisa Lake kupitia Nabii Joseph Smith. Waalike na uwasaidie watu wasome Kitabu cha Mormoni na wasali kuhusu ujumbe wake.

Tumaini ahadi ya kupendeza katika Moroni 10:3–5. Wahimize watu wamuulize Mungu kwa dhati na kwa nia halisi kama Kitabu cha Mormoni ni neno la Mungu. Kusali kwa nia halisi humaanisha kuwa radhi kutenda juu ya jibu ambalo huja kutokana na ushahidi wa Roho Mtakatifu. Ushahidi huo unakuwa msingi wa imani ya mtu kwamba Kristo amerejesha Kanisa Lake. Wasaidie wale unaowafundisha watafute uthibitisho huu wa Roho.

Kujifunza Maandiko

Ni kwa jinsi gani unapaswa kutumia Kitabu cha Mormoni katika kazi ya umisionari?

Kujifunza Binafsi

Fikiria unataka kuandika aya kuhusu ujumbe wa Urejesho kwenye mitandao ya kijamii au kwenye gazeti la eneo lako. Katika shajara yako, andika kichwa cha habari ambacho kinaelezea kiini cha ujumbe. Kisha andika mawazo yako na hisia zako kuhusu ujumbe huu. Jumuisha jinsi kuuelewa vyema kunavyobadilisha jinsi unavyoishi na jinsi unavyouchukulia ulimwengu unaokuzunguka.

Imarisha na Jenga Kanisa

Wakati Yesu Kristo aliporejesha Kanisa Lake, Yeye alimwelekeza Nabii Joseph Smith na wengine “kulianzisha” na “kulijenga” (Mafundisho na Maagano 31:7; 39:13). Kanisa linaanzishwa na kujengwa kama watu walio na ushuhuda wamebatizwa na kuthibitishwa, wanashika maagano yao, wanajiandaa kwenda hekaluni, na kusaidia kuimarisha kata au tawi lao.

Picha
mtu akisali

Kama mmisionari, unasaidia kuanzisha na kujenga Kanisa la Mwokozi. Kuna njia nyingi unazoweza kufanya hili. Unaweza kuwasaidia waumini wanaposhiriki injili kupitia kanuni za penda, shiriki, na alika (ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla, 23.1). Unaweza kuwasaidia watu wapokee ubatizo na kukua katika imani zao. Unaweza kuwasaidia waumini wapya wafanye marekebisho kwenye maisha yao mapya na waendelee kukua kiroho. Unaweza kuwasaidia waumini wanaorejea waimarishe imani yao katika Yesu Kristo.

Waumini wapya na wanaorejea hukua katika ushuhuda na imani wakati wanapopata uzoefu wa injili ikifanya kazi katika maisha yao. Ili kusaidia kutekeleza hili, ni muhimu kwamba:

  • Wawe na marafiki ambao ni waumini wa Kanisa.

  • Wapatiwe jukumu katika Kanisa.

  • Walishwe kwa neno la Mungu.

(Ona Gordon B. Hinckley, “Converts and Young Men,” Ensign, May 1997, 47).

Wamisionari, viongozi wenyeji, na waumini wengine wa Kanisa wanapaswa kukubali kwa moyo mkunjufu fursa ya kuwalisha na kuwaimarisha waumini wapya na waumini wanaorejea. Huduma hii husaidia “kuwaweka katika njia nzuri” (Moroni 6:4).

Kuzunguka huko na huko, Kutenda Kazi Njema

Wakati wa huduma Yake duniani, Mwokozi aliwatumikia wengine. Yeye “alizunguka huko na huko, akitenda kazi njema” na “kuhubiri injili” (Matendo ya Mitume 10:38; Mathayo 4:23). Unapofuata mfano Wake, utapata watu unaoweza kuwahudumia na ambao watakupokea.

Kupitia huduma, utatimiza amri kuu mbili kumpenda Mungu na kuwapenda majirani zetu (ona Mathayo 22:36–40; 25:40; Mosia 2:17). Kupitia huduma, wewe na wengine mnaweza kuja pamoja katika njia yenye nguvu, yenye kushawishi.

Kama mmisionari, wewe utapanga huduma kila wiki (ona Viwango vya Umisionari, 2.7 na 7.2, kwa ajili ya maelezo na mwongozo). Chini ya maelekezo ya rais wako wa misheni, unaweza kupata fursa za kuhudumu katika jamii kupitia JustServe (pale ilipoidhinishwa) na juhudi za Kanisa za huduma za kibinadamu na jitihada za kushughulikia majanga.

Wakati wote kila siku, sali na tafuta fursa ambazo hazikupangwa za kutenda wema. Msikilize Roho ili kutambua nyakati za vitendo vidogo vidogo vya ukarimu unavyoweza kuvifanya.

Picha
Rais Gordon B. Hinckley

Je, unataka kuwa na furaha? Jisahau na ujipoteze katika kazi hii kubwa. Tumia juhudi zako kuwasaidia watu. … Simama juu zaidi, wainue wale walio na magoti yaliyopooza, iinue mikono iliyolegea. Ishi injili ya Yesu Kristo” (Gordon B. Hinckley, Teachings of Presidents of the Church: Gordon B. Hinckley [2016], 209).

Kujifunza Maandiko

Je, huduma ilikuwa na nafasi gani katika maisha ya Mwokozi?

Je, huduma ilikuwa na nafasi gani katika misheni za Ammoni na Haruni?

Je, Bwana anakuomba ufanye kipi?

Mmisionari Mwenye Mafanikio

Mafanikio yako kama mmisionari yataamuliwa kimsingi na hamu yako na kujitolea kwako katika kutafuta, kufundisha, kubatiza, na kuwathibitisha waongofu na kuwasaidia wawe wafuasi waaminifu wa Kristo na waumini wa Kanisa Lake (ona Alma 41:3.).

Mafanikio yako hayaamuliwi na watu wangapi unaowafundisha au unaosaidia kuwaleta kwenye ubatizo. Wala hayaamuliwi kwa kushikilia wadhifa wa uongozi.

Ufanisi wako hautategemea jinsi wengine wanavyochagua kuitikia, mialiko yako, au vitendo vyako vya ukarimu wa dhati. Watu wana haki ya kujiamulia kuchagua kukubali ujumbe wa injili au la. Jukumu lako ni kufundisha kwa uwazi na kwa uwezo ili waweze kufanya chaguzi kwa uelewa ambao utawabariki wao.

Fikiria fumbo la Mwokozi la talanta katika Mathayo 25:14–28. Bwana wa shamba, ambaye anamwakilisha Bwana, aliwasifu watumishi wote waaminifu hata ingawa kiasi cha matoleo yao kilitofautiana (ona Mathayo 25:21, 23). Pia aliwapa wote zawadi ile ile, akiwaalika waingie “katika shangwe ya Bwana wao” kwa sababu walikuza kile walichopewa.

Mungu amekupa wewe talanta na karama za kutumia katika huduma Yake. Talanta na karama zako ni tofauti na zile za wengine. Tambua kwamba hizi zote ni muhimu, ikijumuisha zile ambazo hazionekani sana. Unapoweka wakfu talanta na karama zako Kwake, Yeye atazikuza na kufanya maajabu kwa kile unachotoa.

Epukana na kujilinganisha na wamisionari wengine na kupima matokeo ya nje ya juhudi zako na zao. Kulinganisha kawaida huishia kwenye matokeo hasi, kama vile kuvunjika moyo au kiburi. Kulinganisha pia mara nyingi kunapotosha. Kile Bwana anachotaka ni juhudi zako zilizo bora zaidi —kwako wewe “kumtumikia kwa moyo wako wote, uwezo, akili na nguvu zote” (Mafundisho na Maagano 4:2; msisitizo umeongeweza).

Unaweza kuwa na huzuni kama watu bado hawaikubali injili. Wakati mwingine unaweza kuhisi kuvunjika moyo. Hata wamisionari na manabii wakuu katika maandiko wakati mwingine walihisi kuvunjika moyo (ona 2 Nefi 4:17–19; Alma 26:27). Katika nyakati kama hizo, fuata mfano wa Nefi kwa kumgeukia Bwana, kuweka tumaini lako Kwake, kusali kwa ajili ya nguvu, na kukumbuka mambo mazuri ambayo Yeye amefanya kwa ajili yako (ona 2 Nefi 4:16–35).

Picha
wamisionari wawili wakisali

Unapomgeukia Bwana katika nyakati ngumu, Yeye ameahidi, “nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono” (Isaya 41:10). Kupitia matumizi ya imani katika Kristo, unaweza kupata amani na hakikisho kuhusu juhudi zako. Imani itakusaidia usonge mbele na uendelee katika matamanio ya haki.

Baki umefokasi katika ahadi yako kwa Kristo na dhumuni lako la umisionari—si matokeo ya nje. Matokeo haya mara nyingi si ya wazi kwa mara moja. Wakati huo huo, weka matarajio yako kuwa juu bila kujali changamoto unazokabiliana nazo. Matarajio ya juu yataongeza ufanisi wako, hamu yako, na uwezo wako wa kumfuata Roho.

Baadhi ya njia unazoweza kutathmini ahadi na jitihada zako kwa Bwana za kuwa mmisionari mwenye mafanikio zimetolewa hapo chini.

Unapokuwa umefanya vyema kadiri uwezavyo, bado unaweza kuwa na kuvunjika moyo, lakini hautavunjika moyo kwa sababu yako mwenyewe. Unaweza kuhisi kuhakikishiwa kwamba Bwana anapendezwa wakati unapohisi Roho akifanya kazi kupitia wewe.

Kujifunza Maandiko

Je, watumishi wa Bwana wanahisi vipi kuhusu kazi hii? Je, watumishi wa Bwana wanawashawishi vipi wale wanaowatumikia? Je, unahisi vipi kuhusu kazi hii?

Kujifunza Binafsi

  • Soma Helamani 10:1–5 na 3 Nefi 7:17–18. Ni kwa jinsi gani Bwana anahisi kuhusu wamisionari hawa na huduma yao?

  • Fikiria kuhusu juhudi za umisionari za Abinadi na Amoni (ona Mosia 11–18; Alma 17–20; 23–24). Kwa nini wamisionari wote wawili walikubaliwa na Bwana hata ingawa matokeo ya haraka ya juhudi zao yalikuwa tofauti?

  • Andika kile unachojifunza katika shajara yako ya kujifunzia.


Mawazo kwa ajili ya Kujifunza na Kutumia

Kujifunza Binafsi

Kujifunza Pamoja na Mwenza na Kubadilishana Mwenza

  • Chagua mmoja wa wamisionari mashuhuri wafuatao, na usome maandiko yaliyoorodheshwa. Unaposoma, jadili jinsi mmisionari huyu (1) alivyoelewa na kuweka ahadi yeye mwenyewe kwenye wito wake, (2) alivyoonesha msimamo wake na hamu ya kufanya kazi, na (3) alivyowasaidia wengine waikubali injili.

  • Chagua nyimbo mbili kuhusu Urejesho wa injili. Soma au imba nyimbo hizo. Jadili maana ya maneno hayo.

Baraza la Wilaya, Mikutano ya Kanda na Baraza la Uongozi la Misheni

  • Waalike waongofu wawili au watatu kushiriki uzoefu wa kuongoka kwao. Jinsi gani walihisi kuhusu wamisionari? Jinsi gani walihisi kuhusu kile wamisionari walichofundisha? Nini kiliwasaidia wao washike amri? Nini kilishawishi sana kuongoka kwao?

  • Siku kadhaa kabla ya mkutano, wapangie wamisionari kadhaa watafakari maswali yaliyochaguliwa kutoka kwenye “Zingatia Hili” hapo mwanzo wa sura hii. Muombe kila mmisionari kuandaa hotuba ya dakika mbili au tatu juu ya swali alilopangiwa. Wakati wa baraza la wilaya au mkutano wa kanda, waalike wamisionari watoe hotuba zao. Baada ya hotuba, jadili kile walichojifunza na jinsi ambavyo kingeweza kutumika katika kazi ya umsionari.

  • Wagawe wamisionari katika vikundi vinne. Omba kila kikundi kuorodhesha kweli, maagano, na ibada nyingi kadiri wanavyoweza ambazo zilirejeshwa na kufunuliwa kupitia Nabii Joseph Smith. Ruhusu kila kikundi kushiriki orodha yao. Waalike wamisionari kushiriki jinsi mmoja kati ya kweli hizo zilizofunuliwa kupitia Urejesho zilivyoshawishi maisha yao.

  • Jadili kile inachomaanisha kuwa mmisionari mwenye mafanikio. Waalike wamisionari watoe mifano mahususi.

Viongozi wa Misheni na Washauri wa Misheni

  • Wakati wa mahojiano au katika mazungumzo na wamisionari, mara kwa mara waombe washiriki nawe:

    • Ushuhuda wao juu ya Yesu Kristo.

    • Ushuhuda wao juu ya injili ya urejesho na misheni ya Joseph Smith.

    • Ushuhuda wao wa Kitabu cha Mormoni.

    • Fikra zao kuhusu lengo lao kama mmisionari.

  • Waalike wamisionari waandike katika shajara zao za kujifunzia kile wanachohisi ni baadhi ya malengo yao ya misheni. Wakati wa mahojiano au mazungumzo, waombe washiriki kile walichoandika.

  • Tuma barua ya pongezi kwa waongofu wapya.

Chapisha