Miito ya Misheni
Sura ya 13: Ungana na Viongozi na Waumini ili Kulijenga Kanisa


“Sura ya 13: Ungana na Viongozi na Waumini ili Kulijenga Kanisa,” Hubiri Injili Yangu: Mwongozo wa Kushiriki Injili ya Yesu Kristo (2023)

“Sura ya 13,” Hubiri Injili Yangu

Msikilize Yeye, na Simon Dewey

Sura ya 13

Ungana na Viongozi na Waumini ili Kulijenga Kanisa

Zingatia Hili

  • Ni jinsi gani ninaweza kufanya kazi na viongozi na waumini wa Kata ili Kulijenga Kanisa?

  • Viongozi wa kigingi na kata wana majukumu yapi katika kazi ya umisionari?

  • Ni nini kinapaswa kufanyika katika mkutano wa uratibu wa kila wiki kwa viongozi wa kata?

  • Ni kwa jinsi gani ninaweza kuwasaidia viongozi katika kushiriki injili na kuwaimarisha waumini wapya na wanaorejea?

Wamisionari wanafanya kazi pamoja na viongozi na waumini wenyeji katika kutafuta watu wa kuwafundisha na kuwaongoza kwa Mwokozi. Mnaunganishwa kwa upendo wenu kwa ajili ya Mungu na watoto Wake. Yeye atakuza juhudi zenu hadi kiwango ambacho mnafanya kazi kwa umoja na viongozi na waumini wenyeji. Fanya kufanya kazi pamoja nao kuwe sehemu muhimu ya malengo na mipango yako.

Unapokuja kuwajua na kuwapenda viongozi na waumini wenyeji, utaona jinsi unavyoweza kuwasaidia wao katika miito yao na juhudi za umisionari. Toa vipawa na talanta zako katika njia ambayo itawainua na kuwaimarisha.

Sura hii inaelelezea jinsi gani wewe unaweza kufanya kazi na waumini katika kushiriki injili na kuwaimarisha waumini wapya na wanaorejea. Kwa maelezo zaidi, ona sura ya 23 ya Kitabu cha Maelezo ya Jumla.

Kujifunza Binafsi au na Mwenza

Rejelea hadithi ya uongofu wa Mfalme Lamoni, mke wake na watu wake katika Alma 18–19.

  • Nafasi ya Abishi ilikuwa ipi katika uongofu huu? Ni kitu gani yeye alifanya ambacho Amoni asingeweza kufanya?

  • Unajifunza nini kutokana na mfano wake kuhusu waumini na wamisionari wakifanya kazi pamoja?

Fikiria mifano hii mingine ya waumini wakisaidia katika kazi ya umisionari:

Ni kwa jinsi gani ninaweza kuwahimiza viongozi na waumini wafuate mifano hii?

Jenga uhusiano na Viongozi na Waumini Wenyeji

Viongozi na waumini wenyeji wa Kanisa ni wenzi wako katika kazi ya Mungu. Jenga uhusiano ambao utawasaidia mfanye kazi pamoja ili kuleta injili ya urejesho kwa watoto wa Baba wa Mbinguni. Uhusiano huu unaweza kukubariki katika maisha yako yote.

Jenga urafiki wa kuaminika na halisi na viongozi na waumini wenyeji. Tembelea pamoja nao na ujifunze kuhusu familia zao, asili yao, shauku yao, na uzoefu wao Kanisani. Kuwa na upendeleo halisi katika maisha yao.

Unapotembelea, fanya hivyo kwa lengo. Onesha kwamba wewe unajishughulisha kwa shauku ya kweli katika kazi ya kutafuta na kufundisha. Heshimu muda wao na ratiba yao.

Unapokutana nao au kufundisha injili katika nyumba zao, tafuta kuwasaidia waimarishe imani yao. Kwa sala tafuta kuwa na Roho pamoja nawe. Shiriki uzoefu ulionao katika kazi ya umisionari katika eneo lako.

mkutano wa kikundi

Wasaidie Viongozi Wenyeji katika Wajibu Wao

Baadhi ya miito ya uongozi ina majukumu kwa ajili ya kazi ya umisionari. Kuyaelewa majukumu haya kunakusaidia wewe uwasaidie viongozi hawa. Maelezo yafuatayo yanatoka kwenye sura ya 23 katika Kitabu cha Maelezo ya Jumla.

Rais wa kigingi: Anashikilia funguo za ukuhani katika kigingi kwa ajili ya kushiriki injili na kuwaimarisha waumini wapya na waumini wanaorejea. Yeye na washauri wanatoa maelekezo ya jumla kwa ajili ya juhudi hizi.

Uaskofu: Huratibu pamoja na urais wa akidi ya wazee na Muungano wa Usaidizi pale wanapoongoza juhudi za kata za kushiriki injili na kuwaimarisha waumini wapya na waumini wanaorejea.

Urais wa akidi ya wazee na Muungano wa Usaidizi: Unaongoza juhudi za kila siku za kata za kushiriki injili na kuwaimarisha waumini wapya na waumini wanaorejea. Wanafanya kazi pamoja kuongoza juhudi hizi pamoja na baraza la kata chini ya uratibu wa askofu. Ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla, 8.2; 23.1 na 9.2.3.

Kiongozi wa Misheni wa Kata (kama ameitwa): Huratibu kazi ya waumini wa kata na viongozi, wamisionari wa kata, na wamisionari wa muda wote. Kama kiongozi wa misheni wa kata hajaitwa; mshiriki wa akidi ya wazee huchukua wajibu huu. Ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla, 23.5.3.

Kila mara jiulize, “Je, mimi ni baraka kwa viongozi wenyeji?” Kuza mtazamo wa “Je, ninawezaje kusaidia?

Kujifunza na Mmisionari Mwenza

Ratibuni muda wa kuzungumza kwa ufupi na kiongozi wa kata. Ulizeni jinsi mnavyoweza kumsaidia yeye vyema. Tengenezeni mipango ya kuwa bora.

mkutano wa baraza

Mikutano ya Uratibu ya Kila Wiki

Uratibu pamoja na viongozi wenyeji—ikijumuisha viongozi wa vijana—ni muhimu katika kuwa na umoja katika juhudi zako za umisionari. Kama kiongozi wa kazi ya umisionari katika kata ameitwa, yeye huendesha mikutano ya uratibu ya kila wiki. Vingivevyo, mshauri wa urais wa akidi ya wazee ambaye anachukua wajibu huu huendesha.

Katika hii mikutano mifupi, isiyo rasmi, viongozi wenyeji na wewe mnaratibu juhudi za kushiriki injili na kuwaimarisha waumini wapya na waumini wanaorejea (ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla, 23.4). Mikutano hii inaweza kuwa ya ana kwa ana au ya mtandaoni. Uratibu pia unapaswa kuwa katika njia zingine katikati ya wiki, ikijumuisha kupiga simu, kuandika ujumbe wa maandishi, na barua pepe.

Mzee Quentin L. Cook

“Juhudi za pamoja zilizounganika na fokasi pale upangaji mipango na uwekaji malengo wa wamisionari unapowiana na upangaji mipango na uwekaji malengo wa kata au tawi zinaweza kuwa msaada sana katika kukamilisha kazi ya kuikusanya Israeli” Quentin L. Cook, “Purpose and Planning,” mission leadership seminar, June 25, 2019).

Jiandae kwa ajili ya Mkutano wa Uratibu wa Kila Wiki

Wasaidie viongozi wa kata kwa kuja ukiwa umejiandaa kushiriki katika mikutano ya uratibu ya kila wiki. Kabla ya mkutano, tenga muda wakati wa kujifunza pamoja na mwenza ili kujadili jinsi mnavyoweza kushiriki ipasavyo.

Sasisha kumbukumbu zako katika app ya Hubiri Injili Yangu ili viongozi wawe na taarifa za sasa kuhusu wale unaofanya nao kazi. Andaa ripoti juu ya kazi ulizopewa kutoka katika mikutano iliyopita.

Shiriki katika Mkutano wa Uratibu wa Kila Wiki

Mikutano ya uratibu ya kila wiki imekusudiwa kufokasi kwenye mahitaji ya watu binafsi. Wakati wa mkutano, sema jinsi unavyoweza kuwasaidia waumini wa kata, ikijumuisha vijana, katika kusaidia kukidhi mahitaji ya watu binafsi.

Mkutano wa uratibu wa kila wiki kwa kawaida unashughulikia mada nne:

Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwasaidia wale wanaofundishwa? Vipengele yamkini vya mjadala:

  • Ni waumini gani wangeweza kushiriki katika masomo wiki hii inayokuja? Nani atawaalika kushiriki?

  • Changamoto zipi zipo kwa wale wanaofundishwa? Jinsi gani waumini wanaweza kusaidia ?

  • Ni mahitaji yapi yapo kwa wale waliopangiwa tarehe ya ubatizo? Je ubatizo umeshapangwa? (Ona “Ibada ya Ubatizo” katika sura ya 12.)

Ni jinsi gani tunaweza kuwasaidia wale waliobatizwa hivi karibuni? Vipengele yamkini vya mjadala:

  • Ni waumini gani wapya katika mwaka wao wa kwanza wa uumini wanahudhuria mkutano wa sakramenti? Ni kwa jinsi gani tunaweza kumsaidia yeyote ambaye haudhurii?

  • Ni waumini gani wapya wana marafiki katika kata? Ni jinsi gani akina kaka na akina dada wahudumiaji wanaweza kusaidia? Ni jinsi gani akidi za vijana na madarasa wanaweza kusaidia?

  • Ni waumini gani wapya wamepewa jukumu au wito?

  • Ni jinsi gani tunaweza kuwasaidia waumini wapya waanze kutafiti mababu zao waliokufa ili ibada za hekaluni ziweze kufanywa kwa niaba yao? Je, waumini wapya wana kibali cha hekaluni? Kama hekalu lipo karibu, ni jinsi gani tunaweza kuwasaidia waende hekaluni kufanya ubatizo kwa niaba ya mababu hawa waliokufa?

  • Ni masomo yapi kutoka kwenye sura ya 3 bado yanahitaji kufunzwa tena? Ni kwa jinsi gani waumini wanaweza kushiriki?

  • Rejelea Njia Yangu ya Agano maendeleo kwa ajili ya kila muumini mpya.

Ni jinsi gani tunaweza kuwasaida waumini wanaorejea? Vipengele yamkini vya mjadala:

  • Ni familia zipi ambazo baadhi ya wanafamilia ni waumini ambao wamisionari wanaweza kuwatembelea na kuwafundisha?

  • Ni waumini gani wanaorejea ambao wamisionari wanaweza kuwatembelea na kuwafundisha?

  • Ni waumini gani wanaorejea wana marafiki katika kata na fursa sahihi za kuhudumu?

  • Je, ni kwa jinsi gani tunaweza kuwasaida waumini hawa?

Je, ni kwa jinsi gani tunaweza kupata watu zaidi wa kuwafundisha? Vipengele yamkini vya mjadala:

  • Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwasaidia watu binafsi, ikiwa ni pamoja na vijana, na familia kutumia kanuni ya kupenda, kushiriki, na kualika? (Ona “Ungana na Waumini” katika sura ya 9.)

  • Ni jinsi gani sisi tunaweza kuwasaidia waumini, ikijumuisha viongozi wa Msingi, kuwaalika marafiki kwenye shughuli za kata?

Kujifunza na Mmisionari Mwenza

Tazameni video ya mikutano ya uratibu ya kila wiki katika Kitabu cha Maelezo ya Jumla, 23.4. Je, mlijifunza nini ambacho mngeweza kutumia katika mikutano ya uratibu ya kila wiki? Ni jinsi gani mnaweza kujiandaa vyema kujadili mahitaji na mpango pamoja na viongozi wa kata? Katika kikao chenu kinachofuata cha kupanga mipango, wekeni lengo la ni jinsi gani mtakuwa bora.

Saidia Mpango wa Kata kwa ajili ya Kushiriki Injili

Baraza la kata linatengeneza mpango rahisi kwa ajili ya kushiriki injili (ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla, 23.5.6). Jizoeshe mpango huu. Katika mikutano ya uratibu ya kila wiki, tafuta njia za kuwasaidia viongozi kufanya kazi kuelekea malengo yao. Wataarifu viongozi kila mara kuhusu kile unachofanya kuwasaidia waumini katika kushiriki injili.

Kama umealikwa kuhudhuria mkutano wa baraza la kata, jiandae kutoa taarifa za sasa juu ya maendeleo ya wale unaowafundisha na majukumu yoyote uliyopangiwa (ona Kitabu cha Maelezo Jumla, 29.2.5). Ona fursa hii kama muda wa kujenga imani na tumaini la viongozi.

watu wakisalimiana kwa kushikana mikono

Rekebisha Kulingana na Mahitaji ya Eneo Husika

Kila kata au tawi lina mahitaji ya kipekee kwa ajili yako kutohoa. Unaweza kutumikia katika tawi dogo au kata ya vijana waseja, au unaweza kuhudumu katika kata nyingi. Baadhi ya viongozi wana uzoefu mwingi na wengine wana mchache. Baadhi ya viongozi watakuwa na muda mwingi kuliko wengine.

Tafuta njia za kuwasaidia viongozi wenyeji. Wanaweza kukuomba uwasaidie waumini katika kazi zao za uhudumiaji. Wanaweza kukuomba uwahimize waumini wapya wawaalike rafiki zao wahudhurie kanisani. Unaweza kutoa umaizi wa thamani kuhusu kazi ya umisionari wakati viongozi na waumini wanapojifunza njia za kushiriki injili.

Pale ambapo Kanisa ni jipya kiasi, viongozi wa tawi wanaweza kukuomba uwasaidie waumini wapya waelewe jinsi Bwana alivyolipanga Kanisa Lake.

Kazi yako na viongozi inaweza kuwa tofauti katika maeneo tofauti, lakini shughuli hizi zote ni muhimu katika kuwabariki watu binafsi na kuanzisha Kanisa la Bwana.

Wasaidie Waumini na Viongozi Wapende, Washiriki, na Waalike

Wahimize waumini washiriki injili katika njia za kawaida na za asili kabisa. Kitabu cha Maelezo ya Jumla hutoa maelekezo na video za kuwasaidia waumini wafanye hivi kwa kuishi kanuni za kupenda, kushiriki, na kualika (ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla, 23.1.1, 23.1.2, na 23.1.3). Weka kanuni hizi akilini wakati unapofanya kazi na viongozi.

Utakuwa baraka kwa viongozi pale unapowasaidia katika juhudi zao katika kazi hii. Kama matokeo, mifano yao itawasaidia waumini kujihusisha zaidi katika kushiriki injili na kuwaimarisha waumini wapya na waumini wanaorejea.

Ona “Ungana na Waumini” katika sura ya 9 kwa ajili ya mawazo kuhusu kuwasaidia waumini katika juhudi zao za kushiriki injili.

Kujifunza Maandiko

Jifunze mistari ifuatayo. Ni jinsi gani Mwokozi na wafuasi hawa walipenda, walishiriki, na kualika? Ni matendo yapi mifano hii inayachochea katika ufundishaji wako? Ni kwa jinsi gani wewe unaweza kuwasaidia waumini washiriki injili katika njia za kawaida na za asili kabisa?

Penda

Shiriki

Alika

Kila wakati unapojifunza, andika kile unachojifunza.

wanaume wakizungumza

Wasaidie Viongozi Wenyeji katika Kuwaimarisha Waumini Wapya

Wakati watu wanapobatizwa na kuthibitishwa, wanakuwa “wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu” (Waefeso 2:19; ona pia 1 Wakorintho 12:12–27). Fanya kazi na viongozi wenyeji kuwasaidia waumini wapya “kulishwa na neno zuri la Mungu, kuwaweka kwenye njia nzuri, … wakitegemea tu katika nguvu ya wokovu wa Kristo” (Moroni 6:4).

Mzee Ulisses Soares

“Waongofu wapya wanakuja katika Kanisa kwa shauku kwa sababu ya kile walichokipata. Na lazima sisi mara moja tujenge juu ya shauku hiyo. … Wamisionari wanaweza kusaidia kwa kuwatambulisha na kuwaunganisha watu wanaowafundisha na waongofu wapya kwa waumini waaminifu ambao watawafikia, kuwasikiliza, kuwaongoza, na kuwakaribisha Kanisani hata kabla ya kubatizwa. … Sisi [tunapowahudumia] wale ambao wanaingia ndani ya maji ya ubatizo, tutawaona wengi zaidi wa watoto wa Mungu wakivumilia hadi mwisho na kupokea uzima wa milele” (Ulisses S. Soares, “Convert Retention,” mission leadership seminar, June 25, 2018).

Wasaidie Waumini Wapya Wahudhurie Mkutano wa Sakramenti

Una wajibu muhimu katika kuwasaidia waumini wapya wahudhurie kanisani. Fanya kazi na viongozi ili kuhakikisha kwamba wewe au waumini wa kata mnawasaidia wahudhurie. Viashiria muhimu vikionesha uhudhuriaji kwenye mkutano wa sakramenti wa muumini mpya vinaweza kukusaidia wewe na viongozi wa kata muone wakati anapohitaji kuhimizwa zaidi.

Waumini wapya wana uwezekano mkubwa wa kuendelea kuhudhuria mkutano wa sakramenti na kupokea sakramenti wakati wanapokuwa na marafiki katika kata. Wasaidie wahisi hali ya kujumuishwa, hasa wakati wa mwaka wao wa kwanza wa kuishi injili. (Ona Mafundisho na Maagano 84:106, 108.)

Fundisha Tena Masomo katika Sura ya 3

Wasaidie waumini wapya waendelee kuimarisha imani yao katika Mwokozi Yesu Kristo na Injili Yake. Kweli na kanuni za injili huota mizizi pale waumini wapya wanapoendelea kujifunza kwa njia ya Roho.

Baada ya uthibitisho, fundisha tena masomo ya umisionari. Unaongoza katika kufundisha. Hata hivyo, ratibu pamoja na viongozi wa kata ili wamisionari wa kata au waumini wengine washiriki. Kufundisha tena masomo katika sura ya 3 ni njia muhimu ya kuwasaidia waumini “kulishwa na neno zuri la Mungu” (Moroni 6:4). Unapofundisha, wahimize waumini wapya watimize ahadi zote katika masomo.

Soma maandiko pamoja na waumini wapya, hasa Kitabu cha Mormoni, na ufundishe kanuni za injili. Wasaidie washiriki injili pamoja na marafiki na familia zao. Kila muumini mpya ana mahitaji mahususi, na unaweza kumsaidia ahisi kupendwa na kukaribishwa.

Ripoti ya Maendeleo ya Njia ya Agano na Njia Yangu ya Agano

Viongozi wenyeji wana nyenzo kwa ajili ya juhudi zao za umisionari kama vile wewe unavyofanya. Mojawapo ya hizi ni ripoti ya Maendeleo ya Njia ya Agano, inayopatikana katika app ya Vyombo vya Muumini na Nyenzo za Karani. Ripoti hii huwasaidia viongozi wenyeji waone uzoefu muhimu mtu anaouhitaji ili kuendelea kusonga mbele kwenye njia ya agano kabla na baada ya ubatizo.

Njia Yangu ya Agano ni nyenzo ya kuwasaidia waumini wapya “kubaki wamekita imani [yao] katika Yesu Kristo na kujisikia kuwa wako nyumbani katika Kanisa” (Njia Yangu ya Aganoiv). Inawatambulisha waumini wapya kwenye shughuli na fursa, kama vile historia ya familia na kuwasaidia mababu waliokufa kupokea ibada takatifu katika hekalu. Wahimize waumini wenyeji wawaongoze waumini wapya kupitia uzoefu huu. Toa usaidizi kadiri unapohitajika kufanya hivyo.

Kujifunza Binafsi au na Mwenza

Jifunze Njia Yangu ya Agano. Ulijifunza nini kuhusu wajibu wako katika kuwasaidia waumini wawaimarishe waongofu wapya? Ni kwa jinsi gani unaweza kusaidia juhudi za baraza la kata? Kila wakati unapojifunza sura hii, andika kile unachojifunza.

Wasaidie Viongozi Wenyeji katika Kuwaimarisha Waumini Wanaorejea

Baadhi ya waumini walichagua kuacha kushiriki katika Kanisa. Viongozi na waumini wengine wenyeji wanajitahidi kujenga nao uhusiano thabiti na kuwafikia. Mwokozi alisema:

“Kwani kwa hawa mtaendelea kuwahudumia; kwani hamjui kama watarudi na kutubu, na kuja kwangu kwa moyo wa lengo moja, na nitawaponya; na ndipo mtakuwa njia ya kuwaletea wokovu” (3 Nefi 18:32).

Viongozi wenyeji wanaweza kukuomba uwasaidie waumini wanaorejea wajenge imani. Mara nyingi kazi hizi zitakuwa ni pamoja na familia zilizo na wanafamilia wasio waumini. Kwa sala fikiria jinsi unavyoweza kumwalika Roho katika nyumba za waumini wanaorejea wakati unapowafundisha kanuni za injili na kuwaalika watende. Onesha usikivu na huruma kwa ajili ya wasiwasi wao.

Hali zinaporuhusu, wafundishe injili wale walio ndani ya nyumba ambao bado hawajabatizwa. Upendo na msaada wako unaweza kuwasaidia wao waimarishe imani yao katika Kristo na waongeze shauku yao ya kufanya na kushika maagano.

Ratibu na viongozi wenyeji wakati unapofanya kazi pamoja na waumini wanaorejea. Juhudi hizi zinaweza kuwa na athari ya kudumu juu ya watu binafsi na mkusanyiko wa eneo husika.

Kujifunza Maandiko

Je, ni kipi Yesu Kristo alifundisha kuhusu wale ambao wanaweza kuwa wanahangahika?

Alma na Amuleki waliwafundisha wengi ambao walikuwa wameanguka kutoka kwenye Kanisa. Ni kipi tunaweza kujifunza kutoka kwenye uzoefu huu kuhusu kuwaimarisha waumini wanaorejea?


Mawazo kwa ajili ya Kujifunza na Kutumia

Kujifunza Binafsi

  • Tumia app ya Hubiri Injili Yangu ili kuweka mipango ya kuzungumza na waumini wapya na waumini waliorejea hivi karibuni ambao wanayabadilisha maisha yao na kuhudhuria kanisani. Je, ni kitu gani kiliwasaidia zaidi? Katika shajara yako, andika mawazo yako kuhusu uzoefu wao. Umejifunza kipi ambacho kitakusaidia ufanye kazi na wale unaowafundisha kwa sasa?

  • Jifunze 2 Nefi 31:18–20, Alma 26:1–7, Alma 32:32–43, na Moroni 6. Andika kile unachojifunza kutoka kwenye mistari hii kuhusu kuwaimarisha waumini wapya.

Kujifunza Pamoja na Mwenza na Kubadilishana Mwenza

  • Someni na mjadili sura ya 23 katika Kitabu cha Maelezo ya Jumla. Ni kwa jinsi gani mnaweza kuwasaidia viongozi wenyeji katika majukumu yao?

  • Wakati wa mikutano ya uratibu ya kila wiki, waulizeni viongozi wa kata kama kuna waumini wanaorejea katika sehemu yao ambao wangependa muwatembelee wiki hii. Mnapowatembelea, tafuteni kujenga imani yao katika Yesu Kristo.

  • Watambueni wale wote ambao wamebatizwa na kuthibitishwa katika mwaka uliopita. Pitieni tena rekodi ya mmoja wao na mjadili jinsi mnavyoweza kufanya kazi na viongozi katika mkutano wa uratibu wa kila wiki ili kumsaidia mtu huyu. Andikeni mawazo na mapendekezo yenu katika app ya Hubiri Injili Yangu. Rudieni hili kwa waongofu wote wa hivi karibuni katika eneo lenu.

Baraza la Wilaya, Mikutano ya Kanda na Baraza la Uongozi wa Misheni

  • Mwalike askofu au kiongozi mwingine wa kata azungumze kuhusu kuwaimarisha waumini wapya na waumini wanaorejea. Muombe mtu huyu asisitize jinsi wamisionari wanavyoweza kusaidia.

  • Jadili mfano wa kondoo aliyepotea, shilingi iliyopotea, na mwana mpotevu (ona Luka 15). Waalike wamisionari washiriki kile wanachojifunza na jinsi wanavyoweza kukitumia katika kazi yao ya umisionari.

Viongozi wa Misheni na Washauri wa Misheni

  • Fanya kazi na viongozi wenyeji ili kuwahimiza wao wawasaidie waumini wapya:

    • Watawazwe katika ofisi ya ukuhani (kwa wanaume wa umri unaofaa).

    • Wapangiwe akina kaka wahudumiaji (na akina dada wahudumiaji kwa ajili ya wanawake).

    • Wapokee kibali cha hekaluni kwa ajili ya ubatizo wa babu zao waliofariki.

    • Waandae jina la babu yao aliyefariki ili kulipeleka hekaluni.

    • Wapokee jukumu au wito katika kata yao au tawi lao.

  • Katika kuratibu na rais wa kigingi, wafundishe viongozi wenyeji jinsi ya kuwa na mikutano inayofaa ya uratibu ya kila wiki.

  • Mara moja moja wafuatilie waumini wapya ili kujua jinsi wanavyoendelea na jinsi wamisionari na waumini wanavyoweza kusaidia.

  • Waalike waumini wapya wazungumze na wamisionari na wasimulie uzoefu wao Kanisani.