Miito ya Misheni
Sura ya 9: Tafuta Watu wa Kuwafundisha


“Sura ya 9: Tafuta Watu wa Kuwafundisha,” Hubiri Injili Yangu: Mwongozo wa Kushiriki Injili ya Yesu Kristo (2023)

“Sura ya 9,” Hubiri Injili Yangu

Picha
Mchungaji Mwema, na Del Parson

Sura ya 9

Tafuta Watu wa Kuwafundisha

Zingatia Hili

  • Ni jinsi gani ninaweza kutumia imani katika Kristo ili kutafuta watu wa kuwafundisha?

  • Ni kwa jinsi gani tunaweza kukuza ono letu na kuboresha mipango yetu ya kutafuta watu wa kuwafundisha?

  • Ni kwa jinsi gani ninaweza kukuza uwezo wangu na kujiamini kwangu ili kuzungumza na watu ninaokutana nao kila siku?

  • Ni jinsi gani tunaweza kuungana na waumini katika kushiriki injili?

  • Tunapaswa kufanya nini wakati tunapowapokea watu walioelekezwa kwetu?

  • Ni yapi baadhi ya mawazo kwa ajili ya kutafuta watu wa kuwafundisha ambayo bado hatujayajaribu?

Mwokozi aliyefufuka aliwaambia wafuasi Wake, “Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu” (Mathayo 28:19; ona pia Marko 4:15). Bwana alirudia agizo hili katika siku yetu, “Enendeni ulimwenguni kote, [na] mkaihubiri injili” (Mafundisho na Maagano 68:8; ona pia 50:14).

Kazi ya ummisionari ni kutafuta watu, kuwafundisha, na kuwasaidia wajiandae kwa ajili ya ubatizo. Utatimiza agizo la Bwana la kufundisha injili Yake na kuwabatiza waongofu kadiri “mtakavyowapata watakaowapokea ninyi” (Mafundisho na Maagano 42:8). Hakuna kinachotendeka katika kazi ya umisionari mpaka pale unapompata mtu wa kumfundisha. Kuwa macho wakati wote kwa ajili ya nafasi ya kutambulisha injili. Jifunze kutumia njia ambazo zinafaa katika eneo lako.

Zaidi ni muhimu kufanya kazi na waumini katika kutafuta. Fanya kazi kwa bidii ili kupata kuaminika kwao. Wakati waumini wanapowaamini wamisionari, wanakuwa na uwezekano wa kuwaalika rafiki zao na wanafamilia kukutana na wewe. Watu hawa wana uwezekano mkubwa wa kuongolewa katika Bwana, kubatizwa, na kuendelea katika njia ya injili.

Upatikanaji utatokea kulingana na utayari wa mtu kuisikia injili. Muda utakuwa tofauti kwa kila mtu. Upatikanaji unaweza kutokea kama matokeo ya mchangamano wa mara ya kwanza au kutokana na michangamano mingi katika muda mrefu zaidi ya muda uliopangwa. Watu wengi wana michangamano na wamisionari au waumini wa Kanisa kabla ya kuanza kujifunza injili kwa dhati. Usisite kuwasiliana nao tena.

Juhudi zako za kutafuta zinaweza kuzaa matunda baada ya wewe kuhamishwa au hata baada ya wewe kumaliza misheni yako. Bila kujali muda au matokeo, Bwana ana shukrani kwa ajili ya juhudi zako.

Sura hii inatoa muhtasari wa kanuni na mawazo ya kukusaidia kutafuta. Kanuni hizi ni za ulimwenguni kote. Hata hivyo, wamisionari na viongozi wa misheni wanaweza kuhitaji kuzibadili kulingana na hali zao.

Tumia Imani ili Kutafuta Watu wa Kuwafundisha

Popote pale unapohudumu, Bwana amekuita kufanya kazi “kwa ajili ya wokovu wa nafsi” (Mafundisho na Maagano 100:4). Ili kufanya hivi, unahitaji kutumia imani katika Kristo ili kutafuta watu wa kuwafundisha ili waweze kuchagua kumfuata Yeye na kubatizwa.

Imani ni kanuni ya matendo na nguvu. Kuwa na imani kwamba Bwana anawaanda watu kuipokea injili ya urejesho. Kuwa na subira ya ujasiri kwamba Yeye atakuongoza wewe kwao, au wao kwako. Fanyia kazi imani yako kwa kuweka malengo, kuweka mipango, na kutekeleza mipango yako ya kutafuta watu wa kuwafundisha (ona sura ya 8).

Picha
wamisionari wakisali

Sali kwa imani wakati unapotafuta msaada wa Mungu ili kupata watu wa kuwafundisha. Wakati Alma alipoongoza misheni kwa Wazoramu, yeye alisali: “Ee Bwana, utukubalie sisi kwamba tuwe na mafanikio kwa kuwaleta kwako tena katika Kristo. Tazama, Ee Bwana, roho zao ni za thamani … ; kwa hivyo, tupe sisi Ee Bwana, uwezo na hekima kwamba tuwalete [wao] tena kwako” (Alma 31:34–35).

Watu unaokutana nao kila mara hawatambui kwamba wanatafuta injili ya urejesho mpaka pale watakapoipata. Kwa mfano, muongofu mmoja alisema, “Nilipoisikia injili, ilijaza shimo katika moyo wangu ambalo sikujua kama lilikuwepo pale.” Mwingine alisema, “Nimemaliza uchunguzi ambao sikujua kwamba nilikuwa nikiufanya.” Wengine wanatafuta kwa bidii ukweli lakini hawajui pa kuupata (ona Mafundisho na Maagano 123:12).

Tafuta mwongozo wa Roho wakati unapotafuta watu wa kuwafundisha. Kutafuta kwa Roho ni muhimu kama kufundisha kwa Roho. Kuwa na imani ili uweze kujua jinsi ya kuwapata wale ambao watakupokea.

Kujifunza na Mmisionari Mwenza

Kunaweza kuwa na waumini katika eneo lako ambao ni waongofu katika Kanisa. Uliza jinsi walivyolijua Kanisa. Majibu yao yanaweza kukupa umaizi wa jinsi ya kupata watu. Pia uliza jinsi walivyojua kwamba wamisionari walikuwa wanawafundisha ukweli. Fanya muhtasari wa uzoefu wao katika shajara yako ya kujifunzia.

Kujifunza Maandiko

Ni jinsi gani watoto wa Mungu wameandaliwa na kuongozwa kwenye injili ya urejesho?

Kuza Ono Lako la Kupanga Kutafuta

Unapotafuta kupata watu wa kuwafundisha, fahamu tofauti kati ya kuratibu na kupanga. Kuratibu ni kujaza chati ya upangaji wako na siku yako. Kupanga ni kufanya juhudi kwa maombi, yenye malengo ili kufokasi juu ya watu na njia bora za kuwapata.

Shughuli sahihi, katika muda sahihi na katika sehemu sahihi, zinaweza kukusaidia kupata watu wa kuwafundisha. Jiulize mwenyewe maswali yafuatayo:

  • Ni wapi tungeweza kukutana na watu ambao Bwana anaweza kuwa anawaandaa?

  • Ni sehemu gani nzuri na ni aina gani za shughuli za kuwapata watu katika nyakati mahususi za siku au wiki?

  • Ni jinsi gani tunaweza kuonesha upendo, kuwahudumia au kuleta thamani kwenye maisha yao kwa sasa?

  • Ni kwa jinsi gani tunaweza kutumia nguvu binafsi, ujuzi, na talanta ili kuwainua?

  • Mipango yetu ya akiba ni ipi kama kitu fulani hakitoi jawabu?

Jaribu kutambua njia ambazo kupitia hizo Bwana anawaandaa watu. Je, wako tayari kuzungumza na wewe? Je, wanatafuta msaada au faraja?

Fikiria kuhusu kutafuta juhudi ambazo zimekuwa na ufanisi. Ni wapi kukutana kwa mara ya kwanza kulitokea? Je, juhudi hizo ziliwajumuisha waumini wenyeji? Je, teknolojia ilitumika?

Anza kuweka mipango kwa kufokasi juu ya jinsi unavyoweza kuwabariki watu, na kisha ratiba yako itatengenezeka.

Kujifunza na Mmisionari Mwenza

Pamoja na mwenza wako, tumieni jedwali lililopo hapo chini kutathimini juhudi zenu za kutafuta watu wa kuwafundisha. Wekeni mipango ya kujaribu baadhi ya mawazo ambayo ni mapya kwenu.

Juhudi za Kutafuta

Wakati mwingine

Mara kwa mara

Karibu Kila Mara

Tunapata kuwajua waumini na kuwasaidia katika juhudi zao za kushiriki injili, ikijumuisha waumini wapya, vijana, wale ambao wanajiandaa kutumikia misheni, wamisionari wanaorejea, familia ambazo si wote waumini, na wazee watarajiwa.

Tunafanya kazi kupata kuaminika na waumini ili kwamba wawe wanafarijika kuwaalika wanafamilia wao na marafiki ili kukutana nasi.

Tunafanya kazi pamoja na viongozi wa kata katika mikutano ya uratibu ya kila wiki ili kusaidia juhudi za kutafuta na kujua kama kuna watu ambao tungeweza kuwasiliana nao.

Tunafanya kazi pamoja watu wanaofundishwa sasa, watu waliofundishwa zamani, na watu waliorejelewa na vyombo vya habari.

Tunazungumza na watu wengi kadiri tuwezavyo kila siku.

Tunajiandaa kiroho na kusali kwa ajili ya msaada wa Mungu wakati tunapopanga kutafuta watu wa kuwafundisha.

Tunaamini kwamba Bwana anawaandaa watu kwa ajili yetu kuwafundisha.

Tunafikiria jinsi ya kuwasaidia wale tunaokutana nao wahisi ushawishi wa Roho Mtakatifu.

Tunaweka malengo mahususi ya kutafuta kila wiki na kila siku (ona sura ya 8).

Kwa uthabiti tuwatafuta watu wa kuwafundisha.

Tunabuni na kutumia njia tofauti tofauti za kutafuta watu. Tunajaribu njia mpya na kuepuka kukwama katika mazoea.

Tunapanga mahususi kwa ajili ya kutafuta. Tunapanga lini, wapi, na jinsi tutakavyofokasi.

Tunazingatia ni sehemu zipi nzuri na wakati gani wa siku ungekuwa mzuri kutafuta watu wa kuwafundisha.

Tunazingatia ni shughuli zipi za kutafuta zimekuwa na ufanisi wakati uliopita.

Tunarekebisha mipango yetu ya kutafuta kama inavyohitajika na kuwa na mipango ya akiba wakati matukio yaliyopangwa yanayoshindikana.

Tunatumia app ya Hubiri Injili Yangu kutafuta, kuweka malengo na kuweka mipango, na kupitia upya na kusasisha kumbukumbu zetu kila siku.

Tunatumia vipaji na uwezo wetu binafsi kusaidia kutafuta.

Tunapanga lini na jinsi gani tutatumia mitandao ya kijamii na teknolojia nyingine ili kutafuta watu wa kuwafundisha.

Tunatumia harakati za vyombo ya habari na matoleo ya wenyeji ambayo yanatimiza haja na mahitaji ya watu katika eneo letu.

Tunajibu upesi maombi na jumbe za mtandaoni kutoka kwa watu ambao wangeweza kuwa wanapendelea.

Tunapanga posti zetu za mitandao ya kijamii mapema na kufanya kazi pamoja na waumini ili kutafuta mtandaoni.

Kuwa na Bidii katika Kutafuta

Fanya Utafutaji Uwe Jitihada Endelevu

Katika siku za mwanzoni za Kanisa lililorejeshwa, Bwana kwa kurudia rudia alilielekeza kundi la akina kaka kufundisha injili Yake, “njiani” walipokuwa wakisafiri. Yeye aliwataka watumie kila fursa ya kushiriki injili. (Ona Mafundisho na Maagano 52:9–10, 22–23, 25–27.)

Tumia maelekezo haya katika utafutaji wako. Fanya juhudi za bidii kutafuta siku nzima. Panga juhudi zako za kutafuta—na pia tafuta fursa ambazo hazikupangwa. Kutafuta watu wapya wa kuwafundisha ni hitaji la daima.

Tafuta mwongozo wa kiungu na kuwa radhi kutumia njia tofauti tofauti. Fokasi kwenye njia zenye tija zaidi katika eneo lako.

Picha
Kristo Akiwaita Petro na Andrea, na James T. Harwood

Weka Mishipi Majini

Kuhusu kazi ya ummisionari, Rais Dallin H. Oaks alisema:

“Hakuna yeyote kati yetu anayepaswa kuwa kama mvuvi ambaye hufikiria yeye amekuwa akivua siku nzima wakati kiuhalisia yeye ametumia muda wake mwingi kwenda na kurudi majini, kula chakula, na akiingiwa na wasiwasi kwenye vifaa vyake. Ufanisi wa kuvua unahusiana na ni muda kiasi gani umekuwa na mshipi wako majini, siyo ni muda kiasi gani umekuwa mbali na nyumba yako. Baadhi ya wavuvi walikuwa mbali na nyumbani kwa masaa kumi na mawili na waliweka mishipi yao majini kwa masaa kumi na mawili. Wavuvi wengine walikuwa mbali na nyumbani kwa masaa kumi na mawili na waliweka mshipi yao majini kwa masaa mawili pekee. Aina hii ya mwisho inaweza kushangaa kwa nini hawawi na mafanikio sawa na wengine.

Kanuni hiyo hiyo hutumika kwa wamisionari, ambao Bwana aliwaita ‘wavuvi wa watu’ [Mathayo 4:19]. Mshipi wa mmisionari unapaswa kutupwa kwenye maji ya uvuvi wakati yeye anapoondoka nyumbani” (semina kwa ajili ya marais wapya wa misheni, Juni 20, 2000).

Picha
Fito yingi za uvuvi

Mzee Quentin L. Cook, alifafanua kwenye ulinganifu huu. Kwa kuongezea kwenye kuacha “mshipi wako majini” kwa muda wa vipindi virefu, yeye alifundisha kwamba wamisionari ambao wanatafuta watu wa kuwafundisha “kwa uthabiti wanaweka mishipi mingi majini. …

“Wanatambua na kuwasiliana na familia zenye wanafamilia wasio waumini.

“Wanapekua [app yao ya Hubiri Injili Yangu] kwa ajili ya watu ambao wameshafundishwa kipindi cha nyuma ili kuwasiliana nao kwa simu na ujumbe mfupi.

“Wanatoa huduma kwa waumini, watu ambao walifundishwa kipindi cha nyuma, watu wanaowafundisha sasa, na jamii yote kwa ujumla. …

“Wanawasaidia waumini kutengeneza jumbe za injili ili waziweke kwenye … majukwaa yao ya mitandao ya kijamii.

“Wanapata watu kutoka kwa watu wanaowatembelea na kuwafundisha” (“Be Spiritual Pathfinders and Influencers,” missionary devotional, Sept. 10, 2020; mkazo umeongezwa).

Kujifunza na Mmisionari Mwenza

Jadilini maswali yafuatayo:

  • Ni zipi baadhi ya njia ambazo kupitia hizo mnaweza kuweka “mshipi wenu majini” kwa muda mrefu wakati wa siku?

  • Ni zipi baadhi ya njia ambazo kupitia hizo mnaweza kuweka mishipi mingi majini wakati mnapotafuta watu wa kuwafundisha?

  • Ni vipengele gani katika app ya Hubiri Injili Yangu vinaweza kuwasaidia?

  • Ni kwa jinsi gani mnaweza kutumia teknolojia kuwasaidia muweke mishipi mingi majini?

Zungumza na Kila Mtu

Kuza hamu ya kina ya kuleta nafsi kwa Kristo (ona Mosia 28:3). Unapohisi hamu hii, upendo wako na wasiwasi wako utaakisiwa katika juhudi zako za kutafuta. Upendo wako pia utaakisiwa katika mazungumzo yako.

Zungumza na watu wengi kadiri uwezavyo kila siku. Zungumza nao popote uendapo. Pale inapofaa, nenda nyumba hadi nyumba. Bwana aliwaelekeza baadhi ya wazee wa kale wa Kanisa, “Yawapasa kufumbua vinywa vyenu ili kuitangaza injili yangu.” Yeye kisha aliahidi kwamba vinywa vyao “vingejazwa” na kile ambacho wangefundisha (Mafundisho na Maagano 30:5; ona pia 33:7–10).

Vile vile, Bwana alimwambia Joseph Smith na Sidney Rigdon, “Pazeni sauti zenu kwa watu hawa; yasemeni mawazo nitakayoyaweka mioyoni mwenu.” Yeye kisha alihidi, “Mtapewa … wakati ule ule, kile mnachopaswa kusema” (Mafundisho na Maagano 100: 5–6).

Unapokutana na watu, kila mara utamhisi Roho akikusaidia ujue cha kusema. Hata hivyo, kama hauhisi msukumo, anzia tu mahali fulani—labda kwa kuuliza swali na kusikiliza jibu lao (ona “Tafuta Watu Pale Walipo” katika sura hii). Au pengine zungumza juu ya Bwana Yesu Kristo au wito wa Joseph Smith kuwa nabii wa Mungu.

Kufuata mawazo yafuatayo kunaweza kusaidia wakati unapozungumza na wale unaokutana nao:

  • Kuwa na moyo mkujufu, halisi, na wa urafiki. Tafuta njia za kuunganika na mtu na uanze mazungumzo.

  • Sikiliza kwa uaminifu kile watu wanachokisema. Tafuta kuelewa mahitaji na mapendeleo wa kila mtu. Toa msaada binafsi kadiri inavyofaa.

  • Fikiria jinsi injili inavyoweza kusaidia kukidhi mahitaji yao. Kisha fundisha ukweli wa injili wa msingi na waalike wao wajifunze zaidi. Shiriki jinsi injili ya urejesho inavyoweza kuleta tumaini kubwa na maana katika maisha yao.

  • Uliza kuhusu familia zao. Wasaidie waone jinsi injili ya urejesho inavyoweza kubariki familia zao. Jitolee kuwasaidia wapate majina ya mababu zao waliokufa.

  • Waalike waje katika mkutano wa sakramenti.

  • Toa vipeperushi au nyenzo zingine za Kanisa, zilizochapishwa na za kidijitali.

  • Shiriki nao lengo lako kama mmisionari na kwa nini uliamua kutumikia misheni.

Kanuni hizi pia zinatumika kwenye michangamano yako na waumini.

Ni kawaida kuhofia kiasi fulani kuhusu kuzungumza na watu. Sali kwa ajili ya imani na ujasiri ili kufundisha injili ya urejesho. Kila mmoja unayekutana naye ni kaka au dada yako katika familia ya Mungu. Kumbuka kwamba Yeye “hamkatazi yeyote kuja kwake, weusi, na weupe, wafungwa na walio huru, waume kwa wake; … wote wako sawa mbele za Mungu” (2 Nefi 26:33).

Kujifunza Binafsi au na Mwenza

Soma tukio kutoka kwa Victor Manuel Cabrera katika “Thirsting for the Living Water,” Ensign, Ago. 2001, 60–61. Unapofanya hivyo, tazama jinsi yeye alivyoandaliwa kuwapokea wamisionari na jinsi wamisionari walivyotumia nafasi ambazo hazikupangwa ili kumfundisha injili.

  • Ni kwa jinsi gani mtu huyu alikuwa ameandaliwa kwa ajili ya injili ya urejesho?

  • Ni kipi kingetokea kama wazee hawangeshiriki ujumbe wa injili?

  • Pitia tena kile ulichofanya jana. Je, ulizungumza na watu wengi kadiri ulivyoweza? Kama sivyo, weka malengo na mipango ya kuzungumza na watu wengi zaidi leo.

Kujifunza Maandiko

Je, unaweza kujifunza nini kutoka kwenye maandiko yafuatayo kuhusu kutafuta watu wa kuwafundisha? Je, unaweza kujifunza nini kutoka kwenye maandiko haya kuhusu kile unachopaswa kufundisha? Je! Bwana anaahidi nini?

Jiunge na Waumini

“Kuwaalika watu wote waipokee injili ni sehemu ya kazi ya wokovu na kuinuliwa” (Kitabu cha Maelezo ya Jumla, 23.0). Fanya kazi pamoja na waumini wa Kanisa kutafuta watu wa kuwafundisha. Wakati waumini wanapomleta mtu fulani kwako na kisha kushiriki katika masomo, watu wana uwezekano mkubwa wa kubatizwa na kubakia hai Kanisani.

Jenga Mahusiano Imara na Viongozi Wenyeji

Jenga mahusiano imara na uaskofu na viongozi wengine wa kata. Kiongozi wa misheni wa kata (kama ameitwa) na urais wa akidi ya wazee na urais wa Muungano wa Usaidizi ndiyo watu wako wa msingi wa kuwasiliana nao. Tafuta mwongo wao, na wasaidie katika mkutano wa kata wa uratibu wa kila wiki (ona sura ya 13).

Wakati wa mikutano ya uratibu ya kila wiki, fanya kazi na msaidizi wa akidi ya makuhani na rais wa darasa la wasichana kwa ajili ya darasa la wakubwa. Vijana hawa wana wajibu muhimu katika kushiriki injili. Wasaidie wawahimize washiriki wa akidi na darasa kushiriki injili. Njia moja ni kwa vijana kuwaalika marafiki kwenye shughuli.

Kila mara jiulize, “Je, mimi ni baraka kwa viongozi wenyeji?” Kuza mtazamo wa “Je, ninawezaje kusaidia? Kama vile Amoni katika Kitabu cha Mormoni, waendee viongozi wenyeji kwa mtazamo wa huduma (ona Alma 17:23–25.)

Kwa viongozi wa misheni, Rais Russell M. Nelson alifundisha: “Ninatumaini kwamba mtajifunza kuwapenda viongozi wenyeji na waumini. Wainue na watie msukumo. Uwezo wako wa kuunganisha shauku ya wamisionari kwa uimara na juhudi za upendo za waumini haviwezi kusisitizwa zaidi. Ufanisi wako utazidishwa kwa kasi sana” (“Hopes of My Heart,” seminar for new mission leaders, June 23, 2019).

Picha
wamisionari wakiwafundisha wanawake

Wasaidie Waumini katika Juhudi Zao za Kushiriki Injili

Kuna njia nyingi za kuwasaidia na kuwahimiza waumini washiriki injili. Wasaidie watafakari juu ya jinsi gani injili imebariki maisha yao. Wahimize “wainue juu nuru [yao] kwamba iangaze juu ya dunia” (3 Nefi 18:24).

Wasaidie waumini watumie kanuni ya kupenda, kushiriki, na kualika. Toa mifano ya njia za kawaida na za asili wanazoweza kutumia kanuni hizi.

Penda. Njia moja ya kuonesha upendo kwa Mungu ni kwa kuwapenda na kuwatumikia watoto Wake. Wahimize waumini kufikia kwa upendo kwa wanafamilia, marafiki, majirani, na wengine. Juhudi zozote za kuonesha upendo ni njia muhimu ya kushika maagano waliyoyafanya na Mungu (ona Mosia 18:9–10).

Shiriki. Kwa sababu ya upendo wao kwa ajili ya Mungu na watoto Wake, waumini kwa kawaida wanataka kushiriki baraka ambazo Yeye amewapa (ona Yohana 13:34–35). Wahimize waumini wawaambie wengine kuhusu jinsi ambavyo injili hubariki maisha yao. Wahimize wazungumze juu ya Mwokozi na ushawishi Wake. Wasaidie wahisi shangwe ya kushiriki upendo wao, muda, na matukio ya maisha. Wasaidie wajifunze jinsi ya kushiriki katika njia za kawaida na za asili—kwa urahisi kama sehemu ya kile ambacho tayari wanakifanya katika maisha yao.

Picha
Mzee Gary E. Stevenson

“Sisi sote tunashiriki vitu na wengine. Tunafanya hivi kila mara. Tunashiriki sinema na chakula gani tunakipenda, vitu vya kufurahisha tunavyoviona, mahali tunapotembelea, sanaa tunazozipenda, nukuu zinazotupatia msukumo.

“Ni kwa jinsi gani kwa urahisi tungeongeza kwenye orodha ya vitu ambavyo tayari tunashiriki kile tunachokipenda kuhusu injili ya Yesu Kristo? … Kwa kushiriki na wengine uzoefu wetu chanya katika injili, tutashiriki katika kutimiza agizo kuu la Mwokozi” (Gary E. Stevenson, “Penda, Shiriki, Alika,” Liahona, Mei 2022, 86).

Alika. Mwokozi anawaalika wote waipokee injili Yake na wajiandae kwa ajili ya uzima wa milele (ona Alma 5:33–34). Kama vile ilivyo katika kushiriki, kualika kila mara ni jambo la kawaida la kujumuisha familia, marafiki, na majirani katika kile ambacho waumini tayari wanakifanya. Wahimize waumini wasali kuhusu kuwaalika watu katika njia zifuatazo:

  • Njoo na uone. Waalike watu “waje na waone” baraka wanazoweza kupokea kupitia Yesu Kristo, Injili Yake, na Kanisa Lake.

  • Njoo na utumikie. Waalike watu “waje na wawatumikie” wengine walio na uhitaji.

  • Njoo na uwe wa mahali hapa. Waalike watu “waje na wawe wa mahali hapa” kama waumini wa Kanisa la Yesu Kristo lililorejeshwa.

Mzee Gary E. Stevenson alisema: “Kuna mamia ya mialiko tunayoweza kuitoa kwa wengine. Tunaweza kuwaalika wengine “kuja na kuona” ibada ya sakramenti, shughuli ya kata, video ya mtandaoni ambayo inaelezea injili ya Yesu Kristo. ‘Njoo na uone’ unaweza kuwa mwaliko wa kusoma Kitabu cha Mormoni au kutembelea hekalu jipya wakati wa ufunguzi wake kabla ya kuwekwa wakfu. Wakati mwingine mwaliko ni kitu tunachotoa ndani—mwaliko kwetu wenyewe, ukitupatia ufahamu na ono la fursa zinazotuzunguka, za kushughulikia” (“Penda, Shiriki, Alika,” 86).

Hakikisha unawasaidia vijana kupenda, kushiriki, na kualika. Vijana wana vipawa hasa vya kuwapenda marafiki, kushiriki kile kilicho katika mioyo yao na kuwaalika wao kwenye shughuli.

Wasaidie waumini waelewe kwamba juhudi yoyote ya kuishi kanuni ya kupenda, kushiriki, na kualika ni chanya, iwe mtu anakutana na wamisionari au anajiunga na Kanisa ama la.

Wasaidie waumini wavute nguvu zao katika kushiriki injili. Baadhi ni wazuri katika kutafuta watu wa kuwafundisha, na wengine ni walimu wazuri. Baadhi wana uwezo wa asili wa kuunganika na marafiki, hali wengine wanapenda kusali kwa ajili ya rafiki zao. Wasaidie waone kwamba kuna njia kwa ajili ya kila mmoja kushiriki.

Unapowatembelea waumini, fanya hivyo kwa lengo. Onesha kwamba unajishughulisha kwa shauku katika kazi ya kutafuta na kufundisha. Heshimu muda wao na ratiba yao.

Baadhi ya waumini wangeweza kufurahia kukuruhusu ufundishe ujumbe wako kutoka kwenye mojawapo ya masomo. Kweli za injili zinabadilisha maisha. Kuimarisha uelewa wa waumini wa injili kutaongeza tumaini lao katika wewe na kujenga msisimko wao wa kuishiriki. Wasaidie wamtambue Roho na watende juu ya misukumo.

Tafuta kupata watu wa kuwafundisha kupitia familia ambazo baadhi ya wanafamilia siyo waumini, wazee watarajiwa, waumini wanaorejea na waumini wapya. Wana uwezekano wa kuwa na wanafamilia na marafiki wengi wa madhehebu mengine.

Katika yote unayofanya pamoja na waumini, mfuate Roho na utafute kujenga imani yao katika Mwokozi, Yesu Kristo.

Kwa mawazo zaidi na nyenzo juu ya jinsi unavyoweza kuwasaidia waumini katika kushiriki injili, ona:

Ahidi Baraka kwa ajili ya Kushiriki Injili

Wasaidie waumini waelewe baraka za kupendeza za kushiriki injili. Hizi zinajumuisha:

Kujifunza na Mmisionari Mwenza

  • Pitieni tena mkutano wenu wa kila wiki wa uratibu. Jinsi gani mngeufanya uwe wa kufaa zaidi? Pitieni tena maombi kutoka kwa viongozi wa kata na pangeni jinsi gani na lini mtatoa mrejesho.

  • Pangeni jinsi mtakavyoratibu juhudi zenu za ummisonari katika mkutano wa uratibu unaofuata.

  • Jifunzeni majina ya viongozi wa kata (wanaume na wanawake). Pangeni kile mtakachokifanya wakati wa mwezi ujao ili kukuza mahusiano imara pamoja nao na kuwaunga mkono katika juhudi zao za umisionari.

Tafuta kupitia App ya Hubiri Injili Yangu

App ya Hubiri Injili Yangu ni nyenzo bora kwa ajili ya kutafuta watu wa kuwafundisha. Wamisionari ambao kwa uthabiti wanatumia vipengele katika app hii wanakuwa na ufanisi zaidi. Ili kujizoelesha vipengele hivi, rejelea mafunzo yaliyotolewa katika app hii. Kuwa msikivu kwa misukumo ya kiroho unayoweza kuipata wakati unapopitia majina ya watu.

App hii inajumuisha taarifa kuhusu watu ambao walikuwa wamerejelewa, kuwasiliana nao, au waliofundishwa. Baadhi ya watu hawa wangetaka kukutana tena na wamisionari. Wangeweza pia kuwajua watu wengine ambao wanaweza kuwa na hamu ya kujifunza kuhusu injili.

Katika kuweka mipango yako, tumia ramani na vichujio katika app hii ili kutoa kipaumbele kwa watu wa kuwatembelea. Angalia taarifa zao na jifunze jinsi walivyopatikana. Angalia kama kuna kumbukumbu kuhusu waumini ambao waliwasaidia. Tumia taarifa hii kuamua jinsi bora ya kuwafikia tena.

Picha
wamisionari wakijifunza kwenye simu

Tumia kipengele cha vichujio katika app hii kuwatambua wale wote ambao:

  • Walikuwa awali wamepangiwa tarehe ya ubatizo lakini hawakubatizwa.

  • Walihudhuria mkutano wa sakramenti angalau mara moja lakini hawakubatizwa.

  • Walipokea zaidi ya masomo matatu.

  • Hawakupigiwa simu au kutembelewa hivi karibuni.

Kama watu unaowasiliana nao hawana hamu ya kufundishwa au wanachagua kusitisha kutembelewa, andika taarifa hiyo katika app. Andika jinsi ambavyo utaendelea kuwasiliana nao na kuwalea mpaka wawe tayari kujifunza zaidi. Kwa mfano, fikiria kuwaalika wajiunge kwenye mfululizo wa barua pepe ili kupokea jumbe kuhusu Yesu Kristo au mada zingine za injili. Ungeweza pia kuwaunganisha na muumini ambaye anaweza kujibu maswali na kulea mapendeleo na urafiki wao. Weka ukumbusho katika app wa kufuatilia pamoja nao. Waulize kama wanamjua yeyote ambaye naye pia angependelea.

Unaweza pia kutafuta watu wa kuwafundisha kupitia app ya Hubiri Injili Yangu kwa kutumia vichujio au makundi ili kutuma jumbe za kundi. Hii inaweza kuwa njia bora ya kuwaruhusu watu wajue kuhusu matukio kama shughuli za kata na ibada za ubatizo. Fuatilia kwa mialiko binafsi kwa matukio haya.

Kujifunza na Mmisionari Mwenza

Ili kuona vile app ya Hubiri Injili Yangu inavyoweza kuwa nyenzo bora katika kutafuta, jaribuni shughuli zifuatazo. Mnapofanya hivyo, zingatieni misukumo mnayoipokea.

  • Mkitumia vichujio, watambueni watu wote ambao wameshafunzwa masomo matatu au zaidi. Wapeni mialiko binafsi ya kuhudhuria kanisani Jumapili hii.

  • Tengenezeni kichujio na muwatafute wale wote ambao walikuwa na tarehe ya ubatizo iliyopangwa na walihudhuria kanisani angalau mara mbili.

  • Pangeni kuwatumia ujumbe watu binafsi wajiunge na shughuli ya kata au mradi wa huduma. Mara kwa mara mnaweza kutaka kutuma ujumbe wa kundi na kuwafuatilia mmoja mmoja.

  • Jadiliana na mwenza wako wale ambao umepata msukumo kuwahusu. Weka mipango ya kuwatembelea au vinginevyo wasiliana nao haraka.

Tafuta kupitia Huduma

Toa Fursa kwa ajili Watu Kuja na Kutumikia.

Watu wanaweza kuwa na uzoefu chanya na kuunganika na wamisionari na waumini wenyeji katika shughuli za huduma. Watu wengi wanafurahia kushiriki talanta zao, ujuzi, au huduma na wanahitaji tu kualikwa.

Waalike watu kushiriki katika shughuli za huduma zilizopangwa na kata. Unaweza pia kuwaunganisha watu na fursa za huduma kama vile zile zilizo kwenye JustServe pale inapopatikana. Mnapotumikia pamoja na wengine, mnaweza kuja pamoja katika njia yenye nguvu.

Toa Huduma

Kama Mwokozi, “zunguka huko na huko, ukitenda kazi njema” (Matendo ya Mitume 10:38; ona pia “Zunguka Huko na Huko, Ukitenda Kazi Njema” katika sura ya 1). Sali ili kufahamu fursa za kutenda kazi njema kila siku. Wakati mwingine huduma yako itapangwa, lakini mara nyingi haitakuwa imepangwa. Tafuta njia rahisi za haraka za kutumikia, kusaidia, na kuwainua watu. Kumbuka kwamba Bwana alitumia fursa zisizotarajiwa kuwafikia na kuwabariki wengine.

Tumikia kwa hamu ya dhati ili kuwasaidia watu. Kama huduma inaongoza hadi kwenye fursa ya kufundisha, kuwa na shukrani. Kama sivyo, basi kuwa na shukrani kwamba umefanya kitu chema kwa ajili ya mtu. Jibu maswali kama watu watakuuliza. Kama mtu anaonesha kuvutiwa, jibu kwa ufupi na upange kukutana naye muda tofauti ili kushiriki ujumbe.

Hakikisha unafuata miongozo kwa ajili ya huduma katika Viwango vya Umisionari kwa Wafuasi wa Yesu Kristo, 2.7 na7.2.

Tafuta Watu Pale Walipo

Kutafuta watu pale walipo huanza na kujaribu kuwaona jinsi Mungu anavyowaona. Chukulia kwamba unaweza kuwa umeongozwa kuzungumza na mtu huyu, au yeye ameongozwa kwako. Tafuta kuelewa mahitaji ya kiroho na matamanio ya mtu. Tafuta ni kipi kilicho cha muhimu sana kwao, hasa katika mahusiano yao na familia na pia Mungu. Ungeweza kuuliza maswali kama yale yaliyo hapo chini—na kisha sikiliza kwa uaminifu:

  • Ni kipi unachothamini sana?

  • Ni kipi hukupa shangwe?

  • Ni kipi unataka kwa ajili ya siku zako za usoni na kwa ajili ya wale unaowapenda?

  • Ni changamoto zipi unakabiliana nazo katika kufikia tumaini na ndoto zako?

  • Ni vipengele gani vya maisha yako unataka kuviboresha?

Tafuta mwongozo unapotafakari juu ya kile unachojifunza kuhusu tumaini na matamanio ya mtu. Ni kweli zipi za injili zinaungana kwa njia ya asili na kile ambacho yeye anakitaka?

Fikiria mbinu yako kutokana na mtazamo wa mtu. Ni kipi yeye anajua kukuhusu wewe? Ni kipi unachoweza kutoa ambacho kingeweza kuwa na msaada? Je, mtu huyu anahisi kwamba mmchangamano na wewe utakuwa wa thamani?

Fikiria sababu tofauti tofauti ambazo watu wangetaka kukujua wewe, waumini wengine, au Kanisa. Baadhi ya mifano ya kile unachoweza kutoa imefanyiwa muhtasari hapa chini.

Picha
wamisionari wakizungumza na mwanamke

Toa Uzoefu au Taarifa ambazo Wangezithamini

Tumia nyenzo za Kanisa na talanta zako mwenyewe na nguvu zako ili kuunganika na mapendeleo ya mtu. Tafuta msaada wa Baba wa Mbinguni katika kutoa taarifa au uzoefu ambao mtu atauthamini.

Kuwa muwazi kwa mwongozo na uwe mbunifu unapofikiria kuhusu aina tofauti za uzoefu au taarifa unazoweza kutoa. Baadhi ya mawazo yameorodheshwa hapa chini.

  • Shiriki kiungo cha nyenzo ya Kanisa ambacho kinatoa taarifa kuhusu kitu fulani ambacho kingewapendeza wao.

  • Panga tukio kama ibada (uso kwa uso au mtiririsho mubashara).

  • Toa kitu katika mkusanyiko au tukio la wenyeji (kwa mfano, tengeneza mti wa historia ya familia wa bure katika soko la mtaani).

  • Jitolee kufundisha darasa.

  • Panga darasa la kujifunza maandiko, au jitolee kusoma Biblia na maandiko mengine.

  • Fundisha Kiingereza kama lugha ya pili.

  • Tangaza shughuli za Kanisa za eneo kama vile sherehe za mapumziko au madarasa ya kujitegemea. Tumia vipeperushi au mitandao ya kijamii.

  • Waalike kwenye ibada ya ubatizo.

  • Jitolee kuwatembeza katika jengo la mikutano.

Mojawapo ya uzoefu wa thamani sana unaoweza kuwasaidia watu waupate ni kuhudhuria ibada ya Kanisa. Waalike na waeleze vile itakavyokuwa. Waambie jinsi kuhudhuria mkutano wa sakramenti kutakavyoyabariki maisha yao.

Kuwezesha Mahusiano Halisi

Watu wengi wangetaka kukutana na wengine katika jamii yao au kujuana nao vyema. Baadhi ya watu ni wapweke. Baadhi ya mawazo ya kuwezesha mahusiano halisi yameorodheshwa hapa chini.

  • Watembelee watu ambao wamehamia hivi karibuni katika eneo ili kuwakaribisha.

  • Watambulishe watu katika jamii kwa waumini ambao wana mapendeleo sawa na yao.

  • Waalike watu kwenye mikutano ya kata, shughuli, na ufunguzi.

  • Jitolee kuwasaidia waunganike na viongozi wa kata wa hekalu na historia ya familia, ambao wanaweza kuwasaidia wajifunze zaidi kuhusu wanafamilia wao waliokufa.

  • Jitolee kuwafundisha watu jinsi ya kufanya jioni ya nyumbani au kusoma maandiko kama familia. (Ona Kitabu cha Maelezo ya Jumla, 2.2.4, kwa ajili ya kanuni saidizi ambazo zinaweza kutoholewa kwa hali za watu.)

  • Waalike watu wa umri unaofaa wahudhurie seminari, wahudhurie chuo, au washiriki katika BYU–Pathway Worldwide.

Kuna njia nyingi za heshima za kuwatafuta wale ambao wanaandaliwa kwa ajili ya injili ya urejesho. Fanya kile unachoweza ili uwekwe kwenye njia ya wale ambao wanaandaliwa.

Kujifunza na Mmisionari Mwenza

Tambueni baadhi ya mawazo katika sehemu hii ambayo hamjayajaribu. Wekeni mipango ya kujaribu baadhi ya mawazo wakati wa wiki ijayo.

Wasiliana na Watu Waliopendekezwa KwakoKwako

Watu waliopendekezwa kwako wanaweza kuwa tayari kupokea injili ya Yesu Kristo. Waliopendekezwa wanaweza kutoka kwa waumini wa Kanisa, wamisionari wengine, makao makuu ya Kanisa, na juhudi za mitandao ya kijamii.

Fikia Mara Moja

Mtu anapopendekezwa kwako kupitia makao makuu au mitandao ya kijamii, pitia tena taarifa katika app ya Hubiri Injili Yangu kuhusu mapendeleo yao wao. Jaribu kuwasiliana nao haraka iwezekanavyo.

Picha
wamisionari wakigonga mlango

Tumia mwongozo ufuatao unapofanya kazi na watu waliopendekezwa kwako:

  • Kama mtu alipendekezwa na muumini au wamisionari wengine, wasiliana na mtu aliyetuma pendekezo ili kujifunza zaidi. Kama wamisionari walimpendekeza mtu, wanaweza kufundisha pamoja na wewe kwa njia za mtandaoni kama kiongozi wao wa misheni anaidhinisha. Waumini wanaweza kujiunga uso kwa uso au kushiriki kwa njia za mtandaoni katika kufundisha.

  • Bila kuchelewa jaribu kuwasiliana na mtu huyo kupitia matembezi, simu, ujumbe mfupi, barua pepe au aina nyingine ya mawasiliano. Kama mtu hatajibu, jaribu kuwasiliana naye wakati tofauti wa siku.

  • Kama mawasiliano ya kwanza yalikuwa kwa simu, ujumbe mfupi, au barua pepe fanya mpango wa kukutana na mtu huyu uso kwa uso au kupitia teknolojia.

  • Kama wenzi, pitieni tena ombi la mtu na tumbueni mahitaji na mapendeleo yake. Amua jinsi injili inavyoweza kusaidia kukidhi mahitaji hayo.

  • Wakati mnapokutana, leta vitu vyovyote vilivyoombwa, kama vile Kitabu cha Mormoni. Shiriki kweli za injili kutoka kwenye masomo ya mmisionari ambayo yanakidhi mapendeleo au mahitaji ya mtu.

Wakati mwingine watu ambao walipendekezwa wanaweza kukuongoza kwa wengine ambao Mungu anawaandaa. Kama watu unaowasiliana nao hawana hamu, waulize kama wanawajua wengine ambao wangekuwa wanapendelea au wanahitaji tumaini katika maisha yao. Labda wewe umeongozwa kwa mtu huyu kwa sababu mtu mwingine katika nyumba hiyo au ujirani yuko tayari kwa ajili ya injili.

Kama miadi na mtu imeshindikana, fikiria jinsi ambavyo unaweza kufanya kazi zingine za ummisionari katika eneo hilo. App ya Hubiri Injili Yangu inaweza kukusaidia upate watu katika ujirani ambao hapo mwanzo walifikiwa au kufundishwa.

Pendekeza Watu kwa Wamisionari katika Eneo Lingine

Wakati unapokutana na watu ambao wanapendelea kujifunza zaidi kuhusu injili lakini wanaishi nje ya eneo lako ulilopangiwa, watambulishe kwenye injili. Kisha wasaidie wajiandae kukutana na wamisionari na waumini pale wanapoishi.

Kwa idhini ya rais wako wa misheni, unaweza kuendelea kuwaunga mkono watu hawa ili kuwasaidia waipokee injili (ona Viwango vya Umisionari7.5.4).

Kujifunza na Mmisionari Mwenza

Warejeleeni tena watu wote ambao walipendekezwa katika eneo lenu katika mwezi uliopita. Tambueni watu wowote ambao hamkuweza kuwasiliana nao, na jaribuni kuwasiliana nao tena. Amueni ni yupi kati ya wale ambao walifikiwa wanapaswa kutembelewa tena. Sasisheni kumbukumbu hizi katika app ya Hubiri Injili Yangu.

Picha
wamisionari wakizungumza kwenye simu

Tumia Teknolojia

Kuna njia nyingi ambazo unaweza kutumia teknolojia ili kupata watu wa kuwafundisha. Baadhi ya mifano imeorodheshwa hapa chini:

  • Tumia vyombo vya habari vya kijamii kufanya kazi na waumini ili kutafuta watu.

  • Jenga mahusiano kwa kufikia kupitia barua pepe na mitandao ya kijamii.

  • Shiriki maandiko, nukuu, na jumbe za injili zenye kuinua.

  • Wasaidie watu watumie FamilySearch.org ili kujifunza zaidi kuhusu wanafamilia wao waliofariki.

  • Toa madarasa ya mtandaoni ya kufundisha ujuzi.

  • Fanya miunganiko inayofaa kupitia makundi ya mtandaoni ya mapendeleo yanayofanana.

  • Tengeneza posti ambayo inaelezea kuhusu matukio yajayo ya kata.

Kutumia teknolojia ni njia muhimu ya kuweka “mishipi mingi majini” kwa siku nzima. Kwa nyongeza kwenye juhudi zako zingine za kutafuta, weka mishipi mingi ya intaneti majini.

Picha
Mzee David A. Bednar

Mzee David A. Bednar alifundisha: “Teknolojia hutoa mikondo mingi ya nguvu ambayo kupitia kwayo tunaweza kumtangaza ‘Yesu Kristo, na yeye aliyesulubiwa’ na ‘kuihubiri toba kwa watu’ [1 Wakorintho 2:2; Mafundisho na Maagano 44:3]. Kizazi chipukizi hasa kimeandaliwa vyema kusikia na kujifunza kuhusu ujumbe wa urejesho kupitia njia hizi za mawasiliano” (“Wanapaswa Kuyatangaza Mambo haya kwa Ulimwengu,” semina kwa marais wapya wa misheni, Juni 24, 2016).

Kujifunza na Mmisionari Mwenza

Tafuteni kile misheni yenu inachokifanya kwa mitandao ya kijamii. Jadili na mwenza wako jinsi ambavyo mngeweza kutengeneza posti za mitandao ya kijamii ambazo zinawiana na hili. Posti zenu zinapaswa kuzingatia sera za Kanisa za intaneti (ona “Intaneti” katika sehemu ya 38.8 ya Kitabu cha Maelezo ya Jumla).

Kama misheni yenu ina mtaalumu wa mitandao ya kijamii, pateni ujuzi wake wakati mnapotengeneza posti zako za mitandao ya kijamii.

Picha
wanawake wawili wakizungumza

Tumia Historia ya Familia

Historia ya familia ni njia nyingine ambayo kupitia hiyo unaweza kupata watu wa kuwafundisha. Kote duniani, Roho anawashawishi mamilioni ya watu kuwatambua mababu zao wafu. Wengi wanataka muunganiko wenye nguvu na jamaa zao. Hii inaweza kuongoza kwenye hamu ya kupata muunganiko na utambulisho kama sehemu ya familia ya Mungu.

Kile ambacho wakati mwingine tunakiita roho ya Eliya ni ushawishi wa Roho Mtakatifu akiwavuta watu watambue, waweke kumbukumbu, na wawathamini wanafamilia wao—wote waliopita na wa sasa (ona Malaki 4:5–6).

Katika utafutaji wako, ungeweza kuwatambulisha watu kwenye FamilySearch.org au waalike wapakue app ya FamilySearch Tree au app ya FamilySearch Memories. Wewe ungeweza pia kuwapa nakala za kijitabu cha Familia Yangu: Hadithi Ambazo Hutuleta Pamoja. Nyenzo hizi zinawasaidia watu wagundue jamaa na mababu na kukusanya hadithi zao.

Tambua ni nyenzo zipi za historia ya familia zinazopatikana katika eneo lako na jinsi ambavyo zingeweza kuwasaidia watu unaowasiliana nao. Kiongozi wa hekalu na historia ya familia anaweza kuwasaidia watu wawatambue mababu zao wafu.

Waalike watu kushiriki kumbukumbu za wapendwa wao pamoja nawe. Wanapofanya hivyo, wanaweza kumhisi Roho Mtakatifu akiwashuhudia wao kuhusu umuhimu wa familia katika mpango wa Mungu. Nyakati kama hizi zinaweza kuongoza hadi kwenye mazungumzo kuhusu dhumuni la maisha, mpango wa Mungu wa furaha, na wajibu wa Mwokozi katika mpango huo.

Wakati inapofaa, wafundishe watu mafundisho kuhusu kwa nini waumini wa Kanisa wanafanya kazi ya historia ya familia na jinsi inavyohusiana na mahekalu.

Sali ili kufahamu fursa za kutumia historia ya familia katika juhudi zako za kutafuta. Kuwa mbunifu, na zifahamu rasilimali zinazopatikana.

Kujifunza Maandiko

Jifunze maandiko yafuatayo kuhusu historia ya familia. andika kile unachojifunza.

Nguvu za Kuunganisha Zilirejeshwa kupitia Eliya

Kazi kwa ajili ya Wafu

Kujifunza Binafsi au na Mwenza

Jaribu moja au zaidi ya shughuli zifuatazo ili zikusaidie kutafuta kupitia historia ya familia.

  • Panga kuzungumza na muumini ambaye ana uzoefu wa historia ya familia. Jifunze ni huduma zipi zinapatikana kupitia kiongozi wako wa kata wa hekalu na historia ya familia.

  • Fanyia mazoezi jinsi utakavyotoa msaada wa historia ya familia kwa wale unaokutana nao. Weka mipango ya kutoa historia ya familia katika juhudi zako za kutafuta.

  • Soma na jadili kijitabu cha Families and Temples ili kupata uelewa imara wa kazi ya historia ya familia. Andika kile unachojifunza katika shajara yako ya kujifunzia.

  • Tumia kijitabu cha Familia Yangu au rasilimali za FamilySearch.org unapotafuta watu wa kuwafundisha.

  • Pale inapowezekana, itisha shughuli ya ziara kanisani, fundisha darasa la historia ya familia katika sehemu za umma, au fanya mashauriano.

Tafuta Wakati Unapofundisha

Kutafuta na kufundisha ni shughuli zinazohusiana. Watu unaowafundisha mara nyingi wana marafiki au jamaa ambao wanaandaliwa kupokea injili ya urejesho. Watu unaowafundisha wanapopata baraka za injili, hamu yao ya kuzishiriki itaongezeka (ona 1 Nefi 8:12). Katika hali zote—kama vile kutafuta, kufundisha, na kufanya kazi na waumini—uliza “Je, ni nani unayemjua ambaye angefaidika na ujumbe huu?”

Wakati wale unaowafundisha wanapojiandaa kwa ajili ya ibada yao ya ubatizo, waulize kuhusu wanafamilia na marafiki ambao wangependa kuwaalika kwenye ubatizo wao. Fanya mipango ya kuwaalika na wahimize wote waje. Roho anaweza kuhisiwa kwa nguvu sana wakati wa ibada ya ubatizo.

Kujifunza na Mmisionari Mwenza

Pitieni tena orodha ya watu mnaowafundisha. Tengenezeni orodha ya wale mliowaomba watu wa kuwafundisha na wale ambao hamjawaomba. Fanyieni mazoezi jinsi mtakavyotoa mwaliko wa waliopendekezwa kwa wale walio katika kila kundi. Katika kijitabu cha mipango, andikeni muhtasari wa kutoa mwaliko huu katika matembezi yanayofuata.

Picha
wanawake wakiangalia simu

Fundisha Wakati Ukitafuta

Unapokutana na watu na kutambua mapendeleo yao na mahitaji yao, kuza tabia ya kuanza kufundisha na kushiriki ushuhuda wako. Utawapata watu wengi zaidi wa kuwafundisha kadiri unavyoshuhudia juu ya Mwokozi na injili Yake na kuwaruhusu wahisi nguvu ya Roho Mtakatifu.

Fikiria kufundisha juu ya mada kama vile furaha, dhiki, dhumuni la maisha, au kifo. Bila kujali mbinu yako ya awali ni ipi, rejelea upesi na kwa urahisi kwa Mwokozi, injili Yake na wito Wake kwa Nabii Joseph Smith. Huu ni ujumbe wetu wa kipekee kwa ulimwengu.

Vipengele vifuatavyo vinatoa mifano ya jinsi ambavyo ungeweza kwa ufupi kufundisha kuhusu Urejesho wa injili ya Yesu Kristo na umuhimu wa familia.

Fundisha na shuhudia kuhusu Urejesho wa Injili ya Yesu Kristo.

Shuhudia juu ya Yesu Kristo na fundisha mihutasari mifupi ya ukweli uliorejeshwa. Kwa mfano, unaweza kushuhudia juu ya injili ya urejesho ya Yesu Kristo katika sentensi mbili au tatu tu:

Baada ya karne nyingi za kupotea, kweli zimerejeshwa na Mungu mwenye upendo kupitia nabii aliye hai. Tuna ushahidi wa hili ambao unaweza kuushikilia mikononi mwako, kuusoma, na kuutafakari katika moyo wako. Tunakualika usome na ujifunze kweli zake kwa ajili yako mwenyewe. Je, utaturuhusu sisi …

Kama una muda zaidi, ungeweza kusema zaidi:

Ujumbe wetu ni rahisi. Mungu ni Baba yetu. Sisi ni watoto Wake. Sisi ni sehemu ya familia Yake. Yeye anatujua binafsi na anatupenda. Yeye anataka sisi tupate shangwe. Toka mwanzo wa ulimwengu, Yeye alifuata mpangilio wa kufikia kwa upendo ili kufunua injili ya Yesu Kristo ili kwamba watoto Wake waweze kujua jinsi ya kurudi Kwake. Yeye alifunua injili kwa manabii kama vile Adamu, Nuhu, Ibrahimu na Musa. Lakini watu wengi walirudia kuchagua kuikataa injili na manabii ambao waliifunza. Miaka elfu mbili iliyopita, Yesu Kristo Mwenyewe alifundisha injili Yake. Watu walimkataa hata Yesu. Baada ya vifo vya Mitume wa Yesu, watu walipotosha mafundisho ya kweli, kama vile kuhusu Uungu. Pia walibadili ibada, kama vile ubatizo.

Mwaliko wetu kwako ni kuongezea kwenye kweli ambazo tayari unazithamini. Fikiria ushahidi wetu kwamba Baba yetu wa Mbinguni amenyoosha tena mikono kwa watoto Wake kwa upendo na amefunua mafundisho na ibada za kweli kwa nabii. Jina la nabii huyu ni Joseph Smith. Ushahidi wa ukweli huu unapatikana katika kitabu—Kitabu cha Mormoni. Unaweza kukishika mikononi mwako, kukisoma, na kutafakari kweli zake akilini mwako na katika moyo wako. Tunakualika uhudhurie kanisani na ujifunze zaidi.

Fundisha na Shuhudia kuhusu Umuhimu wa Familia

Kuzungumzia umuhimu wa familia kutakusaidia upate watu wa kuwafundisha, iwe wana historia ya Kikristo au si Wakristo. Unaweza kwa haraka kuhusisha kile ambacho watu wengi wanakijua kuhusu familia na mpango wa wokovu wa Baba wa Mbinguni. Ungeweza kusema kitu fulani kama hiki:

Familia yetu inaweza kuwa mojawapo ya ushawishi muhimu sana katika maisha yetu. Familia yetu hutuunganisha sisi mmoja kwa mwingine na kutusaidia tuhisi kuhitajika na kupendwa.

Kuwa na familia imara, yenye furaha ni kipaumbele cha juu kwa watu wengi. Kuwa na ndoa imara na kulea watoto katika ulimwengu wa leo inaweza kuwa changamoto sana.

Ungeweza kisha kufanya mabadiliko kwenda kwenye ujumbe wa Urejesho:

Umekuwa sehemu ya familia ya Mungu tangu kabla ya kuzaliwa. Yeye ni Baba yetu. Baba wa Mbinguni anatutaka sisi turudi kuishi na Yeye. Wewe ni mtoto Wake na Yeye anakupenda. Yeye ana mpango wa kukusaidia kurudi Kwake.

Kweli hizi na zingine zimerejeshwa ulimwenguni na Baba yetu wa Mbinguni mwenye upendo kupitia nabii aliye hai. Kweli hizi zinaweza kutusaidia tuelewe nafasi yetu katika familia ya Mungu. Je, tunaweza kufundisha zaidi kuhusu kweli hizi? Je, utahudhuria kanisani ili uweze kujifunza zaidi?

Kujifunza na Mmisionari Mwenza

Andaeni ujumbe wa dakika moja wenye msingi wa mojawapo ya masomo katika sura ya 3. Fanyeni mazoezi kuushiriki mmoja na mwingine. Fikirieni njia ambazo mngeweza kushiriki ujumbe huu katika hali ya kutafuta. Pangeni kuushiriki katika hali inayofaa ili kuwaalika wengine wajifunze zaidi kuhusu Yesu Kristo.

Hakuna Juhudi Iliyopotea.

Wakati watu wanapochagua kutojifunza zaidi kuhusu injili ya urejesho, juhudi zako hazijapotea. Labda umepanda mbegu ambayo itakua wakati mwingine. Iwe kwamba itatendeka au haitatenda, huduma yako na dhihirisho lako la upendo halisi vitakubariki wewe na wao.

Kama watu hawako tayari kupokea injili, ona kitu kinginge unachoweza kufanya ili kuimarisha maisha yao. Mahusiano unayokuza bado ni ya maana na yenye thamani. Endelea kuwa rafiki.

Watu wakati mwingine wanahitaji muda wa kufikiria mabadiliko ambayo wameombwa wayafanye. Wasaidie wapokee jumbe kupitia barua pepe au tovuti za Kanisa. Jumbe hizi zingeweza kuwasaidia watu kukubali mialiko ya kujifunza zaidi ya siku zijazo.

Wakati mtu haikubali injili, ni kawaida kuvunjika moyo. Hata hivyo, unapomgeukia Bwana katika nyakati kama hizo, Yeye aliahidi, “Nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono” (Isaya 41:10).

Kupitia imani katika Kristo, unaweza kupata amani na hakikisho kuhusu juhudi zako. Dumisha ono la wewe ni nani na kwa nini unamtumikia Bwana kama mmisionari. Imani itakusaidia usonge mbele na uendelee katika matamanio ya haki.


Mawazo kwa ajili ya Kujifunza na Kutumia

Kujifunza Binafsi

Kujifunza Pamoja na Mwenza na Kubadilishana Mwenza

  • Wekeni mipango ya kukutana na waumini wapya katika eneo lenu. Kama inahitajika, tumieni app ya Hubiri Injili Yangu kuwatambua. Ulizeni maswali kama haya:

    • Ni jinsi gani ulijiandaa kwa ajili ya injili?

    • Ni lini na kwa jinsi gani ulilifahamu Kanisa kwa mara ya kwanza?

    • Ni kipi kilikufanya ukutane na wamsionari?

    • Ni kwa jinsi gani tunaweza kuunga mkono maendeleo yako endelevu?

    Kutoka kwenye mikutano hii, ni kipi ulijifunza kuhusu kutafuta watu ambao wanapiga hatua hadi kufikia ubatizo? Weka mipango ya kutumia kile ambacho umejifunza wiki hii.

  • Pitia tena moja ya mada zifuatazo. Ukitumia masomo katika sura ya 3, andaa mbinu rahisi ya kutafuta. Fanya mazoezi ya kufundisha katika mazingira ya kutafuta.

    • Kuhisi hitaji la maelekezo zaidi na dhumuni katika maisha

    • Kutaka kuhisi kuwa karibu zaidi na Mungu

    • Kuhitaji msaada katika maamuzi muhimu

Baraza la Wilaya, Mikutano ya Kanda na Baraza la Uongozi la Misheni

  • Someni na jadilini sehemu ya “Kuza Ono Lako la Kuweka Mipango ya Kutafuta.” Waruhusu kila wenza wakamilishe tathmini.

    • Jidilini jinsi ambavyo mawazo haya yamewasaidia wamisionari kupata watu wa kuwafundisha.

    • Orodhesheni mawazo mengine ya kutafuta watu wa kuwafundisha. Waalike wamisionari wafanye maonyesho ya mawazo yao.

    • Waalike wamisionari waweke malengo kwa ajili ya kuboresha juhudi zao za kutafuta.

  • Tengeneza orodha ya fursa kadhaa za kutafuta.

    • Mpangie kila mmisionari mojawapo ya fursa hizi. Mpe kila mmisionari dakika tano kuandaa jinsi ambavyo yeye angefundisha sehemu ya somo katika hali iliyopangwa.

    • Sisitiza hitaji la kufanya urefu wa ujumbe uendane na mazingira.

    • Waalike wamisionari kadhaa wafundishe somo walilopanga katika hali zao walizopangiwa.

  • Waalike wamisionari wafanye mazoezi ya kushiriki ujumbe wa dakika moja wa injili kwa mmoja na mwingine. Unaweza kutaka kupanga aina tofauti za mazingira ya kutafuta, kama vile kufundisha katika nyumba ya muumini, kufundisha mlangoni, kufundisha njiani, au kuwasiliana na aliyependekezwa. Waruhusu wamisionari wafanye mazoezi ya kufundishana katika kila moja ya mazingira haya.

Viongozi wa Misheni na Washauri wa Misheni

  • Weka mfano wa kazi ya muumini-mmisionari katika familia yako. Shiriki uzoefu wako kwa wamisionari na waumini.

  • Shauriana na viongozi wenyeji wa ukuhani na vikundi kuhusu njia bora kwa ajili ya wamisionari kutafuta watu wa kuwafundisha katika misheni yako.

  • Panga ibada za wamisionari ambapo unaweza kuzungumza na watu wanaofundishwa katika misheni yako. Ratibu na viongozi wenyeji wa ukuhani ili waumini wawalete rafiki zao. Waalike waumini wapya kushiriki shuhuda zao na kusimulia hadithi za kuongoka kwao kabla hujazungumza.

  • Mara kwa mara nenda na wamisionari ili kuwasaidia kutafuta watu wa kuwafundisha.

Chapisha