Miito ya Misheni
Sura ya 8: Kamilisha Kazi kupitia Malengo na Mipango


“Sura ya 8: Kamilisha Kazi kupitia Malengo na Mipango,” Hubiri Injili Yangu: Mwongozo wa Kushiriki Injili ya Yesu Kristo (2023)

“Sura ya 8,” Hubiri Injili Yangu

Basi, Enendeni ( Basi, Enendeni, Mkawafundishe Mataifa Yote), na Harry Anderson

Sura ya 8

Kamilisha Kazi kupitia Malengo na Mipango

Zingatia Hili

  • Kwa nini ninahitaji kuweka malengo?

  • Ni kwa jinsi gani viashiria muhimu vya uongofu vinaweza kunisaidia nifokasi kwenye maendeleo ya kiroho ya mtu binafsi.

  • Ni kwa jinsi gani ninaweka malengo, ninaweka mipango ili kuitimiza, na kutekeleza mipango yangu.

  • Ni kwa jinsi gani ninaendesha vikao vya kupanga kila wiki na kila siku?

  • Ni kwa jinsi gani ninaweza kutumia app ya Hubiri Injili Yangu ili inisaidie nikamilishe kazi?

  • Kanuni ya uwajibikaji ni nini? Ni kwa jinsi gani itabariki juhudi zangu?

Umepangiwa kusaidia katika kazi ya Bwana katika eneo mahususi. Yeye anakutaka uwabariki watu kwa upendo na ukweli Wake. Yeye anakutaka uwaalike na uwasaidie waje kwa Kristo.

Bwana anatamani kwamba wewe “ujishughulishe kwa shauku katika [hii] kazi njema.” Yeye anakuomba kwamba “[ufanye] mambo mengi mazuri kwa hiari [yako] mwenyewe, na kutekeleza haki nyingi” (Mafundisho na Maagano 58:27; ona mstari wa 26–29). Fanya yote unayoweza ili kuacha kila kata au tawi pale unapotumikia liwe imara kuliko wakati ulipowasili.

Sura hii itakusaidia ujifunze jinsi ya kuweka malengo, kuweka mipango ili kuitimiza, na kwa bidii kutekeleza mipango yako. Inaelezea viashiria muhimu kwa ajili ya uongofu, ambavyo vinaongoza juhudi zako za kuwasaidia watoto wa Mungu wapige hatua kiroho. Kisha inawasilisha mchakato rahisi wa kuweka lengo unaoweza kuutumia katika vipengele vyote vya kazi ya umisionari, ikijumuisha malengo yako binafsi na ya wenza. Pia inatoa muhtasari wa jinsi ya kuendesha vikao vya kila wiki au kila siku pamoja na mwenza wako.

Kujifunza kuweka malengo na kuweka mipango kunaweza kukubariki katika maisha yako yote. Kunaweza kukusaidia ufanye na ushike maagano na Mungu, utumikie kwa uaminifu katika Kanisa, utafute elimu, ukue katika ajira yako, na ujenge familia imara.

Kujifunza Maandiko

Je, unaweza kujifunza nini kutokana na maandiko yafuatayo kuhusu kupanga ili kukusaidie utimize kazi ya Mungu?

Yeye Aliponya Magonjwa Mengi ya Kila Aina, na J. Kirk Richards

Wasaidie Wengine Waongoke kwa Mwokozi

Fokasi kwenye Dhumuni Lako la Umisionari

Labda umejiuliza ni ni yapi kati ya majukumu yako mengi ya umisionari ni muhimu sana. Hili ni swali zuri la kufikiria unapoweka malengo na kupanga kila wiki na kila siku. Ili kusaidia kulijibu, fikiria kuhusu dhumuni lako kama mmisionari:

“Kuwaalika wengine kuja kwa Kristo kwa kuwasaidia wapokee injili ya urejesho kupitia imani katika Yesu Kristo na Upatanisho Wake, toba, ubatizo, kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu na kuvumilia hadi mwisho.”

Ruhusu ldhumuni lako la umisionari liongoze malengo na mipango yako. Fokasi juu ya jinsi gani unaweza kuwasaidia watu binafsi watumie haki yao ya kujiamulia kuwa walioongoka kwa Mwokozi na wapokee injili Yake.

Tafuta mwongozo wa Roho na ushauriane na mwenza wako unapoweka malengo na kuweka mipango. Kisha fuatilia mipango yako na utumie muda wako ipasavyo.

Rais Dallin H. Oaks

“Sisi hatuhubiri na kufundisha ili ‘kuleta watu Kanisani’ au kuongeza idadi ya waumini wa Kanisa. Hatuhubiri na kufundisha ili tu kuwashawishi watu waishi maisha bora zaidi. … Tunawaalika wote kuja kwa Kristo kwa njia ya toba na ubatizo na uthibitisho ili kufungua milango ya ufalme wa selestia kwa wana na mabinti za Mungu. Hakuna yeyote anayeweza kufanya hili” (Dallin H. Oaks, “The Purpose of Missionary Work,” missionary satellite broadcast, Apr. 1995).

Kujifunza Maandiko

Ni jinsi gani wamisionari na manabii hawa walitimiza mipango yao kwa msaada wa Bwana?

Fungamana na Viashiria Muhimu kwa ajili ya Uongofu

Viongozi wa Kanisa wametambua viashiria sita muhimu kwa ajili ya uongofu. Viashiria muhimu vinakusaidia ufokasi kwenye maendeleo ya kiroho ya watoto wa Mungu. Vimekusudiwa kukusaidia wewe ufungamanishe juhudi zako za kila siku na dhumuni lako la umisionari.

Viashiria muhimu kwa ajili ya uongofu vimeoneshwa hapo chini.

wamisionari wakisalimiana na mtu kwa kushikana mikono

Watu Wapya Wakiwa Wanafundishwa. Kila mtu (ambaye hajabatizwa) ambaye amepokea somo katika wiki fulani waliyopewa (lakini hakuwa amefundishwa katika miezi mitatu iliyopita) na alikubali miadi maalumu ya kurudi. Somo kwa kawaida hujumuisha kusali (wakati inapofaa), kufundisha angalau kanuni moja ya injili, na kutoa mwaliko.

wamisionari wakifundisha

Masomo yenye Muumini Akishiriki Idadi ya masomo yaliyotolewa katika wiki ambayo mtu (ambaye hajabatizwa) alifundishwa na muumini alishiriki.

familia ikiwa kanisani

Watu Wanaofundishwa Ambao Wanahudhuria Mkutano wa Sakramenti. Kila mtu (ambaye hajabatizwa) unayemfundisha ambaye alihudhuria mkutano wa sakramenti katika wiki iliyotolewa kwake.

familia ikisali

Watu walio na Tarehe ya Ubatizo Kila mtu ambaye amekubali kubatizwa na kuthibitishwa tarehe mahususi.

ubatizo

Watu Ambao Wamebatizwa na Kuthibitishwa. Kila muumini mpya ambaye amepokea ibada za ubatizo na uthibitsho na ambaye fomu yake iliwasilishwa kielektroniki katika wiki iliyotolewa. (Ona sura ya 12 kwa ajili ya maelezo ya ubatizo wa waongofu na kwa ajili ya taarifa za kutengeneza kumbukumbu.

wanawake kanisani

Waumini Wapya Wakihudhuria Mkutano wa Sakramenti. Kila muumini mpya ambaye Fomu yake ya Ubatizo na Uthibitisho iliwasilishwa ndani ya miezi 12 ambaye alihudhuria mkutano wa sakramenti katika wiki iliyotolewa.

Kwa muhtasari, weka kipaumbele kwenye kuwasaidia watu wachague kushiriki katika uzoefu huu. Weka kiini cha jitihada zako kwenye shughuli zifuatazo:

  • Zile ambazo zinakusaidia upate watu wapya wa kuwafundisha

  • Zile ambazo zinawasaidia watu wasonge mbele kuelekea kufanya na kushika maagano.

  • Zile ambazo zinawasaidia watu ambao wamebatizwa na kuthibitishwa katika mwaka uliopita.

Kama hauwezi kuona jinsi ambavyo juhudi zako zingeweza kumsaidia mtu aendelee katika njia ambayo inaakisiwa katika viashiria vyako muhimu, tathmini kama shughuli ni matumizi mazuri ya muda wako.

Kwa ajili ya watu unaotumia nao muda kidogo, endelea kulea matamanio yao katika injili. Ungeweza kuwaalika waumini wawafikie. Ungeweza pia kutumia teknolojia kuwahimiza na kuendelea kuwahudumia. Ona “Tumia Teknolojia” katika sura ya 9 kwa ajili ya mawazo ya ziada.

Mzee Quentin L. Cook

“Kusudi la msingi la kupanga na kuweka malengo ni kuwafanya wafuasi—ambako ni, kuwa na waongofu waliojiweka wakfu ambao wanafanya na kushika maagano matakatifu, kuanzia na agano la ubatizo linaloongoza kwenye maagano ya hekaluni” (Quentin L. Cook, “Purpose and Planning,” mission leadership seminar, June 25, 2019).

Weka Kiashiria Muhimu cha Malengo na Weka Mipango

Wakati wa kuweka mipango ya kila wiki, wewe na mwenza wako mnaweka malengo kwa ajili ya viashiria vyote muhimu. Malengo yako ya kiashiria muhimu yanapaswa kuakisi hamu yako ya kuwasaidia watu wengi wapate uzoefu wa baraka za uongofu.

Weka malengo na weka mipango ya kufanya mambo yaliyo katika udhibiti wako ambayo yanaweza kushawishi matokeo ya kiashiria muhimu. Kwa mfano:

  • Ungeweza kuweka lengo la kiashiria muhimu cha kuanza kufundisha idadi mahususi ya watu wapya kwa kipindi cha wiki. Iwe utafikia lengo hilo au la hutegemea haki ya kujiamulia ya watu wengine. Lakini fanya kile kilicho katika udhibiti wako na ukitimize. Njia mojawapo ni kuweka lengo la kuzungumza na idadi fulani ya watu wapya kila siku. Kisha panga jinsi utakavyofanya hivyo. Ona mawazo katika Kiambatisho 2 cha sura hii na katika sura ya 9.

  • Ungeweza kuweka malengo ya kiashiria muhimu ya kuwa na idadi mahususi ya waumini wapya na watu unaowafundisha wahudhurie mkutano wa sakramenti. Iwe wanakuja au hawaji hutegemea haki yao ya kujiamulia. Lakini wewe fanya kile kilicho katika udhibiti wako ili kushawishi matokeo ya kiashiria hiki muhimu. Panga wakati wa kuwaalika na jinsi ya kufuatilia.

  • Ungeweza kuweka lengo la kiashiria muhimu cha kuwa na waumini washiriki katika idadi mahususi ya masomo wakati wa wiki. Kufikia lengo hilo ama la inategemea waumini na watu unaowafundisha. Lakini fanya kile uwezacho ili kushawishi matokeo ya kiashiria hiki muhimu. Weka lengo la kufanya kazi na viongozi wa kata ili kuwa na uwepo wa waumini. Kisha panga jinsi utakavyoratibu kushiriki kwao.

Kama wenza, mnaweka malengo ya viashiria muhimu kwa ajili ya eneo lenu mwenyewe. Yafanyeni yawe na msingi kwenye (1) maendeleo ya wale unaowafundisha na (2) hitaji la kupata watu wapya wa kufundisha. Kutafuta watu wapya wa kufundisha ni hitaji endelevu.

Malengo ya kiashiria muhimu cha misheni yote yana msingi kwenye malengo yaliyowekwa na kila mwenza.

Aplikesheni ya Hubiri Injili Yangu itakusaidia ubaki umefokasi juu ya watu pale unapoweka malengo ya kiashiria muhimu. App hii pia itakusaidia ujifunze kutokana na malengo yaliyopita na kuonesha maendeleo kuelekea malengo ya sasa.

Malengo ya kiashiria muhimu na matokeo yanaripotiwa moja kwa moja kwa viongozi wako wa misheni na viongozi wa wamisionari vijana kupitia app ya Hubiri Injili Yangu.

Kuwa mwangalifu kutoweka mkazo kwenye lengo moja la kiashiria muhimu kushinda mengine. Fokasi endelevu kwenye viashiria muhimu vyote itakusaidia kwa uthabiti uwaalike wengine waje kwa Kristo na wafanye maagano.

Rais Thomas S. Monson

“Wakati utendaji unapopimwa, utendaji huboreka. Wakati utendaji unapopimwa na kuripotiwa, kiwango cha kuwa bora kinaongezeka zaidi” (ilinukuliwa na Thomas S. Monson, “Thou Art a Teacher Come from God,” Improvement Era, Dec. 1970, 101).

Fanya Kazi kwa Bidii

Bwana anatamani kwamba wewe “utende kazi … kwa bidii yote” katika huduma yako ya umisionari (Mafundisho na Maagano 107:99). Bidii ni juhudi thabiti, na ya ushupavu.

Fanya kazi kwa bidii kwenye malengo yako muhimu ya kiashiria. Waalike watu waweke ahadi ambazo zinaongoza kwenye uongofu. Jitihada zako zenye bidii zinaweza kuwavutia wachukue hatua ambazo zitawasaidia waje kwa Kristo (ona 2 Nefi 2:14–16).

Fundisha injili katika njia ambayo inakidhi mahitaji ya watu. Mafundisho, yanapoeleweka kwa njia ya Roho, yana uwezekano wa kuwashawishi watende kuliko kitu chochote kinavyoweza kuwashawishi.

Wakati huo huo, tambua kwamba malengo ya kiashiria muhimu yanategemea haki ya kujiamulia ya wengine. Kila mara heshimu haki ya watu ya kujiamulia.

Kumbuka kwamba viashiria muhimu sio mwisho wa lengo. Badala yake, vinawakilisha uwezekano wa mtu wa kuendelea kiroho kuelekea ubatizo, uthibitisho, na uongofu wa kudumu. Maendeleo halisi ya watu yatategemea chaguzi zao. Unasaidia maendeleo yao kwa kuonesha imani katika Kristo kwa niaba yao wakati unapoweka malengo, kupanga, kutenda kwa bidii, na kuwahudumia katika njia yenye mwongozo wa kiungu.

Jinsi ya Kuweka Malengo na Kuweka Mipango na Kuitimiza

Kuweka lengo na kuweka mipango ni vitendo vya imani. Malengo yanaakisi tamanio la moyo wako na ono lako la kujisaidia mwenyewe na kuwasaidia wengine waje kwa Mwokozi.

Malengo na mipango iliyozingatiwa kwa makini itakupa mwelekeo wa wazi. Yanaweza kukusaidia upate watu zaidi wa kuwafundisha. Yanaweza kukuongoza katika kuwasaidia wale unaowafundisha waimarishe imani na maendeleo yao kuelekea uongofu.

Fanya uwekaji wako wa malengo na mipango liwe tukio lenye mwongozo wa kiungu. Sali kwa bidii, onesha imani, shauriana na mwenza wako, na fuata misukumo ya Roho. Unapopanga kwa njia hii, utahisi Bwana akifanya kazi kupitia wewe ili kuwabariki wengine.

Rais M. Russell Ballard

“Lengo ni mwisho wa safari au tamati, wakati mpango ni njia ambayo kwayo utafika huko. … Kuweka malengo kimsingi ni kuanza ukiwa na mwisho akilini. Na kuweka mipango ni kutengeneza njia ya kufikia mwisho huo” (M. Russell Ballard, “Kurudi na Kupokea,” Liahona, Mei 2017, 62–63).

Kanuni kwa ajili ya Kuweka na Kutimiza Malengo

Mchakato ufuatao utakusaidia uweke na utimize malengo.

chati ya uwekaji-lengo
  1. Kwa maombi weka malengo na uweke mipango. Weka malengo ambayo ni ya kweli lakini ambayo yanaweza kukusukuma na kuhitaji imani. Epukana na kuweka malengo ambayo ni ya juu sana au ya chini sana. Panga jinsi utakavyo yakamilisha.

  2. Weka kumbukumbu na ratiba. Andika malengo yako na mipango katika ratiba yenye maelezo ya kina.

  3. Fanyia kazi mipango yako. Fanya kazi kwa bidii ili kutimiza malengo yako. Onesha imani katika Bwana ili akusaidie.

  4. Pitia tena na fuatilia. Tathmini maendeleo na andika juhudi zako kila mara. Amua nini cha kufanya kitofauti na jinsi ya kuboresha. Rekebisha mipango kadiri inavyohitajika.

Unapotumia mchakato huu wa uwekaji wa lengo, Bwana atakuza juhudi zako. Utakua katika uwezo wako kama chombo katika mikono Yake. Utaleta mazuri mengi katika kuwabariki watoto wa Baba wa Mbinguni.

Weka Malengo na Weka Mipango katika Maeneo Yote ya Kazi

Kwa maombi tafuta mwongozo wa Roho wakati unapotumia mchakato wa uwekaji-lengo kwenye vipengele vyote vya kazi ya umisionari. Baadhi ya haya yanajumuisha:

  • Kuwasaidia watu unaowafundisha wapige hatua (ona Kiambatisho 1 katika sura hii).

  • Kuwatafuta watu wapya wa kufundisha (ona Kiambatisho 2 katika sura hii).

  • Kufanya kazi na waumini na kuwahudumia watu katika jamii na kata (ona sura ya 9 na13).

  • Kufanya kazi kwa umoja na mmisionari mwenza (ona kipengele cha 6 katika “Kikao cha Kufanya Mipango Kila Wiki”).

  • Kuimarisha imani yako katika Yesu Kristo.

  • Kuboresha ujuzi wako na uwezo, ikijumuisha kujifunza lugha (ona sura ya 7).

Weka Malengo Sahihi

Epuka kuweka malengo ya kiashiria muhimu kwa ajili ya wamisionari wengine. Hata hivyo, unaweza kuwaongoza na kuwahimiza katika kutumia kanuni za kuweka lengo wanapoweka malengo yao wenyewe.

Kuwa makini usifanye ulinganishi na wengine.

Usitumie mafanikio ya malengo kama ukomo, kutambuliwa na umma au kumkosoa au kumwaibisha yeyote hadharani.

Rais Spencer W. Kimball

“Tunaamini katika kuweka malengo. Tunaishi kwa malengo. … Lengo [moja] muhimu ni kuleta injili kwa watu wote. … Lengo letu ni kupata uzima wa milele. Hilo ndilo lengo kuu zaidi duniani” (Spencer W. Kimball, regional representatives’ seminar, Apr. 3, 1975, 6).

Kuendesha Vikao vya Kuweka Mipango Kila Wiki na Kila Siku

Kuweka mipango kila wiki hukusaidia uone picha kubwa na ufokasi kwenye watu. Pia hukusaidia ufokasi kwenye shughuli ambazo ni muhimu zaidi. Kuweka mipango kila siku hunakusaidia wewe kutohoa na kujiandaa kuchukua hatua mahususi kila siku. Unataka kuwa mzalishaji, siyo tu kuwa mwenye shughuli nyingi.

Wakati wa vikao vya kuweka mipango, jiulize maswali ya msingi kuhusu kile ambacho unahisi Bwana angetaka wewe ufanye. Tafuta mwongozo wa kiungu ili kujibu maswali haya katika njia ambayo ni sahihi kwa kila hali na kila mtu. Majibu yanapaswa kisha kuongoza mipango yako.

Kikao cha Kuweka Mipango cha Kila Wiki

Fanya kikao cha kuweka mipango kila wiki pamoja na mwenza wako katika siku na wakati uliopangwa na rais wako wa misheni. Fuata hatua zilizo hapo chini.

  1. Sali na utafute mwongozo wa kiungu. Muombe Baba wa Mbinguni akuongoze katika kuweka mipango ambayo itakusaidia utimize madhumuni Yake. Muombe Yeye abariki juhudi zako za kuwasaidia watu wasonge na waje kwa Kristo.

  2. Weka malengo na weka mipango kwa ajili ya viashiria muhimu ukitumia app ya Hubiri Injili Yangu. Tumia mchakato wa uwekaji-lengo ulioelezwa mwanzoni katika sura hii. Anza na:

    • Watu ambao walibatizwa na kuthibitishwa katika mwaka uliopita.

    • Watu ambao wana tarehe ya ubatizo.

    • Watu unaowafundisha ambao wanahudhuria mkutano wa sakramenti.

    • Watu wapya wanaofundishwa.

    • Waumini wanaorejea, familia ambazo zina watu wasio waumini, na wazee watarajiwa.

    • Watu waliofundishwa hapo awali.

    Ona Kiambatisho 1 katika sura hii kwa ajili ya mawazo ya kutumia mchakato wa uwekaji-lengo katika kufanya kazi na watu unaowafundisha.

  3. Tumia mchakato wa uwekaji-lengo kupata watu wa kuwafundisha (ona Kiambatisho 2 katika sura hii na sura ya 9 kwa ajili ya msaada kwenye utafutaji).

  4. Tumia mchakato wa uwekaji-lengo kujenga mahusiano na viongozi wa kata na waumini. Weka malengo na weka mipango kwa ajili ya jinsi utakavyowasaidia katika juhudi zao za kushiriki injili (ona mawazo katika sura ya 9 na 13). Jiandae kwa ajili ya mkutano wa uratibu katika kata wa kila wiki (ona sura ya 13).

  5. Rejelea mipango na malengo yako katika app ya Hubiri Injili Yangu. Thibitisha miadi na mikutano yako.

  6. Fanyeni baraza la wenza. Hii kwa kawaida hujumuisha mambo yafuatayo:

    • Kama itapendelewa, shiriki malengo binafsi yaliyo sahihi na muombe mwenza wako msaada katika kuyatimiza.

    • Jadilini nguvu ya uhusiano wenu. Jadilini changamoto zozote za kuwa watiifu au kufanya kazi katika umoja. Tatueni migongano yoyote (1) kwa kumruhusu kila mtu aeleze kwa ukamilifu maoni yake, (2) kuelewa na kukubali mashaka ya kila mmoja, na (3) kujenga suluhisho pamoja ambalo linajibu mashaka yaliyo muhimu zaidi.

    • Shiriki na mwenza wako nguvu zake ni nini hasa. Mwulize maoni yake juu ya jinsi gani wewe unaweza kuwa bora.

    • Weka malengo ambayo yatawasaidia mboreshe uhusiano wenu.

    Mabaraza ya wenza yanaweza kukusaidia ukuze ujuzi muhimu ambao unaweza kuutumia kwenye maisha yako binafsi na maisha ya familia, huduma ya Kanisa, ajira, na ushirikiano mwingine.

  7. Hitimisha kwa sala.

Kikao cha Kuweka Mipango Kila Siku

Weka malengo na uweke mipango pamoja na mwenza wako kwa dakika 30 kila asubuhi. Fuata hatua zilizo hapo chini.

  1. Sali na utafute mwongozo.

  2. Rejelea maendeleo yako kufikia malengo yako ya kiashiria muhimu cha kila wiki.

  3. Rejelea mipango yako ili kuwasaidia watu unaowafundisha. Weka kipaumbele kwenye jitihada zako za kuwasaidia wale wanaopiga hatua zaidi Rekebisha malengo na mipango ya kila siku kadiri inavyohitajika.

  4. Jipe sharti kwenye matendo utakayofanya siku hiyo ili kutafuta watu wapya wa kuwafundisha na kuwasaidia watu unaowafundisha.

  5. Panga jinsi utakavyofanya kazi ya viongozi na waumini wenyeji.

  6. Hitimisha kwa sala.

Kujifunza na Mmisionari Mwenza

Pitia tena Kiambatisho 1 na Kiambatisho 2 mwisho wa sura hii kwa ajili ya mawazo kuhusu jinsi ya kutumia mchakato wa uwekaji-lengo katika kufundisha na kutafuta. Tambua jinsi unavyoweza kutumia baadhi ya mawazo haya.

Tumia App ya Hubiri Injili Yangu

Kuhusu wale ambao walibatizwa katika siku yake, Moroni alisema, “Majina yao yalichukuliwa ili wakumbukwe na kulishwa na neno zuri la Mungu, kuwaweka kwa njia nzuri” (Moroni 6:4). Kuweka kumbukumbu nzuri ni njia mojawapo unayoweza kutumia kanuni hii.

Andika Juhudi Zako

Kuweka kumbukumbu ni sehemu ya kulinda eneo lako kwa upendo na shauku. Weka kumbukumbu zako kwa usahihi na ziwe zilizosasishwa. Hii itakusaidia ukumbuke kile unachohitaji kufanya ili kuwasaidia watu.

App ya Hubiri Injili Yangu hukuruhusu uratibu na ushiriki taarifa muhimu na viongozi na waumini wenyeji juu ya maendeleo ya watu na kazi.

Fuata Miongozo ya Data na Usiri

Fuata miongozo na usiri wa kubakiza data wakati ukiandika malengo na mipango katika app ya Hubiri Injili Yangu na nyenzo zilizochapishwa. Kwa ajili ya taarifa, ona Viwango vya Umisionari kwa Wafuasi wa Yesu Kristo, 7.5.

Jiulize mwenyewe maswali yafuatayo kabla ya kuandika na kushiriki taarifa katika app ya Hubiri Injili Yangu, barua pepe, mitandao ya kijamii, muhtasari, au mawasiliano mengine:

  • Ni kwa jinsi gani mtu huyu angehisi kuhusu kile ninachokiandika?

  • Ni kwa jinsi gani mimi ningehisi kama mtu alishirki aina hii ya taarifa kunihusu mimi na wengine?

  • Je, mimi ninafuata sera za Kanisa na sheria za usiri wa data kwa ajili ya eneo langu kama nikiandika au kushiriki habari hii?

wamisionari wakisali

Uwajibikaji

Kanuni ya uwajibikaji ni ya msingi katika mpango wa milele wa Mungu (ona Alma 5:15–19, Mafundisho na Maagano 104:8, 137:9). Kanuni hii hushawishi jinsi unavyofikiri na kuhisi kuhusu jukumu takatifu ambalo Bwana amekupatia. Uwajibikaji pia hushawishi jinsi gani unavyoichukulia kazi yako.

Wakati wa huduma Yake duniani, Mwokozi alitoa majukumu kwa wafuasi Wake ili kuwasaidia wakue, waendelee, na watimize kazi Yake. Yeye pia aliwapa fursa za kutoa ripoti ya kazi walizopewa wafanye (ona Luka 9:10; 3 Nefi 23:6–13). Kama mmisionari, wajibika vile vile kwa ajili ya kazi ambazo Bwana amekupatia uzifanye.

Anza uwekaji wako malengo na kuweka mipango ukiwa na wazo kwamba utawajibika kwa Bwana kupitia sala ya kila siku. Pia unawajibika kwako mwenyewe na kwa viongozi wako wa misheni.

Kutoa ripoti kunapaswa kuwa kwa upendo, uzoefu chanya ambapo jitihada zako zinaonekana na unatambua jinsi unavyoweza kuboresha.

Kujifunza Maandiko

Kuwajibika ina maana gani?

Kwa nini haki ya kujiamulia ni muhimu katika kuwajibika?

Ni kwa jinsi gani mmisionari na kiongozi wa misheni wanapaswa kufanya kazi pamoja?

Bwana anaahidi nini kwa wale ambao ni waaminifu katika majukumu yao?


Mawazo kwa ajili ya Kujifunza na Kutumia

Kujifunza Binafsi

  • Fikiria sentensi ifuatayo kutoka kwenye barua yako ya wito: “Unapojitolea muda na usikivu wako kumtumikia Bwana, ukiacha nyuma mambo yako mengine binafsi, Bwana atakubariki kwa ongezeko la ufahamu na ushuhuda juu ya Yesu Kristo na injili Yake iliyorejeshwa.” Jiulize maswali yafuatayo, na uandike misukumo yako.

    • Ninafanya vipi katika kujitolea muda na usikivu wangu kwenye kumtumikia Bwana?

    • Nimepata uzoefu wa baraka zipi?

    • Ni kwa jinsi gani ushuhuda wangu umeimarishwa?

    • Ni kwa jinsi gani ninaweza kuboresha?

  • Chukua dakika chache kufikiria kuhusu siku zako za mwisho katika eneo la misheni. Wakati siku hiyo inapofika:

    • Unataka uhusiano wako na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo uwe vipi?

    • Ungetaka uwe nani?

    Katika shajara yako ya kujifunzia, andika majibu ya maswali yafuatayo. Tumia mchakato na uwekaji-lengo kupanga kile unachoweza kufanya sasa ili kufanya kazi kuelekea malengo haya. Andika mipango yako.

Kujifunza pamoja na Mwenza na Kubadilishana Mwenza

  • Tumieni aplikesheni ya Hubiri Injili Yangu ili kujibu maswali yaliyo hapo chini.

    • Je, kumbukumbu zote ni za sasa na ni sahihi?

    • Je, mmisionari ambaye ni mpya katika eneo atafaidika kutokana na kumbukumbu za juhudi zenu za kutafuta watu wapya wa kuwafundisha?

    • Kama mngerejelea app yenu sasa hivi, je, ingewasaidia mjue mahala watu walipo? Je, ingewasaidia mjue kuhusu maendeleo yao?

Baraza la Wilaya, Mikutano ya Kanda na Baraza la Uongozi wa Misheni

  • Waalike wamisionari washiriki uzoefu wa malengo waliyojiwekea na mipango waliyopanga ili kuwasaidia watu wapige hatua. Mifano ingeweza kujumuisha malengo na mipango ya kuwasaidia watu:

    • Wakuze imani kuu zaidi katika Mwokozi.

    • Watubu na wafanye mabadiliko ya kusonga karibu na Mungu.

    • Wabatizwe na wathibitishwe.

    • Warudi Kanisani na wafanye upya agano lao la ubatizo.

  • Soma mojawapo ya hali zifuatazo kwa wamisionari. Waruhusu wamisionari wagawanyike katika vikundi vidogo. Waruhusu kila kikundi kitumie hatua ya 1 na ya 2 katika mchakato wa uwekaji-lengo ili kuwasidia watu katika mifano hii wapige hatua kuelekea ubatizo na uthibitisho. Waruhusu kila kikundi washiriki mawazo yao.

    • Mtu unayemfundisha amekubali mwaliko wa kuhudhuria kanisani wiki hii.

    • Mtu amekubali mwaliko wa ubatizo na ameweka lengo pamoja na wewe la kubatizwa.

    • Mtu amekubali mwaliko wako wa kusoma Kitabu cha Mormoni na ameweka ahadi ya kusoma 1 Nefi 1.

  • Waalike wamisionari watumie app ya Hubiri Injili Yangu ili iwasaidie waweke malengo yenye uhalisia lakini yenye kukusaidia usonge kwa:

    • Kurejelea kiashiria muhimu cha awali cha historia na maendeleo.

    • Kuweka malengo ya kila siku, kila wiki, na kila mwezi.

    • Kuongeza watu kwenye malengo ya kiashiria muhimu.

    Jadili jinsi hatua hizi zinavyoweza kuwasaidia wamisionari wapange kwa tija zaidi pale wanapowasaidia watu wapige hatua. Waombe wamisionari wafikirie yafuatayo:

    • Ni kwa jinsi gani utatumia app ya Hubiri Injili Yangu katika siku zijazo wakati unapofanya mipango?

    • Ni njia zipi zingine umegundua za kutumia app kwa ufanisi zaidi?

Viongozi wa Misheni na Washauri wa Misheni

  • Kila mara rejelea app ya wamisionari ya Hubiri Injili Yangu Waalike washiriki jinsi wanavyoitumia kufuatilia malengo na mipango na kuwasaidia watu wapige hatua.

  • Mara kadhaa tazama vikao vya kuweka mipango vya wamisionari vya kila wiki au kila siku.

Kiambatisho 1

Tumia Mchakato wa Uwekaji-Lengo katika Kufanya Kazi na Watu Unaowafundisha

Sehemu hii hutoa mifano ya jinsi ambavyo ungeweza kutumia mchakato wa uwekaji-lengo kuwasaidia watu unaowafundisha.

1. Weka malengo na Weka Mipango

Kwa maombi fikiria mahitaji ya kiroho ya watu unaowafundisha. Weka malengo na uweke mipango ya kuwasaidia watimize mahitaji haya. Tumia app ya Hubiri Injili Yangu ili kupitia maendeleo ya kila mtu. Tumia kiashiria muhimu kwa ajili ya uongofu ili kutambua matendo ambayo yatamsaidia kila mtu achukue hatua inayofuata katika kuja kwa Kristo.

Unapoweka malengo na kuweka mipango, jiulize maswali kama haya:

  • Ni chaguzi gani mtu anafanya ambazo zinaonesha ukuaji wa imani katika Yesu Kristo?

  • Ni uzoefu upi mtu anapata kutoka kwa Roho?

  • Ni changamoto zipi ambazo yeye anakabiliana nazo?

  • Ni kipi tunaweza kujifunza kutoka kwa mtu huyu ili kumsaidia?

  • Ni kipi kinahitajika kufanyika ili kumsaidia mtu huyu akuze imani katika Yesu Kristo, amhisi na amtambue Roho, atubu, na abatizwe?

  • Ni kwa jinsi gani tunaweza kujiandaa kwa ajili ya mkutano wa uratibu wa kila wiki ili kuwajumuisha viongozi na waumini wa kata katika kumsaidia mtu huyu? (Ona sehemu ya 13.)

  • Ni malengo yapi ya kiashiria muhimu tunaweza kuyaweka ambayo yanaakisi imani yao katika Bwana?

2. Andika Kumbukumbu na Weka Ratiba ya Mipango Yako

Tumia app ya Hubiri Injili Yangu ili kuandika kumbukumbu na kutengeneza ratiba ya malengo na mipango kwa maelezo ya kina. Hii itakusaidia upangilie kazi na kutambua matendo ya kufanya kila siku. Fuata sheria za usiri wa data kwa ajili ya eneo lako.

Unapoandika na kuratibu mipango yako, jiulize maswali kama haya:

  • Ni mambo yapi mahususi tunaweza kufanya leo na wiki hii ili kusaidia maendeleo ya mtu huyu?

  • Ni mafundisho yapi au (somo) litamsaidia mtu huyu kukuza imani imara sana katika Kristo na kuishi injili? Ni kwa jinsi gani tungeweza kufundisha fundisho hili ili alielewa na aelimishwe na Roho Mtakatifu?

  • Jinsi gani na lini utathibitisha miadi?

  • Ni mialiko gani tungeweza kutoa au kufuatilia? Ni kwa jinsi gani na lini tutafuatilia?

  • Ni kwa jinsi gani na lini tutamsaidia mtu huyu ahudhurie kanisani, asome maandiko, asali, na aweke ahadi ambayo itamwongoza kwenye kufanya maagano na Mungu?

  • Ni kwa jinsi gani waumini wanaweza kushiriki?

  • Ni nyenzo zipi za mtandaoni tungeweza kushiriki na mtu huyu?

  • Ni mipango ipi ya akiba tunaweza kuiweka kama kitu fulani hakiendi tulivyopanga?

3. Fanyia kazi Mipango Yako

Kuwa na sala katika moyo wako siku nzima unapofanyia kazi mipango yako. Roho atakusaidia ujue wapi pa kwenda, kipi cha kufanya, na kipi cha kusema, na ni marekebisho yapi ya kufanya.

Wakati wa siku, jiulizeni maswali kama haya:

  • Ni kwa jinsi gani tunaweza kufanya kazi kwa imani, kumtumainia Bwana kutusaidia na kupanua juhudi zetu za kuwahudumia watoto Wake?

  • Ni kwa jinsi tunaweza kuwa wabunifu na majasiri wakati tunapoifanyia kazi mipango yetu?

  • Ni kwa jinsi gani tunaweza kutohoa mipango yetu kulingana na mahitaji na hali za watu?

Mipango daima haitaenda vile tunavyotumainia. Kuwa mwepesi kugeuka na kutumia mipango ya akiba pale inapohitajika.

4. Pitia Tena Maendeleo na Fuatilia

Pamoja na mwenza wako, rejelea maendeleo kuelekea kwenye malengo mliyoweka ya kuwafundisha watu na kuwasaidia wapige hatua. Panga njia za kufuatilia. Rekebisha mipango yako kama inavyohitajika pale unapojitahidi kufikia malengo yako.

Jiulizeni maswali kama haya:

  • Watu tunaowafundisha wanasonga mbele kuelekea kufanya maagano na Mungu?

  • Ni changamoto zipi wanakabiliana nazo? Wasiwasi wao ni upi?

  • Tunaweza kufanya kipi leo kuwasaidia na kuwatia moyo watende—ana kwa ana au kupitia teknolojia?

  • Je, wanapata uzoefu wa kumhisi Roho?

  • Je, wanaunganika na viongozi wa Kanisa na waumini na kujenga urafiki? Ni nani anaweza kushiriki wakati ujao tunapofundisha?

  • Tunaweza kujifunza kipi kutokana na vipingamizi?

  • Ni kwa jinsi gani tulifanya vyema katika kufikia malengo yetu? Kuna chochote tunapaswa kurekebisha au kukifanya tofauti?

  • Je, ni wakati wa kupunguza kuwatembelea?

Ona sura ya 11 kwa ajili kanuni na mawazo zaidi juu ya jinsi ya kufuatilia na kuwasaidia watu wapige hatua.

Kiambatisho 2

Mchakato wa Uwekaji Lengo katika Kutafuta Watu wa Kuwafundisha

Sehemu hii hutoa mifano ya jinsi ambavyo ungeweza kutumia mchakato wa uwekaji-lengo katika kutafuta watu wapya wa kuwafundisha. Tumia mchakato huu katika kuweka mipango yako kila wiki na kila siku.

1. Weka Malengo na Tengeneza Mipango

Pamoja na mwenza wako, kwa maombi fikirieni kile ambacho Baba wa Mbinguni angetaka mfanye ili kupata watu zaidi wa kuwafundisha. Fanyeni hivi kila wiki na kila siku. Kuweni na imani kwamba Yeye anawaandaa watu kwa ajili yenu (ona Mafundisho na Maagano 100: 3–8).

Wekeni malengo ya kutafuta kila siku. Wekeni mipango kwa ajili ya matendo yaliyo katika udhibiti wenu ambayo yanaathiri matokeo ya kiashiria muhimu. Mifano inajumuisha:

  • Ni watu wangapi wapya mtazungumza nao kuhusu injili kila siku.

  • Ni mara ngapi mtawauliza waumini, watu mnaowafundisha, na watu mtakaowasiliana nao kama wanamjua mtu ambaye angependa kusikia ujumbe wenu.

  • Ni upesi kiasi gani mtawashughulikia watu walioletwa kwenu na waumini au kujibu maoni kwenye mitandao ya kijamii.

Pitieni app ya Hubiri Injili Yangu na jiulizeni maswali kama haya:

  • Ni kipi Baba wa Mbinguni angetaka sisi tufanye leo na wiki hii ili kupata watu wa kuwafundisha?

  • Ni malengo yapi ya kiashiria muhimu tunaweza kuweka ili kupata watu wa kuwafundisha?

  • Ni shughuli zipi za kutafuta watu ni bora kwa muda huu wa siku na mahala?

  • Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwatia moyo na kuwasaidia waumini wa kata katika juhudi zao za kushiriki injili kupitia kanuni za penda, shiriki, na alika?

  • Ni waumini gani wapya tunaweza kuwasiliana nao ili kuwasaidia wahudhurie mkutano wa sakramenti? Je, wana marafiki wowote ambao wangeweza kuwaalika?

  • Ni kwa jinsi gani tunaweza kufanya kazi na baraza la kata au washiriki katika mkutano wa kata wa uratibu wa kila wiki ili kutambua familia zenye watu ambao si waumini, waumini wanaorejea, na wazee watarajiwa wa kuwasiliana nao?

  • Ni watu gani ambao kwa sasa wanafundishwa, watu waliofundishwa zamani, na watu walioletwa kwetu na waumini tunaoweza kuwasiliana nao? Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwasiliana nao? (Ana kwa ana, kupitia teknolojia, kwa simu, au katika njia zingine)

  • Ni zipi baadhi ya njia mpya tunazoweza kuzitumia kuwatafuta watu?

  • Ni kipaji na uwezo upi binafsi tunaweza kuutumia?

  • Ni kwa jinsi gani tunaweza kuboresha uwezo wetu wa kutafuta watu?

  • Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwasaidia wale tunaowasiliana nao wahisi ushawishi wa Roho Mtakatifu?

Kwa mifano ya shughuli za kutafuta, ona sura ya 910, na 13.

Tumia app ya Hubiri Injili Yangu ili kukusaidia kutambua shughuli za kutafuta ambazo zimekuwa na ufanisi katika kipindi cha nyuma. Kwa mfano, unaweza kuona jinsi waongofu wa hivi karibuni walivyopatikana.

Tafuta mwongozo wa kiungu na kuwa muwazi kwa misukumo na mawazo mapya. Epukana na kukwama katika mazoea. Wamisionari ambao mara zote wanapata watu wapya wa kuwafundisha kila mara wanatumia njia tofauti tofauti kila wiki. Wanafanya kazi kwa uthabiti.

2. Andika Kumbukumbu na Weka Ratiba ya Mipango Yako

Pamoja na mwenza wako, tumieni app ya Hubiri Injili Yangu ili kuandika na kutengeneza ratiba ya malengo na mipango yenu kwa maelezo ya kina. Kuandika kumbukumbu na kuratibu mipango yako kutakusaidia utambue ni matendo yapi ya kufanya na ni wakati gani wa kuyafanya.

Jiulizeni maswali kama haya:

  • Ni lini na ni kwa jinsi gani tutawasiliana na watu? Ni njia ipi bora ya kuonana nao? Ni sehemu zipi bora zaidi? Ni nyakati zipi bora za siku kwa ajili ya njia tofauti za kupata watu?

  • Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwa na mazungumzo ya maana na watu tunaokutana nao?

  • Ni kwa jinsi gani na wakati gani tutatafuta mtandaoni tukitumia mitandao ya kijamii na teknolojia?

  • Ni lini tutawasiliana na watu walioletwa kwetu na waumini?

  • Ni mipango gani ya akiba tutakayoiweka kwa ajili ya wakati ambapo mipango mingine itashindwa?

3. Tendea Kazi Mipango Yako

Kwa bidii jitahidi kutimiza malengo yako ya kupata watu wa kuwafundisha. Kuwa na sala katika moyo wako katika siku nzima. Kuwa muwazi katika kuwasalimia watu na kuzungumza na watu unaokutana nao. Roho atakusaidia ujue wapi pa kwenda, kipi cha kufanya, na kipi cha kusema, na ni marekebisho yapi ya kufanya.

Wakati wa siku, jiulizeni maswali kama haya:

  • Ni kwa jinsi gani tunaweza kufanya kazi kwa imani, kumtumainia Bwana kutusaidia na kupanua juhudi zetu za kuwahudumia watoto Wake?

  • Ni kwa jinsi tunaweza kuwa wabunifu na majasiri wakati tunapoifanyia kazi mipango yetu?

  • Ni kwa jinsi gani tunaweza kutohoa mipango yetu kulingana na mahitaji na hali za watu?

  • Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwasaidia watu wahisi ushawishi wa Roho Mtakatifu?

Mipango daima haitaenda vile tunavyotumainia. Kuwa mwepesi kugeuka na kutumia mipango ya akiba pale inapohitajika.

4. Rejelea Maendeleo na Fuatilia

Kote katika siku na wiki, kwa maombi pitia tena maendeleo katika kuyafikia malengo yako ili kupata watu wa kuwafundisha. Jiulizeni maswali kama haya:

  • Ni kwa jinsi gani tulifanya vyema katika kufikia malengo yetu na kufuatilia mipango yetu?

  • Ni marekebisho yapi tungeweza kufanya ili kufikia malengo yetu ya kupata watu?

  • Ni kwa jinsi gani tunaweza kuepuka kuangukia katika mambo ya kawaida ambayo hayafai katika kutafuta watu wa kuwafundisha?

  • Ni kitu gani kipya tunachoweza kujaribu wakati huu wa siku?

  • Ni yapi baadhi ya mawazo tunayoweza kuyajadili katika mkutano wa kata wa uratibu wa kila wiki ili yatusaidie kupata watu wa kuwafundisha. (Ona sura ya 13.)

Kama wenza, tumieni chati ya “Juhudi za Kutafuta” katika sura ya 9 ili kutathmini juhudi zenu za kila wiki na kila siku za kutafuta. Tambueni mambo yale mnayofanya vizuri, na fikirieni jinsi mnavyoweza kuboresha.

Katika siku nzima, tulieni kwa dakika chake ili kutambua mkono wa Bwana katika kazi yenu.